Nafsi Inayoamrisha Maovu.

Egypt's Dar Al-Ifta

Nafsi Inayoamrisha Maovu.

Question

 Ni ipi Nafsi inayoamrisha maovu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwa hakika Qur`ani Tukufu imetuhadithia juu ya nafsi hii na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika kisa cha Yusuf A.S. {Kwa hakika nafsi ni mno kuamrisha maovu} [YUSUF: 53]. Na neno hili la kuamrisha kwa mfumo huu wa kupindukia ni dalili ya wazi juu ya uhatari wa nafsi kwa binadamu, kwa hivyo, waislamu wote wanaoshughulikia maadili na malezi, na waislamu Masufi, wanalazimika kujihadhari daima katika nafsi zao, na wajitahidi kuzigundua hali zake za maovu ili kuepusha upotovu.
Na mwanadamu katika mapambano yake na nafsi inayoamrisha uovu na jihadi yake ana hali tatu:
Ya Kwanza: Hali hii mwanadamu huwa anazidiwa na mambo ya matamanio na haiwezekani kamwe kujiepusha na kinyume chake, na hali hii ni hali ya watu wengi, na Qur`ani imeiashiria hali hiyo kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Je! Umemwona aliye yafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake?}. [AL FURQAN:43], hakuna maana yoyote hapa ya neno mungu ila Muabudiwa wa haki na kwamba muabudiwa ndiye ambaye ishara yake inafuatwa, kwa hivyo, mwanadamu anayesitasita katika maisha yake yote nyuma ya matamanio yake ya kimwili na kihisia anakuwa ni mtu aliyechukua matamanio yake kinyume na atakavyo Mwenyezi Mungu.
Ya Pili: Ni kuwepo kwa vita vya mvutano baina ya mwanadamu na matamanio yake, mara huwa kwa ajili yake na mara nyingine dhidi yake. Na mwanadamu katika hali hii anakuwa katika hali ya jihadi baina ya nafsi na matamanio yake, kwani yeye anapofanya jihadi dhidi ya matamanio yake ni kama mtu mwenye kufanya jihadi dhidi ya adui yake.
Ya Tatu: Ni hali ya mwanadamu ambaye anaweza kuyashinda matamanio yake na kuyatawala. Na matamanio yake hayawezi kumshinda kwa hali yeyote tena. Na wakati huu tunaweza kusema kwamba: Mwanadamu anapata ufalme mkubwa, neema kubwa na raha kamili.
Na huenda hali hii ya tatu ikawa imewachanganya baadhi ya watu, hii ni kama njia ya kuyafikia mambo yao binafsi, na baadhi yao wanadhani wamepata daraja hii na ilhali wamembeba shetani mkubwa ndani ya nafsi zao, na wanayafuata matamanio yao na nafsi za kuamrisha maovu na ilhali wanazidanganya nafsi zao kwa kuyafanya hayo eti kwa ajili ya dini. Imam Al Ghazaliy amesema kwamba ameushuhudia Umma mmoja uliojishughulisha na mafundisho na waadhi na ukadhi pamoja na hutoba na namna mbali mbali za uongozi wa kidini na ilhali wanayafuata matamanio na wakati huo huo wanajidai kwamba wanayafanya hayo kwa ajili ya dini ili wapate thawabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Watu hao wanajidai pia kwamba wanayafanya mambo hayo yote wakiufuata upande wa sheria ya dini tu.
Kwa ajili ya hayo, Imam Al-Ghazaliy anatupatia njia ya kimalezi ili tuweze kugundua tofauti baina ya uhalisia wa kweli na ubatili wa mambo, kwa mfano Mlinganiaji anaweza akawa Mkweli katika ulinganiaji wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu, au akawa si mkweli bali kwa ajili ya umaarufu, na kukubalika kwake mbele za watu. Al-Ghazaly alisema kwamba alama ya mlinganiaji mkweli ni kwamba lau mlinganiaji mwingine angekaa sehemu yake na akamtaja vizuri mwenzake kuwa ni hodari zaidi kuliko yeye katika mawaidha na kwa elimu yake tele pamoja na lugha yake ya kimawaidha na watu wanamkubali zaidi, wakati huo Mlinganiaji wa kwanza akimfurahikia ndugu yake Mlinganiaji huyu na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuutenga muda wake kwa ajili ya faradhi hii ya kuwalingania wengine tena kwa ubora wake katika uwanja huu wa kulingania. Ama akiwa na kigeugeu kwenye nafsi yake au akawa anajihisi uchungu au ghadhabu dhidi ya Mlinganiaji huyu wa pili, basi haya yote yatakuwa ni alama na dalili ya uwongo wake katika uwanja wa kulingania.
Na hali kama hii haijui mtu yeyote isipokuwa walii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yaani muumini wa kweli anayejitenga na mambo kama hayo kila wakati na kwa bidii kiasi akiwezacho na kujiepusha na matamanio ya kidunia. Na jambo kama hili linahitaji mzinduko wa kudumu ili kuiepusha nafsi yake na wasiwasi wa shetani na pia kujiepusha na utawala wa matamanio ya shetani. Lakini utenganishaji baina ya ishara ya akili na ishara ya matamanio ni jambo kubwa sana na haliwezi kuepukika ila kwa elimu ya kweli inayomwezesha mtu kuugundua mchanganyiko huu baina hali hizo.
Na mwislamu akipambana na jambo la kusitasita lazima ashituke kutokana na jambo hilo na lazima ajue kwamba kurejea kwa akili ni bora zaidi kwa manufaa ya matokeo yote yanapokuwa magumu katika maisha. Ama jambo la matamanio kwa hakika linaashiria mapumziko na kuacha uzito, kwa hivyo ni wajibu kwa mwenye akili kupambana na jambo lolote asilolijua uhakika wake kwa yakini, na alazimike kuchukia anachokichukia bila kumili upande wa anachokitamani asilolipenda kwani maadili ya juu yanakuwa pamoja na yale yanayochukiwa na nafsi kwa kauli ya Mtume S.A.W “Pazia la pepo hufunguliwa kwa kuendelea kuyaepuka yote yanayochukiza na pazia la Moto hufunguliwa kwa Matamanio” (2822) kutoka kwa Anas Bin Malik.
Na tunakuta fikra hii ndani ya Qur`ani Tukufu ni kama katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu {Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake} [AN-NISAA: 19] Na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.}[ AL-BAQARA: 216].
Kwa hivyo tunaweza kusema kwamba lazima aituhumu nafsi yake kila jambo lililomwashiria mwanadamu kuwa na raha na starehe, kwani upendo wa kitu chochote humtia mwanadamu akawa kipofu na kiziwi.
Na yapasa juu ya mwanadamu arejee na kumtegemea daima Mwenyezi Mungu katika kila kitu kwa njia ya kuswali rakaa mbili za Istikharah, na kumwomba Mwenyezi Mungu kwa Dua yake mashuhuri iliyothibiti kwa Mtume S.A.W. Amesema Jaabir Bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake, alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W akitufundisha Swala ya Istikhara kama vile anavyotufunza sura ya Qur’an. Anasema: “Akikusudia mmoja wenu kufanya jambo, aswali rakaa mbili zisizo za faradhi, kisha aseme: [Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakutaka ushauri (muelekezo) kwa ujuzi Wako, na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe unaweza, nami siwezi, nawe unajua nami sijui, nawe nimjuzi wa yale yaliyofichikana. Ewe Mwenyezi Mungu iwapo jambo hili kutokana na ujuzi wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali) basi nakuomba uniwezeshe nilipate, na unifanyie wepesi, kisha unibariki, na iwapo unajua kwamba jambo hili ni shari kangu katika dini yangu namaisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali) basi liepushe na mimi naminiepushe nalo, na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo”. [Imepokewa na Al-Bukhariy:1109].
Kwa hivyo tunalazimika kutoacha wala kusahau swala ya Istikharah na kuomba ushauri kutoka kwa wenye akili, kwani aghalabu ya mambo yanayochanganyika baina ya matamanio na nafsi na kuyaamrisha maovu ni nyudhuru zilizopambwa, na kama tujuavyo kwamba aghalabu ya tabia ya binadamu ni kujaribu mara nyingi kujidanganya yeye mwenyewe, na hakuna suluhisho kwa jambo hilo ila kwa kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu.
Na kuna vigezo vya maudhui hii ambavyo kwa kifupi ni kuwa akili ikielemea upande wa maumivu kwa haraka basi huwa na manufaa hapo mwishoni mwake, na makinzano na kushikiliana kwa nguvu ya akili inayoendesha fikra, nuru ya Mwenyezi Mungu huharakisha kuinusuru akili, na kwa upande mwengine wasiwasi ya shetani na wafuasi wake wao huenda mbio kwa ajili ya kuyanusuru matamanio yao, na na ukatuka ugomvi baina yao, na kama nguvu zinazoongoza zinatokana na shetani pamoja na wasaidizi wake zimejitenga na nuru ya haki na zikashindwa kuleta manufaa ya baadae na kudanganyika na ladha ya ya muda mfupi, na kuelekea katika kuwatenza nguvu mawalii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hata kama nguvu hizo zinazoongoza ni kutoka kwa kundi la Mwenyezi Mungu na mawalii wake zimeongoka kwa nuru yake, na kupunguza makali ya wakati uliopo kwa ajili ya wakati ujao, na kwa ajili hii, Qur`ani Tukufu inalizungumzia jambo hilo kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walioamini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashetani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu} [AL- BAQARA: 257]. Na Qur`ani Tukufu inaifananisha akili kwa mti mzuri na kuyafananisha matamanio kwa mti mbaya. Mwenyezi Mungu Anasema: {Hebu hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyo piga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni} [IBRAHIM: 24-27].
Na katika makutano baina ya safu za Mawalii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kundi la Shetani wa kutia wasiwasi na matamanio pamoja na nafsi inayoamirisha mambo maovu zingepambana miongoni mwao wakati huo huo, basi hakuna njia ila kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na kujikinga kwake na shetani aliyefukuzwa katika rehma za Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama asemavyo Mwenyezi Mungu: {Na kama wasiwasi wa shetani ukikusumbua (kuona kwa nini nisiwajibu masafihi hawa) basi (sema Audhu Billahi) jikinge kwa Mwenyezi Mungu (na kuchezewa na shetani, ukaacha wasia wake Mwenyezi Mungu), Bila shaka Yeye ndiye asikiaye na ajuaye}. [Al-AARAF: 200]. Na kauli ya Mwenyezi Mungu asema: {Wale wanaomuogopa (Mwenyezi Mungu) zinapowagusa pepesi za shetani (wakaasi; kama hivyo kujibizana na masafihi) mara hukumbuka, kutahamaki wamekwishaona njia.} [Al-AARAF: 201]. Kwa hivyo ni lazima kuzinduka hapa na kuujua uhusiano baina ya matamanio na mihemko, kwani kuna matamani yanayozingatiwa kuwa ni mihemko, na mengine yasiyozingatiwa kuwa hivyo. Na miongoni mwa matamanio mazuri ni kama vile uwezo uliyoumbwa na Mwenyezi Mungu ndani ya mwanadamu ili kuisaidia nafsi yake hiyo kupata kinachounufaisha mwili wake, au kuuendeleza mwili wake huo au kuiendeleza aina ya mtu huyo au kwa ajili ya maboresho ya vyote viwili kwa pamoja. Na miongoni mwa matamanio mabaya yanayofanywa na nafsi ya kuyaamrisha maovu, ni kukipendezesha kila chenye ladha kimwili, na ikiyashinda matamanio haya itaitwa matamanio kwani itaifuata fikra na kuitumia ili kuuchukua wakati wake kwa unyenyekevu chini ya amri zake, na wakati ule ule fikra inasitasita baina ya matamanio na akili, na akili nayo inaishughulikia fikra ili kuihudumia. Na inajaribu kuyadharau matamanio hayo na uzito wake. Na fikra ikifuatana na akili itakua juu na matokeo yake yatakuwa mazuri tena kwa wingi, na ikimili upande wa matamani, basi matokeo yake ni maovu na madhara makubwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye Muwafikishaji wa kila jambo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Chanzo: Profesa. Abdullatef Al Abd, Derasat fi Alfikri Al-Islamiy, Kairo, Maktabat Anglo Al-Masreyah.1977 (ku.44 – 47).

Share this:

Related Fatwas