Uthibitisho wa Ruhusa kwa Upimaji

Egypt's Dar Al-Ifta

Uthibitisho wa Ruhusa kwa Upimaji

Question

Je, Inaruhusiwa kuthibitisha ruhusa kwa Upimaji au kupima kwa ruhusa? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Kuna urahisi wa Sheria tukufu katika baadhi ya hukumu zake, na hali hii inajulikana katika Fiqhi kwa jina la ruhusa ya Kisheria, na ubaguaji huu wa dalili za kiujumla kwa ajili ya kuondoa kwa aibu kutoka kwa Waislamu unadhaniwa kuwa ni kinyume na asili. Je, inaruhusiwa -Baada ya kuangalia sababu yake- kwa mwanachuoni wa Fiqhi kupima au la?
Maana ya ruhusa katika Lugha ni: Urahisi. Al-Fayoumi alisema katika kitabu chake “Al-Misbahul Muniir”: “Ruhusa ni urahisi wa jambo, inasemwa kuwa: Sheria ilituruhusu. [Al-Misbahul Muniir, Uk. 223, kidahizo cha: RUKHSA, Al-Maktabah Al-Ilmiyyah].
Ama kuhusu maana ya ruhusa katika Istilahi inafanana na maana yake ya kilugha, nayo ni urahisi uliopatikana kinyume na asili kwa ajili ya kuondoa ugumu, Al-Asnawi alisema: Kwa mujibu wa Sheria, ruhusa ni hukumu thabiti kinyume na dalili kwa sababu ya ugumu au aibu. [At-Tamhiid fii Takhriij Al-Fruu’ ala Al-Usuul, uk. 71, Mu’asasatur Resalah, Beirut].
Ibn Al-Najjar alisema kuwa: Ruhusa (Kwa mujibu wa Sheria: ni jambo lililothibitishwa kinyume na dalili ya kisheria kwa hukumu iliyopinga na iliyo bora zaidi). Kauli yake: (ni jambo lililothibitishwa kinyume na dalili ya kisheria) inabagua mambo yaliyothibitishwa kwa mujibu wa dalili, mambo hayo hayana ruhusa, bali ni uamuzi kama vile; kufunga swaumu kwa mkazi wa mji. Na kauli yake: (Kwa hukumu iliyopinga na iliyo bora zaidi) inabagua hukumu zilizopinga na zisizo bora zaidi, bali ni sawa nayo, basi ni lazima kupata hukumu zilizo bora zaidi, au hukumu hazifiki usawa wa dalili ya Kisheria, basi haziathiri, na uamuzi unabaki kama ulivyo”. [Sharhul Kawkab Al-Muniir 1/478, Maktabatul Abeikan]. Ama kuhusu maana ya Upimaji katika lugha, inaonesha maana ya usawa kwa ujumla. Al-Juhari alisema: Nilipima kitu fulani kwa kingine. [Al-Sahah Tajul Lugha na Sahah Al-Arabia, 3/967, kidahizo cha Qausa (kupima), Darul Elmi lelmalayiin].
Upimaji kwa mujibu wa Sheria ni kusawazisha kwa njia hasa kati ya suala lililopimiwa na suala lililopimwa, Ibn Qudaamah alisema: Upimaji kwa mujibu wa Sheria ni kupima hukumu ya suala na hukumu ya suala lengine kwa njia ya uhusiano baina yao. Na imesemekana kuwa: kutoa hukumu maalumu katika suala fulani ni kutoa hukumu ile ile katika suala lengine kwa ushiriki wao katika sababu maalumu. [Rawdhatul Nadhir wajantul Manadhir 2/141, Mu’asatul Rayan Leltiba’atu wan Nashr wat Tawzii’]. Wanavyuoni wengi walizungumzia suala hili juu la Upimaji na ukiwa unahusika na ruhusa, adhabu, na kadhalika au la?
Mtazamo sahihi zaidi wa suala hili ni kwamba inaruhusiwa kupima kwa ruhusa katika kuthibitisha hukumu ya Kisheria, na hakuna jambo lolote katika hilo kama tukijua sababu na tukiwa tumeihakikisha.
Ama dalili ya usahihi wa hivyo ni ujumla wa dalili zilizothibitika kwa Upimaji wa Qur`ani na Sunna na makubaliano yaliyokubaliwa kiakili, kila hukumu ya kisheria sababu yake ilifahamika na hukumu yake ilipatikana katika suala lingine, na masharti yote ya Upimaji yamepatikana, basi hukumu ya suala hili ni ile ile, kwa sababu ruhusa siyo chochote bali ni hukumu ya Kisheria tu, na hakuna katika Sheria kitu ambacho kinauondosha ujumla wa dalili.
Vile vile ruhusa inathibitishwa kwa Upimaji kupitia Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa mmoja wa masahaba na iliyo na maana ya udhana, uhusiano baina yao ni maana ya kudhania, na inawezekana kuwapo kwa makosa na usahaulifu katika kila moja.
Na kwa mujibu wa tuliyoyataja, makundi mengi ya wanavyuoni yalisema kama ifuatavyo:
Al-Ghazali alisema: “Sehemu ya pili: Ni ile iliyotolewa (vuliwa) kwenye kanuni iliyotangulia na inagusia kutolewa kwake kimaana, hali hii huwa inapimwa katika kila suala lililokuwepo baina ya iliyotolewa na iliyotangulia na ilishirikiana na iliyotolewa katika sababu ya utenganishaji, mfano wake ni utenganishaji wa suala la Al-A’raya (maana yake ni kukopesha mtende kwa mwingine ili kula tende zake kwa muda), kwa sababu hakuna kufuta kwa msingi wa riba, lakini utenganishaji ulikuwepo kwa ajili ya haja tu, kwa hivyo, zabibu zinapimwa na tende, kwa sababu zinafanana. [Al-Mustasfa. Uk. 326, Darul Kutub Al-Ilmiyah].
Al-Nawawi alisema kuwa: “Mwandishi alisema kwamba: matajiri hawashiriki katika haja ya kutopima kwani hakuna ushirikiano katika sababu, madhehebu yetu ni kuruhusiwa kwa Upimaji katika ruhusa kama kuna ushirikiano katika sababu”. [Al-MaJu’ 10/349, Al-Moniria].
Vile vile imepokelewa kutoka kwa Wanavyuoni wa medhehebu ya Hanafi na baadhi ya wafuasi wa Al-Mu’tazila kwamba wanazuia Upimaji katika ruhusa. [Rejea: Al-Fusuul Minal Usuul kwa Al-Jassas 4/105, Wizara ya Awqaf ya Kuwait, Taysiir Al-Tahrir kwa Amir Badshah 4/103, Darul Fikr].
Al-Ghazali alisema: “ Vile vile kauli yao kuwa kula maiti ni ruhusa nje ya Upimaji ni mtazamo kosa; kwa sababu inafikiriwa kwamba hakuna Upimaji ila katika dharura tu, kwa sababu si katika maana yake, au mvinyo unapimwa kwa maiti, na anayelazimishwa kwa mwenye dharura. [Al-Mustasfa. Uk. 326, Darul Kutub Al-Ilmiyah].
Hiyo Wanavyuoni wa medhehebu ya Hanafi wenyewe wanakiri kuwa Upimaji ni kama sababu itadhihirika, kama ilivyofahamika kupitia matini zao, Ibn Amir Al-Hajj alisema: “Katika vyanzo vya Fiqhi kwa Imam Abu Bakr Al-Razi: Kama ikisemwa kuwa hairuhusiwi kwenu kuthibitisha adhabu kwa Upimaji, kama Masahaba wakikubaliana kuthibitisha adhabu ya mwenye kunywa pombe kwa Upimaji, basi hali hii huubatilisha msingi wenu wa kuthibitisha adhabu kwa Upimaji. Ilisemwa kuwa inayozuiliwa ni kuanza adhabu kwa Upimaji pasipo na kuwepo kwa matini, ama matumizi ya jitihada katika suala lililotajwa katika matini za Kisheria na maana ya matini hizi inahikikishwa, hali hii inaruhusiwa kwetu, na matumizi ya jitihada kwa Masahaba katika adhabu ya kunywa pombe ni kama hivyo, kwa sababu imethibitishwa kwamba Mtume S.A.W., alipiga katika adhabu ya kunywa pombe kwa viatu na matawi ya mtende. Imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W., kwamba mwenye kuadhibiwa alipigwa na wanaume arobaini kila mmoja wao alimpiga kwa viatu vyake mapigo mawili, kwa hivyo Masahaba wamechunguza amri yake Mtume S.A.W., kupitia jitihada yao, kwa hivyo wamefanya adhabu hii ni viboko themanini, na wamepokea kwamba adhabu hii hutekelezeka kwa viatu na matawi ya mtende au na hata kwa mjeledi, kama anajitahidi mwenye kupiga. Na anaweza pia kuchagua mjeledi ambao unafaa kwa ngozi kwa jitihada yake. [Tahadhari] Kafara katika hali hii huwa sawa sawa na adhabu, lakini inasemekana kuwa inakusudiwa kuwa inayoshughulikiwa kwa mambo yote” [At-Taqriri Wat-Tahbiir fi Sharhil Tahriir 3/241, Darul Kutub Al-Ilmiyah].
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, maoni yaliyo bora kutoka kwa wanavyuoni, inaruhusiwa kuthibitisha ruhusa kwa Upimaji kwa sharti la kujua sababu na kuihakikisha.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas