Ruhusa Wakati wa Shida

Egypt's Dar Al-Ifta

Ruhusa Wakati wa Shida

Question

Inajulikana katika Fiqhi ya kiislamu kuwa shida ni miongoni mwa sababu za wepesi, nini mipaka ya shida hii inayosababishia kuwepo ruhusa?  

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, Aali zake na Masahaba zake, na waliomfuata, na baada ya hayo:
Msingi wa shida na uhusiano wake kwa wepesi na kuwepo ruhusa ni miongoni mwa misingi muhimu ambayo Mwanachuoni wa Fiqih anapaswa kuizingatia, kwa kuwa shida huenda ikanageuza hukumu ya makalifisho kutoka hukumu ya wajibu kuwa hukumu ya ruhusa, mambo yaliyokatazwa yalikuwa yanaruhusiwa kuyafanywa, na yale yaliyokuwa wajibu yanaruhusiwa kuachwa, hivyo tu kwa sababu shida inasababisha aibu au usumbufu inayolazimisha wepesi na kuwepo ruhusa, lakini hakika shida ni miongoni mwa sababu za wepesi zinazohusiana na masuala ya kifiqhi, athari zake hazihusiana na suala maalumu la kifiqhi tu, bali mara nyingi zinahusiana na masuala yote ya kifiqhi, ingawa mara nyingi shida ni sababu zinazohusiana na ibada, hasa masuala ya usafi na kuondoa uchafu, lakini kupitia kutafakari katika matawi ya kifiqhi inadhihirika kuwa shida inahusiana na masuala mengine, baada ya kutaja matawi mengi ya kifiqhi yanayohusiana na suala la shida, Al-Suyuti anasema kuwa: “Imedhihirika kuwa msingi huu unahusiana na masuala mengi ya kifiqhi” (Al-Ashbah uk.: 80, Ch. Dar Al-Kutub).
Anayeangalia kuhusu vilivyoandikwa na Wanavyuoni anaweza kuigawa shida katika sehemu mbili, nazo ni shida ya ujumla na ya binafsi, na kila sehemu ina udhibiti wake, ingawa athari inayotokana na kila sehemu ni moja.
Sehemu ya kwanza – Shida ya ujumla – maana yake: wengi wa wenye kukalifishwa au kundi maalumu miongoni mwao kuwa na haja kubwa ya kuepesishiwa jambo la kawaida linalokaririwa au kuliepuka, ambapo kama wakikalifishwa kuliepuka jambo hili, watapata shida isiyo ya kawaida. Al-Sanaani amesema: “Maana ya ujumla wa shida ni kujumuisha kalifisho kwa wenye kukalifishwa wote au wengi wao”. (Ijabatul Sail Sharhu Bughyatul Amil uk. 109, Muasasatul Resalah).
Alauddin Al-Bukhariy alielezea jambo linalosababisha shida: “Ni jambo linalohitajika katika hali zote” [Kashful Asraar 3/16, Darul kutub Al-Islami, Kairo]. Shamsu Ddin Al-Aswfahaniy alielezea kuwa “Ni jambo ambalo watu wengi wanalihitaji”. (Bayan Al-Mukhtasar 1/746, Chuo Kikuu cha Umm Al-Qura, Makkah).
Al-Kamal Bin Hammam alielezea jambo linalosababisha mtihani, kwamba: “Ni jambo ambalo watu wote wanalihitaji mara kwa mara”. [At-Tahriir pamoja na maelezo yake 2/295, Dar Al- Fikr].
Kwa mfano, jambo ambalo ni vigumu kuachwa kwa umuhimu wake: nalo ni usingizi, mara nyingi ni jambo linajikariri kwa watu wote, wala halihusiani na mtu mmoja tu, ni wazi kwamba hali ya kuuachwa usingizi kabisa haiwezikani kwa watu wote kwa sababu wanauhitaji kwa dharura, kama wakikalifishwa kuepuka usingizi kabisa wangekuwa na shida zaidi ya kawaida ambayo haiwezi kuvumiliwa, hivyo, ni wazi kwamba usingizi ni miongoni mwa mambo yanayosababisha shida, pamoja na kuangalia kuwa chanzo cha sheria ni kuharimisha kila kinachosababisha kukosekana kwa akili au kupotea kwa ufahamu -kama vile pombe, madawa ya kulevya n.k., lakini wakati watu walipohitaji usingizi ingawa usingizi ni sababu ya kupoteza akili uliruhusiwa kinyume na chanzo hiki, kwani kukalifishwa kwa kuachwa usingizi ni aibu na haiwezekani, Mwenyezi Mungu anasema: {Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo} [AL-BAQARAH: 286], {Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini} [HAJJ: 78].
Imepokelewa kutoka kwa Mama wa waumini Aisha, R.A, kutoka kwa Mtume S.A.W alisema: “Wamesamehewa (watu wa aina) tatu”, alisema miongoni mwao ni: “aliyelala mpaka aamke” (Abu Dawud, Ibn Majah na An-Nasaiy).
Mfano wa jambo ambalo haiwezekani kuliepuka: ni damu ndogo iliyobaki katika nyama ya mnyama baada ya kumchinjwa, ni vigumu kwa watu kuiepuka damu hii, wala haipaswi kuiosha kabla au baada ya kupika nyama, ingawa ni sehemu tofauti ya damu inayomwagikia mnyama aliyechinjwa, na ambayo ni chafu kwa mujibu wa makubaliano ya Wanavyuoni wote, lakini wakati damu hii chache ilipokuwa vigumu kuiepukwa, pamoja na umuhimu wa kula nyama kwa watu wengi, ilikuwepo shida, na ilisamehewa kwa jambo hili, kinyume na kama mtu akikusudia kukusanya damu chache iliyosamehewa, na akanywa pekee, ni haramu kufanya hivi kwa sababu hakuna haja kwa hilo.
Aina ya pili ya shida, ni shida ya kibinafsi, nayo ni haja ya anayekalifishwa kwa dharura kwa wepesi wa jambo fulani linalojirejea -kwa njia maalumu- ni vigumu kuliacha au kuliepuka. Ambapo kama anayekalifishwa akilazimishwa kwa kuliepuka jambo hili atapata shida isiyo ya kawaida, hivyo kama mtu akipata shida ya kibofu cha mkojo kwa mfano, basi ni vigumu kwake kutia udhu mpya kwa ajili ya kusali kila linapoangukia tone la mkojo, kwa ugumu wa kujilinda na kutoweza kwa kudhibiti pamoja na wingi wa kupata hadathi, basi anayekalifishwa ana haja kubwa ya kusali pamoja na wepesi wa hukumu za usafi, hii ni shida ya kibinafsi ambayo haipatikani kwa mtu wa kawaida, lakini inapatikana kwa baadhi ya wanaokalifishwa kwa njia maalumu, ugumu wake unatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, jambo ambalo linamlazimisha Mufti kusoma mambo mbalimbali yanayozunguka tukio kisha kutoa fatwa kwa kila mtu maalumu, kwa mujibu wa shida yake, zaidi ya iliyotolewa na Mufti kuhusu hukumu za jumla katika ujumla wa shida.
Kutokana na ufafanuzi wa shida kwa aina zake mbili na mifano ya kila aina inawezekana kutambua jambo linalodhibiti hali ya shida yenyewe, jambo linalosababisha shida ni lazima liwe na masharti mawili:
La kwanza: ushirikishwaji wa wengi: suala la ujumla wa shida linatofautisha suala la shida ambayo ni maalumu kwa sharti hili, hivyo, kwani katika ujumla inatazamiwa hali ya wengi wa wanaokalifishwa, au baadhi yao, na kupatikana ruhusa kunathibitishwa katika hali hii pasipo na haja ya kuomba fatwa ya pekee, Ibn Qudamah anasema: [Al-Mughni 2/59, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy): “Kama kuna dharura ya jumla dharura hii inathibitisha hukumu kwa kisicho na haja, kama vile kuruhusiwa kumnunua mbwa kwa ajili ya kuwinda na mifugo kwa asiyehitaji viwili hivyo, na kwa sababu imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W., kuwa amekusanya kati ya sala katika mvua, na hakuna umbali kati ya chumba chake na msikiti”.
Wakati ambapo kuhusu shida ya kibinafsi inatazamiwa hali ya kila mtu pekee yake na sababu za tukio hilo linaloombwa fatwa kwake, basi fatwa zinatofautiana kulingana na tofauti za hali za wanaokalifishwa na masuala yao.
Ujumla wa shida unategemea tofauti kati ya Fiqhi ya watu na Fiqhi ya umma au kikundi, imepokelewa katika matini za kisheria, vyanzo vyake, na hukumu zake zinazothibitisha tofauti hii, na miongoni mwasura za tofauti kati ya hukumu za mtu na za kikundi ni zilizofanyiwa utafiti na Wanavyuoni katika vitabu vyao kuhusu tofauti kati ya wajibu na wajibu-wa kutoshelezeana (Kifaya). Tofauti hii ni miongoni mwa masuala ya vyanzo vya Fiqhi, na ukweli ni kwamba kama mwenye Sheria alivyoangalia hali ya kundi katika suala la wajibu-wa kutoshelezeana (kifaya) ambapo alilazimisha wanaokalifishwa kwa kufanya jambo fualni na kama akilazimisha kila mtu kufanya jambo hilo hilo itakuwa ni shida kwa wengi wao, hivyo pia mwenye Sheria aliangalia hali zao katika suala la ujumla wa shida ambapo aliwarahisishia mambo ambayo kama akiyalazimisha kwa kila mtu itakuwa shida kwa wengi wao tena watapata aibu, ndiyo kuna watu ambao hawana shida katika kufanya wajibu –wa kutoshelezeana (kifaya) au kutorahisisha sababu za shida, lakini kama wale ni wachache, na msingi ni kwamba wengi wanazingatiwa lakini siyo wachache, kuzingatia kwa hukumu ya wengi ni msingi thabiti katika matini za Qur`ani na Sunna katika nafasi na masuala tofauti, miongoni mwao ni: kama pombe ikiwa na faida fulani, lakini ni chache ukiilingana na madhara mengi yanayosababishwa kwa kunywa pombe, na iliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W inathibitisha maana hiyo, alipoulizwa kuwa: tunaweza kuangamizwa na pamoja nasi watu wema? Akasema: ((Ndio, kama uovu ukienea)) (Hadithi hii imekubaliwa).
Wanavyuoni wa Fiqhi wametaja misingi mingi inayohusu maana hii. [Al-Mabsout kwa Al-Sarkhasi 19/19, Darul Maarifah – Beirut].
Miongoni mwa misingi hii: “Wingi unabadilisha nafasi ya uchache.” [Al-Mabsout 25/28].
Na miongoni mwa misingi hii pia ni: “Wepesi unafuata wingi, na sio wingi unaotegemea wepesi”. [Al-Hawi Al-Kabiir kwa Mawardi 7/366, Darul Fikr].
Kutokana na yaliyotangulia ni wazi kwamba ujumla wa jambo kwa wengi wa wanaokalifishwa au wengi wa kundi maalumu ni miongoni mwa mambo yanayoathiri katika hukumu za kisheria, na pia miongoni wa mambo ambayo hutegemewa usahihi wa kuelezea msiba kuwa ni sababu ya kuenea shida yenyewe.
La pili: ni marudio na wingi wa kutokea: binadamu huenda kukalifishwa kufanya jambo pasipo na shida yoyote mara moja au mara kwa mara katika vipindi vya muda, lakini kama akikalifishwa kufanya jambo hili mara kwa mara katika vipindi mara kwa mara hupata shida kwake, chochote wepesi wake, hivyo marudio na ya wingi wa kutendwa ni miongoni mwa udhibiti wa ujumla wa shida, kwa sababu suala linalokaririwa mara chache halisababishi shida hata kama likijumuisha wanaokalifishwa wote.
Na marudio ambayo hutegemea suala la ujumla wa shida ni marudio makuu katika kiwango cha pamoja, kama vile marudio ya usafiri katika kuruhusu kwa kutofunga saumu na kuchanganya na kufupisha sala, ingawa mara nyingi kila aliyekalifishwa hana haja ya kusafiri mara nyingi, lakini kama marudio ya kusafiri mara nyingi pia kwa ujumla kila siku, ruhusa ilikuwa kwa watu wote, kwani fiqhi ya umma au fiqhi ya watu inawaangalia wanaokalifishwa kama ni mtu mmoja, hiyo marudio ya kutenda tendo hili linasababisha shida.
Siyo yote yanayokaririwa yanawakilisha ugumu, lakini udhibiti wa marudio ni kuwepo kwa ugumu usio wa kawaida. Gumu labda hazizingatiwi kwa mwenye Sheria, nazo ni ngumu zilizozoelewa na watu katika maisha yao na wanazivumilia kwa ajili ya kupata kwa malipo, kama vile ugumu wa kupata riziki, kujenga kwa majengo na makazi n.k. Kulingana na hivyo ugumu wa ibada: kama vile kuhiji, kufunga na kusali, na kuna ugumu unaozingatiwa, kama vile: ugumu unaotokana na uvunjaji wa makusudi tano au makusudi moja miongoni mwao, na makusudi hayo yanaitwa dharura kwa ukubwa wa haja ya daima, na aina hii ya ugumu haizingatiwi kwa ujumla wa shida au ubinafsi wake, bali aina hii ya ugumu inazingatwa kisheria katika kila hali na kwa kila mtu, isipokuwa masuala yaliyoachwa na Sheria katika adhabu na kisasi na kadhalika kuhusu msingi unaopendelea dharura ya umma juu ya dharura ya kibinafsi, na kuna aina ya ugumu kati ya aina mbili zilizotangulia, nao ni ugumu unaotofautiana kati ya ukali wa udhaifu, basi mara ugumu huu unapendelea na mara nyingine unapendelewa kufuatana na hali, kila linalokaribia ugumu unaozingatiwa linaambatanishwa nao, na mara nyingi hali hii inatokea katika dharura, basi kama shida ikienea ilizingatiwa miongoni mwa dharura katika mbali na msingi unaopinga hivyo, na kama shida haikuenea basi imefutwa kwa mujibu wa asili, kama vile udongo wa barabara ambazo haziepukani uchafu, ni vigumu kwa watu kujilinda, kama si vigumu kwa baadhi yao kujilinda, basi haina kurahisisha katika hukumu hii ya kisheria kwa ujumla kwani hakuna shida, lakini inatazamiwa katika kila hali kwa mujibu wa shida aliyo nayo, kwa sababu shida zitatofautiana.
Inaruhusiwa kwetu kusema kuwa: “Hakika suala la ujumla wa shida na ubinafsi wake linawekwa chini ya msingi mkubwa nao ni msingi wa: “Ugumu huleta wepesi”, hali ambayo tulitaka kuitaja katika mtazamo wetu ambao ni: athari ya kifiqhi inayotokana na ujumla wa shida na ubinafsi wake ni moja tu, kama udhibiti wa shida ukiwa sahihi ruhusa imetolewa, ambayo inaweza kwa kuruhusiwa kwa jambo lisiloruhusiwa: kama katika kufuli ndogo ya fedha kwa ajili ya dharura, na kama kuvaa silki kwa yule anaye na mkwaruzo katika ngozi yake. Inawezekana kwa kutangulia jambo linalostahiki kulichelewesha, au kuchelewesha jambo linalostahiki kulitanguliwa, kama katika mchanganyiko wa sala mbili katika kusafiri. Huenda kwa kufuata kwa anayeruhu, kwamba mtu anaanza kufanya jambo fulani na jambo hili lianruhusiwa kisheria na baadhi ya wanavyuoni, hata kama halipendelewi kwa mujibu wa mtazamo wake, na hali hii ni bora kwake kuliko kufunga mbele yake milango yote wala hapati njia isipokuwa kufanya jambo la haramu, ingawa alikuwa na ruhusa ya kufuata wanavyuoni walioruhu jambo hili. Al-Sheikh Al-Bajori alisema katika kitabu chake akieleza maelezo ya Al-Qasim kwa matini ya Abi Shujaa katika fiqhi ya Al-Shafii – mwelezaji aliposema: “Hairuhusiwi kwa mtu au mwanamke kutumia vyombo vya dhahabu na fedha pasipo na dharura” - Alisema: “Al-Balqaniy, pamoja na Al-Demeiriy walisema kuwa jambo hilo ni dhambi kubwa, na Al-Adhraiy alitaja kutoka kwa Wanavyuoni wa umma kwamba dhambi hii ni ndogo, na rai hii ndiyo iliyochaguliwa. Dawud Ad-Dhahiriy alisema: inachukiza kutumia vyombo vya dhahabu na fedha, nayo ni maoni ya Al-shafi, imesemekana kuwa uharamu unahusiana na kula na kunywa tu; kufuatana na matini ya Hadithi isemayo: “Na msinywe katika vyombo vya dhahabu wala vya fedha wala msile katika vyombo hivi hivi. [1/41, na mfano wake katika maelezo ya Al-Shirwani juu ya Al-Tuhfah 1/119, Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas