Ishara ya Bubu kwa Qur`ani

Egypt's Dar Al-Ifta

Ishara ya Bubu kwa Qur`ani

Question

Je, ishara ya bubu kwa Qur`ani inafanana na kutamka kwa ulimi kuhusu ibada na kuharamisha kusoma Qur`ani kwa mwenye hedhi na mwenye janaba? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Wanachuoni wamekubali pamoja kuwa: kusoma Qur`ani kwa kawaida ni kwa kutikisa ulimi, na kuisoma kwa macho na moyo ni aina ya kuzingatia na tafakuri, na si kusoma. Wafuasi wa madhehebu ya Malik, na Al-Karkhiy mfuasi wa madhehebu ya Hanafiy, na Ibn Taimiyyah mfuasi wa madhehebu ya Hanbal walihusisha kutikisa ulimi, hata asipojisililiza, lakini wafuasi wa madhehebu ya Malik wanasema: ni bora zaidi ajisikilize, kisha wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy, Shafiy, na Hanbal waliongeza kuwa: lazima ajisikilize; kwa sababu kutikisa tu kwa ulimi hakuhesabiwi kusoma bila ya sauti, kwa kuwa maneno ndiyo yanayosikilizwa na kufahamiwa.
Al-Halabiy mfuasi wa madhehebu ya Hanafiy anasema: “Kusoma ni kutamka herufi kwa ulimi wake ambapo anajisikiliza, na kama alitamka herufi bila ya kujisikiliza, basi huku si kusoma, kutokana na maoni ya Al-Hindawaniy na Al-Fudhaliy. Na inasemekana kuwa: akitamka herufi basi ni sawa hata asipojisikiliza, kwa maoni ya Al-Karkhiy, na katika kitabu cha Al-Muhiit: kauli ya Mashekhe wawili ni bora zaidi, na katika Al-Kafiy, Imamu Shams Al-Aimmah Al-Halawaniy anasema: haitoshi asipojisikia pamoja na aliye karibu naye”. [Mwisho], [Ghuniyatul-Mutamaliy Sharh Muniyatul-Musalliy: Uk. 136, Ch. Ya Dar Saadaat].
Al-Arabiy Al-azhariy Al-Malikiy anasema: “Kusoma ni kwa kutikisa ulimi, na haitoshi kwa moyo, na inatosha kujisikiliza, na pia pasipo kujisikiliza, hii inatosha kutekeleza wajibu”. [Jawahir Al-Ikliil Sharh Mukhtasar Khalil: 1/47, Ch. Ya Dar Al-Fikr].
Bubu anayekosea kutamka, halazimiki kuutikisa ulimi wake, hata akiwa na uwezo huu, na wafuasi wa madhehebu ya Malik na Hanball, na pia Hanafiy walisema: Bubu halazimiki kuutikisa ulimi wake, na kwenye sala, anainuia kwa moyo wake tu, kwani kuutikisa ulimi wake ni bure, na hakuna dalili ya kisheria.
Al-Haskafiy Al-Hanafiy mtungaji wa [Ad-Durul-Mukhtar] anasema: “(Halazimiki mwenye kasoro ya kutamka) kama vile bubu (kuutikisa ulimi wake) na pia katika kusoma, na hii ni sawa, kwa kutokuwepo wajibu na dalili”. [Ad-Durul-mukhtar: 1/324, Ch. Ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy).
Al-Bahutiy Al-Hanbaliy anasema: “Bubu na mwenye kukatika ulimi anainuia ihramu kwa moyo wake, kwa sababu ya kasoro ya ulimi wake, na hatikisi ulimi, na hapa yeye ni mfano wa yule ambaye halazimiki kusimama, basi halazimiki kutekeleza, hata akiwa na uwezo wa kufanya, kwani ni bure kwake, na hakuna dalili ya kisheria, na huu ni mfano wa kutumia kiungo cho chote, kwa hiyo inalazimika mwenye uwezo wa kufanya hivi. Na hukumu hii inahusu pia kusoma, tasbihi, na nyininezo kama vile, tahmidi, tasmii, tashahudi, na salamu, hizi zote bubu anazifanya kwa moyo wake, na hatikisi ulimi wake, kwa ilivyotangulia”. [Kashful-Qinaa’: 1/331, Ch. Ya Dar Alfikr].
Al-Hatwab Al-Malikiy anasema: “Ibn Arafah anasema: nia inatosha kwa bubu [Mwisho], na Ibn Nagiy anasema: hakuna tofauti katika suala hili”. [Mawahib Al-Jaliil Sharh Mukhtasar Khalil: 1/519, Ch. Ya Dar Al-Fikr].
Bubu anapoashiria kwa madhumuni ya kusoma, basi ishara hii ni kama kutamka, kwa sababu inabainisha muradi wake mfano wa kutamka. Imamu Az-Zarkashiy anasema: “sababu yake kuwa ishara ina maana, na wenye kutamka ibada yao inaambatana na kutamka, na kwa sababu ya kasoro ya bubu ya kutamka, ishara yake inatekeleza maana ya kutamka kisheria”. [Al-manthuur Fil-Qawi’d: 1/164, Ch. Ya Wizara ya Waqfu na mambo ya kiislamu, Kuwait].
Al-Jassas Al-Hanafiy anasema: “Kauli yake mwenyezi Mungu: {na akawaashiria} (kwani keshakuwa hawezi kusema). [MARYAM; 11], ishara hapa inatekeleza maana ya kauli, kwa sababu inamaanisha muradi wake, na hii ni dalili kuwa ishara ya bubu imekubalika na inatekeleza maana ya kauli. Na wanachuoni hawakutofautiana kuwa ishara ya aliye mzima haimaanishi muradi wake, na ishara ya bubu ipo, kwa sababu mazoea, matumizi, na mahitaji hupelekea kuwa ishara ya bubu ni mfano wa kutamka, lakini mtu mzima hana mazoea ya kudumu hata kuweza kuyategemea. Kwa hiyo, wanachuoni wanasema: mtu aliye mzima akipata kasoro katika ulimi wake, kisha akatumia ishara inayoonesha wasia n.k., basi haitegemewi, kwa sababu hana mazoea ya kudumu yanayomfanya kama bubu”. [Ahkaam Al-Quraan na Al-Jassas: 3/321, Ch. Ya Dar Al-Fikr].
Al-Izz Ibn Abdislaam anasema: “Ishara ya wazi ya bubu ni mfano wa kauli ya wazi, ambapo imefahamiwa na wote, kama kwamba akiulizwa: talaka ngapi umemtaliki mkeo? Akaashiri kwa vidole vitatu, au dirham ngapi umezichukua? Akaashiria kwa vidole vitano kwa mfano”. [Qawai’d Al-Ahkaam Fi Masalih Al-Anaam; 2/135, Ch. Ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Ibn Muflih Al-Hanbaliy anasema: “Ishara wazi ya bubu ni maneno”. [Al-Furuu’ na Ibn Muflih: 2/127, Ch. Ya Aalam Al-Kutub].
Na Ibn Nujaim Al-Hanafiy katika Al-Bahr Ar-Raaiq anasema: “Al-Hafidh An-Nasafiy, Mungu amrehemu, anasema: Ishara ya bubu na kuandika kwake ni kama maneno, kwa sababu ishara ni mfano wa maneno ikiwa wazi, na kama hivi ilivyo, basi bubu analazimika na hukumu kwa kutumia ishara na kuandika, hata itekelezwe kwa ndoa, talaka, kumpa mtumwa uhuru, kuuza, kununua, na nyinginezo miongoni mwa hukumu, kwa sababu ishara ni kueleza kutoka kwa mwenye uwezo wa kutamka, hasa kwa upande wa mwenye kasoro yake, na pia mtume S.A.W, aliainisha muda wa mwezi kwa ishara, akisema: “Mwezi ni hivi, akaashiria kwa kidole chake”. [Sharh Kanz Ad-Daqaaiq: 2/54, Ch. Ya Dar Al-kitaab Al-Islamiy].
Kauli zote zilizotangulia zinaonesha kuwa ishara ya bubu ya wazi ni kama maneno, na kama hivi iwavyo, basi wafuasi wa madhehebu ya Malik na ya Shafiy waliongeza kuwa: bubu akiashiria wakati akifanya sala, basi sala yake ni batili.
Al-Hatwab anasema: “Ibn Al-Arabiy anasema: suala limetokea baghdad kuhusu bubu aliyeashiria katika sala yake, na baadhi ya wanachuoni walisema: sala yake ni batili, kwani ishara ya bubu ni kama maneno yake”. [mawahibul-Jalil na Al-Hatwab: 2/32, Ch. Ya Dar Al-Fikr].
Wanachuoni waliongeza pia kuwa uharamu wa ishara ya Qur`ani kwa mwenye janaba na mwenye hedhi, na Sheikh wa Uislamu Zakariya Al-Ansariy anasema: “Inajuzu kwa mwenye janaba kusoma Qur`ani kwa moyo, na kutazama msahafuni, na kusoma Aya zilizofutwa, na kutikisa ulimi, na kunong’oneza bila ya kujisikiliza, kwani hayo yote si kusoma kwa Qur`ani, kinyume cha ishara ya bubu”. [Asnal-Matalib Sharh Raudatut-Talib; 1/67, Ch. Ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy].
As-Siyutiy katika kitabu cha: [Al_Ashbah wan-Nadhair] anasema: “Al-Ianawiy anasema: ishara ya bubu ya kusoma, akiwa na janaba, ni mfano wa kutamka, aliieleza Kadhi Hussein katika fatwa zake’. [Al-Ashbah wan-Nadhair: Uk. 314, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Inaharamisha kusoma Qur`ani kwa mwenye janaba na mwenye hedhi katika kauli ya wengi wa wanachuoni. Na Al-Jalal Al-Mahaliy katika kitabu cha: [Sharhul-minhaj na An-Nawawiy] alitaja: miongoni mwa vitu haramu kwa mwenye janaba ni kusoma Qur`ani, akasema: “inaharamishwa kusoma Qur`ani kwa mwenye janaba, hata ikiwa sehemu ya Aya, kwa Hadithi ya At-Tirmidhiy na wengineo: “mwenye janaba na mwenye hedhi hawasomi kitu cho chote cha Qur`ani”, kwa maana ya kukanusha na kukataza pamoja, na ilitajwa katika Sharh Al-Muhadhab: inajuzu kwa madhumuni ya kumtaja mwenyezi Mungu, bila ya kukusudia Qur`ani, kama vile kusema kwake kwenye kupanda kipando: {Ametukuka Mwenyezi Mungu aliyemfanya huyu atutumikie na tusingaliweza kutenda haya wenyewe}, au kwenye msiba: {Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea (atatupa jaza yake)}, kama akikusudia Qur`ani peke yake, au pamoja na Kumtaja Mungu, basi ni haramu”. [Sharh Al-muhalla Ala Al-Minhaj Bihashiyat Qalyubi Wa A’mirah: 1/74, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Qalyubi katika [Hashiya yake kwa Sharh Al-Muhalla] anasema: “Ishara ya bubu ni kama kutamka, Sheikh wetu aliianisha kwa ulimi wake, na hii si mbali, lakini rai ya kwanza inafaa na kauli yao: ishara ya bubu ni kama kutamka, isipokuwa mambo matatu; shahada, kuvunja kiapo, na kuvunja sala”. [Hashiyata Qalyubi wa A’mirah: 1/74, Ch. ya Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah].
Katika kitabu cha: [Qurrat Uyun Al-Akhyar Takmilat Hashiyat Ibn A’bidin]: “Ishara ya bubu ni kama maneno yake katika kila kitu, kama vile; kuuza, ajira, hiba, rehani, ndoa, talaka, kumpa mtumwa uhuru, msamaha, kukiri, na kisasi, kwa rai sahihi, isipokuwa adhabu, hata adhabu ya kusingizia zinaa, na shahada. Ni ishara yake inatekelezwa, hata akiwa na uwezo wa kuandika, kwa rai sahihi, Katika kitabu cha [Al-Ashbah]: amefupisha kwa kusema isipokuwa adhabu, na katika kitabu cha At-Tahdhib ameongeza: shahada yake pia haikubaliki, na kuhusu yamini yake katika madai, tumeibainisha, na ni dhahiri kuwa wanachuoni wamevua adhabu tu, kwa sababu ya usahihi wa uislamu wake kwa kutumia ishara, lakini sioni rai hii kwa uwazi. Na kama bubu akiashiria kusoma hali ya kuwa mwenye janaba, ni bora kuharamishwa, kwa kauli yao; bubu anawajibika kuutikisa ulimi wake, ambapo wanahesabia kutikisa ni kusoma. Na talaka ya bubu inayoambatana na sharti itekelezwe kwa ishara yake, na kwa kuwepo sharti, na mfano wake mtu mzima akawa bubu kisha akaashiria, talaka itekelezwe”. [2/82, Ch. ya Dar ihiyaa At-Turath Al-Arabiy].
Hakuna tofauti kati ya mwenye janaba, mwenye hedhi, na na mwanamke baada ya kuzaa, na hii ni madhehebu ya wengi wa wanachuoni, na wafuasi wa madhehebu ya Hanbal wajuzisha kusoma sehemu ya Aya; kwani haihesabiwi Qur`ani, na Az-Zailai’y Al-hanafiy anasema: wenye hedhi wakatazwe kusoma Qur`ani, na mfano wake janaba; kwa kauli yake Mtume S.A.W: “Mwenye hedhi na mwenye janaba hawasomi kitu cho chote cha Qur`ani”. [waeipokelea At-tirmidhiy, Ahmad, na Al-Baihaqiy, kutoka kwa Abdillhi ibn umar. [Tabiyn Al-Haqaiq sharh Kanz Ad-Daqaiq: 1/57, Ch. ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy].
Imamu An-Nawawiy Ashafiy anasema katika kitabu cha [Al-Majmuu’]: “Madhehebu yetu kuwa inaharamishwa kwa mwenye janaba na mwenye hedhi kusoma kitu chochote katika Qur`ani, ama kwa chache au kwa wingi, hata sehemu ya Aya”. [Al-Majmuu’ Sharh Al-Muhadhab; 2/182, Ch. ya Al-Muniriyah].
Al-Bahutiy Al-Hanbaliy anasema: “Mwenye kuwajibika kuoshwa kwa janaba anakatazwa kusoma Aya moja au zaidi, kwa Hadithi ya Aly: “Mtume S.A.W, alikuwa hakatazwi, au haepushwi kwa Qur`ani kitu chochote, isipokuwa janaba”. [wameipokea Ibn Khuzaimah, Al-Hakim, na Ad-dara Qutniy, na walisema ni sahihi, na mwenye kuwajibika kuoshwa kwa janaba hakatazwi kusoma sehemu ya Aya, kwani haihesabiwi Qur`ani, na inajuzu kusoma zile zinazohesabiwa kumtaja Mungu, ambapo hakukusudia Qur`ani, kama vile: Basmalah, na shukrani zote za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote, Aya za toba, na kupanda kipando, lakini akikusudia kusoma basi ni haramu”. [Daqaiq Ulin-Nuha Sharh Al-Muntaha: 1/81, Ch. ya Alam Al-Kutub].
Wafuasi wa madhehebu ya Malik walijuzisha kusoma Qur`ani kwa mwenye hedhi, na kuharamishwa kwa mwenye janaba, Sheikh Ad-Dardir katika kitabu cha: [Asharh Al-kabiir] anasema: “(Janaba inaepusha vitu), vya sababu (ndogo), ambavyo vilitangulia katika kauli yake: sababu ndogo inakataza sala, tawafu, na kugusa msahafu, na inazidisha kukataza kusoma kwa kuutikisa ulimi isipokuwa mwenye hedhi, kama itakuja”. [1/138, Ch. ya dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy].
Kisha akasema baada ya hayo: “Ilikataza, yaani hedhi (kugusa Msahafu), (na haikataza kusoma) Qur`ani, hata akiwa na janaba kabla yake, na hiyo hiyo baada ya kukatwa, isipokuwa awe na janaba kabla yake, basi haijuzu, kwa mtazamo wa janaba, pamoja na uwezo wa kuiondoa”. [Asharh Al-Kabiir: 1/174, Ch. ya dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah].
Kwa hiyo: ishara ya bubu ni kama kutamka kwake katika ibada, na inaharamishwa kwake kuashiria kwa Qur`ani hali ya kuwa na janaba, na inaharamishwa kwa mwanamke bubu kuashiria kwa Qur`ani hali ya kuwa na hedhi, kwa maoni ya wengi wa wanachuoni, na inajuzu kwa rai ya wafuasi wa madhehebu ya Malik.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas