Kunyimwa Urithi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kunyimwa Urithi

Question

Kunyimwa urithi, je ni katika kuadhibu kwa mali ikiwa mrithi ni mlemavu kwa yule amrithie? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Baadhi ya watu wanafanya makusudi kuwanyima urithi baadhi ya warithi kwa kuandika wasia kwa njia hiyo, na inawezekana ikawa katika nchi yenye sheria inayoruhusu jambo hilo, na anaweza mtu baleghe akadhani kuwa hiyo ni haki yake binafsi hasa iwapo mrithi ni mlemavu.
Na kizuizi hicho kilichotajwa, ndani yake kina mielekeo mingi ya kisheria; na miongoni mwake: kwamba hiyo huzingatiwa ni katika njia za kuzuia haki za waja alizowapa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na huhesabika kuwa ni madhara katika wasia, na ndani yake pia ni kuacha kutenda kheri na hekima kutokana na ufafanuzi huu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Abu Al-Qasem Asuhailiy alisema katika kitabu chake: [Al-Fara'edh wa Sharhu Ayaatu Al-Wasia, Uk. 37, Ch. Al-Maktabah Al-Faiswalia, Makkah Al-Mukaramah]; "Na ugawia wa Mirathi kutegemea sheria ndani yake ni heri zote; kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa rehema yake, uadili wake na hekima yake Yeye ambaye Aliugawia. Na Amezianzisha aya za Mirathi kwa wasia kwa watoto; kwa kuwa Yeye ni Mwenye rehema kwetu zaidi kuliko sisi wenyewe kwa nafsi zetu, anasema Suhailiy: kisha mimi nimetazama katika alichokibainisha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'ani katika halali na haramu, Adhabu maalumu ziitwazo Mipaka na hukumu mbali mbali sijakuta ameanzisha kitu chochote katika hivyo kama alivyoanza hivyo kwenye aya ya Mirathi, na wala hajamaliza kitu chochote hivyo kama alivyomalizia hivyo katika aya hiyo, naye anasema mwanzo wake: kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema katika mwanzo wa aya hiyo: {Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu}.
Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu ametueleza kuhusu Yeye kwamba Yeye ni muusiaji kama njia ya kututanabahisha juu ya hekima yake kwa kile alichokiusia kwacho na uadilifu wake pamoja na huruma aliyonayo, ama kuhusu hekima yake hakika yeye alitambua kwa utukufu wake, masilahi yaliyomo katika amri yake kwa waja wake, na yaliyomo katika utekelezaji wao amri hii kabla ya hili jambo kutokana na ufisadi uliopo, ambapo walikuwa wamemrithisha wakubwa na hawawarithishi wadogo, na wamewarithisha watoto wa kiume na hawawarithishi watoto wa kike, na wanasema: je tunamrithisha mali zetu mtu asiyepanda farasi wala asiyeweza kupigana kwa upanga na kuiswaga mifugo, na kama Mwenyezi Mungu Mtukufu angeliwasemesha kwa mtazamo wao kisha akawaacha na matamanio yao basi matamanio hayo yangewasababishia umauti wao kwa baadhi ya watoto wao na wengine kuwa hai, hilo lingepelekea ugomvi na kutengana, ujeuri na uchache wa uadilifu na mtu akawanyang'anya wasia huo na kujirejeshea kwake kinyume na kuwapa wao ili ajiridhishe kwa kutumia elimu na busara zake binafsi.
Kwa hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema mwishoni mwa aya hiyo: {Huu ndio wasia ulio toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mpole}. Na Akasema kabla ya hayo: {Hiyo ni Sheria iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka Mwenyezi Munguni ni Mjuzi na Mwenye hekima}.
Ama kwa upande wa uadilifu wake, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesawazisha baina ya watoto wa kiume; kwa kuwa wao, iwe katika hukumu za fidia, Akili na utarajia wa manufaa, hata kama watakuwa wadogo kiasi gani haibatilishi haki yao ya kuzaliwa wala maana ya nasaba na kwamba kila mmoja wao ni sehemu ya damu ya mtu. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu}. Na wala hajasema kwa watoto wenu kwa kuwa alitaka uadilifu kwao na kuonya juu ya ujeuri juu yao na limekuja tamko la kijumla lisiloishia katika urithi au kitu kingine.
Na hukumu katika jambo hilo ni wazi kwamba ni haramu, na mtu baleghe haihalalishwa kuisadikika licha ya kuitendea kwake.
Na dalili za mambo hayo ni nyingi na mbalimbali, miongono mwake ni:
Ya Kwanza: Ufafanuzi wa mfumo wa sheria katika Mirathi kinyume na sheria zingine kwa namna ambayo inapelekea kutoacha ufafanuzi wa Jitihada: Basi kwa hivyo ugawaji wa Mirathi umetajwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ufafanuzi Zaidi; kwa ajili ya kuujali: na wala hakumpa jukumu hilo yeyote kama ilivyo katika Sheira nyingine nyingi.
Al-Zelaiy alisema katika kitabu chake cha: [Sharhu Al-Kenz 229/6, Ch. Al-Matwba'ah Al-Ameriah Al-Kubra] Kitabu cha Mafaridha, na hiyo ni wingi wa neno faridha, na faradhi ni kukadirisha, inasemwa kuwa Kadhi amepitisha maamuzi ya matumizi kwa maana ameyakadiria, na elimu hii imeitwa Faraaidhu (Elimu ya Mirathi) kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amekadiria viwango yeye mwenyewe na wala hajampa malaika aliye karibu sana naye, au Mtume yeyote, jukumu la kuvikadiria viwango hivyo, na akabainisha kiwango cha kila mtu katika kurithi kutoka nusu, robo, thumuni, thuluthi mbili, thuluthi moja, na sudusi kinyume na hukumu nyingine zote kama vile; Sala, Zaka na Hija na nyingineo, kwani matni katika mambo hayo ni kwa ujumla kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na shikeni Sala na toeni Zaka}na {Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia yakwendea}lakini Sunna ilizielezea.
Ya Pili: Uhamaji wa dharura wa Mirathi, kwa maana kwamba Mali inahamia kwa warithi bila ya kutaka kwake, Basi Urithi unahamia kutoka kwa anayerithiwa kwenda kwa warithi kwa kufa kwake tu, na wala haihitajiki hatua nyingine yoyote; kwani hakuna uhamishaji wa kuchagua kama vile wasia au kuuza na kununua, bali ni uhamishaji wa mali kwa dharura.
Al-Hswakafiy akasema katika kitabu chake: [Adurru Al-Mukhtaar 757/6, Ch. Dar Al-Fikr] Mlango wa Mirathi (faraaidh) ni Elimu ya Misingi ya Fiqhi na hesabu ambapo hujulikana kwayo haki ya kila mrithi wa kilichoachwa na Marehemu, mali na haki, na hapa kuna aina tano kwa uchambuzi Zaidi; kwani haki inaweza kuwa ya maiti au dhidi yake na si ya kwanza wala ya pili: Ya kwanza ni Maandalizi, na ya pili ima inahusiana na Jukumu nalo ni deni lolote au kama sio hivyo ni kuhusu kitu kinachoonekana, na ya tatu ni ima ya kujichagulia ambayo ni wasi au ya kulazimika ambayo ni Mirathi.
Ya Tatu: Kuufungamanisha wasia na theluthi moja tu, na wala hakuna wasia kwa mrithi yeyote, na lau kama amri ingelikuwa ya kuachwa kwa mrithishi isingelifungamanishwa hivyo, bali jambo hili angeachiwa mwenye mali. Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Baada ya wasia uliousiwa au kulipa deni, pasio kuleta dhara. Huu ndio wasia ulio toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Munguni Mjuzi na Mpole (12). Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Yeye atamtia katika Pepo zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa. (13) Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.(14) [AN NISAA 12-14].
Imam Ibn Kathiir alisema alipoeleza aya hizo; Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Baada ya wasia uliousiwa au kulipa deni, pasio kuleta dhara}, yaani; ili wasia wake uwe kwa uadilifu, wala sio kwa ajili ya kudhuru na ujeuri au unyang'anyi kwa namna ambayo baadhi ya warithi wananyimwa haki yao, au inapunguzwa au inazidishwa Zaidi ya kiwango alichokikadiria Mwenyezi Mungu kwa kila mtu katika fungu lake, na mtu atakayekimbilia hivyo basi atakuwa kama mtu aliyeenda kinyume na Mwenyezi Mungu kwa hekima na ugavi wake.
Halafu akaitaja hadithi ya Ibn Abbas: "Hakika Mwenyezi Mungu amempa kila mwenye haki haki yake, na hakuna wasia wowote kwa mrithi". Hadithi hii ina hukumu ya Marfuu na Mauquuf. Kisha akasema: "Na kwa ajili hii Wanazuoni wamehitilafiana katika maamuzi ya Mrithi: Je ni sahihi au hapana? Kuna kauli mbili: ya kwanza yake: haisihi tuhuma za kukisia kuwa amemuusia kwa tamko la kukiri"
Na imethibiti katika hadithi sahihi kwamba Mtume S.A.W., akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu amempa kila mwenye haki haki yake, na hakuna wasia wowote kwa mrithi". Na hiyo ni madehebu ya Abi Hanifa, Malik, Ahmad Bin Hambal, na tamko la zamani kwa Shafiy, rehema ya Mwenyezi Mungu juu yao wote. Na Shafiy ana tamko jipya kwamba ukiri uanasihi, na hiyo ni madhehebu ya Twawus, Atwaa, Al-Hassan na Omar Bin Abdulazizi, na huo ni uchaguzi wa Abi Abdullahi Al-Bukhariy katika kitabu chake: [Sahihu Al-Bukhariy]…
Unapokuwapo ukiri sahihi unaolingana na jambo lenyewe tofauti iliyopo imepita ndani yake, na panapokuwapo ujanja wowote na njia ya kuongeza baadhi ya warithi na kuwapunguzia wengine hii ni haramu kwa makubaliano ya wanazuoni wote na kwa tamko la aya tukufu: {au kulipa deni, pasio kuleta dhara. Huu ndio wasia ulio toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Munguni Mjuzi na Mpole}. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Yeye atamtia katika Pepo zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa. (13) Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha. (14) [AN NISAA 12-14]. Yaani ugavi huu wa Mirathi na viiwango vyake alivyovikadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa warithi kwa mujibu wa undugu wao kwa marehemu na mahitaji yao kwake pamoja na kumpoteza kwao pale anapofariki, ni mipaka ya Mwenyezi Mungu basi msiipindukie na wala msiipitie.
Kwa hiyo Akasema: {Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake}, yaani katika mipaka hiyo, na baadhi ya warithi hawajajiongezea wala kujipunguzia wao kwa wao kwa ujanja na kwa njia yoyote bali amewaachia hukumu ya Mwenyezi Mungu na faradhi yake pamoja na mgao wake. {Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Yeye atamtia katika Pepo zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa. (13) Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.}. Yaani kwa kuwa kwake kinyume na alivyoamua Mwenyezi Mungu na akayapinga maamuzi ya Mwenyezi Mungu. Na jambo hili hakika linatokana na kutokuridhika na ugavi wa Mwenyezi Mungu na uamuzi wake katika hili, na kwa ajili hii humlipa udhalili kwa kumwadhibu adhabu kali na ya kudumu. [Tafsiir Ibn Kathiir 231.232/2, Ch. Dar Twibah, Ariyaadh]
Na katika hadithi tukufu kutoka kwa Abi Umamah kutoka kwa Mtume S.A.W., "Hakika Mwenyezi Mungu amempa kila mwenye haki yake, na hakuna wasia wowote kwa mrithi". [Imetolewa na Abu Dawud, Ansassaiy katika Al-Fatawa Al-Kubra na Ibn Majah]
AL-Khatwabiy alisema: "Tamko lake: Hakika Mwenyezi Mungu amempa kila mwenye haki yake, ni ishara kwa aya ya Mirathi. Na wasia ulikuwa kabla ya kuteremeka kwa aya hiyo ni wajibu kwa wadugu na jamaa, na hilo ni tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mmeandikiwa -- mmoja wenu anapo fikwa na mauti,kama akiacha mali -- afanye wasia kwa wazazi wake na jamaa zake kwa namna nzuri inayo pendeza. Ni waajibu haya kwa wacha mngu.} [AL-BAQARAH 180]
Kisha ikafutwa na aya ya Mirathi, hakika mambo yalivyo, wasia hubatilika kwa mrithi kwa tamko la wengi wa wanazuoni kwa ajili ya haki za warithi wengine, na ikiwa wataruhusu basi itaruhusika kama ambavyo wakiruhusu nyongeza zaidi ya theluthi moja kwa mtu baki itaruhusika na kujuzu. Na baadhi yao wanaona kuwa wasia kwa mrithi haujuzu kwa hali yoyote hata kama warithi wengine wataruhusu hivyo; kwani kizuizi chake hakika kimeletwa na sheria, na kama tungelijuzisha tungelikuwa tumetumia hukumu iliyofutwa na jambo hili halijuzu, kama ambavyo wasia haujuzu kwa muuaji hata kama warithi wataupitisha. [Ma'alem Assunan 85/4, Ch. Al-Matwba'ah Al-Elmiyah, Halab.]
Na Ibn Rajab Al-Hanbaliy alisema: "Na kuleta madhara katika wasia mara nyingine huwa ni kwa kuwahusu baadhi ya warithi kwa kuongeza kiwango alichomwekea Mwenyezi Mungu na wakadhurika warithi waliobakia kwa kujitengea kwake kiwango maalumu na wakati mwingine ni pale anapousia mtu baki kwa kuongeza Zaidi ya theluthi moja, na kupelekea haki za warithi kupungua, kwa hiyo Mtume S.A.W., akasema: "Thuluthi na thuluthi ni nyingi",
Na pindi mtu anapomuusia mrithi wake au kwa mtu mgeni kiasi zaidi ya theluthi moja basi wasia huo hautekelezwi isipokuwa kwa kuruhusiwa na warithi wengine, iwe kwa kukusudia madhara au bila ya kukusudia madhara yoyote, na iwapo atakusudia madhara katika wasia wa mtu baki kwa theluthi moja tu ya mali, basi atapata dhambi kwa kukusudia kwake madhara, na je wasia wake utarejeshwa ikithibitika kuwa aliupitisha yeye mwenyewe au hapana? Ibn Atwiah alisimilia usimulizo kutoka kwa Malik kwamba unarudishwa. Na lisemekana kwamba ni kipimo cha madhehebu ya Malik. [Jame.u Al-Ulum Wal-Hekam 213/2, Ch. Muasasat Aresalah, Bairut].
Ya Nne: Haki ya warithi inaambatana na mali kwa kuwepo maradhi ya kifo, na wala haijuzu kuchukua hatua yoyote nayo.
Ibn Qudamah alisema: "Suala akasema: Na atakayeweka wakfu wakati wa kuumwa kwake ugonjwa uliompotezea maisha yake, au akasema: Hii ni wakfu baada ya kufa kwangu, haitatolewa katika theluthi moja, itakuwa imewekwa wakfu kwa kiasi cha theluthi isipokuwa kwa kuruhusu warithi. Na ujumla wake kwamba kuweka wakfu katika hali ya kuwa na ugonjwa wa umauti ni kama wasia kwa kuuzingatia kuwa ni katika theluthi tu ya mali; kwani huko ni kujitolea sadaka, na kwa hiyo akazingatia katika maradhi ya kifo kuwa theluthi moja tu, kama vile kumwachia huru mtumwa au kutoa zawadi.
Na iwapo kiwango hicho kitakuwa zaidi ya theluthi inajuzu bila ya ridhaa ya warithi na itakuwa wajibu kutekelezwa, na kikizidi kiwango hicho zaidi ya theluthi moja ni lazima kusitishwa na kuwa kiwango cha theluthi moja tu, na nyongeza itategemea ruhusa ya warithi.
Katika jambo hili hatujui sisi tofauti ya wasemao kuwa ni wajibu; na hivyo ni kutokana na kuwa haki ya warithi inafungamana na mali kwa kuwepo ugonjwa; na kwa hiyo pakazuiwa kutoa sadaka Zaidi ya theluthi moja, kama vile zawadi na kumwachia huru mtumwa. [Al-Mughniy 25/6, Ch. MaKtabat Al Qaherah]
Na kutokana kwa yaliyotanguliza inadhihirisha kutojuzu kumwadhibu mtoto mlemavu au asiekuwa hivyo katika warithi kwa kumnyima haki yake ya urithi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas