Maana ya Hadithi ya"Enyi Waja wake ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya Hadithi ya"Enyi Waja wake Mwenyezi Mungu Mtukufu Niokoeni".

Question

Ni ipi Maana ya Hadithi ya: "Enyi Waja wake Mwenyezi Mungu Mtukufu Niokoeni"? Na nini Usahihi wake na kuifanyia kwake kazi kwa kuitegemea? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Imamu Atwabaraniy alipokea katika kitabu chake cha: [Al Mu'jam Al Kabeer]; akasema: Al Husein Bin Ishaq alitusimulia At Tasaturiy, na Ahmad Bin Yahyia As Swfiy, na Abdulrahman Bin Sahl akasema: baba yangu alinisimulia kutoka na Abdullahi Bin Issa, kutoka kwa Zaid Bin Aliy, kutoka kwa Autbah Bin Ghazawan, kutoka kwa Mtume S.A.W., kwamba anasema: "Iwapo mmoja wenu atapoteza kitu na akahitaji msaada akiwa katika ardhi isiyo kuwa na watu basi na aseme: Enyi waja wake Mwenyezi Mungu Mtukufu niokoeni, Enyi waja wake Mwenyezi Mungu Mtukufu nisaidieni, kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ana waja tusiowaona". Atwabaraniy akasema: "Na yeye akaijaribu hiyo Hadithi" [Al Mu'jam Al Kabeer kwa Atwbaraniy 117/17, Ch. Maktabat Ibn Taimiah].
Al Haithamiu akasema katika kitabu cha: [Majma' Azawaid na Manba' Al Fawaid] katika kitabu cha: [Al Adhkaar]; "Imepokelewa na Atwabaraniy na watu wake wanaamini uwepo wa udhaifu kwa baadhi yake! Sio kwamba Zaid bin Ali hakumfikia Autbah"
Na Ina dalili katika Hadithi ya Ibn Abas, ilipokelewa na Al Bzar katika Musnad wake, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ana malaika wake ardhini ambao si chochote isipokuwa Walinzi wanaandika kila jani la mti linalodondoka, na yoyote miongo mwenu atakaepotea jangwani basi aite; Nisaidieni enyi waja wa Mwenyezi Mungu". Na akasema: "Maneno hayo hatujui kama yalipokelewa kutoka Mtume S.A.W, kwa lafudhi hiyo ila kwa tamko hilo na kwa Isnadi hiyo" [Musnad Al Bazar 181/11, Ch. Makatabat Al Eluum Wa Al Hekam]. Al Haithamiy akasema: "Al Bazar akaipokea na watu wake ni waaminifu" [Majma' Az Zawaid kwa Al Haithamiy 132/10, Maktabat Al Qudsiy]
Na Al Baihaqiy aliisimulia katika kitabu cha: [Shua'b Al Imaan] kwa tamko hilo hilo: " Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ana malaika wake ardhini ambao si chochote isipokuwa Walinzi na wanaandika kila jani la mti linalodondoka, na yoyote miongo mwenu atakaepotea ardhini na hana uwezo wa kuwapata wasaidizi basi na atoe sauti kubwa huku akisema: Enyi waja wake Mwenyezi Mungu Mtukufu niokoeni nisaidieni na Mola wenu atakurehemuni. Basi ni kweli, Mtu huyo atasaidiwa"
Na katika tamko lingine: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ana malaika wake ardhini ambao wanaitwa Walinzi wanaandika kila jani la mti linalodondoka, Basi yoyote miongoni mwenu atakaepatwa na hali ya kupotea au akahitaji kitu anapokuwa katika ardhi isiyokuwa na watu basi na aseme: "Tusaidieni Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola akurehemuni, basi hakika atasaidiwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu." Na Ibn Shaibah aliipokea Hadithi hii katika kitabu cha: [Al Musanaf].
Na Ina dalili nyingine kutoka katika Hadithi ya Abdullahi Bin Masu'od iliyopokelewa na Atwabaraniy, na Abu Ya'liy katika Musnadi wake, na Ibn As Suniy katika kitabu cha: [Amalu Al Yaum wa Al Lailah], kutoka kwa abu Ya'liy, na Ibn Hajar Al Asqalaniy katika kitabu cha: {Al Matwaleb Al Aliyah], na An Nawawiy aliitaja katika kitabu cha: [Al Adhkaar] kutoka kwa Ibn As Suniy, kutoka katika Hadithi ya Ibn Masu'od alisema: Mtume S.A.W. anasema: "Kama mnyama wa mmoja wenu atamponyoka katika ardhi isiyokaliwa na watu, basi na aseme hivi: Enyi waja wake Mwenyezi Mungu Mtukufu mfungeni mnyama huyo kwa ajili yangu kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu yupo na atamzuia mnyama huyo kwa ajili yenu."
Ibn Alaan Al Swadiqiy alisema katika kitabu cha: [Sharhu El Adhkaar]: "Al Hafedh Bin Hajar anasema: "Hadithi hiyo ni yenye Isnadi Nzuri, ni ngeni sana, ilitolewa na Al Bazar na akasema: hatujui kama ilipokelwa kutoka kwa Mtume S.A.W, kwa tamko hilo, isipokuwa upande huo na Isnadi hiyo. [Sharhu Ibn Alan Al Swadiqiy juu ya Al Adhkaar An Nawawiyah 151/5, Ch. Dar Ehyaa At Turath Al Arabiy].
Na Asakhawiy alisema kwamba ni Nzuri pia katika kitabu cha: [Al Ibtahaj Badhkaaru Al Musafer Al Haj], Na Al Haithamiya akasema: "Watu wake ni waaminifu" [Majma' Azawai'd wa Manba'u Al Fawaid 132/10]. Na hiyo ni Nzuri (Hasan) kwa sababu ya njia zake kadhaa na kuzitegemea, kama alivyotaja Ibn Alaan katika maelezo yake kwa Adhkaar An Nawawiy.
Na Hadithi hii inamaanisha kuwa mtu anapoponyokwa na mnyama wake katika sehemu isiyokuwa na watu, au akipoteza kitu, au akapotea njia, au chochote mfano wa hivyo, hakika mambo yalivyo ataisoma dua hii aliyotufundisha Mtume S.A.W, atasaidiwa na waja wake Mwenyezi Mungu, wawe ni Binadamu au Majini, au hata Malaika, na watamfunga mnyama huyo na kumsimamisha, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Al Haafedh Abdullah Bin Alswadiq Al Ghemariy alisema: "Kwa hiyo katika Hadithi hii kuna kujuzu uombaji wa kuokolewa na viumbe na kutaka msaada wao, na kufanya hivyo haiwi kwa dharura yeyote isipokuwa kwa uwezo wake alonao, na unaoendana naye.
Ama kwa upande wa uokoaji na msaada usio na mipaka, hivyo vinamuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala haviombwi isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na jambo hili katika Dini linajulikana hivyo kama lilivyo hivyo hivyo." [Ar Radu Al Muhkam Al Matin Ala Kitabu Al Qawl Al Mubin Uk. 41, Ch. Maktabatu-l Ahd Aj Jadidah].
Na Imamu Nawawiy alipokea katika kitabu cha: [Al Adhkar] Hadithi hiyo kutoka kwa Ibn As Suniy kisha akasema: "Nikasema: wamenisimulia mimi baadhi ya Mashekhe zetu wakubwa katika Elimu, ya kwamba mtu mmoja alitorokwa na mnyama wake na ninadhani kuwa mnyama huyo ni nyumbu, na alikuwa anaijua Hadithi hii, na akaisoma: na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamfunga mnyama huyo kwa ajili yake papo hapo. Nami siku moja nilikuwa na jamaa, mnyama akawaponyoka nao wakashindwa kumkamata, mimi nikaisoma hiyo Hadithi, basi huyo mnyama akasimama hapo hapo bila ya sababu yeyote isipokuwa maneno hayo (niliyoyasema)." [Al Adhkar kwa An Nawawiy Uk. 224, Ch. Dar Al Fikr]
Na Abdullahi Bin Ahmad alipokea kutoka kwa baba yake Imamu Ahmad Bin Hambal rehema ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake akasema: "Nilihiji Hija tano, nikapotea njia, na nilikuwa nikitembea nikawa ninasema: Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, nielekezeni njia. Na sikuacha kusema hivyo hadi nikajikuta nimesimama njiani." [Masae'l Al Imama Ahmad kwa simulizi ya mwana wa Abdullah Uk. 245, Ch. Al Maktab Al Islamiy].
Na Syutwiy aliipokea Hadithi hiyo katika kitabu cha: [Aj Jame' Aswaghir], na Al Menawiy aliielezea na akasema: "Na iwapo mnyama wa mmoja wenu atatoroka na kukimbia (katika ardhi kame) kwa maana kuwa ardhi hiyo haina maji ndani yake, lakini kinachokusudiwa hapa ni ile ambayo haina wakazi ndani yake kama inavyofahamishwa na riwaya, ni ile ambayo haikaliwi (basi na aite) kwa sauti ya juu kwa kusema: (enyi waja wa Mwenyezi Mungu nifungieni mnyama wangu) kwa maana kuwa mzuieni asikimbie. (Hakika Mwenyezi Mungu ana viumbe vyake ardhini) kwa maana ya alivyoviumba na miongoni mwavyo ni mwanadamu, au jinni, au mfalme, hapotei (atamfunga kwa ajili yenu), kwa maana ya mnyama aliyewaponyoka, na iwapo atayasema hayo kwa nia ya kweli na mwelekeo kamili, basi atajipatia anachokitaka kwa msaada wa Mfalme Mtoaji. [At Taiseir kwa Sharhu Aj Jame' As Swaghir 82/1, Ch. Maktabatu Al Imam Ashafiy]
Na kutokana na hayo maelezo yaliyotangulia Hakika Hadithi iliyotajwa ina hukumu ya Hassan kwa vithibitisho vyake, na inafidisha kujuzu kutaka msaada na kuomba kuokolewa na viumbe katika yale wanayoyaweza katika kukidhi mahitaji yao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas