Kutamka kwa Ibara ya (Anayoyataka M...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutamka kwa Ibara ya (Anayoyataka Mwenyezi Mungu Yanakuwa)

Question

Tumezoea hapa katika jamii ya Misri kusikia ibara nyingi za kawaida kupitia mazungumzo kati ya watu, kama vile ibara ya (Anayoyataka Mwenyezi Mungu yanakuwa), lakini kuna baadhi ya ndugu wenye kushikamana na dini wamesema kuwa: Ibara kama hiyo haijuzu kisheria kutamkwa; kwa sababu haisihi kwa upande wa utukufu wa Mwenyezi Mungu kusemewa (Anayotaka). Je, nini ukweli wa jambo hili? Na nini hukumu sahihi ya Sheria? 

Answer

Sifa njema za Mwenyezi Mungu na rehema na amani zimshukie Bwana wetu, Mtume wa Mwenyezi Mungu, Aali na Masahaba zake na waliomfuata, na baada ya hayo;
Kauli inayotajwa si miongoni mwa lugha ya Kiarabu fasihi, bali ni Kiarabu kilichobadilishwa kwa lugha ya mitaani mwa Misri, asili yake ni neno la (Aaiyz au Aawiz) na asili yake katika kiarabu cha fasaha ni kidahizo cha (Awaza), inayomaanisha: Ufakiri na uhitaji. Mtaalamu Ibn Faris katika kamusi ya [maqaaiys Al-Lugha, 4/186, ch. Ya Dar Al-Fikr] anasema: “Ain, Waw, na Zaa ni herufi za neno moja linalomaanisha: hali mbaya , kama vile: (Al-Awaz), maana yake ni binadamu anahitaji kitu chochote, lakini hawezi kukipata”. [Mwisho].
Na Al-Jawhariy katika kamusi ya [As-Sihah, 3/888, ch. Ya dar Al-Ilm Lilmalaiyn] anasema: “(Aawazahu) yaani akihitaji kitu lakini hana; (Ali’waz) yaani ufakiri; (Mu’wiz) yaani fakiri; (Awiza na Awaza) yaani akawa fakiri; na (Aawazahu) yaani anahitaji kitu”. [mwisho].
Katika kamusi ya [Al-Misbah Al-Muniir, na Al-fayyumiy, 2/437, Ch. Al-maktabah Al-Ilimiyah] maneno kama hayo yaliyotangulia.
Kwa muhtasari kuwa: Asili ya lugha ya neno hili (Aaiyz au Aawiz) ina maana ya ufakiri, uhitaji na kutokuweza kupata matakwa, na muundo wa lugha wa neno unamaanisha hali mbaya, kama alivyosema Ibn Faris.
Qur`ani tukufu imesajili kuhusu mayahudi kosa la matusi ya Dhati ya Mwenyezi Mungu na kuwaelezea Mwenyezi Mungu Mtukufu awe na ufakiri na uhitaji, kama walivyomuelezea kuwa na uchoyo na ubahili, Mwenyezi Mungu awalaani, na Yeye amesema: {Mwenyezi Mungu Amekwisha sikia kauli ya wale (Mayahudi) waliosema: “Mwenyezi Mungu ni fakiri, na sisi ni matajiri.” Tumeyaandika haya waliyoyasema, na (tumeandika) kuua kwao Manabii bila ya haki, na tutawaambia (Siku ya Kiyama): “Onjeni adhabu ya kuungua.”}. [AAL IMRAN: 181], Pia Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mayahudi walisema: “Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba; (hatuoni kupata mali kama zamani).” (siyo, bali) mikono yao ndiyo iliyofumba (haifanyi kheri ila kudhulumu na kupokonya); na wamelaaniwa kwa sababu ya yale waliyosema . Lakini mikono yake (Mwenyezi Mungu) iwazi, hutoa apendavyo. Kwa yakini yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako yatawazidisha wengi katika wao (hao Mayahudi) uadui na kufuru}. [AL MAIDAH: 64].
Na wao walisema hivi kwa njia ya kudhihaki, au kwa njia ya kupinga, kukashifu, na kutoa mashaka katika unabii wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W, na huu ni mwenendo wao kwa ajili ya kupunguza ngazi ya mababii, kumwaga damu zao, kutoa mashaka ya misingi ya dini zote, na kuyaingiza mabadiliko ndani yake, kwa ajili ya kupotosha watu, na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu.
Kutokana na Mwenyezi Mungu kuwaahidi adhabu mayahudi hawa kwa adhabu ya kuungua; kwa sababu wao walimueleza Mwenyezi Mungu awe na ufakiri na uhitaji, na Yeye ametakasika na wanayoyasema, ambapo wao hawaitakidi hivi kikweli, lakini walisema hivi kwa njia ya kudhihaki na kukashifu dini; basi tishio hili lina maana ya uharamishaji wa kutamka maneno kama haya au mifano yake, zaidi ya hayo, imekatazwa kutamka maneno yenye uwezo wa kufasiriwa kwa maana mabaya, wakati mayahudi wameyatumia kwa ajili ya kupunguza ngazi ya Mtume S.A.W., kama vile, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amekataza waumini watumie neno la (Raai’naa) ambapo mayahudi walivyolitumia kwa ajili ya kumtukana Mtume S.A.W., na kumdhihaki; kwa sababu neno hili ingekuwa na maana mbili, ama ya (Tuangalie) au (tulete upumbavu), maana ya pili ndiyo mayahudi waliikusudia, kama alivyosema baadhi ya wafasiri wa Qur`ani, Mwenyezi Mungu Mtukufu Alisema: {Enyi mlioamini! Msiseme: “Raai’naa” bali; semeni “Ndhurnaa” ; na sikilizeni (amri). Na makafiri watapata adhabu inayoumiza. [AL BAQARAH: 104], na pia alisema: {Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahali pake, na husema (midomoni mwao): “Tumesikia”; Na (nyoyoni mwao husema): “Tumeasi”. (Na wanasema kumwambia Mtume): “Sikia bila kusikilizwa”; Na (hulitamka tamko la): “Raai’naa”kwa kuzipotoa ndimi zao (hata igeuke maana yake) ili kuitukana dini. Na kama wao wangalisema, “Tumesikia na tumetii. Na usikie na utuangalie” (kwa tamko la Undhurna badala ya tamko la Raai’na), ingalikuwa bora kwao na vizuri zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru zao; basi hawaamini ila kidogo tu}.[AN NISAA: 46].
Imamu An-Nasafiy katika Tafsiri yake [Madarikut-Tanziil Wa Haqaikut-Taa’wiil: 1/362, Ch. Dar Al-Kalim At-Taiyb] anasema: “kauli yake: {Raai’naa}maana yake ama yawezekana kuwa: tutizame tuzungumzie, yaani tuangalie, tungoje, au ina maana ya kutukana, kwani ni neno la Kiibrania au Kisuriania, walikuwa wakitukanana nalo wenyewe kwa wenyewe, kwa maana ya kuidhihaki dini na kumtukana Mtume S.A.W, na wao wanamzungumza kwa maneno yanayotatiza; wananuia kumtukana na kumdharau, lakini wanadhihirisha heshima na utukufu. {kwa kuzipotoa ndimi zao}kwa kugeuza na kubadilisha, yaani wanageuza ndimi zao waweke batili mahali pa haki, waweke (Raai’naa) mahali pa (Undhurna), na (bila ya kusikilizwa) mahali pa (husikii kitu kibaya), au wanageuza ndimi zao kwa kuficha matusi, pamoja na kudhihirisha heshimakiunafiki, {ili kuitukana dini}: ni ndiyo kauli yao: Yeye angalikuwa Nabii kikweli, basi angalitoa habari ya nia yetu”. [Mwisho].
Imamu Ar-Raziy katika Tafsiri yake [3/634] anaeleza mambo mbali mbali yanayoonesha katazo la kulitumia neno hili, akisema: “Wengi wa wafasiri wanaona kuwa Mwenyezi Mungu amekataza kauli ya: {Raai’naa}kwa sababu inamaanisha maana mbaya, kisha Wafasiri walitaja sababu kadhaa.
Kwanza: Mtume S.A.W, anaposoma waislamu kitu cha elimu, walikuwa wakisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Raai’naa, na mayahudi walikuwa na neno la Kiibrania linalotumiwa katika kutukana, na linalofanana na neno hili, nalo ni: (Raai’inaa), maana yake ni (sikia nawe husikii kitu), na waliposikia waumini husema: Raai’naa, waliikopa na kuitumia kwa Nabii, wakamaanisha kutukana, kwa hiyo, waumini walikatazwa kuitumia, na kuamriwa kutumia neno lingine, ni kauli yake: (Undhurna), na dalili ya usahihi wa Taa’wiil hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu katika Suratun-Nisaa: {na husema (midomoni mwao): “Tumesikia”; Na (nyoyoni mwao husema): “Tumeasi”. (Na wanasema kumwambia Mtume): “Sikia bila kusikilizwa”; Na (hulitamka tamko la): “Raai’naa”kwa kuzipotoa ndimi zao (hata igeuke maana yake) ili kuitukana dini}. [AN NISAA: 46].
Na imepokelewa kuwa Saad Ibn Mua’adh amesikia kauli hii namayahudi, akasema: Enyi maadui wa Mwenyezi Mungu, Allah Akulaaneni, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, nikisikia mtu kati yenu husema hivi kwa Mtume, basi nitalipiga shingo lake, wakasema: Je, nanyi hamsemi? Baadaye, Aya hii ikashuka.
Pili: Al-Qutrubiy anasema: “Neno hili lina maana sahihi, lakini watu wa Hijaz hawakulisema isipokuwa katika hali ya kudhihaki, kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu amekataza kulitumiwa .
Tatu: Mayahudi walikuwa wakisema: Rai’inaa, kwa maana ya: Wewe ni mchungaji wa mbuzi zetu, basi Mwenyezi Mungu amelikataza.
Nne: Kauli yake Raai’naa, limechukuliwa na kuangaliana kati ya watu wawili, yaani usawazishi kati ya wanaozungumziana, kama kwamba walisema: tupe sikio lako, ili kukupa masikio yetu, kwa hiyo, Mwenyezi Mungu amewakataza kufanya hivi, kisha akabainisha kuwa hakuna budi kumtukuza Mtume S.A.W, hali ya mazungumzo, na kusema: {Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi}. [AN NUUR: 63].
Tano: Kauli yake Raai’naa ni mazungumzo kwa njia ya utukufu, kama kwamba anasema: angalia maneno yangu, usizembee na usishughlike na kitu kingine, kinyume cha Undhurna, ambapo linamaanisha kumwambia subiri hata wafahamu anavyosema.
Sita: Kauli yake Raai’naa, imechukuliwa na (upumbavu), yaani: umefanya upumbavu, kwa hiyo, walipokusudia maana hizi mbaya, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amekataza kutumiwa neno hili.
Saba: Kauli ya Raai’naa, yaani msiseme kauli yenye upumbavu.
Kwa mujibu wa hayo, neno (Aaiyz) linalobeba maana ya upungufu na ufakiri kwa Mwenyezi Mungu, kutokana na msingi wake wa kilugha; hakika kulitumia katika kuzungumzia Dhati Takatifu ni haramu, na huenda kupelekea ukafiri, tunajikinga kwa Allah, kwa sababu linanasibisha upungufu kwa Dhati Takatifu, na hii inapelekea laana na tishio kali, pia unakadhibisha Aya zote zinazoonesha utajiri wazi wa Mwenyezi Mungu kuliko viumbe vyote, kama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na atakayekanusha (asende, na hali ya kuwa anaweza) basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kuwahitajia walimwengu}. [AAL IMRAN: 97].
Kwa vyovyote, kusemwa kuwa matumizi mengi ya watu wa kawaida na wajinga kwa neno hili, huenda kubadilisha maana yake ya ufakiri, uhitaji, na kuombwa kitu bila ya kuweza kukipata, yawe maana ya kuombwa kitu au kukitaka kitu, kama wanavyofahamu watu wa kawaida siku hizi, hii haijuzu kuinasibisha kwa upande wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani inawezekana, kwa mtazamo wa asili yake, kumaanisha maana isiyolingana na Dhati Takatifu, na kupingana na itikadi za Uislamu kwa uwazi, kama ilivyotajwa hapo juu kukatazwa kulitamka neno la (Raai’naa), kwa sababu ya kuchanganywa maana mbali mbali, na baadhi yake ni mbaya, hakika neno kama (Aaiyz) asili yake ya kilugha inamaanisha uovu na upungufu, kwa hiyo, kukatazwa kwake ni wazi.
Rai inayochaguliwa, kutokana na maenezi ya ujinga, ni kutoa fatwa ya kukatazwa sana kulitamka neno hili, kwa mtazamo wa maenezi ya ujinga wa watu wa kawaida na asili ya maneno ya kiarabu, na kuwazoea kwao kuzitamka ibara kama hizi, na kuzitumia bila ya kujali maana yake ya kiovu, na hii inaonesha kuwa neno hili limebadilishwa katika lahaja ya kiarabu ya Misri liwe na maana isiyo na upungufu, mfano wake neno (mnyama) ambayo asili ya maana yake ni: kila anayetembea ardhini, miongoni mwake ni binadamu, ambapo maana yake imebadilishwa kuwa: kila anayetembea ardhini na wenye miguu minne tu.
Kwa hiyo, kanuni ya kisheria kuhusu maenezi ya mambo ya kutahiniwa ni “Mambo ya kutahiniwa yakienezwa, basi hukumu yake yatarahisishwa”, [Al-Ashbah wan- Nadhaair, na Ibn Nujaym: Uk. 84, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah], na Mtungaji wa [Tahdhiibul- Furuuq Wal Qawqid As_Saniyah Fil Asraar Al-Fiqhiyah: 3/182, Pamoja na: Anwaar Al-Buruuq na Al-Qaraafiy, na Hashiyat Ibn Ash-Shaat, Ch. Alam Al-Kutub]anasema: “Kanuni ya Sheria Nyepesi ni kurahisisha katika maenezi ya mambo ya kutahiniwa, na kukemewa katika yasiyokuwa hayo”. [Mwisho}.
Kwa mujibu wa yaliyotangulia: Haijuzu kisheria kuitamka ibara ya “Anayehitaji mwenyezi Mungu itakuwa” na wala kumwelezea Mwenyezi Mungu maneno kama : (Aaiyz) au (Aawiz), na hasa kwa yule anayejua asili ya maana ya maneno haya, isipokuwa asikusudia, lakini akitumia maneno haya katika muktadha unaoonesha matusi au kupunguza utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi ni haramu kuyatumiwa, na ni lazima kumkataza, kama asipokusudia matusi au bila ya kukusudia, basi matumizi yake ni makuruhi sana.
Inawajibika kwa wanachuoni na walinganiaji na kila aliyejua hukumu ya swala hili, kuwafahamisha watu, kwa njia ya hekima na mawaidha mema, na kuwanasihi yaachwe matumizi ya maneno haya kuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Namna hivi iwe; Na anayevitukuza vitu vitakatifu vya Mwenyezi Mungu, basi (kufanya) hivyo ni kheri yake mwenyewe mbele ya Mola wake}.[AL HAJJ; 30].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas