Akili Kuifuta Hukumu ya Kisheria.

Egypt's Dar Al-Ifta

Akili Kuifuta Hukumu ya Kisheria.

Question

Je! Inaruhusiwa akili kuifuta hukumu ya Kisheria? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu..
Al-Naskh (kufuta) katika lugha ya Kiarabu ni: kubatilisha kitu na kukiweka kingine pahala pake, na tukisema kitu kinafuta kingine, maana yake kinakiondosha kabisa. Husemwa jua linakifuta kivuli yaani linakiondosha [Rejea: Lisaanu Al-Arab 3/61, Dar Sadir], Al-Naskh ina maana ya kunukuu, Az-Zarkashiy alisema hivyo [5/19/1956, Dar Al-Kutub].
Al-Naskh katika istilahi ni: kuondoa hukumu ya kisheri kutokana na matini za kisheria. Husemwa kuwa: Ni taarifa ya kumalizika kwa hukumu fulani ya kisheria kutokana na matini za kisheria. Ufafanuzi wa kwanza ndio uliochaguliwa. [Sharhul Jalal Al-Mahali ala jamil jawami 2/107 - 108, na ala Hashyatil Attar, Darul Kutub Al-Elmiyah].
Ukweli wa kufutwa kwa hukumu unategemea mambo mawili: La kwanza: Kuthibitishwa kwa hukumu ya kisheria kwa ufunuo uliowateremkia manabii, A.S. wao wote na ambao unawasilishwa kwa maneno, matendo na kwa kukubalika mbele yao. La Pili: Mwisho wa kutekeleza hukumu ya zamani ya kisheria baada ya ujio wa matini nyingine za kisheria zinazozuia kutekeleza hukumu ya kwanza, au inaonyesha kuwa hukumu ya kwanza ilikuwa ya muda tu na hivi sasa imefutwa.
Az-Zarkashiy anasema katika kitabu cha: [Al-Bahr Al-Muhiit 5/197, Dar Al-Kutub.], akielezea ufafanuzi uliochaguliwa na akionesha vizuizi vyake: Katika istilahi kuna hitilafu katika ukali wake, na maana iliyoteuliwa ni: hukumu ya kisheria huondoshwa kwa maandishi. Na maana ya hukumu ni kile kinachomtokea mwenye kukalifishwa baada ya kutokuwepo... na kukifungamanisha na hukumu ya kisheria kunaondoa hukumu ya kiakili, kama vile uhalali imara wa usahihi wa asili kwa anaeuzungumzia hivyo, kwani kama ingelimzuia mtu mmoja miongoni mwa watu basi isingeitwa kufuta, na tukasema: kwa maandiko, zienee aina mbali mbali za dalili, na na kuondosha Ijmaa na Kiasi, kwani haileti sura ya kufuta ndani ya Ijmaa na Kiasi, au hata kwa vyote viliwi, na hivyo kutoka uondoshaji wake kwa kifo au mfano wake, kwani hakika hiyo haiitwi kuwa ni kufuta, na ni kama vile mtu kuidondosha miguu yake miwili, basi hiyo haisemwi: kwa kuidondosha huko hukumu ya kuioshaa imefutika. Na alichokisema Imamu Fakhru Diin katika Almahsuul ya kuwa huko ni kufuta kuliko dhaifu] na kuendelea.
Imam Ar-Raziy aliruhusu kufutwa hukumu ya kisheria kwa akili, na alithibitisha hivyo kwa hali ya kuondolewa kwa kuosha miguu kwa aliyekatwa miguu yake katika ajali, kwa mfano, Imam Ar-Razi alisema katika kitabu chake kinachoitwa: [Al-Mahsuul 3 / 74-75, Muasasatur Resalah] kuwa: Ikiwa ikisemekana kuwa inaruhusiwa kuainisha kitu kwa akili, je, inaruhusiwa kukifutia pia? Tulisema: Ndio, kwa sababu aliyekatwa miguu yake hatakiwi kuiosha, na hali hii imejulikana kutokana na akili tu]. Mtazamo huu sio mtazamo wa Imam Ar-Razi pekee yake, bali imepokelewa kutoka kwa Imam Abu Ishaq Al-Maruzi kutoka kwa kundi la Wanavyuoni kuwa kuondolewa hukumu kwa sababu ya kuondolewa kwa sharti yake au sababu yake hali hii inaitwa kufutwa kwa hukumu [Rejea: Al-Bahri Al-Muhiit kwa Az-Zarkashiy 5/305], lakini Wanavyuoni wengi wenye mtazamo mkali walikubaliana juu ya kuruhusiwa kufutwa hukumu kwa akili].
At-Taj As-Sobkiy anasema katika kitabu cha: [Al-Ibhaj 2/167, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] kuwa: “Imam alisema kuwa inaruhusiwa kufutwa hukumu kwa akili akithibitisha hiyo kwa aliyekatwa miguu yake hatakiwi kuiosha, yaani hukumu ya kuiosha miguu imefutwa, lakini kwa kweli hukumu katika hali hii haikufutwa, bali imeondolewa kwa sababu ya kutoweza tu, Kisha kile alichotaja Imam ni kinyume na kile alichosema kuhusu hali ya kufutwa hukumu kwamba lazima iwe kwa njia ya kisheria”. Al-Banaaniy alisema katika maelezo yake juu ya [Sharhil Mahalli lijamil Jawami 2/76, Darul Fikr]: ... lakini Imam alisema maneno kinyume aliposema kwamba: Ulemavu haulazimishi kufutwa hukumu ya kisheria, kwani ulemavu siyo kwa njia ya kisheria]. Basi hali ya kuondolewa kwa wajibu kutokana na kutoweza haithibitishwa kwa akili lakini imethibitishwa kwa matini za kisheria zinazothibitisha kwamba Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika Qur’ani: {Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alichompa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraji} [AT TALAKA: 7], na kumkalifisha mlemavu aliyepotea kiungo chake kwa kukiosha ni kukalifisha kwa jambo lisilo kwa kadiri yake, na hali hii ni kinyume na yaliyotajwa katika aya hizi, nayo si kufutwa hukumu kwa akili, lakini hukumu haikuwepo kabisa kwani halikwepo sharti lake au sababu yake.
Al-Quraafiy anasema katika majadiliano ya suala lililothibitishwa na Imam Ar-Raziy kuhusu kuondolewa kwa sababu ya hukumu [Nafais Al-Ussul 5/2073, 2074, Nizar Mustafa El-Baz.]: “Hatukubali kwamba hali hii ni kufutwa kwa hukumu, kwani wajibu hauthibitishwi mwanzoni ila kwa sharti la uwezo na kuendelea kwa uhai, na hali ya kutokuwepo kwa hukumu wakati ambapo hakuna sharti siyo kufutwa, kwa hivyo basi vizuizi hutokea kwa mambo yasiyowezekana na hukumu pamoja na urefu wa muda vile vile pasipo na masharti, kwa hiyo, hali hii haiitwi kufutwa kwa hukumu, basi anayesafiri katika mwezi wa Ramadhani, hukumu ya kufunga na kusali hakuikufutwa kwake, kwani hukumu hizi ni wajibu kwa sharti ya kukaa. Pia kama mwanamke akipata hedhi, haisemekani kuwa hukumu ya kufunga na kusali zimefutwa, bali kufutwa kwa hukumu kunatokea katika hukumu inayotegemea sharti wakati wa kutotegemea sharti hili, au hukumu inayotegemea sababu pasipo na sharti ilhali haikwepo sababu hii, matokeo ya hali hii ni kwamba hukumu imeondolewa baada ya kuthibitika, na hukumu hizi hazithibitiki katika Sheria ila kwa masharti maalum. Kwa hiyo hakuna kitu kilichobadilishwa ili inasemekana kwamba ni kufutwa kwa hukumu”.
Sababu ya hukumu inaweza kuwa mtendaji, inaweza kuwa mtendewa ambaye tendo linatokea kwake, pia inaweza kuwa mahali au wakati wa kutenda. Kwa mfano, wajibu wa sala unahusiana na mtu Mwislamu mzima na mwenye uwezo. Kama hakuna mtu ana sifa hizi, Sala haiwajibiki kwa yeyote, hii haina maana kwamba sala imefutwa lakini haiwajibiki kwani sharti la wajibu limepotezwa, kama masharti hayo yakipatikana katika mwanadamu ni wajibu juu yake kusali, wakati ambapo hukumu iliyofutwa inaendelea kwa hali ile ile na kamwe haibadilishwi hata kama masharti na sababu zilipatikana. Inawezekana kuwa na mtendaji na hakuna mahali au wakati wa kutenda, kama vile kukengeuka jua ni wakati wa adhuhuri, kuzama jua ni wakati wa Magharibi, sala haikuwa wajibu ila kwa kufika wakati wake tu, inawezekana kuna mtendaji, inawezekana kuna mahali au wakati wa kutenda na hakuna mtendewa kama anayekatwa miguu hukumu ya kusimama katika sala imeondolewa kwake kwa sababu hakuna mtendewa.
Wanavyuoni wamesema kuwa mgogoro pamoja na Imam Ar-Raziy kuhusu suala hili ni mgogoro wa kitamko tu wala hautegemewi na athari kubwa, kusudi ni kwamba Imam Ar-Raziy amepanua maana ya kufutwa, na akataka kwake maana ya kuondoa kabisa, kwa sababu inashirikiana na kufutwa na aina zake na kuondoa kwa sababu ya hukumu, na kwa mujibu wa hiyo, makundi mawili ya Wanavyuoni wanakubaliana kuwa hukumu ya kuosha kwa miguu inaondolewa kwa aliyekatwa miguu yake, ikiwa ilisemekana: hali hii imesababishwa kwa kutokwepo kwa sababu au kwa ajili ya kufutwa hukumu kwa akili kwa mtu yule, au kwa ajili ya kuondolewa kwa sababu au vinginevyo.
Al-Attar anasema katika maelezo yake juu ya [Sharhil Mahalli lijamil Jawami 2/108]: akisema: “kama alieleza hivyo kwa upana) yaani kuhusu kufutwa kwa hukumu”.
Az-Zarkashiy anasema katika kitabu cha: [Tashniif Al-Masami 2 / 858.859, Muasast Qurtubah.] kuwa: Hali ya kuondolewa kwa hukumu kwa kuondolewa kwa sababu yake haiitwi kufutwa kwa hukumu, lakini mgogoro wake ni rahisi kwa sababu unahusisha kuitwa tu.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, ni dhahiri kuwa kauli sahihi zaidi kati ya kauli za wanavyuoni ni kwamba hukumu ya kisheria haifutwi kwa akili, kama ilivyokubaliwa na wengi wao, na kwamba tofauti iliyopo katika suala hili sio zaidi ya kuwa tofauti ya kimatamshi ambayo haileti athari ya kiutendaji inayoweza kutajwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas