Upatanisho Baina ya Madhehebu ya K...

Egypt's Dar Al-Ifta

Upatanisho Baina ya Madhehebu ya Kifiqhi

Question

Tulisikia kwamba hairuhusiwi kupatanisha baina ya madhehebu ya kifiqhi, inakusudiwa nini kutoka neno la upatanisho? nini hukumu ya kufanya hiyo? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu.
Neno la Al-Talfiiq (upatanisho) lina maana kadhaa katika lugha, miongoni mwao ni: ungana wa vitu ili kuwa kitu kimoja, inasemekana: alishona mavazi, hivyo kwa kuunga sehemu ya mavazi kwa sehemu nyingine na kuzishona. Inasemekana kuwa watu wamepatanishwa. [Rejea: Al-Misbah Al-Muniir kwa Al-Faiyumi, kidahizo cha Lafaqa, na Tajul Arus kwa Az-Zubaidi kidahizo cha Lafaqa].
Kwa mujibu wa Wanavyuoni wa misingi ya Fiqhi, Al-Talfiiq ni miongoni mwa istilahi zilizojitokeza karibuni baada ya utulivu wa madhehebu za kifiqhi na kuzienea hukumu zake katika nchi na mikoa, lakini istilahi iliyojitokeza na inafanana na “Al-Talfiiq” ni istilahi “kufuatilia ruhusa” yaani kutafuta maoni ya kifiqhi yaliyo rahisi zaidi katika kila madhehebu na kuyatekeleza kwa ajili ya kurahisisha kalifisho za kishria, pamoja na kupuuzwa kwa matokeo ya mambo na kiwangu cha kufaa kwa makusudi ya Sheria na uwezo wa kuyatekeleza mambo hayo au la.
Upande wa kufanana kati ya kufuatilia ruhusa na kupatanisha ni kwamba istilahi hizi zote zinafuata na kuchagua kwa baadhi ya masuala ya kifiqhi kutoka madhehebu mbalimbali, lakini tofauti kati ya istilahi hizi mbili ni kwamba kufuatilia ruhusa huwa katika masuala mbalimbali ambayo hayaundwi ibada moja, kama vile aliyechukua ruhusa ya madhehebu ya Hanafi katika kutawadha, na ruhusa ya madhehbu ya Shafii kuhusu talaka, ruhusa ya madhehbu ya Malik kuhusu mauzo kwa sababu ruhusa hizi zina urahisi; lakini kupatanisha kutakuwa katika sehemu ambazo zinajumuisha suala moja, na hali hii inatokana nayo hukumu moja ambayo hakusemwa na mwenye jitihada yeyote, hivyo kama aliyefuata madhehebu ya Hanafi katika kuruhusiwa kwa kuacha utaratibu wa vitendo vya udhu, na kuigwa kwa madhehebu ya Shafiy katika kuruhusiwa kwa kufuta chini ya robo ya kichwa tu. Ingawa utaratibu wa vitendo vya udhu ni suala moja na kufuta kichwa ni suala lenigine, lakini yote ni sehemu moja inayojumuisha suala moja kubwa nalo ni: Je, udhu kufuatana na jinsi hii ya kupatanisha kati ya maoni hayo ni kweli au la?
Kupatanisha katika istilahi ni: mchanganyiko kati ya mitazamo ya madhehebu tofauti za kifiqhi katika sehemu za hukumu moja kwa jinsi isiyosemwa na madhehebu yoyote. [Rejea: Al-Talfiiq wa hukmuh fi Al-Fiqh Al-Isalmi kwa Dkt. Abdullah Ibn Mohammed Ibn Hassan Saidi, uk. 12, pasipo na toleo, na Omdatu Ltahqiiq fii Al-Taqliid wal Talfiiq kwa Mohamed Said Al-Bani uk. 91, Al-Maktab Al-Islami – Dameski].
Kwa mujibu wa saiklopidia ya kifiqhi [13/293, istilahi: kupatanisha]: “Maana ya kupatanisha kati ya mitazamo ya madhehebu ni kufuata ukweli wa tendo moja kutoka madhehebu mbili pamoja baada ya kutoa hukumu ya ubatili wake kwa kila mmoja wao”. Kwa hiyo, ukweli wa kupatanisha ni kutekeleza mitazamo ya madhehebu zaidi ya moja katika wakati mmoja na katika suala moja ili inatokana na hali hii hukumu moja ambayo haikusemwa na yeyote miongoni mwao, lakini baadhi ya wanavyuoni hao wakasema baadhi ya maelezo kuhusu suala hili na wengine walisema maelezo mengine kuhusu suala ile ile.
Baadhi ya wanaoandika kuhusu suala la upatanisho wanaamini kuwa upatanisho ni kufuata kwa madhehebu nyingi katika masuala mbalimbali ambayo hayajumuishi katika suala moja, kama vile kufuata kwa madhehebu ya Imamu Malik katika hukumu za ibada, kwa mfano, na kufuata kwa madhehebu ya Imamu Ahmad Ibn Hanbal katika miamala, lakini usahihi ni kufuata kwa zaidi ya madhehebu moja katika masuala ya kujitegemea, hali hii haiitwi upatanisho; kwa sababu mtazamo ulio ni sahihi zaidi ni kwamba watu wa kawaida hawapaswi kufuata madhehebu fulani katika masuala yote, lakini madhehebu ya mtu ya kawaida ni madhehebu ya Mufti wake, na hapaswi kufuata Mufti mmoja, lakini inaweza kufuata zaidi ya Mufti moja, kama Mufti huyo anafuata madhehebu ya Maliki au Shafi’i au mengineyo, kisha inaruhusiwa kwa aombaye fatwa kufuata fatwa anayopendelea wakati wa kutokubaliana kwa mamufti, kama ilivyokuwa katika enzi ya Masahaba wakarimu bila ya kukanusha, hata kama mtu wa kawaida alijilazimisha kufuata madhehebu fulani kisha akafuata madhehebu nyingine katika suala au jambo fulani bila ya kusababisha kwa hukumu maalumu ambayo haikutajwa na yeyote miongoni mwa Wanavyuoni, basi hali hii haiitwi upatanisho, lakini inasemekana aligeuka kutoka madhehebu yake kwa madhehebu nyingine katika baadhi ya masuala, lakini kama ikisababisha hukumu maalumu ambayo haikutajwa na yeyote miongoni mwa Wanavyuoni, basi huu ni upatanisho.
Hivyo, kama akichanganya kati ya kufuata kwa madhehebu ya Imamu Shafiy katika suala la udhu na alifuta baadhi ya nywele kichwani tu, tena akafuta madhehebu ya Imamu Abu Hanifa katika usahihi wa sala kwa udhu hii bila kumtuliza au heshima katika matendo yake, basi akajumuisha kati ya madhehebu ya Shafiy katika mlango wa udhu na kati ya kufuata kwa madhehbu ya Hanafiy katika mlango wa sala, lakini hali hii imesababisha hukumu maalumu ambayo hakuna yeyote anayesema kwa uhalali wake miongoni mwa Wanavyuoni wa madhehbu hayo mawili, kwa sababu ya kutotulia katika sala hii; na Wanavyuoni wanasema kuwa sala hii ni batili kwa sababu ya kutopata usafi kwa kufuta baadhi ya nywele kichwani ambazo ni chini ya robo ya kichwa. Upatanisho unagawanywa kwa mujibu wa kuwepo au kutokwepo kwa makusudi kwa aina mbili; aina ya kwanza ni upatanisho unaotokea kwa makusudi, kama wanaofuata madhehebu, kufahamu mitazamo, kisha anajumuisha kati ya mitazamo hii kwa makusudi. Aina ya pili ni upatanisho unaotokea bila ya makusudi, kama hali ya watu wa kawaida wanapoomba fatwa kutoka mamufti wengi, kisha wanajumuisha majibu hayo katika jibu moja tu.
Vile vile upatanisho unagawanywa kwa mujibu wa hukumu kwa aina mbili; aina ya kwanza ni upatanisho kati ya hukumu mbili lakini katika sula moja, kama aliyejumuisha katika usahihi wa udhu yake kati ya kufuata kwa madhehbu ya Shaafi'i kuhusu kutovunjika kwa udhu kwa hali ya kuwa na kinyesi au mkojo, tena kufuata kwa madhehebu ya Hanafi kuhusu kutovunjika kwa udhu kwa kugusa wanawake, hali hii ni ujumuisho kati ya hukumu mbili katika suala moja, nalo ni usahihi wa udhu.
Na aina ya pili ni upatanisho kati ya hukumu zaidi ya moja katika suala zaidi ya moja, kama aliyejumuisha katika usahihi was ala yake kati ya kufuata kwa madhehebu ya Shaafi'i katika kufuta kwa baadhi ya nywele kichwani, na kati ya kufuata kwa madhehbu ya Hanafi katika usahihi wa sala pasipo na utulivu, hali hii ni upatanisho kati ya hukumu mbili na katika masuala mawili, nayo ni udhu na sala.
Pia upatanisho unagawanywa kwa mujibu wa wakati katika aina mbili; aina ya kwanza ni upatanisho ulio kabla ya kutokea tendo, kwa lengo la kuchukua hatua kwa kutenda tendo hili. Na aina ya pili ni upatanisho ulio baada ya tendo, kwa lengo la kutafuta tatuo ili kurekebisha kosa lisilokusudiwa, na kurekebisha tendo baada ya kulitendwa kwa ajili ya kuepuka aibu na shida.
Hakuna matini wazi kuhusu hukumu ya upatanisho iliyotokana na Wanavyuoni wa Fiqhi waliotangulia na wenye jitihada miongoni mwa madhehbu ya kifiqhi yanayofutwa, lakini mitazamo inayohusiana na isitlahi hii (upatanisho) ilidhihirika hivi karibuni tu. Wanavyuoni waliokuja baadaye walitofuatiana kuhusu hukumu ya upatanisho, wengi wao walisema kuwa upatanisho hauruhusiwi kabisa, na baadhi yao walisema kuwa upatanisho unaruhusiwa kwa masharti tu, na rai hii ndiyo iliyochaguliwa, na masharti hayo yataelezwa baadaye. Dalili ya rai iliyochaguliwa:
Kwanza: upatanisho umetungwa kwa ajili ya kurahisisha kwa wenye kalifisho, na tofauti ya maimamu wa jitihada ni huruma kwa watu, Mwenyezi Mungu alisema: {Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini.} [AL-HAJJ: 78], Kwa hiyo, si lazima kwa mtu kufuata madhehebu maalumu katika masuala yote, kama walivyosema wengi wa wanavyuoni, lakini inaruhusiwa kutafuta madhehebu yoyote miongoni mwa madhehbu ya maimamu yaliyofuatwa katika kila suala, hii ni ruhusa kwa mtu ambaye hakufikia kiwango cha bidii, hakuna tofauti katika suala hili kati ya kufuata kwa zaidi ya madhehebu moja katika masuala mbalimbali, na kufuata kwa madhehebu zaidi ya moja katika sehemu za suala moja na masharti yake na udhibiti wake. Masuala mengi ya kifiqhi za yanategemea dhana. Na si sahihi kuwa rai mtu yeyote mwenye jitihada ni rai iliyo sahihi na haiwezekani kuwa kosa, bali inawezekana kuwa sahihi katika baadhi ya pande zake na ni kosa katika baadhi nyingine, na hakuna tofauti katika hali hii kati ya suala moja na masuala mbalimbali, na kufuata baadhi ya mitazamo ya mwenye jitihada katika suala moja, na baadhi ya mitazamo ya mwenye jitihada mwengine katika suala hilo hilo si kutofuata kwa madhehebu zote hizi mbili, bali ni kama kujumuisha kati ya mitazamo hii katika zaidi ya suala moja, na kulingana na hii inaruhusiwa kwa mwenye kufuata kupatanisha kati ya mitazamo katika suala moja, kama katika ibada au katika miamala.
Pili: inaruhusiwa kwa Mufti kutoa fatwa kutoka madhehebu nyingine, kutokana na maendeleo ya enzi, jamii na uwiano tofauti ya faida na hasara kulingana na tofauti ya nyakati na maeneo, watu na hali, kushikamana na rai moja hata kama rai nyingine inafaa zaidi na ukweli, basi hali hii si sahihi kwa mujibu wa Fiqhi, kwa hiyo, masuala ya Fiqhi yanategemea dhana kama ilivyotajwa hapo juu ili maoni yawe mbalimbali na kwa ajili ya kuwarehemu watu; na kama inaruhusiwa kwa Mufti kutoa fatwa kutoka madhehebu nyingine kulingana na makusudi ya sheria na mabadiliko ya hali, basi ni hakuna tofauti kati ya kuacha maneno ya imamu wake katika kila suala na kutoa fatwa kwa maoni ya imamu mwingine, na kati ya kuacha maoni ya imamu wake katika baadhi ya masharti ya suala na udhibiti wake na kufuata maoni ya imam mwingine.
Tatu: haikupokelewa kutoka kwa Masahaba wakarimu au wafuasi katika idadi kubwa ya madhehebu na tofuati yao kwamba hakuna yeyote alimwambia aliyemwuliza kuwa: ni lazima juu yako kufuata hukumu za madhehebu yako, ili usipatanishe katika ibada yako kati ya madhehebu mbili au zaidi, na kama upatanisho ni marufuku, hawakuonya nao.
Nne: kusema kuwa kutoruhusiwa kwa upatanisho kunapelekea hukumu ya ufisadi wa ibada za watu wa kawaida, ni nadra kupata mtu wa kawaida anajilazimishia kufuata madhehebu maalumu katika ibada zake zote na miamala yake yote, na kulazimisha watu wa kawaida kwa hali hii ina aibu na ugumu, matatizo ya watu wa kawaida yameenea kwa kusema usahihi wa ibada zao zianzopatanishwa na zisizo sahihi kama zikilinganishwa na na kigezo na masharti ya madhehebu moja tu.
Tano: kusema kwa kutoruhusiwa kwa upatanisho ni kinyume na urahisi wa Sheria na upana wake, jambo fulani linaweza kuwa jipya katika suala au linafutiwa na athari mpya, hivyo jitihada za Wanavyuoni wa Fiqhi wa kale na kufuata kwa idadi fulani ya maoni ambayo hayakuhitaji kushikamana na maoni haya hasa, lakini inawezekana kuwa suluhisho bora kwa Mufti ili kukabiliana na maendeleo ya suala ni kufuata zaidi ya madhehebu moja na anajumuisha katika masharti yao na udhabiti wao kinachofanya fatwa yake sambamba na makusudi ya sheria na hali, si katika upatanisho huu kusema kwa ubatili katika kila madhehebu kutokana na ukosefu wa baadhi ya masharti yanayohusiana na kila madhehebu, kila mwenye jitihada miongoni mwa waliotangulia atapata baadhi ya masharti na hatapata baadhi mengine katika suala lililopatanishwa, lakini hii haihitaji ubatili wake wakati wote, lakini inahitaji ubatili wake katika haki ya anayefuata peke yake hakujumuisha pamoja na rai yake rai ya mwenye jitihada mwingine, hivyo madhehebu ya Imamu Shafiy, kwa mfano, inahitajika kuwepo kwa mashahidi ili mkataba wa ndoa uwe sahihi kinyume na madhehebu ya Imam Malik, na katika wakati ule ule, madhehebu ya Imamu Shafiy haikusema kwamba anayefuata madhehebu ya Imamu Malik katika ndoa bila ya kuwepo mashahidi, ndoa yake ni batili, na pia madhehebu ya Imamu Malik haikusema ubatili wa ndoa ya aliyefuata madhehebu ya Imamu Shafiy kuhusu kutohitajika kwa mahari.
Sita: maneno ya wenye jitihada kwa anayefuata kuwa ni kama matini za Sheria na dalili zake kwa mwenye jitihada, na hapa upatanisho kati ya maoni ya weney jitihada unafanana na upatanisho kati ya dalili za hukumu zinazopingana, na kama maoni ya wenye jitihada yanawezekana kuwa makosa na sahihi, labda kuchanganya zaidi ya maoni moja kuwa karibu na sahihi.
Kuna masharti kadhaa kama yakipotezwa hakuna upatanisho, nayo ni kama ifuatayo:
Sharti la Kwanza: inahitajika kufuata upatanisho kati ya mitazamo, lakini hairuhusiwi tu kwa ajili ya kuchezea au matamanio au kukwepa kalifisho au kupenda kuonekana na madai ya upya wa fiqhi, kwa sababu kuna kupuuzwa kwa maoni ya Wanavyuoni wetu yanayowakilisha utajiri wa kisayansi na uhuru wa mawazo ambao ni fahari kwa taifa la Kiislam kwa zaidi ya karne.
Sharti la Pili: upatanisho kati ya mitazamo hakusababishi utoaji hukumu kinyume na makubaliano au kinyume na matini thabiti, kama aliyefuata Imamu Shafiy katika kusema kwamba mvinyo na pombe, ni sawa katika hukumu, kisha akafuata Imamu Abu Hanifa katika kusema kuwa mvinyo ni halali, akapatanisha kati ya mitazamo hii mbili, akatoa hukumu kuwa pombe ni halali, kwa sababu mvinyo ni halali kwa Abu Hanifa, na mvinyo na pombe ni sawa katika hukumu kwa Shafiy, basi upatanisho huu ni batili na kinyume na makubaliano na matini za wazi na thabiti zinazoharimisha pombe.
Sharti la Tatu: upatanisho kati ya mitazamo hauwi kinyume na makusudi ya sheria na tabia yake, kama aliyepatanisha kati ya mitazamo katika mkataba wa ndoa na ameoa bila ya mashahidi akifuata madhehbu ya Imamu Malik kwani Imamu hyuu hakuweka sharti hili, vile vile amefuata madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, ambapo akaoa pasipo na walii, na alifuata madhehbu ya Imamu Shafiy, ambapo alioa bila ya kulipa mahari, basi upatanisho huu ni kinyume na makusudi ya sheria kwa sababu ya unapelekea maovu kama kuwashutumu mume na mke, na kupoteza kwa haki ya mwanawake, na kurahisisha uzinzi na kudanganya kwa upatanisho huu kwa ajili ya kuizuia shutuma kwa waliofanya zina.
Sharti la Nne: kutochukua upatanisho kama sababu ya kuvunja hukumu iliyo thabiti akitekeleza madhehebu fulani, ikilinganishwa na kauli yake: “Jitihada haivunjiki kwa jitihada nyingine”, basi katika nafasi ya kwanza jitihada haivunjiki kwa upatanisho, kama yule aliyefuata madhehebu ya Imamu Abu Hanifa katika suala la ndoa bila ya walii, kisha akataliki mke mara tatu, basi ni haramu kwake kumwoa mke yule mpaka kuolewa na mume mwingine, lakini alitaka kumuoa tena akafuata madhehbu ya Imamu Shafiy kuhusu suala la ndoa bila ya walii ni batili, na kwa hiyo talaka haipo kwenye ndoa ya ubatili, basi inaruhusiwa kwake kumuoa. Upatanisho huu kati ya madhehebu mbili si sahihi na unapingana, kana kwamba yule mwenye kupatanisha anataka kusema kuwa: wakati nilipomwoa bila ya walii, ndoa hii siyo uzinzi kwa mujibu wa madhehbu ya Imamu Abu Hanifa, na siyo ndoa sahihi kwa mujibu wa madhehbu ya Imamu Shafiy, na talaka hizi hazizingatiwi kwa sababu ndoa haikuwa sahihi kwa mujibu wa madhehbu ya Imamu Shafiy, lakini upatanusho huu ni batili, kwani Imamu Shafiy kama akiweka sharti ya kuwepo kwa walii, lakini hakusema kwa ubatili wa ndoa ya anayefuata madhehbu ya Imamu Abu Hanifa, hakusema kuwa hakuna talaka katika hali hii, kwani “Jitihada haivunjiki kwa jitihada nyingine”.
