Upimaji (Qiyaas) Katika Ibada.

Egypt's Dar Al-Ifta

Upimaji (Qiyaas) Katika Ibada.

Question

Wanaozuia kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W., na wanakataa kwamba thawabu za kusoma Qur`ani zinamfikia mfu, wanategemea kwamba amali hizi ni miongoni mwa ibada, na ibada zinahitaji dalili, lakini Upimaji haufai nazo, je, sababu hii ni ya kweli? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Upimaji katika ibada na masuala muhimu ya Fiqhi na misingi ya Kifiqhi, ambayo huathiri mtafiti na masuala anayopambana nayo unahitaji kufikiriwa kwa kina. Wanavyuoni wametofautiana kuhusu msingi wa vyanzo vya hukumu, je msingi huu unasababishwa pasipo na dalili au asili yake ni kusababishwa ila kwa mujibu wa dalili inayouzuia? Hii ni mitazamo miwili iliyopokelewa kutoka kwa Maimamu wawili nao ni Ad-Dabussy na Shamsul Aimah ambao madhehbu yao ni Hanafi walisema: “Kwa mujibu wa madhehebu ya Shafi, asili ya msingi wa vyanzo vya hukumu unaletewa sababu, lakini ni lazima kuwepo kwa dalili wazi kwa ajili ya kuruhusiwa kwa kuuletea sababu” [Taqwiim Al-Adellah kwa Ad-Dabussy uk. 301, Darul Kutub Al-Ilmiyyah, Ussulul Fiqhi kwa Al-Sarkhasi 2/144, Al-Bahrul Muhiit 7/404, Al-Kutubi], Imam Al-Shatwbiy alijaribu kutoa kwetu maelekezo kuhusu suala hili, akasema: “Kila dalili ya Kisheria imethibitika katika Qur`ani pasipo na sharti lolote, basi mambo ya kawaida ambayo yana maana, kama vile haki, upendo, msamaha, kusubiri na kushukuru katika amri zote, udhalimu, uovu, machukizo na kuvunja ahadi katika makatazo yote, yanarejea huko. Na kila dalili imethibitika katika Qur`ani kwa sharti, basi maana ya kiibada inarejea kwake, Mwislamu haongozwi kwa maana hii; kwa sababu hairuhusiwi kufikiri katika asili ya mambo ya ibada au jinsi yake” [Al-Muwafaqaat 3/46, Darul maarifah- Beirut.].
Maana ya kauli ya wanavyuoni kwamba hukumu fulani ni jambo la Ibada yaani haina sabnabu kwa mujibu wa Sheria isipokuwa ni ibada na kutii tu. Pengine hukumu ya Kiibada inahusiana na ibada au mambo yasiyo na ibada katika asili yake, kama katika hali ya kuhakikisha kwamba kijakazi aliyenunuliwa kutoka kwa muuzaji wake katika baraza la mauzo hana mimba na amerudiwa tena kwa sababu ya uvunjikaji wa mkataba kabla ya kuondoka kwa mnunuzi.
Hali ya kutofahamu maana ya hukumu, ina maana ya kuificha hekima ya sheria kwetu tu, na haina maana ya kwamba hukumu hii haina hekima. Mambo yote ya Kiibada -kama anavyosema Al-Qarafiy - yana maana lakini labda hatukuifahamu maana hii, si kwa sababu hayana maana” [Al-Fruuq 2/141, Alam Al-Kutub], pia anasema: “kwa sababu Sheria huhudumu maslahi ya watu katika amri zote, na maovu katika makatazo yote, - kama wanvyosema wafuasi wa Al-Motazilh- basi ni lazima kuamini kuwa amri zote za Kisheria zina maslahi, na makatazo yote yana maovu, kama tukisema kuhusu nyakati za sala: kuwa zinajumuisha maslahi ambayo hatuyajui. Vivyo hivyo kuhusu ibada zote zina maana kwamba zina maslahi ambayo hatuyajui” [Al-Fruuq 2/80].
Maelezo ya mwanavyuoni mmoja kwa ibada fulani kwamba sababu ya hukumu yake ni ya kiibada ni jambo la kijitihada, kwa sababu akili zinatofautiana katika kuweka ibada moja katika sehemu hii au nyingine, hali hii inatokana na mitazamo tofauti, pengine mwanavyuoni mmoja anasoma kitu kisichosomwa na wanavyuoni wengine, au pengine anafahamu sababu na hekima isiyoongozwa na wengine isipokuwa yeye tu. [Rejea: Al-Qiyaas fi Al-Ibadaat, kwa Mandhuur Ilahi uk. 308, Ar-Rashiid]. Na wakati tunaposema kwamba hukumu hii ni ya Kiibada, basi haturuhusiwi kuuliza kuhusu maana yake [Rejea: Hashiyatul Shabramlasi ala Nihaytul Muhtaaj 15/71, Darul Fikr].
Maana ya Upimaji katika ibada ni kuifahamu maana yake na kwamba maana hii ndiyo iliyokusudiwa kwa kuweka hukumu hii, maana ile ile ikafanywa maelezo kamili, ambapo maana ile itakuwa sababu inayotegemewa kwa Upimaji, na kisha kwa kupima na hukumu ya asili inapita kwa suala linalopimwa -pamoja na kukamilisha masharti ya Upimaji-, ambapo hukumu yake haikutajwa katika matini yoyote. Hakuna Upimaji katika ibada na mambo mengine yasiyofahamika maana yake; kwa sababu Upimaji ni sehemu ya kufahamu maan, kwa hivyo, kila ibada ambayo maana yake haifahamiki, basi ni ibada tu wala hairuhusiwi kuipimiwa. Upimaji wa ibada haukukusudiwa kuongeza ibada mpya, au kuthibitisha jinsi maalumu kwa ibada. Hairuhusiwa kuthibitisha ibada mpya kupitia Upimaji, kama vile: kuongeza sala ya sita au Hija nyingine, kwa sababu ibada zote zinafahamika kutokana na dalili wazi siyo kutokana na maoni na jitihada. Kwa hivyo hairuhusiwi kuthibitisha ibada kwa njia ya Upimaji [Nibras Al-Ukuul kwa Sheikh Issa Menon uk. 139, Al-Tadhamun Al-Akhawi].
Wanavyuoni wa madhehebu mbili wametofautiana kuhusu Upimaji katika ibada:
- Wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi wanaona kwamba hairuhusiwi Upimaji katika ibada, Sheikh Al-Asmonda Al-Hanafi anasema: “Wanavyuoni wametofautiana katika kuthibitisha ibada na mambo mwngine kama kafara, na adhabu kupitia Upimaji, Al-Karkhi pamoja na idadi ya wanavyuoni wamekataza hivyo, na mtazamo huu umepokelewa kutoka kwa Al-Karkhi kutoka kwa Abu Hanifa” [kitabu cha Badhlun Nadhar fil Usuul 623, Maktabat darut Turath]. Al-Fakhr Ar-Razi alisimulia mtazamo huu huu kutoka kwa Al-Jubai [Al-Mahsuul 5/348, Ar-Risalah).
- Al-Shafi na wenzake wanasema kuwa inaruhusiwa Upimaji katika mambo yanayokubaliwa kiakili iwapo ni ibada au nyinginezo, na wameharamisha Upimaji katika mambo yasiyokubaliwa kiakili, na matazamo huu ni wa Wanavyuoni wa umma. Vile vile Imam Ar-Razi pamoja na wafuasi wake, na At-Taj As-Sobki walichagua mtazamo huu pia [Rejea: Al-Mahsuul 5/348, Nihayatul Suul kwa Al-Isnawi 1/357, Darul Kutub Al-Ilmiyah, Sharhul Mahali ala Jamu’ Al-Jawami 2/257, Darul Kutub Al-Ilmiyah, Sharhul Kawkab Al-Muniir 4/224, Al-Abeikan], kwa hivyo Wafuasi wa Madhehebu ya Shafiy wanaafikiana na wale wasioruhusu Upimaji wa mambo ya ibada kwamba kila yasiyokubaliwa kimaana hairuhusiwi kupimiwa, kwani sababu yake haijulikani, na kwao miongoni mwa masharti ya Upimaji kwamba jambo linalopimiwa si miongoni mwa mambo ya kiibada, kwa sababu mambo ya ibada hayapimiwi.
Na chanzo cha tofauti ya wanavyuoni juu ya kuruhusiwa kwa kupima katika ibada na kutopima ni kutokana na mambo mawili:
Jambo la kwanza: tofauti yao kuhusu kuwa ibada zote na maana yake inakubaliwa kiakili kwa hivyo, inaruhusiwa Upimaji katika ibada hizi, au kwamba baadhi yao maana yake haikubaliwi kiakili kwa hivyo, utaratibu wa Upimaji hauruhusiwi? Pamoja na makubaliano ya wote –kufuatana na yanayojitokeza kupitia matini zao- kuhusu maana inayokubaliwa kiakili inapimiwa, na maana isiyokubaliwa kiakili hainapimiwi.
Jambo la pili: Nalo ni tawi la jambo la kwanza: Je “Ishara ya matini” ni ya kipimo ili tuseme kuwa: hukumu ni thabiti kwa ishara hii na pia ni thabiti kwa Upimaji, au ishara ya matini ni ya matamshi tu ili tuseme kuwa: hukumu ni thabiti kwa ishara hii lakini si thabiti kwa Upimaji?
Wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi wanaona kwamba ishara ya matini ni: inayothibitishwa kwa maana ya matamshi siyo kwa jitihada wala kwa kutoa maana kutokana na maoni, nayo ni ishara ya matamshi kuhusu uthibitisho wa hukumu iliyotajwa kwa hukumu isiyotajwa, kwa ushirikiano wao katika sababu ya hukumu iliyoweza kufahamika kupitia lugha pasipo na jitihada ya Kisheria, hivyo iwapo hukumu isiyotajwa ni sawa na hukumu iliyotajwa kwa usawa wa sababu au ni muhimu zaidi kwa hukumu kwa unguvu wa sababu yake.
Wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi wanaona kwamba hukumu iliyo thabiti kwa ishara ya matini haikuthibitishwa kwa maneno ya matini tu, vile vile haikuthibitishwa kwa jitihada na kutoa maana kutokana na maoni ili kuthibitishwa kwa Upimaji. Lakini imethibitishwa kwa sababu ya hukumu; hivyo kwani maana iliyofahamika kwa matini ni kama sababu ilyotajwa katika matini za Kiseria, nayo ni ishara inayotegemea maana ya matini na inayofahamika kutokana na lugha yenyewe.
Ama kwa wanavyuoni wa madhehebu ya Shaafi'i na baadhi ya Wanavyuoni wa madhehebu ya Hanbali, wanaona kwamba hukumu ya jambo lisilotajwa katika matini inafahamika kupitia jitihada au Upimaji wa Kisheria, siyo kupitia lugha tu. Upimaji ni maana inayofahamika kutokana na maoni, ili hukumu ifikie suala lisilotajwa katika matini za Kisheria, nayo siyo kutoa maana tu kwa kuzingatia lugha, kwa hivyo wanavyuoni wameshughulika sana kwa kufahamu suala la kutoa maana kutokana na maoni. Kutokana na yaliyotangulia, kwao “ishra ya matini” ni kipimo, kwa hivyo, wakati hukumu za ibada zinapothibitishwa kwa ishara ya matini, zinathibitishwa kwa Upimaji pia.
Wanavyuoni wa umma wamethibitisha kupima kwa ibada kama ikikubaliwa maana yake kiakili kupitia dalili nyingi zikiwemo:
1. Iliyopokelewa kutoka kwa masheikh wawili (Al-Bukhari na Muslim) kutoka kwa Ammar Ibn Yasser R.A., kwamba alisema: Mtume S.A.W., amenituma ili kufanya kitu kwake, nikapata janaba, sikupata maji, nikajisambaragata juu ya udongo kama anavyofanya mnyama, kisha nilikuja Mtume S.A.W., nikamwambia iliyotokea, akasema: “Lakini ilikuwa inatosha kwako kuweka mikono yako tu, kama hivi. Kisha akapiga udongo pigo moja kwa mikono yake, kisha akaufuta mkono wa kulia kwa mkono wa kushoto, na viganja vya mikono yake na uso wake pia”.
ushahidi ni kwamba: Amara alitumia Upimaji katika ibada, ambapo alipima jinsi ya kujisafishia udongo kwa kujisafishia maji, kama kwamba maji yanazama mwili katika kukoga janaba, hivyo ndivyo inapimiwa katika kujisafishia udongo unasambazwa juu ya mwili, na Mtume, S.A.W., hakukataa aliyofanya Ammar kwa kutumia Upimaji katika ibada, lakini alimwambia kuwa Upimaji wake sio sahihi, na makosa katika suala fulani hayamaanishi ubatili wa Upimaji, lakini Upimaji huu umepitishwa na Mtume Muhammad, S.A.W., ambapo hakukana Upimaji katika ibada alipomwona Ammar alipima kwa njia hii, na hali hii inaonyesha kwamba inaruhusiwa kupima katika ibada; Kwa sababu haikubaliki kuchelewesha kwa taarifa wakati wa haja.
2. Inaruhusiwa kuthibitishwa kwa hukumu za ibada kupitia hadithi za Ahaad, na pia inaruhusiwa kuthibitishwa kwa maana ya matini iliyodhahiri, kama dalili hizi zinaweza kuwa na dhana, na kama inaruhusiwa kuthibitishwa kwa hukumu za ibada kwa Hadithi ya Ahaad, vile vile inaruhusiwa kuzithibitishwa kwa Upimaji kwa sababu Hadithi ya Ahaad na Upimaji unategemea dhana tu.
3. Dalili za Upimaji ni za jumla, hali hii inaonyesha kwamba inaruhusiwa Upimaji katika hukumu zote za Kifiqhi, na hazikutofautisha kati yanayohusiana na ibada, au shughuli au nyinginezo, na inategemewa kujua sababu ambayo kwa ajili yake hukumu iliwekewa katika Sheria, wakati tunapojua sababu katika hukumu iliyotajwa katika matini za Sheria, na tunagundua sababu ile ile katika suala lengine linalopimwa, inaruhusiwa kupima pamoja na kukamilika kwa masharti ya Upimaji [Rejea: Al-Bahrul Muhiit kwa Az-Zarkashi 5/129, At-Taqriri Wat-Tahbiir kwa Ibn Amir Haj 1 / 109-110 Darul Kutub Al-Ilmiyyah, Sharhul Mahalli ala Al-Jam’ 2 / 244-245, na Sharhul Kawkab Al-Muniir 3/486].
Wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi wamethibitisha mtazamo wao kuptia vifuatavyo:
1- Ibada zina makadirio amabayo hayakubaliwa kiakili, kama idadi ya sala, idadi za raka, na Zaka. Mambo hayo yote miongoni mwa ibada na hatujui sababu ambayo kwa ajili yake mambo hayo yalianzishwa, kwa hivyo hairuhusiwi kuyapimiwa. Kwa sababu Upimaji unategemea kufahamu maana, na hukumu isiyofahamika sababu yake hairuhusiwi kupimiwa. Al-Asmandi Al-Hanafi anasema: “Dalili inayothibitisha maoni yetu – yanayohusu kutopimwa katika asili za ibada – ni kwamba Upimaji ni uthibitisho wa hukumu kwa mujibu wa dalili inayodhaniwa kuwa inakubaliwa kiakili, na akili haikubali kuongeza sala ya sita, au Zaka ya ngamia ni tano ... basi haiwezikani kuithibitisha kwa Upimaji” (uk. 623).
Suala hili linajibiwa kama ifuatavyo: Hatuwezi kupimia makadirio ya ibada au katika mengineyo ila tunapoijua sababu ambayo kwa ajili yake hukumu ilianzishwa, kama tukijua sababu, na tukipata sababu ile ile katika suala lengine -baadfa ya kukamilisha masharti- tukamilishe mchakato wa Upimaji, lakini kama hatujui sababu, basi hairuhusiwi kupima katika masuala hayo kwa mujibu wa makubaliano ya Wanavyuoni wote, kwa sababu mchakato wa Upimaji umepotea nguzo moja muhimu zaidi kuliko nguzo nyingine, nayo ni sababu.
1. Matumizi ya Upimaji katika ibada inathibitisha ibada mpya, kama vile sala kwa ishara ya nyusi za macho, na mambo kama hayo yanayo na umuhimu wa kupokelewa, kama ikiruhusiwa basi ilikuwa ni lazima kwa Mtume kuayabainisha, na kuyafikishwa kwetu ili yajulikane kwetu, na kwani hali si hivyo, tulijua kwamba Upimaji katika hali hii ni batili.
Suala hili linajibiwa kama ifuatavyo: hali ya kutofikisha haiashirii kutoruhusiwa, vile vile upinzani weno unajibiwa kwa uwajibu wa sala ya Witri kwenu; ambapo sala ya Witri ni wajibu kwenu wakati ambapo haijuliwi kwa yakini hukumu hii [Nibras Al-Ukuul kwa Sheikh Issa Menon Uk. 140].
2. Viwango ni sawa, basi havionekani katika akili kutofautisha kati ya kiwango na kingine.
Suala hili linajibiwa kama ifuatavyo: hatupimi ila ikidhihirika tofauti, kama hakuna tofauti, basi hakuna kupendelea, na hakuna Upimaji, kama Abu Hanifa alivyosema katika makadirio ya kufuta kichwa kwa vidole vitatu kupimiana na kufuta juu ya vyatu vya ngozi (Khuf).
3. Ibada zilianzishwa kwa manufaa ya watu na Mweneyzi Mungu anayajua manufaa haya, nazo ibada ni haki ya Mwenyezi Mungu, kama idadi ya sala na idadi ya rakat na viwango vya Zaka, kwa kuwa hatuwezi kutambua wala hatujui maslahi ambayo zilianzishwa kwa ajili yake ibada, na hakuna njia kwa ajili ya kupima ujuzi wa maslahi na haki za Mwenyezi Mungu, basi hairuhusiwi kupimiwa ibada hizi.
Suala hili linajibiwa kama ifuatavyo: maneno yanu haya kuhusu kukataa kwa Upimaji katika suala la ibada inaongoza kwa kubatilisha matumizi ya Upimaji katika hukumu zote za kisheria, na kwamba hukumu zote zinategemea maslahi ambayo hakuna yeyote anayajua isipokuwa Mwenyezi Mungu tu, basi maoni hayo yamebatilika na yamejibiwa katika majibu yetu yalaiyoelekezwa kwa wenye kukanusha Upimaji katika hukumu zote [Rejea: Sharhul Mahalli ala Al-Jam’ 2/245].
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu, kusababisha maoni ya mwenye kusema kwamba hairuhusiwi kupima katika ibada kwani ibada inategemea matini za Qur`ani na Sunnah, kwa hivyo, na matini hizi hazina maoni, mtazomo huu ni dhaifu kwa sababu kutegemea matini za Qur`ani na Sunnah hakuhusiani na ibada peke yake, lakini zinategemewa katika hukumu zote za Kisheria kama vile ibada, Fiqhi ya Muamala (kutendeana), mambo yanayohusu ndoa, na nyinginezo, kwa hivyo, hali ya kuthibitisha kwamba hakuna Upimaji katika ibada kwani ibada zinategemea matini za Qur`ani na sunnah ni mtazamo dhaifu, na lazima katika kila suala kufikiriwa kuwa ni linalokubaliwa kiakili au la, kwa hiyo ni lazima kufikiri katika kila suala pekee yake, na ukusanyaji wa dalili za Kisheria zinazohusu suala hili, kufikiria masuala yanayofanana nayo, na kufahamu maana yake, sababu zake, na hekima zake.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, inaruhusiwa kupima katika ibada na mambo mengine yanayokubaliwa kiakili, kukamilisha mchakato wa Upimaji, nguzo zake na masharti yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas