Uimbaji na Muziki

Egypt's Dar Al-Ifta

Uimbaji na Muziki

Question

Swala la muziki na uimbaji linazingaitiwa kuwa ni jambo la hatari kwa waislamu wa Ulaya, na hasa rai zilitofautiana kuhusu jambo hilo, na madhehebu manne ya Fiqhi yameharamisha vyombo vya muziki, na wakasema: Uimbaji pia ni makruhu au haramu, wakati ambapo waislamu wengi walioshikamana na dini wanatumia vyombo vya muziki, na baadhi ya wanazuoni wanaruhusu muziki, muda wa kuwa yaliyomo ni bora, na hii ni nadra katika nchi za kimagharibi.
Je, kuna vyombo vya muziki halali (visivyokuwa dufu)?
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Swala la kusikiliza muziki ni swala lenye hitilafu za kifiqhi, si kutoka misingi ya Akida, na si kutokana mambo ya kidharura katika dini,na waislamu hawapaswi kutuhumiana kwa ufasiki au kukanushana baadhi yao kwa ajili ya maswala hayo yenye hitilafu; kwani hali ilivyo hukanushwa wenye kukubaliana wala hawakanushwi wenye kutofautiana, na muda wa kuwa kuna miongoni mwa wanachuoni wamehalalisha muziki - na hawa wanazingatiwa katika kauli yao na inajuzu kuwafuata – basi haijuzu kuugawanya Umma kwa sababu ya maswala yenye hitilafu hiyo, na hasa kwa kuwa hakuna matini sahihi na za wazi katika Sheria yaliyoharamisha muziki, kwa ajili hiyo kuna hitilafu. Na hoja ya waliosema kwa kuharimisha muziki ni maana ya Dhahiri kutokana baadhi ya aya za Qur`ani tukufu ambazo wafasiri walizichukua kama ni uimbaji na muziki, kama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara} [LUQMAAN 6], na kauli yake: {Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi} [AL MUMINUN 3], na kauli yake: {Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako}[AL ISRAA 64], na kutoka Sunna hadithi ya Abu-Amir au Abu-Malik Al-Ashari R.A kutokana na Mtume S.A.W aliyesema: "Watakuwa kutokana na Umma wangu watu wanaohalalisha uzinifu, nguo zahariri, (kwa mwanaume) pombe na vyombo vya muziki" na Imamu Al-Bukhariy katika sahihi yake, na kadhalika kutokana na Hadithi zilizokuwa na maana hiyo, na wingi wa maulama kutoka kwa Masahaba na waliowafuata walisema kwamba kucheza muziki na vyombo vyake si chochote ila ni sauti tu: nzuri yake ni nzuri na na mbaya yake ni mbaya, na aya za Qur`ani hazina katazo wazi juu ya muziki na vyombo vyake mashuhuri, na katazo katika Hadithi ya Imamu Bukhariy ni kwa baadhi sio kwa zote kwa maana zote zilizokatazwa katika Hadithi zilijumuisha pamoja katika Sura moja, Uzinifu, na Hariri iliyoharamishwa juu ya mwanaume; na makusudio ni kukataza maisha ya anasa si muziki hasa hasa, na misingi ya Usuul ilikiri kwamba kuambatana si hoja; na kutajwa kwa muziki baada uzinifu si hoja kuharimisha muziki, na Hadithi zingine kutokana na hizo si sahihi au inahusisha miziki inayowasahaulisha juu ya Dhikri na ibada ya Mwenyezi Mungu au inasabibisha maovu na mambo ya haramu; na Hadithi sahihi kutokana na Hadithi hizo si kwa maana Dhahiri na iliyo na maana Dhahiri si sahihi. Na hii rai ya madhehebu ya watu wa Madinah, na iliyopokelewa na kundi la Masahaba kama Abdullah Ibn Az-Zubair na Hassan Ibn Thabit na Muawiya na Amr Ibn Al-Aas R.A na kutokana na waliofuata Al-Kadhi Shuraih na Said Ibn Al-Mosaiyab na Attaa Ibn Abi Rabah na Al-Zuhariy na Al-Shaabiy na Saad Ibn Ibrahim Ibn Abd Ar-Rahman Ibn Auf –Na alikuwa hazungumzi mazungumzo ila kwa kupiga udi– na wengineo; na Imam wa Haram mbili (Makka na Madinah) alisema katika kitabu cha: [Al-Nihaya] (Mwisho): "Ilipokelewa kwa uthabiti kutoka kwa wanahistoria kwamba Abdullah Ibn Az-Zubair R.A alikuwa na wajakazi waliopiga udi na Ibn Omar R.A aliingia na pembeni mwake kuna udi, na akasema: Kitu gani hicho Ewe, sahibu wa Mtume S.A.W? kisha akaichukua, na Ibn Oma aliiangali na kusema: Hii ni mizani ya Shamu, Ibn Az-Zubai alijibu: Akili hupimwa nayo" mwisho. Na wanaokubaliana na madhehebu hii ni Ibn Hazm na watu wa Dhahiri na baadhi ya Shafi na miongoni mwao Ustadh Abu Eshak Ash-Shirazi na Al-Mawardimna Al- na Ruyani na Abu Mansur Al-Baghdadi na Al-Rafiy na Hoja ya Uislamu Al-Ghazali na Abu Al-Fadl Ibn Tahir Al-Kisarani na Imamu Ezul-Din Ibn Absul-Salam na Shekhe wa Uislamu Takiy Al- Din Ibn Dakik Al-Eid na Abd Al-Ghani Al-Nabulsi Al-Hanafi… na wingineo.
Na waliandika juu ya uhalali wa muziki na vyombo vyake kundi la maulamaa kama: Ibn Hazm Al-Dhahiri katika risala yake katika kusikiliza, na Ibn Al-Kisarani katika kitabu chake " Al-Samaiy" "kusikilizia", na Al-Edfiwiy katika "Al-Imtaii Bi Ahkam Al-Samaiy", na Abu Al-Mawahib Al-Shazliy Al-Malikiy katika "Farah Al-Asmaiy Bi Rukhs Al-Samaiy", na wingineo wengi, na aliyeweka wazi juu ya uhalali wa vyombo vya muziki Hoja wa Uislamu Al-Ghazaly –R.A- aliposema: " Pumbao linasaidia juu ya kufanya bidii, na kufanya bidii hakuwezekani kusubiriwa juu yake ila kwa nafsi za Mitume A.S, na pumbao ni dawa ya moyo kutokana na taabu na kero, basi inapaswa kuwa ni halali, lakini sio kwa wingi, kama dawa haipaswi kuzidishwa juu ya haja, basi pumbao kwa makusudio na hii heri, na hii ni kwa asiye hisisha na kusikiliza sifa nzuri zinazotakiwa kuhisisha moyoni, lakini hawezi kuhisi na pumbao ila kwa ladha na raha tupu tu, na inapaswa kufanya hivyo ili kupata makusudio yaliyotajwa, ndiyo hii ni kasoro juu ya sifa ya ukamilifu na ukamilifu ni sifa ya aliyekuwa hahitaji pumbao au raha kwa isiye haki, kwani mema ya watu wema ni mabaya ya waliokaribu/wachamumu. Na aliyefahamisha kwa makini elimu ya utabibu wa mioyo na jinsi ya kuitunza nayo, ili kuiendesha kwa haki na wema alijua kikweli kwamba pumbao lake kwa mambo kama hayo ni dawa iliyo bora" [Ihiau Ulum Al-Din, Imam Al-Ghazaly, 2/226, chapa ya Al-Matbaa Al-Azharia], na pia Sultani wa maulama Al-Ezz Ibn Abd As-Salam alisema kwamba uimbaji na vyombo vya muziki na visivyokuwa hivyo vimeweza kuwa sababu ya kuboresha mioyo, akasema: "Njia ya kurekebisha mioyo inakuwa kwa sababu za kutoka nje; kama kusikiliza Qur`ani na hiyo ni bora zaidi kwa wasikilizaji waadhi na ukumbusho, na inakuwa kwa wimbo kwa maana kusikilizia mashairi ya kidini, au kwa uimbaji kwa kutumia vyombo vya muziki na msikilizaji aliyehalalisha kusikia vyombo hivyo anapaswa kusikia mema na kuacha maasi kwa kusikiliza waliyohitilafiana katika mambo yanayosikilizwa" [Al-Taj wa Al-Iklil, Abd Rabiy Al-Malikiy, 2/62, Dar Al-Fikr]. Na Shekhe Ibn Kamah alisema: Shekhe Ezz Al-Din Ibn Abd As-Salam alipoulizwa juu ya vyombo vyote, alisema: Mubaha -yaani halali- na Sheikh Sharaf Al-Din At-Tilmisani alisema: Ibn Abd As-Salam alitaka kusema kwamba hakuna dalili sahihi kutokana na Sunna kwa kuviharimisha, akiwaambia maneno hayo watu wa Misri- Na Shekhe Ezz Ibn Abd As-Salam alimsikia maneno yake na alimjibu: Hapana, nilitaka kusema hayo ni halali.[kutoka Farah Al-Asmaiy Bi Rukhs Al-Samaiy, Abu Al-Mawahib Al-Shazly], na Al-Kurtubiy aliandika katika " Al-Jamii Li Ahkam Al-Quran" kauli ya Al-Kushiriy: Muziki ulipigwa mbele ya Mtume S.A.W siku ya kuingia Madinah na Abu Bakr alikemea hayo lakini Mtume S.A.W alisema: "Waacheni Ewe Abu Bakr; ili Mayahudu wajue kwamba dini yetu ni pana" na wanawake wa Madina walikuwa wakipiga muziki na kuimba: Sisi ni mabinti wa Al-Najar, na Muhamad ni jirani bora zaidi, kisha Kurtubiy alisema: "Imesemekana kwamba ngoma katika ndoa ni kama dufu, na pia vyombo vya muziki vinavyoitangaza ndoa inajuzu kuvitumia kwa maneno yaliyo mazuri na si maneno machafu" [Tafsiri Al-Kurtubiy, 14/54]. Na Al-Shaukaniy aliandika kauli ya walioharimisha muziki na waliohalalisha na aliashiria juu ya dalili za makundi yote mawili katika "Nailu Al-Awtwa" Katika mlango wa yaliyokuja katika chombo cha pumbazo, na alitoa maoni yake juu ya Hadithi: "Kila kinachompumbaza mtu ni batili ila kulenga kwa upinde wake na kumfunza farasi wake na kuwapumbaza jamaa zake basi mambo hayo ni haki" Kwa kauli ya Al-Ghazaly: Tumesema kwamba kauli yake S.A.W "Batili" haimaanisha ni haramu; bali inamaanisha hakuna faida , kisha Al-Shaukaniy alisema: "Na halo ni jawabu sahihi; kwani yasiyo na faida ni katika mlango wa mubaha" na alitoa mifano mingine juu ya kuhalalisha muziki kama Hadithi ya mwanamke liyeweka nadhiri ya kupiga dufu mbele ya Mtume S.A.W Mwenyezi Mungu akimrudisha salama katika vita miongoni mwa vita na Mtume S.A.W alitoa ruhusa kwake ili kutekeleza nadhiri na dufu ikapigwa. Imepokelewa na kusahihishwa na At-Tirmiziy kutoka Hadithi ya Buraida R.A, na ruhusu yake ilimaanisha kwamba kutenda kwake si maasia katika msimamo kama huo. Na Al-Shaukani aliashiria kwenye risala yake kwa anwani" Ibtal Daawa Al-Ijmaa ala Tahrim Mutlak As-Samaiy" (kubatilisha madai ya kuwa kuna Ijmaii katika swala la kuharamisha kusikilizia muziki kwa ujumla). [Nail Al-Autwar 8/118], na Ibn Hazm alisema: "Kwamba Mtume S.A.W alisema: Matendo hutegemea nia, na kila mtu atalipwa kwa nia yake" na aliyenuia kusikia wimbo ili kumwasi Mwenyezi Mungu basi yeye ni fasiki, na pia kila kitu sio uimbaji tu, kilichosaidia mtu kumwasi Mwenyezi Mungu mwenye kukitenda ni fasiki, na aliyenuia kutokana na wimbo kuburudisha nafsi yake ili apate nguvu za kumcha Mwenyezi Mungu na kuchangamsha nafsi yake ili kufanya wema basi yeye ni mtiifu mwenye vizuri na kitendo chake ni haki, na asiye nuia utii au maasia kitendo chake hakina maana ni chenye kusamehewa, kama mtu kutoka kwenda kuitembelea bustani yake na kukaa kwake mbele ya mlango wa nyumba yake na kutizama". [Al-Mahali, Ibn Hazm (7/567)].
Na kutokana na yaliyotangulia tunakuta kwamba uimbaji kwa kutumia chombo cha muziki au kutotumia chombo cha muziki ni swala lililokuwa na majadiliano mengi na mazungumzo kati ya wanazuoni wa kiislamu tangu zama za awali; waliafikiana katika maudhui na kuhitalifiana katika maudhui nyingine. Waliafikiana kwamba wimbo ukiwa na maneno machafu ni haramu au ufasiki au kuchochea maasia; kwa maana wimbo ni maneno tu: Uzuri wake ni uzuri na ubaya wake ni ubaya, na kila kauli yenye mambo ya haramu ni haramu. Basi ni nini fikira yako katika hali ya mkusanyiko wa mizani, wimbo na athari? Na wameafikiana kutokana na hayo uimbaji wa kimaumbile uliokuwa bila ya vyombo na uchocheo/ ushawishi, na hayo ni katika minasaba ya furaha iliyo halali kama Arusi, na kurejea aliyekuwa mbali, siku za Eid, na kadhalika, na wamehitalifiana katika uimbaji kwa kutumia vyombo vya muziki. Na kauli tulioichagua ni kuruhusu kutumia vyombo vya muziki na kuvisikia kwa sharti ya kuchagua ubora na kutoshughulishwa na yanayomuweka mbali juu ya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu au yanayosabibisha ufisadi na hayaambatani na sheria tukufu; kwani hakuna yaliyohukumu na kukataza kwa kusikia sauti nzuri zenye mizani pamoja na chombo cha muziki katika Qur`ani na Sunna ya Mtume S.A.W au Qiyasi au kupata dalili za kisheria kutokana na vyanzo. Na maumbile safi yanahisi sauti nzuri na yanapenda, hata inasemekana kwamba sababu ya hayo ni tamko la Mwenyezi Mungu kwa wanadamu katika ulimwengu kabla ya kuanza uumbaji alipowaleta wanadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? , na hii ndiyo tunayoona inaafikiana kwa wakati wetu.na inapaswa katika hali hii kuonya juu ya mambo yafuatayo:
1- Inajuzu kuchagua baina ya madhehebu ya wenyekujitahidi na Maimamu wanaofuatwa: kwani maswala ya kisheria ni pande mbili: Upande ulio na makubaliano kutoka kwa maulama (Ijmaa) na ikajulikana kama ni udharura katika dini na upande huu haijuzu kuhitilafiana nao; kwani inamaanisha dhati ya Uislamu, na kutia shaka ni kama kuitilia shaka misingi ya dini. Upande mwingine ni: Maswala hayo waliyohitilafiana katika hukumu yake Maulama na hakuna Ijmaa kati yake; na jambo lake ni pana , na hitilafu juu yake ni rehema, na Mwislamu ana hiari kuchagua rai yeyote kutoka kauli za Maulama kuhusu maswala hayo.
2- Ukanushaji unakuwa katika yenye Ijmaa: Al-Suyuti katika kitabu cha: [Al-Ashbah wa Al- Nadhair] Alitaja kwanba: "Yaliyo na hitilafu hayakanushwi, lakini yaliyo na Ijmaa yanakanushwa" na hii inamaanisha kwamba swala likiwa na hitilafu kwa wenye madhehebu mbalimbali za kifiqhi haijuzu kwa watu wa madhehebu nyingine kuzikanusha rai za watu wa madhehebu nyingine katika swala hilo; kwani kuna hitilafu kati yao.
3- Kutofautisha baina ya mpaka wa Fiqhi na hukumu ya mpaka wa ucha Mungu: Na Maulama waliafikiana juu ya mpaka wa Ucha Mungu kuwa ni mpana zaidi kuliko mpaka wa hukumu ya Kifiqhi; na hiyo ni kwa sababu Mwislamu anaweza kuacha mambo mengi ya halali mambo kwa uchamungu, na hii haina maana ya kumlazimisha mwingine mambo hayo kama ni wajibu kisheria, ataingia katika kuharamisha halali, na pia hapaswi kutumia hukumu za dhana zenye hitilafu kama hukumu zisizo na shaka ya ijmaa na ataingia katika hali ya Bidaa kwa kuyabana aliyeyapanua Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake S.A.W, bali anapaswa kutumia maadili mema katika hali ya hitilafu kama katika mwenendo wa Al-Salaf katika maswala waliyohitalifiana nayo na ya jitihada ili kutoa hukumu yake.
Na kwa mujibu wa hayo na katika jibu la swali hilo: Hakuna kizuizi kinachokuzuia kusikiliza vyombo vya muziki muda wa kuwa muziki huo sio njia ya kukupelekea katika kufanya vitendo vya haramu au haukushughulishi mpaka ukaacha ya wajibu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas