Hoja ya Makubaliano na Uwezekano Wa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hoja ya Makubaliano na Uwezekano Wake

Question

Imekuwa ikitokea mara kwa mara, baadhi ya watu wanasema kwamba anayedai makubaliano ni mwongo, na kauli hii inahusishwa na Imam Ahmad ibn Hanbal, na kutokana na hivyo wanaona kuwa makubaliano hayo siyo ya msingi, na hayawezi kutokea kabisa, ni yapi maoni ya kweli kati ya hayo yote? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Herufi za Jiim, Miim, na Ain katika lugha ya Kiarabu zina maana ya Kuungana kwa kitu fulani. Na kutokana na herufi hizi, neno la Ijmaa likatungwa, na lina maana ya maandalizi na uamuzi juu ya suala fulani, kama Mwenyezi Mungu Alivyosema: {Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu} [YUNUS: 71]. Vile vile neno la makubaliano lina maana ya kuafikiana. [Rejea: Kidahizo cha "Jamaa" katika: Mujam Maqayiis Al-Lugha kwa Ibn Fares 10/179, Dar Al-Fikr, na Lisaan Al-arab kwa Ibn Mansur 8/75, Dar Sader, na tajil Arusi kwa Zubaidi 20/463, Dar Al-Hidayah].
Na katika istilahi: Ni kuafikiana kwa wenye jitihada wa Umma baada ya kifo cha Mtume Muhammad, S.A.W., katika enzi maalum juu ya amri yeyote. [Sharhu Jam Al-Jawami kwa Jalalud Diin Al-Mahali 2/209, Darul Kutub Al-Ilmiyah].
Na makubaliano yana umuhimu mkubwa katika sheria ya Kiislamu, kwa hivyo Imamu wa Misikiti Miwili Mitakatifu (Imamul Haramain) alisema: “Makubaliano ni ulinzi wa sheria na ni uti wake wa mgongo”. [Al-Burhan kwa Imam Al-Haramain 1/436, Dar Al-Wafaa katika Al-Mansoura].
Makubaliano ni udhibiti wa utambulisho wa dini ya Kiislamu, na huhifadhi kile kilichokubaliwa na Waislamu miongoni mwa misingi ambayo haitofautiani kulingana na wakati na mahali, haja kwake inatokana na haja ya kuondoa uvurugaji wa dini, ugeuzaji wa dhana kwa yakinifu na kwa njia ambayo haikubali majadiliano.
Maana ya hoja ya makubaliano: Ni lazima kwa kila mwislamu kuyatekeleza makubaliano, na kuamini kwamba hukumu inayokubaliwa ni haki isiyoruhusiwa kuvunjwa, wala kujitahidi katika hukumu husika mara nyingine.
Na kuelewa kwa hoja ya makubaliano kunategemea mambo yafuatayo:
Kwanza: Uwezekano wa makubaliano.
Pili: Uwezekano wa kujifunza makubaliano kutoka kwa watu wenye bidii wenyewe kama yakitokea.
Tatu: Uwezekano wa kuhamishia mtu yeyote anaeipinga kwa njia ya kusikia na kusimulia.
Makubaliano yana sehemu mbili: Makubaliano ya kibinafsi, na makubaliano ya kiujumla.
Sehemu ya kwanza: Makubaliano ya kibinafsi:
Nayo ni ya wenye kujitahidi peke yao, na wengi wa maulamaa wa Umma wameona kwamba mambo matatu yanayotajwa hapo juu yanawezekana kuyatekeleza, na kwamba makubaliano ni hoja, wachache wao wamekanusha hoja yake. Wakatoa dalili juu ya hoja ya makubaliano kutoka aya za Qur`ani na Hadithi za Sunnah za Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. Pia wakatoa dalili kutoka akili kwamba dalili ya kiakili inayotegemea kufahamu kwa Qur`ani na Sunnah nzima ina nguvu zaidi kuliko kutoa dalili za kinaganaga, ambayo ni kuwa makubaliano kweli yapo, na ukweli wake ni dalili kubwa ya uwezekano wake, na unaweza kujua, na umuhimu wake ni umuhimu wa kidini.
Makubaliano yanajitokeza kati ya Waislamu wenye jitihada na Waislamu wa kawaida pia, nayo yanaitwa “Makubaliano ya Umma” kama itakavyoelezwa baadaye – kuhusu wajibu wa sala tano kila siku, kufunga Ramadhani, kutoa Zaka, nk. Basi makubaliano yapo tayari katika masuala kama hayo, na hii ni dalili kubwa ya uwezekano wake, vile vile kuyajua, na kupokelewa kwetu ni tayari, hali hii pia inaonesha uwezekano wa makubaliano.
Na kukubaliana juu ya hukumu maalumu kunazifanya hukumu hizi kuwa zenye uhakika, nazo ni miongoni mwa mambo ya kidini yanayofahamika, kwa kweli mambo hayo bado yako hadi siku ya Kiyama, hakuna nafasi ya kusema kwamba matini zilizotajwa kuhusu mambo hayo ndizo zilizotufundisha kuhusu hilo na kudumu kwake; kwa sababu matini hizi ni za kidhana na zinawezekana kufutwa, makubaliano yalikuja na yakakuza udhana na yakakataa uwezekano wa kufuta.
Ikiwa kupatikana -Makubaliano ya umma-, inawezekana kujua na kupokelewa kwetu, basi mambo haya yote yanawezekana pia katika makubaliano ya wenye jitihada -ambao ni makubaliano ya kibinafsi- nayo ni makubaliano ya watu maalumu peke yao kuhusu hukumu ya kisheria, kwa sababu, kama makongamano hayo yakiwezekana kwa watu wa umma wote, nao ni wengi, basi makongamano yanawezekana pia kwa wenye jitihada tu ambao ni wachache. [Rejea: Hakikatul Ijmaa wa Hujjiyatuh kwa Sheikh Abdul Ghani Abdul Khaliq uk. 12].
Wanaokanusha hoja ya makubaliano ya kibinafsi ni makundi mawili maalumu:
Kundi la kwanza: Lilikanusha hoja yake tu. Kundi la pili lilikanusha uwezekano wa mambo matatu pamoja -yaani lilikanusha uwezekanao wa makubaliano, hoja yake na kupokelewa, na lilisema kuwa makubaliano hayawezekani kabisa.
Basi kundi la kwanza lililokanusha hoja ya makubaliano na wala halikukataa uwezekano wake, miongoni mwao ni: Al-Nidham, Shia Imami, Jaafar ibn Harb, Jaafar ibn mubashir kutoka Al-Mu'tazilah, na Khawarij kama alivyotaja Al-Baidhawi. Ibn Al-Hajib alisema: Baadhi ya Khawarij, vivyo hivyo katika kitabu cha "Muslim Al-Thubout " [Rejea: Nihatul Sul kwa Jamalu Dini Al-Isnawi 3/245, Alam Al-Kutub, Sharhul Mukhtasar kwa Al-Adhud 2/319, Darul Kutub Al-Elmiyah, Fawatihul Rahmut Bisharhi Muslim Al-Thubout kwa Abdul Ali Mohammed Al Ansari 2/262, Al-Matbaa Al-Amiriah].
Dhana ya maneno yake ya Abu Jaafar Al-Tusi katika kitabu chake cha: [Iddatul Usuul] kutoka vitabu vya Shia [3/64, Muassasat A’lul Baiyt kwa uchapishaji] kwamba Mashia wanakiri makubaliano wakati wa kuwepo kwa imamu wao, ambapo maimamu wao ni miongoni mwa mwenye jitihada watakubaliana nasi katika wakati wa muda wa maimamu wao Al-Ithna Ashr, na watatupinga baada ya hapo, ambapo kwao Imamu aliyesamehewa alizuiliwa kutokana na kujificha chini, kwa mujibu wa madai yao. Lakini wasio wa Imamu kama Al-Zaidiyah, basi wao wanaunga mkonowanachuoni wa Ummah kuhusu kuthibitisha makubaliano.
Kundi la pili lililosema kuwa makubaliano hayawezekani na lilikana uwezekano wa mambo yaliyotangulia hapo juu nalo ni kundi lisiloainishwa kwa kweli, halikutajwa kwa undani na hawakutajwa wale waliounga mkono madhehebu hii kama Al-Ghazaliy, Al-Amadi, Al-Baidhawi, na Ibn Al-Subki. Ibn Al-Hajib alisema katika kitabu cha: [Al-Mokhtasar]: “Ni serikali na baadhi ya Arrawafidh miongoni mwa Mashia.” [Sharhul Mukhtasr lelladhud maa Hawashih 2/316, Darul Kutub Al-Elmiyah].
Pengine inakusudiwa baadhi ya waliokiuka mipaka miongoni mwa Rawafidh wa Mashia. [Rejea: Al-Ijmaa Inda Al-Usuuliin kwa Dkt. Ali Juma, uk. 33, Daru Rresalah].
Sehemu ya pili: Makubaliano ya Umma:
Nayo ni makubaliano kuhusu mambo ya kidini yanayofahamika, hakuna kukanusha kwa hoja yake, wala katika mambo yanayotegemewa kwa hoja hii, nayo inaitwa “Makubaliano ya Umma” kama ilivyopokelewa kutoka kwa Al-Shafiy R.A., nayo ni makubaliano yaliyokubaliwa na umma kwa ujumla, wakiwemo wenye jitihada na watu wa kawaida.
Waislamu wamekubaliana juu ya kuwepo kwa makubaliano hayo, wenye jitihada wameyafahamu, usahihi wake kuhusu mambo ya kidini yanayofahamika, hivyo kama vile, makubaliano ya wajibu wa sala na zaka, na kwamba ni lazima kusali sala tano kila siku, vivyo hivyo kila jambo la kidini ambalo yeyote atakaye kuwa na wasiwasi au atakayelikataa atakuwa kafiri, hata kama akitegemea makubaliano katika kuthibitisha kwake.
Dalili ya kuwepo kwa makubaliano ya umma, uwezekano wa kuyajua, na uwezekano wa upokezi wake ni kuwepo kwa kitendo ambapo tunakuona wazi katika hukumu nyingi za kisheria, hata katika masuala mengi ya Sheria. Wanavyuoni wa umma wamekubaliana kwamba mwezi wa kufunga ni mwezi wa Ramadhani, kwamba Kaaba ni upande wa Qiblah, na kwamba hairuhusiwi kuoa zaidi ya wanawake wanne, uhalali wa kuuza, kukodisha, uharamu wa Kusengenya, na uvumi, uongo, kushuhudia jambo la uongo, kula nyama ya nguruwe, na kwa kauli moja walikubaliana kuwalazimisha wanawake kuvaa Hijaab, na kulinda akili, kuhifadhi nafsi, kutunza hishima, kulinda dini, kutunza mali, na mambo mengine ambayo hayawezi kuyakiuka kwa hali yoyote.
Kuhusu mambo ya kidini yanayojulikana, si watu wote wanayafahamu kwa usawa, lakini watu wanaweza kutofautiana katika kuyafanya. Hukumu za Ilaa na Dhihaar hazijulikani kwa Waislamu wengi, ingawa hukumu hizi ni miongoni mwa hukumu za kidini zinazojulikana kwa mujibu wa mtazamo wa Wanavyuoni.
Hakika kuna miongoni mwa hukumu zisizojulikana kwa baadhi ya watafiti, kama vile, adhabu kuwaacha wanawake katika Hadithi ya Al-Mukhlifina katika vita vya Tabuk, na Hadithi hii imepokelewa katika Sahihi ya Bukhari na Muslim pia, kwamba hairuhusiwi kwa Imam yeyote baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W, nalo ni jambo maalumu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W, bila ya kupingwa, basi hairuhusiwi kwa mtawala baada yake kutoa dalili kutoka hukumu hii, akiifanya kama aina ya adhabu kwa aliyefanya kosa kama lile.
manufaa ya makubaliano kwa njia hii ni kukanusha kwa udhana wa dalili yenyewe ili dalili iwe thabiti na hairuhusiwi kupinga makubaliano hayo.
Miongoni mwa mifano ya kukanusha makubaliano kwa ajili ya udhana wa dalili, na kuifanya dalili iwe thabiti ni makubaliano ya kwamba kutia udhu ni jambo linalotangulia sala kwa mujibu wa aya hii: {Mnaposimama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu} [AL-MAIDAH: 6], ambapo Wanavyuoni wa umma wamekubaliana kwamba udhu ni kabla ya kusali, na kuwa maana ya aya ni: Kama mkitaka kusali, basi osheni nyuso zenu. Imamu Ar-Raziy alisema katika tafsiri yake [11/153, Darul Fikr]: “Jua kwamba maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mnaposimama kwa ajili ya Sala} yaani wakati mnapotaka kusali.
Vile vile makubaliano ya uharamu wa pombe, inagwa neno la haramu halikutajwa katika Qur'ani, lakini lililotajwa katika aya inayohusu pombe ni neno la: {Basi jiepusheni navyo...} [AL MAIDAH: 90], ambapo bila kupingwa Wanavyuoni wa umma wamekubaliana kuwa pombe ni haramu, kwa hivyo hairuhusiwi kwa yeyote kufahamu kuwa maana ya aya ni kuchukiza pombe kwa sababu Mwenyezi Mungu hakutumia neno la uharamu kwa uwazi. Imamu Al-Qurtubi anasema katika tafsiri yake [8/160, Muasasatu Resalah]: Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi jiepusheni navyo} Anakusudia jiepusheni navyo: Mwenyezi Mungu aliamuru kuepukana na mambo haya. Wanavyuoni wa Kiislamu wamekubaliana kuwa Suratul Maidah imeshuka kwa ajili ya kuharimisha pombe, nayo imeshuka katika Al-Madinah nayo ni miongoni mwa Surah zilizoshuka mwishoni.
Pia uharamu ulitajwa kuhusu wafu, damu na nyama ya nguruwe katika kauli ya Mwenyezi Mungu: {Sema: Sioni} [AL-ANAAM: 145] na aya nyingine zilizotajwa kwa njia ya habari, nyingine kuhusu pombe zilizotajwa kwa njia ya kukataza na kukemea. Njia hii ni miongoni mwa njia zenye nguvu zaidi za kuharimisha. Imepokelewa kutoka kwa Ibn Abbas, alisema kuwa, wakati iliposhuka hukumu ya kuharimisha pombe Masahaba wa Mtume S.A.W wameambiana kuwa: pombe iliharimishwa na ilifanywa sawa na ushirikina. Ina maana ya kwamba: uharimisho wa pombe uliambatana na na kuabudu masanamu, hivyo ni miongoni mwa usharikina, kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu Alisema: {ili mpate kufanikiwa} ili kusisitizia wajibu wa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi”. Imam Al-Shafiy, Abubakar Al-Sayrafiy, Abu Ishaq Al-Shiraziy, Al-Khatib Al-Boghdad, Imamu wa Miskiti miwili Mitakatifu Al-Jouini, Ibn Burhan, Al-Ghazaliy, na Al-Dabbousiy, walisisitizia uthibitisho wa makubaliano ya Umma, na imepokelewa kutoka kwa zaidi ya mmoja kuwa makubaliano ya wale ambao wanasema kuwa makubaliano imethibitika, na miongoni mwao Ar-Raziy ingawa amekiuka hiyo. Ibn Al-Najaar alisema katika kitabu cha [Sharhul Kawkab, uk. 226, Maktabatul Al-Obeikan.]: “Makubaliano ni (hoja thabiti kwa mujibu wa Sheria) yaani: kwa mujibu wa dalili ya Sheria makubaliano ni hoja thabiti. Hii ni madhehebu ya Maimamu wanaojulikana, miongoni mwao ni madhehebu manne, wafuasi wao na wanavyuoni wengine. Al-Amdi Al-Razi alisema: Makubaliano ni hoja ya kidhana na siyo thabiti”.
Imamu Al-Qarafiy alisema katika kitabu cha [Nafais Al-Ussul, 6/2770, Maktabt Nizar Mustafa Al-Baz mjini Makkah Al-Mukaramah]: “Makubaliano ni thabiti, na asili yake ni thabiti, lakini kwa mujibu wa baadhi ya wanavyuoni makubaliano si thabiti”.
Al-Qarafiy pia alijibu wenye kupinga kuhusu makubaliano akisema: “Hakika wanavyuoni wamethibitisha makubaliano kwa mujibu wa aya za Qur`ani na Hadithi, na wamekubaliana kwamba anayekanusha hukumu inayothibitishwa na aya na Hadithi hizi hakuwa kafiri wala wala mwovu kama kukanusha kulikuwa kwa ajili ya tafsiri, kisha wanasema kuwa: hukumu inayooneshwa kwa Makubaliano imethibitika, na asiyeiamini ni kafiri.”
Al-Quraafi alisema akijibu pingamizi hili katika kitabu cha [Nafais Al-Ussul, 6/2583] kuwa: “Makubaliano ni thabiti kwa dalili hizo, siyo kwa kuzingatia dalili hizo peke yake, lakini Usuul Al-Fiqh zote pia ni thabiti, na anayefahamu matini za Kisheria vizuri, hali za Masahaba katika fatwa zao, mijadala yao, kuangalia idadi kubwa za Hadithi zinazohusiana na masuala hayo, katika wakati huu anafahamu uthibitisho wa makubaliano. lakini siyo kutokana na kujua aya moja au Hadithi moja tu, hii ni maana ya maneno ya wanavyuoni kuwa masuala ya Ussul Al-Fiqh ni thabiti, na haiwezekani kuweka mambo yote ya kupata elimu katika kitabu kimoja, kama kwamba tunathibitisha ukarimu wa Hatem Al-Tai’, na ujasiri wa Ali Ibn Abi Talib, kutokana na kusoma visa vyao, kama hatukupata ila kitabu kimoja tu kinachoandikwa visa vingi vyao, basi hatutathibitisha visa hivi. Kwa hivyo wanavyuoni waliweka katika vitabu vya Ussul Al-Fiqh malengo bila ya mwisho kwa ajili ya kuyaonya. Wakati huu kauli yao inaelekea kuwa anayepinga makubaliano atakufuru kwa kukiuka kwake kwa jambo thabiti, na anayepinga jambo ambalo si thabili hatakufuru kwa kukiuka kwake kwa jambo la kidhana. Katika hali hii hakuna kupendelea asili zaidi kuliko tawi, kwa sababu asili ya makubaliano katika uchunguzi ni kiasi cha haya tuliyoyataja hapo juu.
Maneno ya Imamu Ahmad: “Aliyedai makubaliano ni mwongo”, maneno hayo yamepokelewa naye. Ilitajwa katika [Al-Musawadah kwa Aal Taymiyyah. uk. 315, Matbaat Al-Madani]: “Ilitolewa kauli katika upokezi wa Abdullah akisema: aliyedai makubaliano basi alisema uongo, labda watu wanatofautiana, hii ni dai la Bishr Al-Marisi na Al-Asam, lakini anasema: “Hatujui watu wanatofautiana kama hawana taarifa”, ilipokelewa kutoka kwa Ibn Hazm mapokezi yake kwa Abdullah Ibn Ahmed Ibn Hanbal alisema: “Nikasikia baba yangu anasema kuwa: aliyedai makubaliano katika jambo maalum basi alisema uongo, aliyedai makubaliano ni mwongo, pengine watu wanatofautiana, anasema: “Hatujui watu wanatofautiana, hili ni dai la Bishr Al-Marisi na Al-Asam, lakini anasema: Hatujui watu wanatofautiana, wala sikuambiwa hivyo. “[Al-Mahali 10/422, Toleo la Al-Moniriah].
Wanavyuoni wametaja uwezekano kadhaa kwa makusudia ya maneno ya Imam Ahmad:
Miongoni mwao ni: Inawezekana maneno yake yanakanusha asili ya makubaliano, na uwezekano huu umepingwa; kwa sababu ni kinyume na aya na Hadithi ambazo wanavyuoni walizozithibitishia makubaliano, nayo ni moja ya vyanzo vya sheria ambavyo ni mbalimbali kwa mujibu wa wengi wa wanavyuoni, lakini ni lazima kuamini kwamba haiwezikani kupendelea madhehebu ya watu wanaopinga madhehebu ya wanavyuoni wa umma. Imam Ahmad ni miongoni mwa wanavyuoni ambao walithibitisha baadhi ya masuala ya kifiqhi kutokana na makubaliano. Pia wafuasi wa Imam Ahmad vitabu vyao vimejazwa na masharti ya mkataba wao unaothibitisha makubaliano, miongoni mwa hivyo ni: maneno ya Ibn Qudaamah katika kitabu cha “Rawdhit Al-Nadhir” [uk. 138, Chuo Kikuu cha Imam Muhammad Ibn Saud]: “Makubaliano ni hoja thabiti kwa mujibu wa Wanavyuoni wa Umma”. Na maneno ya Ibn Taimiah: Makubaliano yanawezekana nayo ni hoja thabiti” [Al-Muswadah, uk. 315], na kwa maneno ya Ibn kulaham katika “Muhtasari wake” [uk. 74, Chuo Kikuu cha Mfalme Abdul Aziz]: “Nayo ni -yaani makubaliano- - hoja thabiti”.
Vile vile mapokezi ya Ibn Al-Najaar tayari yalitangulia hapo juu yanayothibitisha maana hiyo hiyo. Imepokewa kutoka kwa Imam Ahmad kwamba kutegemea makubaliano katika kuthibitisha hukumu za baadhi ya masuala ya kifiqhi, kwa mfano: kauli ya Mwenyezi Mujngu: {Na isomwapo Qur'ani isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemewa} [AL-AARAF: 204], Ibn Qudamah katika kitabu cha: [Al-Mughni 1/636, Darul Fikr] alisema: “Imam Ahmed alisema katika mapokezi ya iliyopokelewa kutoka kwa Abu Dawood: watu wote walikubaliana kuwa aya hii inahusiana na Sala”.
Miongoni mwa makusudi ya Imam Ahmad pia ni: Uwezekano wa kuwa maneno yake katika haki ya anayetwaa makubaliano ya watu wenye jitihada miongoni mwa watu wa zama zake baada ya upanuzi wa Uislamu na kuenezwa kwa wenye jitihada katika nchi za mbali sana, basi haiwezekani kuyajua makubaliano wala haiwezekani upokezi wake katika hali kama hiyo, uwezekano huu haupinga usahihi wa upokezi wa makubaliano katika vipindi vya awali kabla zama za Imamu Ahmad.
Vile vile miongoni mwa makusudi ya Imam Ahmad ni: Inawezekana kwamba alikusudia kuwa anayetwaa makubaliano yasiyo ya Masahaba, hivyo Imam Ahmad anakusudia kwamba makubaliano yanahusiana na enzi ya Masahaba R.A. tu kama walivyosema wafuasi wa madhehebu ya Ad-Dhahiriyah. Lakini uwezekano huu umejibiwa; kwa sababu dalili zilizotegemewa na wanavyuoni wa Ussul katika kuthibitisha hoja ya makubaliano zilishughulikiwa na watu wa kila zama; zama za Maswahaba, zama za wafuasi nk., basi akaainisha makubaliano katika enzi ya Masahaba tu, na hali hii si sahihi, watu wenye haki wapo katika kila enzi, Si katika enzi ya Maswahaba tu.
Na miongoni mwa makusudi ya Imam Ahmad ni: Kwamba maneno yake yanahusiana na watu wasio na maarifa, au labda alisema hivyo kwa sababu kuna kutokubaliana naye hakukujua, au alisema hivyo katika “Makubaliano ya kunyamaza” kwa hivyo hasemi katika hali hii kwamba Wanavyuoni: “Walikubaliana”, kwa sababu inawezekana kwamba mwenye kunyamaza akawa mpinzani, lakini katika hali hii husemwa kuwa: “Mtu alisema hivyo, na hatujui hata mmoja anayeyapinga hayo”, au labda Imam Ahmad alisema hivyo kwa ajili ya kukanusha kundi la Mut'azila wanaodai kwamba Makubaliano ya watu juu ya yale wanayoyasema, nao walikuwa wanajua maneno machache sana ya Masahaba na ya wafuasi zaidi kuliko wengine, basi labda maneno hayo ya Imam Ahmad yalikuwa yanalenga kuwatenganisha watu kutokana na kudai Makubaliano bila ya hoja na dalili. Na uwezekano wa mwisho huu ulipendelewa na Mwanachuoni Ibn Rajab kama ulivyopokelewa kutoka kwa Al-Mardaawi katika kitabu cha: [At-Tahbiir, 4/1528], kwa hivyo, hairuhusiwi kudai Makubaliano kwa wale wasio Wanavyuoni wa kweli. Vile vile dai la Makubaliano halikubaliwi ila kutoka kwa wenye ujuzi wa kutoa maoni ya wenye jitihada kielimu tu.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, inadhihirika maana ya Makubaliano na Uthibitisho wa hoja yake na sababu za kisheria za kuyategemea Makubaliano. Pia yanadhihirika makosa ya wanaothibitisha ubatili wake na kutokuwepo kwake kupitia maelezo yanayopokelewa kutoka kwa Imam Ahmad Ibn Hanbal, R.A. aliposema kuwa: Anayedai Makubaliano ni mwongo, kama tulivyoelezea katika Fatwa hii na kama tulivyobainisha makusudio ya maneno hayo ya Imamu Ahmad kwa njia isiyopingana na maoni ya Imamu Ahmad mwenyewe kuhusu Makubaliano katika masuala mengi ya Fiqhi ya Kiislam.
Na Mwenye Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas