Kumwondolea Mashine Mtu Mwenye Ubo...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumwondolea Mashine Mtu Mwenye Ubongo Uliosimama Kufanya Kazi.

Question

Nini hukumu ya kuondoa mashine kwa mgonjwa aliye mahututi baada ya ubongo wake kusimama kufanya kazi 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Matumizi ya mashine hizi kwa mambo ya tiba na dawa na yanayoangaliwa kwenye Sheria za Kiislamu, wanachuoni wengi wanaona kuwa kuzitumia kwa kazi za matibabu si jambo la lazima, kwa maana mwenye kuziacha mashine hizi kwa kutozitumia kimatibabu hatakuwa na madhambi au makosa au kuhesabiwa kuwa amefanya jambo lilio haramu. Imepokelewa Hadithi na Imamu Bukhari na Imamu Muslimu katika vitabu vyao kuwa mwanamke mmoja alikwenda kwa Mtume S.A.W. na akamwambia: “Mimi ninasumbuliwa na maumivu ya kichwa na ninafanya vipimo, basi niombee dua kwa Mwenyezi Mungu, Mtume akasema: “Ikiwa utataka, kuwa na subira utakuwa na pepo, na ukiwa unataka nikuombee dua na Mwenyezi Mungu atakuponya” basi yule mwanamke akasema: Nasubiri. Kisha akasema: Mimi ninataka kufanya vipimo hivyo niombee dua kwa Mwenyezi Mungu nisivifanye, basi Mtume akamuombea”. Hadithi hii ina dalili ya wazi juu ya kufaa kuacha mtu kutumia dawa za matibabu, kwani Mtume S.A.W. alimpa hiyari mbili huyu mwanamke kati ya kusubiri juu ya matatizo yake na ataingia Peponi au kuombewa dua kwa ajili ya kupata uzima, basi mwanamke akachagua kusubiri na kuingia Peponi.
Jamhuri ya wanachuoni wamezungumzia kufanya matibabu kwa ujumla wake kuwa ni jambo lenalofaa kulifanya lakini pia ni bora zaidi kuliacha.
Anasema Imam Al-Murghnaany Al- Hanafiy katika ufafanuzi wa kitabu cha: [Al-Bidaya 4/381]: (hakuna ubaya wowote kuchoma sindano kwa lengo la matibabu), kwa sababu kufanya dawa ni Halali kwa kauli za wanachuoni wote, na kuna Hadithi iliyopokelewa juu ya uhalali wa kufanya dawa. Na wala hakuna tofauti kati ya wanaume na wanawake.
Na anasema An-Nafraawiy Al-Maaliky kwenye kitabu cha: [Al-Fawakihi Ad-dawaany 2/339] kuwa: “Vile vile hakuna ubaya wowote kufanya tiba” nayo ni jaribio la kupambana na ugonjwa kutokana na Hadithi sahihi, kauli yake Mtume S.A.W. kuwa: “Hakika ya Mwenyezi Mungu – Mwenye Utukufu - hakuteremsha ugonjwa isipokuwa ameuteremshia na tiba yake” ameipokea Bukhari na ni Hadithi itokayo kwa Abu Huraira. Kuteremshwa kwa ugonjwa ni ishara ya kufaa kufanya dawa”.
Na ibara zinapatikana kwenye vitabu vya Imamu An-Nawawy na kwenye vitabu vya Imam Shaafiy pia (5/98) “Na inapendeza kufanya tiba kwa mujibu wa iliyotajwa na mtunzi wa kitabu na wengineo kutokana na Hadithi mashuhuri katika mambo ya kufanya dawa. Na ikiwa mtu ataacha kutumia dawa kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, basi hilo ni jambo bora zaidi”
Na anasema Al-Bahuuty Al-Hambaly katika cha: [Sharhu ya Al-Iqnaai 2/76]: “Kuacha kutumia dawa ni bora zaidi”. Ametamka – Imam Ahmad – kuwa ni jambo lililokaribu zaidi na kumtegemea Mwenyezi Mungu. Na wakateua Abul wafaa na Ibn Al-Juzy na wengineo Hadithi nyingi za kufanya tiba, kwa hivyo si lazima kutumia dawa hata mtu akidhani kuwa dawa hiyo itamsaidia. Lakini inafaa kwa makubaliano ya wanachuoni na wala haipingani na dhana ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, kwa Hadithi ya Abu Dardaai kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Hakika ya Mwnyezi Mungu ameteremsha ugonjwa na dawa, na akafanya kila ugonjwa kuwa na dawa yake, hivyo tumieni dawa, na wala musitumie dawa zilizo haramu” (imepokelewa na Abu Daud katika).
Na wametaja baadhi ya wasomi wa kishaafy kuwa sababu ya kutokuwa lazima kutumia dawa ni kuto kunufaika kwake, na wakasema kuwa lau yatakatwa manufaa yake itakuwa ni lazima. Na amenukuu As-shams Al-Ramly katika sherehe yake ya kitabu cha: [Minhaaj 2/19] kutoka kwa kadhi Iyaadh, jumla ya kauli za wanachuoni juu ya kutokuwepo ulazima wa kutumia dawa, na kutoa sababu kuwa: “hakika haikulazimishwa kutumia dawa ni kama vile kula mzoga kwa mtu aliyelazimika na kuchanganya tonge ya chakula na kilevi ili kutopoteza manufaa yake kinyume na kutofanya hivyo”
Abu dhiyaa amesema kwenye kitabu chake juu ya kauli ya: (ili kutopoteza manufaa yake) kwa kusema: “Ninafahamu kuwa lau manufaa yake yatakatika kama vile mshipa wa sehemu ya kutolea damu basi itakuwa ni lazima, nayo ni kauli iliyo karibu”.
Kwa hivyo inafaa kisheria (kufanya au kuacha) kuweka mashine ya uhai kwenye mwili wa mgonjwa na kubakia ikiendelea kufanya kazi kama njia ya matibabu, ikiwa faida zake hazitokani na hali ya kusimama kwa ubongo “Kifo cha kitabibu”. Ikiwa madaktari watahusisha wenye weledi hali hiyo basi itafaa kuiondoa, na wala si haramu kufanya hivyo na wala hawatapata madhambi. Na ikiwa uunganishaji wa mashine hii kwa mgonjwa ni kwa lengo la kusaidia mwili wa mgonjwa huyo uondoe vimiminiko ili kurahisisha upumuaji au mfano wa hayo, na kukawa na hali ya uhai kwa kutumia tiba ya mashine hizi basi haifai kuziondoa kwa mgonjwa, kwa dhana kubwa ya kufaidika nazo, na haya yanakubaliana na yale yaliyosemwa na wanachuoni wa madhehebu ya Imam Shaafy.
Si jukumu la daktari kuchukuwa maamuzi ya kusimamisha matumizi ya mashine hizi kwa mgonjwa kwa kutaka kwake, bali anayeamua hivyo ni mgonjwa mwenyewe kama vile akitoa maagizo au wasia katika hilo au kwa maamuzi ya msimamizi wake, wakati huo daktari hatabeba jukumu lolote la kisheria.
Na wala haizingatiwi kuondoa hizi mashine ni katika kumuuwa mgonjwa, kwa sababu kuuwa ni kukusudia kitendo hicho moja kwa moja, tofauti na hali hii, na uuwaji unakuwa kwa kuacha kufunga mashine, na kuuwa kunakofanywa na daktari kwa kumaliza uhai wa mgonjwa ni sawa sawa kitendo hiki kimefanyika kwa upande wake daktari kutokana na huruma yake kwa mgonjwa, au ombi la mgonjwa mwenyewe kwa kutokuwa na uwezo wa kuhimili maumivu, au msimamizi wake, jambo hilo ni haramu moja kwa moja, kwa sababu uhai wa mgonjwa hapa ni wenye kuendelea na wala si wenye kusitishwa na vifaa hivi vya matibabu, basi kuthubutu kuukatisha uhai wa mgonjwa kwa hali hii kunazingatiwa kuwa ni kuitoa roho na kuuwa nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameiharamisha isiuawe isipokuwa kwa njia ya haki.
Na tofauti ya hili na lile ni kuwa kutumia dawa si sharti la kupatikana njia ya kupona, isipokuwa huenda mtu akapata kupona pasi na kutumia dawa na mfano wake, na ni katika sababu ya hiyari, isipokuwa kupona ni katika vile alivyoviweka Mwenyezi Mungu kwenye mwili wa mwanadamu ikiwa ni pamoja na nguvu asilia za mwili na mfano wake. Kuacha kutumia dawa hakutozingatiwa kuwa ni makosa kwa sababu tu ya kuacha halali. Na kuacha halali – kwa upande wake – ni halali. Ama kuuwa – nako ni kuupoteza uhai wa mgonjwa – matokeo yake ni kinyume na hayo ya mwanzo.
Kutokana na maelezo hayo: Inafaa kisheria kuondoa mashine au vyombo vilivyotengenezwa kwa ajili ya kuendeleza uhai wa mgonjwa aliyekata tamaa ya kupona kwake, mashine ambazo hutumika kusaidia tu katika kubakisha uhai wake pasi na kuiboresha hali yake ya kiafya, nayo ni hali ambayo huitwa “kifo cha kitabibu, ikiwa madaktari watashauri hivyo, na pia mgonjwa akiusia hivyo au msimamizi wake kuruhusu hivyo. Ama vifaa hivyo vikiwa ni kwa lengo lengine kama vile kusaidia kuondoa vimiminiko mwilini ili kumrahisishia mgonjwa kupumua au mfano wa hayo basi haifai kuviondoa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas