Kuipuuza Elimu ya Thiolojia.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuipuuza Elimu ya Thiolojia.

Question

Je, elimu ya Thiolojia inapuuzwa? Ikiwa haipuuzwi, basi ni hukumu gani juu ya yale yaliyoandikwa kutoka kwa makatazo ya wanavyuoni kuhusu kutoshughulikia elimu hii, na baadhi yao wamesimama kuishughulikia? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu,
Elimu ya Thiolojia, ni elimu ya Misingi ya Dini, na elimu ya Tawheed (kumpwekesha Allah) na sifa zake, majina haya ni matatu kwa suala moja. Na Saad Eddin At-Tiftizaniy alibainisha sababu za kuitaja elimu hii, kwa jina la: Elimu ya Thiolojia, akisema: “Kwa sababu kichwa cha maudhui kilikuwa ni: kuizungumzia hivi na vile, na kwa sababu suala la Thiolojia ni suala maarufu zaidi na lina migogoro zaidi na utata, hata baadhi ya Watu waliwaua wengine walio katika haki, kwa sababu hawakusema kuwa Qur'ani imeumbwa”. [Sharhul Aqaid Al-Nasafiah kwa Al-Tiftizani, uk. 10, Maktabat Al-Kulliat Al-Azhariah].
Na Wanavyuoni wamesema vinginevyo, vile vile elimu hii iliitwa kwa jina la Elimu ya Tawheed, kwa sababu maudhui ya kumpwekesha Allah ni maarufu zaidi, pia imeitwa kwa jina la Misingi ya Dini kwa sababu Dini inajengwa juu yake.
Thiolojia ni: Elimu ya kuanzishwa kwa dalili za usahihi wa Akida na imani, na kwa maana hii haifai kuipuuzia hata kidogo. Lakini suala hili limeshughulikiwa na Qur`ani na Sunna ya Mtume wetu, S.A.W. wanavyuoni walijua kwamba elimu ya Thiolojia ni: elimu inayothibitisha Akida za dini kutokana na dalili zake za uhakika. [Tohfatul Murid ala Jawharatul Tawheed kwa Al-Bajuriy uk. 38, Dar es Salaam].
Hii ni elimu kubwa sana, na inagusia masuala muhimu ya binadamu katika dunia hii, kama vile: suala la dini, na suala la utume, na suala la kuhesabiwa siku ya Kiyama, na kadhalika.
Sababu ya kuibuka kwa Elimu ya Thiolojia ni jibu la wazushi, ambao walikuwa na mjadala na wanavyuoni wa Kiislamu, na wametaja masuala yenye shaka kwa yaliyothibitishwa na wema waliotangulia, na wakachanganya masuala haya na misingi mingi ya falsafa. Wanavyuoni wa watu wa Sunna wakahitaji kupingana na kujadiliana nao ili wasiwavurugie dini watu walio wanyonge, na ili wasiingize katika dini masuala yasiyo ni sehemu yake. Kama Wanavyuoni wangeliwaacha wazushi hawa bila ya kupambana nao, basi wangezitawala akili za wanyonge, Waislamu wa kawaida, na Wanavyuoni wao, wakawapoteza na wakabadilisha yaliyomo miongoni wa Akida sahihi, na bila shaka jambo hili ni zuri, kwani mambo yote yanategemea makusudio yake.
Kabla ya kushughulikia kwa wanavyuoni, haukuwepo upinzani wowote, na namna gani wanapinga wakati maneno yao hayaeleweki kwani hayashughulikiwi; kwa sababu hajibiwi kwake ila aliyeelewa, na ukimya wao huu ulisababisha uenezaji wa maneno ya wazushi hawa mpaka baadhi ya wajinga wakaamini maneno yao hayo, ni wajibu kwa wanavyuoni wa Kiislamu kujibu washuzi hawa kupitia kujifunza kwa elimu hii kwa bidii; kwani kuwashangaza kwa dalali zao kunasimamisha wao na kuwalazimisha kwa kufuata haki, wakawajibu na wakabatilisha tuhuma zao, na njia yao ya kujibu ilikuwa ni kuthibitisha Akida za Kiislamu, na kuzithibitisha kwa hoja zinazofanana na hoja za Qur'ani, kama maneno na ushawishi mkubwa katika mioyo, yanayoshawishi nafsi, yanayofurahisha mioyo, miongoni mwa dalili wazi na dhahiri.
Al-Ghazaliy alisema kuhusu marufuku ya Maulamaa waliotangulia kutoka katika kushughulikia elimu ya Thiolojia: “Ukisema kuwa: kujifunza kwa kubishana na kuzungumza kulipuuzwa kama kujifunza elimu ya nyota au inaruhusiwa au inapendeza, basi jua kwamba hali ya watu katika jambo hili ni kupita kiasi na ubadhirifu, baadhi ya watu walisema: Ni bidaa au haramu, na kwamba mja akikufa na akikutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kila dhambi isipokuwa ushirikina, ni bora kwake kuliko kukutana naye kwa kushighulikia elimu ya Thiolojia, na baadhi yao walisema: ni wajibu na ni faradhi ama ya kutosheleza au ni faradhi kwa wote, elimu ya Thiolojia ni kazi bora, ngazi juu, kutekeleza kwa elimu ya Tawheed na mapambano kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ambapo Maimamu Al-Shafiy, Malik, Ahmad Ibn Hanbal, Sufian, na watu wote wa Hadithi miongoni mwa waliotangulia walisema kuwa kushughulikia elimu ya Thiolojia ni haramu, na kama ilikuwa kutoka dini ilikuwa miongoni mwa masuala muhimu zaidi yaliyoamiriwa nayo, na miongoni mwa mitazamo hii ni mtazamo uliopokelewa kutoka kwa Abi Yusuf R.A, kuwa alisema: mwenye kuomba dini kupitia kushughulikia elimu ya Thiolojia basi akapotea”. [Ihyaa Uluum Ad-Dini 1/163, 164, Daru Ash-Shab].