Sharti la Tano: upatanisho kati ya mitazamo hakusababishi kuvunjika kwa hukumu za mahakama; kwa sababu uamuzi wa jaji huondoa migogoro kuizuia machafuko, pia kama akipatanisha kati ya mitazamo kinyume nayo hali hii inasababisha kuondoa machafuko na kukosekana kwa utulivu wa maamuzi ya mahakama.
Sahrti la Sita: kuamini kuwa hukumu iliyopatanishwa ni bora zaidi, anakadiri kuwa, kama mmoja wa maimamu amechunguza suala kwa mabadiliko yake mapya au mabadiliko yanayohusiana na mtu yule aliyefuata kauli hii, basi inawezekana madhehebu yake inakubaliana na mtazamo aliyeufikia kupitia upatanisho huu, lakini ni lazima hii ni dhana yake, kwani kauli za mwenye jitihada kwake kama matini za Sheria kwa mwenye jitihada, hivyo upatanisho wake unazingatiwa kwani kuna dalili thabiti na yenye nguvu zaidi. Wataalamu wengi wamesema kuwa inaruhusiwa kupatanisha kati ya mitazamo:
Miongoni mwa Wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa: Al-Amir Badshah aliyejadili kwa maelezo yake yaliyosemwa na Al-Quraafiy kuhusu kuruhusiwa kwa kufuata mtu wa kawaida kwa mwenye jitihada mwengine sio imamu wake ili kutosababisha kile kinachomzuia, kama aliyefuata madhehebu ya Imamu Shafiy kuhusu kutolazimisha kwa kusinga na akafuata madhehebu ya Imamu Malik katika kutovunjika kwa udhu akigusia mwanamke bila ya matamanio kisha akasali kwa udhu huu huu, sala yake si sahihi kwa mujibu wa yaliyotajwa na Al-Quraafiy, lakini Amir Badshah alisema katika kutoa maoni juu ya hilo: “Alipinga hilo kwamba ubatili wa hali hii iliyotajwa nao si sahihi, kwa mfano, Imamu Malik hakusema kuwa aliyefuata madhehebu ya Imamu Shafiy katika kutolipa mahari kuwa ndoa yake ni batili, wala Imamu Shafiy hakusema kwamba aliyefuata madhehebu ya Imamu Malik katika kutokwepo kwa mashahidi kuwa ndoa yake ni batili. Alitaja kuwa kutosema kwa ubatili wa aliyefuata mmoja wao na kazingatia madhahebu yake katika mambo yaliyotegemewa na usahihi wa kazi na hali tuliyo nayo, na kutosema kwa ubatili wa hali hii hailazimishi kutosema kwa hivyo, na pengine inajibiwa kuwa: tofauti kati yao si tu kwamba kila mmoja wa wenye jitihada hapati katika mfumo wa upatanisho mashati yote ya usahihi wake, lakini anapata baadhi ya masharti hayo tu, tofauti hii hatusemi kuwa inalazimisha hukumu kwa ubatili, na namna gani kusema hivyo na ukiukaji katika baadhi ya masharti ni mdogo zaidi kuliko ukiukaji katika masharti yote, basi ni lazima kuhukumu kwa usahihi wake katika hali iliyo mdogo kwa njia ya kwanza, na anayedai kuwa kuna tofauti au au kuna dalili nyingine ya ubatili wa hali ya upatanisho kinyume na hali ya kwanza, basi juu yake alete dalili, kama ukisema kuwa ukiukaji katika baadhi ya masharti ni mdogo zaidi kuliko ukiukaji katika masharti yote; kwa sababu ukiukaji katika masharti yote hufuata mwenye jitihada moja tu katika kila kinachotegemewa na usahihi wa kazi na katika hali hii hakufuata mmoja tu, nitasema kuwa hali hii ni sawa kama unayo dalili kutoka matini au makubaliano au kipimo chenye nguvu inayoonyesha kuwa kazi kama ina masharti ni lazima kwa mtu kufuata mwenye jitihada moja tu katika hali zote. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi”. [Taisiir Al-Tahriir 4/371, Darul Fikr].
Miongoni mwa Wanavyuoni wa madhehbu ya Imamu Abu HAnifa pia: ni Imamu Al-Tarsusi, na Sheikh Al-Islam Abu Al-Saud, Ibn Abidin katika Al-Uqood Al-Durriya katika kitabu cha: [Tanqiih Al-Fatawa Al-Haamidiyah 1/109, Darul Maarifa], alisema: “Katika fatwa za Al-Shalabi kuhusu kufanya majengo ni waqf bila ya ardhi ni sahihi na hukumu yake ni sahihi lakini waqf juu ya mtu mwenyewe ni matata kwa upande kwamba waqf juu ya mtu kwa mwenyewe imeruhusishwa na Abu Yusuf na haikuruhusishwa na Muhammad, na waqf ya majengo bila ya ardhi ni kama waqf ya vitu vinavyoweza kuhamishika na Abu Yusuf hakusema hivyo, lakini Muhammad anakubali hiyo, sasa hukumu imetungwa kwa madhehebu mbili, nayo hairuhusiwi, lakini Al-Tarsusi alisema kuwa katika Moniat Al-Mufti ina maana kuwa hukumu inayochanganywa kutoka madhehbu mbili inaruhusiwa, kutokana na hivyo hukumu ya waqf juu ya mtu mwenyewe inapitishwa nchini Misri katika wakati nyingi, kwa hukumu hii majaji waliotangulia wamehukumu, na labda wametunga hukumu hii kama tulivyotaja kuhusu kuruhusiwa kwa hukumu iliyochanganywa kutoka madhehbu mbili. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.”
Pia nasema: pengine suala hili linaelekezwa kuwa si kutoka hukumu iliyopatanishwa ambayo imepokelewa kutoka kwa Mwanavyuoni Qassem kuwa ni batili kwa makubaliano ya Wanavyuoni wote, kwa sababu maana ya ubatili wa hukumu hii kama ikitokana na madhehbu tofauti kama ikihukumiwa kwa usahihi wa ndoa fulani bila ya kuwepo kwa walii kufuatana na madhehebu ya Imamu Abu Hanifa na bila ya mashahidi kulingana na madhehebu ya Imamu Malik, kinyume na ikipatanishwa kutoka maneno ya wafuasi wa madhehebu moja, basi hukumu hii haipingani na iliyotajwa katika madhehebu ile ile, maneno ya Abu Yusuf na Muhammad na wengine yanategemea misingi ya Abu Hanifa au ni maneno yaliyopokelewa kutoka kwake yeye, lakini yamehusishwa kwao siyo kwake yeye, kwa sababu wamefahamu maneno hayo kutoka misingi ya Abu Hanifa au kwa sababu wameyachagua kama nilivyoeleza hivyo katika dibaji ya kitabu changu juu [Durar Al-Mukhtar], na yaliyotajwa katika Durar kutoka Kitabu cha Al-Qadhaa wakati mtunzi wake aliposema: hukumu katika suala fulani lililojitahidiwa kinyume na maoni yake kwa kusahau madhehebu yake au kwa makusudi kwa Abu Hanifa ni sawa, katika suala hili kuna maoni mawili ambapo alisema: Maana ya kinyume na maoni ni kinyume na asili ya madhehebu kama mfuasi wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa akihukumia madhehebu ya Imamu Shafiy n.k. au kinyume chake. Lakini kama mfuasi wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa akihukumu kufuatana na Abu Yusuf au Muhammad au wengine miongoni mwa wenzake Imamu Abu Hanifa, basi hukumu yake sio kinyume na maoni yake."
Ali Haider katika kitabu cha: [Durar Al-Ahkaam Sharhu Mijalatul Ahkaam 4/674, Darul Jiil, Toleo la Kwanza]: “Katika hali hii, imekuwa upatanisho katika hukumu hizi zilizotolewa dhidi ya mtu ambaye hayupo zina maana ya kwamba utoaji wa hukumu dhidi ya mtu ambaye hayupo naye ni adui anayejificha ni maoni ya Imam Shafiy, na kutoa hukumu bila ya kuapa ni kufuatana na madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, hivyo swali linaulizwa kuhusu hukumu hizi linajibiwa kwa kutoruhusiwa kwa upatanisho, hakika asili na msingi ni kutoruhusiwa kwa hukumu dhidi ya mtu ambaye hayupo, na kama haiwezekani kuletwa kwa adui yaani kuletwa kwa nguvu mahakamani, hii inasababisha kupoteza kwa haki ya mdai basi ni lazima kuhukumu dhidi ya mtu ambaye hayupo ili kuepuka aibu, dharura, na kuhifadhi haki kutoka kupoteza . Jawahir Zadah alitoa fatwa kuhusu kuruhusiwa kwa kuhukumu dhidi ya adui ambaye hayupo na aliyejificha tu.”
Sheikh Mohammed Abdel Adhim Al-Makki katika kitabu cha [Al-Qaul Al-Sadiid alisema: uk. 113, Darul Da'wah- Kuwait]: “Baada ya muda wa kufahamu kwa kuruhusiwa kwa upatanisho kutokana na swali langu kwa Abu Yusuf na baadhi ya wanavyuoni wa Kawarizm na suala la usahihi wa hukumu juu ya mtu asiyekwepo kwa usahihi wa ndoa baada ya kuifanyika, kama ilivyotajwa katika suala lililotajwa licha ya makala ya mwandishi wa kitabu cha: [Al-Tahriir], juu ya binadamu kuchagua iliyo rahisi katika kazi, kisha nilikuta Sheikh Al-Islam na mwisho wa maimamu waliokuja baadaye ambaye ni Zainuddin ibn Nujaim katika kijitabu kilichoandikwa kuhusu mauzo ya waqf kwa uingizwaji alisema kuwa: kile kilichotokea mwishoni mwa kitabu cha: [Al-Tahriir] kuhusu kauli ya kutoruhusishwa kwa upatanisho inahusishwa na baadhi ya wale waliokuja baadaye, na haihusishwi na madhehebu hii. Kauli yake imemalizika, nimemshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu maoni yangu inakubaliana na matini ya maoni ya Mwananvyuoni Ibn Nujaim.”
Sheikh Mohammed Bekhit Al-Motaey katika kitabu chake cha: [Sarhul Esnawi ala Manhajul Baidhawi 4/630, Alam Al-Kutub] alisema kuwa: “Suala la upatanisho linategemea suala la kuundwa kwa kauli tatu, hali hii inazuiliwa kama jumla ya watu wanaofuata mtazamo huu ni kinyume na makubaliano ya wenye jitihada wote ili kama mwenye jitihada akiona kuwa hairuhusiwi kwake kusema kwa jumla hii."
Miongoni mwa Wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Malik ni Al-Dusuqi, aliyesema katika kitabu chake cha: [Al-Sharhul Kabiir 1/20, Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiah]: “Tuliyosikia kutoka sheikh wetu, kupokelewa kutoka kwa Sheikh wake mdogo na wengine kuwa rai iliyo sahihi ni kuruhusiwa kwake nayo ni upana. Na katika jumla upatanisho katika ibada moja ya madhehebu mbili ni njia mbili. Kuzuia, ni mtazamo wa Wamisri na kuruhusiwa ni mtazamo wa wamoroko na mtazamo huu uliochaguliwa”.
Katika kitabu cha: [Lughatu Salik 1/19, Darul Maarif]: “Aliyoyasema sheikh wetu, Al-Amiir kupokelewa kutoka kwa Sheikh wake Al-Adawi kupokelewa kutoka kwa Sheikh wake madogo na wengine: kuwa rai iliyo sahihi ni kuruhusiwa kwake nayo ni upana, lakini hailazimiki kufanywa katika ndoa, kwa sababu ni tahadhari katika tupu za wanawake zaidi kuliko vitu vingine.
Katika kitabu cha: [Al-Fawakih Al-Dwani 2/357, Darul Fikr]: “Al-Quraafiy alisema kupokelewa kutoka kwa wengine isipokuwa Az-Zanaty: inaruhusiwa kufuata madhehebu na kuchagua kati yao katika masuala yote yasiyobatilishwa na jaji, nayo ni masuala manne: jambo linalokiuka makubaliano au misingi au matini au kipimo kinacho wazi, kwa hivyo, inaruhusiwa kufuata madhehebu ya Imamu Malik katika suala la mavi ya wanyama kwa mfano, na kuacha maneno katika mikataba”.
Katika kitabu cha: [Tahdhiib Al-Fruuq wal Qawaid Al-Sunniah 2/34, Alam Al-Kutub]: “Kama akifuata inaruhusiwa kwake kula kutoka mnyama aliyechinjwa kwa mujibu wa kuruhusiwa kwa upatanisho katika ibada moja kutoka madhehebu mbili, kwa sababu hali hii ina upana katika dini, na dini ya Mwenyezi Mungu ni rahisi kama Sheikh Ali Al-Adawi alivyosema katika kitabu cha Al-Kharashi” .
Miongoni mwa wanavyuoni wa madhehbu ya Imamu Shafiy: yaliyotajwa katik kitabu cha: [Fathul Muiin kilichoandikwa na Ibn Ziad na na Al-Balqani 4/359, Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Sheikh Ibn Ziad Mwenyezi Mungu amrehemu alisema katika fatwa zake: yale tuliyoyaelewa kutokana na mifano yao ni kwamba kutunga hukumu vibaya hakuruhusiwi kama katika suala moja, miongoni mwa mifano yao kama mtu akitia udhu na aligusa mwanamke kufuatana na madhehbu ya Imamu Abu Hanifa na akamwga damu kufuatana na madhehbu ya Imamu Shafiy kisha akasali, basi sala yake ni batili kwa mujibu wa makubaliano maimamu wawili juu ya ubatili sala hii.
Vile vile kama mtu akitia udhu na aligusa bila ya matamanio kufuatana na Imamu Malik, na hakusinga kufuatana na madhehbu ya Imamu Shafiy, kisha akasali, basi salal yake ni batili kwa mujibu wa makubaliano ya maimamu wawili juu ya ubatili wa usafi wake, kinyume na kama kutunga kutoka masuala mawili, ambapo inaonyesha kuwa hali hii hapuuzi kufuata kwa maoni haya, kama akitia udhu na alifuta baadhi ya nywele za kichwa kisha akasali akielekea kibla kufatana na madhehbu ya Imamu Abu Hanifa, jambo ambalo linaonyesha usahihi wa sala yake; kwa sababu tunasema hali ya kukubaliana kunatokana na kujumuisha kwa masuala mawili. Na tuliyoyafahamu kuwa hapuuzi kufuata maoni n.k kama akifuata madhehebu ya Imamu Ahmad kuhusu viuno ni viungo vya siri, na kuachwa kwa kusafisha kinywaji na pua au kusema kwa jina la Mwenezi Mungu ambapo Imamu Ahmad anasema kwa ulazimu wake, jambo linaloonesha usahihi wa sala yake kama akiifuata madhehebu hii katika kiasi ya uchi, kwa sababu Wanavyuoni hawakukubaliana juu ubatili wa usafi ambao ni suala moja, na kukubaliana kwao hakupuuzwi juu ya ubatili wa sala yake ambayo ni masuala mawili na hali hii haipuuzi kufuata inaoneshwa kupitia mifano yao. Nimeona katika fatwa za Al-Belqini inayomaanisha kuwa utungaji wa masuala mawili hauzuilwi. Muhtasari umekwisha”.
Miongoni mwa wanavyuoni wa madhehbu ya Imamu Ahmad Ibn Hanbal ni Sheikh Marii Al-Karami, imetajwa katika kitabu cha: [Matalib Uli Nuha fi Sharhi Ghaytul Muntaha 1/390, Al-Maktab Al-Islami] alisema: “Mwandishi alisema -naye ni Sheikh Marii Al-Karami- katika vielelezi vyake kuwa: jua kwamba Wanavyuoni wengi wamependelea kutoruhusisha kufuata, ambapo hali hii ilipelekea upatanisho katika kila madhehebu, kwani wanavyuoni wa kila madhehebu wanaona ubatili wake, kama vile aliyetia udhu na akafuta nyewele za kichwa chake akifuata madhehebu ya Imamu Shafiy, kisha akagusa uchi wake akifuata madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, wakati huo kufuata si sahihi” Vile vile kama akifuta nywele zake, alicha kusoma nyuma ya Imam akifuata maimamu watatu, au alijeruhiwa kinyume na maimamu watatu, na wala hakusoma akifuata wao, hali hii ingawa ni dhahiri katika akili, hoja ni wazi, lakini aibu na usumbufu, hasa kwa watu wa kawaida, ambao Wanavyuoni wamesema kwamba hawana madhehbu maalum. Zaidi ya Mmoja walisema:
Si lazima kwa watu wa kawaida kufuata madhehebu maalum, pia si lazima katika wakati wa mwanzo wa umma. Na rai ambayo niliyoichagua: inaruhusiwa kufuata katika upatanisho, si kwa lengo la kufuatilia hivyo; kwa sababu anayefuatilia ruhusa alipotea, lakini ambapo ilitokea hali hii kwa makubaliano, hasa kutoka watu wa kawaida ambao hawana uwezo wengine. Ikiwa mtu alitia udhu na akafuta sehemu ya kichwa chake kufuatana na madhehebu ya Imamu Al-Shafi'i, bila shaka udhu wake ni sahihi. Kama aligusa uchi wake baada ya hivyo kufuatana na madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, imeruhusiwa; kwa sababu udhu wake ni sahihi, na kugusa uchi hakuvunji udhu kufuatana na madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, kama mtu akifuata madhehebu hii katika kutopingana na masuala yaliyo sahihi kwa Imamu Shafiy, udhu uliendelea huo akifuata madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, na hii ni faida ya kufuata. Katika wakati huo haisemekani kuwa: Imamu Shafiy anaona ubatili wa udhu huu kwa sababu ya kugusa uchi, na Abu Hanifa anaona ubatili wake kwa sababau ya kutofuta robo ya kichwa na zaidi; kwani masuala haya ni mawili tofauti; kwa sababu udhu umetimizwa kwa usahihi kufuatana na madhehebu ya Imamu Shafiy, na unaendelea baada ya kugusa uchi kufuatana na madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, basi kufuata kwa Abu Hanifa ni muendelezo wa usahihi, sio katika kuanza kwake, na Abu Hanifa ni miongoni mwa Wanavyuoni wanaosema kwa usahihi wa udhu wa mtu yule, ambapo alifuata Abu Hanifa katika suala alilohukumu kuwa ni sahihi”.
Kulingana na yaliyotajwa hapo juu: inaruhusiwa upatanisho kati ya Madhehebu ya Wanavyuoni wa Fiqhi na maoni ya wenye jitihada kama masharti yaliyotajwa yalitekelezwa, inaruhusiwa kwa Mufti kupatanisha katika Fatwa, kwa mujibu wa ile hali anayoiona inatekeleza makusudi ya Sheria na inaitikia mahitaji ya weney kalifisho, na inaruhusiwa kwa aombaye fatwa katika wakati huu kufuata hukumu iliyopatanishwa kama aliihakikishia ya moyo wake na alifikiri kuwa hukumu hii iliyopendelewa zaidi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas