Kutoka kwenye Makubaliano ya Umma

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutoka kwenye Makubaliano ya Umma

Question

Ni upi mfano wa masuala ambayo baadhi ya makundi ya kigaidi yalikwenda kinyume na Makubaliano ya Umma?

Answer

Kutoka kwenye Makubaliano ya Umma au kufuata maoni ambayo ni kinyume na Makubaliano ya Umma ni sifa mojawapo ya sifa zilizotawala fikra za makundi ya kigaidi kuanzia Al-Khawariji mpaka makundi ya kigaidi ya kisasa, ambao hawatofautiani na Khawariji hata kidogo, hali ambayo Hadithi ya Mtume iliiashiria kwa kuwaeleza watu hawa kuwa wenye kutekeleza ibada nyingi hali ya kuwa wanakwenda katika njia potofu, kutoka kwa Zaidu bin Wahb Al-Jahny kuwa alikuwa katika jeshi la Imamu Ali (R.A.) waliopigana dhidi ya kundi la Khawariji, akasema Imamu Ali (R.A.): "Enyi watu! Hakika nimemsikia Mtume (S.A.W.) akisema: Itatokea kuwa baadhi ya umma wangu watatoka wakiwa wanasoma Qur`ani vizuri zaidi kuliko nyinyi, wanasimamisha Swala na kutekeleza ibada vizuri zaidi kuliko nyinyi, kufunga saumu vizuri zaidi kuliko nyinyi, wanasoma Qur`ani wakidhani kuwa wanafanya mazuri hali ya kuwa wanakwenda kinyume na njia iliyonyooka, Swala zao hazina faida hata kidogo, hakika wanatoka katika dini kama inavyotoka mshale kwa mnyama anayewindwa" Imesimuliwa na Muslim.

Alama za jambo hilo:

Alama za kutoka kwa makundi haya ya kisasa kutoka katika dini ni nyingi ikiwemo; kurejelea maoni na fikra ambazo hazina usahihi kwa Waislamu, ambapo wanategemea kupata elimu kutoka kwa wataalamu maalumu na kutupa elimu na maoni ya wengine, bali kukataa elimu ya wataalamu wanaotofautiana na matamanio yao, na kuelewa maoni yao kimakosa kwa lengo la kuyapatanisha maoni haya na matakwa yao.

Pia, miongoni mwa alama na sifa za makundi hayo, kuwashutumu wataalamu wa dini kuwa ni wataalamu wa mtawala ambao wanatoa maoni yanayoafikiana na matamanio ya serikali hasa wale ambao wanapewa hadhi ya kuwa na mamlaka katika serikali.

Isitoshe, bali miongoni mwa sifa za makundi hayo kuwashutumu watu wa kawaida kuwa wanafuata bida'a na kuwa wanafuata njia potofu kimakusudi, lakini inajulikana kuwa wataalamu wakati wa kuchunguza masuala haya huwa na maoni manane au zaidi, na ni wazi kuwa mfuasi huwa analazimika kwa maoni ya Imamu wake, naye mtoaji Fatwa ana uhuru wa kuchagua miongoni mwa maoni ya watafiti waliotoa jitihada za kufikia hukumu ya suala husika kwa kurekebisha vitendo vya watu, kwa ajili ya kuepukana na kufanya kosa lolote la kisheria kutokana na kanuni na vidhibiti vya kufasiri matini ya sheria, hivyo, kupunguza tabia ya kuwashutumu watu kuwa wanafanya bida'a, kinyume na wanayoyafanya makundi ya kigaidi ya kisasa ambayo yanatumia vurugu na ukatili, kwa kuwa wanategemea vyanzo maalumu na kupuuza vyanzo vilivyotambulika na wanavyuoni wa Waislamu kwa karne nyingi.

Share this:

Related Fatwas