Katazo la wanavyuoni katika matini hizi zilizopokelewa kutoka kwao si la moja kwa moja, lakini linakusudia waliotumia elimu ya Thiolojia kwa njia ya wanafalsafa, na kwa njia ya watu wenye matamanio na wenye bidaa waliopendelea upande wa akili, wakiacha Qur`ani na Sunna, wakategemea akili zao tu, wakaongeza tuhuma, bali walikuwa wakikana sana kwa anayeruhusishia kubishana, kwa hivyo Mtume, S.A.W. alisema, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Imamu Muslim na Ahmad: “Wameangamia wapindukiaji mipaka”, yaani: wenye kutafuta na kuchunguza; kwa sababu elimu hii ya Thiolojia ina maneno mengi ya tata na ya falasafa yenye upotofu na yasiyoonesha makusudi yake, kwa hivyo yanasababisha kutikisika kwa Akida.
Hii ni maana ya elimu ya Thiolojia iliyopuuzwa na Maulamaa waliotangulia, na walipiga marufuku kushughulikia nayo, kana kwamba elimu ya Theolojia maana yake ni hivyo tu, na kwa hivyo walisema kuwa elimu hii ilipuuzwa tu, na mpaka siku hizi aina hii ya elimu imeitwa kwa jina hili ambalo limepuuzwa, ambapo linapotajwa linafikiriwa aina hii tu, ingawa ufafanuzi wake unaotajwa na Wanavyuoni ni wa kiujumla.
Saad Eddin Al-Tiftizaniy alisema: “Katazo lililopokelewa kutoka kwa Maulamaa waliotangulia kuhusu elimu ya Thiolojia ni katazo la wenye mtazamo mkali, asiyeweza kupata haki, aliyekusudia kuharibu Akida za Waislamu, na aliyeshughulikia maneno ya wanafalsafa, kama sivyo, basi namna gani inakatazwa asili ya wajibu na msingi wa mambo yaliyoruhusiwa”. [Sharhul Aqaid Al-Nasafiah kwa Al-Tiftizaniy uk. 12, Maktabat Al-Kulliat Al-Azhariah].
Inaruhusiwa kufahamika kuwa katazo la Maulamaa waliotangulia kuhusu elimu ya Thiolojia ni kwa sababu elimu hii inasimulia madhehebu ya watu wenye matamanio na bidaa, na kutajwa kwa tuhuma zilizopingana na Akida ya watu wa Sunna, hali hii inasababisha kueneza kwa madhehebu hizi -ambazo tumeamuriwa kwa kutozieneza- vile vile, hali hii inathibitisha tuhuma hizi katika mioyo, mara nyingi tuhuma ni wazi na jibu lake si wazi, hali ambayo inapelekea maoni na kubishana katika dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwa hiyo ndiyo iliyopokelewa kuwa Imamu Ahmad Ibn Hanbal aliipuuza elimu ya Thiolojia sana mpaka akaacha Al-Harith Al-Muhasabi ingawa uchaji wake; kwa sababu alitunga kitabu kinachohusiana na kujibu kwa wazushi, akamwambia: “Ole wako, huitaji bidaa zao mwanzoni, kisha unazijibu, hugawanyi watu kufuatana na kuangalia kwa bidaa, na kutafakari juu ya tuhuma hizo, hali hii inawapelekea kutafuta na kutoa maoni.” [Rejea: Ihyaa Uluum Ad-Dini 1/163, 164].
Inawezekana kufahamu katazo la Maulamaa waliotangulia kuhusu elimu ya Thiolojia – kwa sababu pengine elimu hii inadhoofisha Akida na inapunguza heshima ya Mola moyoni - na kuondoka elimu nyingine za Kiislamu.
Vile vile Inawezekana kufahamu katazo la Maulamaa waliotangulia kuhusu elimu ya Thiolojia kuwa linahusisha aliyeishughulikia na akazungumza kuhusu elimu hii katika wakati ambapo hakuna haja kwake, kwa sababu dalili za wataalamu kama dawa inayofaa watu wachache tu, na isiyofaa wengine, kwa hivyo ni lazima kutoa dalili hizi kufuatana na haja na wakati tu.
Kama ikisemekana kuwa: Hatuna haja ya kueneza elimu ya Thiolojia, lakini inatosha kujibu tuhuma ya mzushi tu? Tunasema kuwa: haitoshi kufanya hivyo kwa ajili ya kubatilisha tuhuma ya mzushi.
Kile kilichosemwa kuhusu kurudi kwa Wanavyuoni wa elimu ya Thiolojia katika mwisho wa maisha yao, na majuto yao kuhusu wakati walioupoteza katika kushughulikia elimu hii ina maana ya kurejea kinyume na tafsiri kwa kutegemea. Kama alivyoelezwa na Al-Subki katika kitabu chake (5/191, Dar Hajar).
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, basi yaliyotajwa na Wanazuoni waliotangulia kuhusu matini zinazokataza kuishughulikia Elimu ya Thiolojia yanamaanisha kuwa anayetumia elimu hii kama wanavyoitumia wanafalsafa, wenye matamanio, na wazushi wanauopendelea upande wa akili, wakaacha Qur`ani na Sunna. Lakini matini zile hazikatazi moja kwa moja. Pia ni lazima kuzijibu - ipasavyo - tuhuma za wazushi na wengineo.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia, yamedhihirika yote yaliyopuuzwa katika elimu ya Thiolojia na yaliyolazimishwa.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas