Hukumu ya (Tajwidi): Kusoma Qur`an...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya (Tajwidi): Kusoma Qur`ani Vizuri.

Question

Nini hukumu ya kuisoma Qur`ani kwa Tajwidi: kusoma Qur`ani vizuri? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, Aali zake na Masahaba zake, na waliomfuata, na baada ya hayo:
Kitu kizuri katika lugha ya Kiarabu ni: kitu chenye uzuri, na Ibn Mandhuur anasema: “kizuri ni kinyume cha kibaya…, na mfano wake ni: Tajwidi”. [Lisaan Al-Arab: 3/135, Kidahizo: JA WA DA, Dar Sadir, Bairuit ].
Na maana yake ya kiistilahi ni: Kuzipa herufi haki zake, kuzipangilia ngazi zake, kuirejea herufi mahala pa kuitamka na asili yake, kuiambatanisha mfano na sura yake, kuikaza lafudhi yake, na kurahisisha kuitamka, kutokana na mfumo na sura yake, na bila ya ziada wala ukali, na upanuzi wala kujilazimisha. [At-Tamhid Fi Ilm At-Tajwid, na Ibn Al-Jazriy, Uk. 47, Ch. ya Maktabat Al-Maarif, Riyadh].
Asili ya suala hili ni: hukumu za Tajwidi zilizo zaidi ya umbo la neno la kiarabu, kwa mfano kutandaza sauti na ghuna, ambazo hazigeuzi maana ya asili ya neno katika Kiarabu, je, ni lazima au siyo?
Na rai yenye nguvu zaidi ni kuwa jambo hilo si lazima, bali lazima ni kulitamka neno kama anavyolitamka mwarabu, kadiri iwezekanavyo.
Dalili ya hayo kuwa Mwenyezi Mungu alitaja kuwa Wahyi ni kiarabu, yaani iliteremshwa kwa lugha ya Waarabu, kwa hiyo, asili ya lafudhi zake ni kiarabu, na waarabu wanazifahamu, na mwarabu alikuwa hakuzitumia hukumu kama hizi katika lugha yake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Na bila shaka tunajua kwamba wanasema: “Yuko mtu anayemfundisha” (Lakini) lugha ya yule wanayemwelekezea (kuwa anamfundisha Mtume) ni ya kigeni, na hii (lugha inayotumika katika Qur`ani) ni lugha ya Kiarabu bulbul}.[AN NAHL: 103]. Na Mwenyezi Mungu alisema: {Hakika Sisi tumeiteremsha Qur`ani kwa Kirabu ili mupate kufahamu}. [YUSUF: 2]. Na Mwenyezi Mungu alisema: {Na namna hivi tumekufunulia Qur`ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio (katika nchi zilizo) pembeni mwake}.[ASH SHURA:7].
Mwelekeo wa dalili ya Aya hii kuwa Qur`ani Tukufu imeteremshwa kwa waarabu wote kutokana na lahaja zao mbali mbali, na ilikuwa ruhusa ya kusoma namna walivyosoma makabila ya kiarabu, na hii inabainishwa kwa waliyopokea Bukari na Muslim, kutoka kwa Abdir-Rahman Ibn Abdil-Qariy, alisema kuwa: Nilisikia Umar Ibn Al-Khattab R.A, akisema: Nilisikia Hisham Ibn Hakim Ibn Hizam akisoma Suratul-Furqan namna kinyume cha nilivyosoma, wakati Mtume S.A.W, alikuwa akinisomesha, hata mimi nitake kummpinga, kisha mimi nilimwacha aondoke, kisha nilimkaba roho kwa nguo yake, nikamletea Mtume S.A.W, nikasema: Mimi nilisikia mtu huyu akisoma namna kinyume cha ulivyonisomesha, na Mtume ameniamuru (nimwache), kisha akamwambia (soma), akasoma, kisha akasema: (iliteremshwa hivi hivi), kisha aliniambia (soma), nikasoma, akasema: (iliteremshwa hivi hivi, hakika Qur`ani imeteremshwa kwa herufu saba, kwa hivyo someni kilicho chepesi humo).
Kauli yake (herufi saba) yaani kwa mujibu wa lahaja za kiarabu na vilugha vyao. Na inajulikana kuwa vilugha vya waarabu vilikuwa vikitofautiana katika baadhi ya maneno, kwa mfano (Njoo) ni ((Haluma) au (Aqbil), kwa hiyo, tofauti kubwa imedhihirika mwanzoni mwanzoni, jambo lilipelekea Umar Ibn Al-Khatwab kumpinga mwingine kwa ukali huu.
Na inajulikana pia kuwa waarabu walikuwa umma wa Ummiyah yaani hawajui kuandika, basi hakuwa budi kuwarahisishia jambo hili.
Na hii inadhihirika katika alivyopokea Abu_dawuud At-Tayalisiy katika kitabu chake, kutoka kwa Ubaiy Ibn Kaa’b, kuwa Jibrili S.A.W, alikuja kwa Mtume S.A.W, kwenye mahali pa Ahjaar Al-Mira, akasema Mtume: “Ewe Jibrili, hakika mimi nilipelekwa kwa Umma wa Ummiyah, na miongoni mwao ni mkongwe, mzee, kijana, mjakazi, na mtu wa maumbile ambaye hakusoma katu kitabu”, na Jibrili akasema: “Hakika Qur`ani imeteremshwa katika herufi saba”.
Urahisishi huu ambao unafikia kiasi cha kukiri lahaja za makabila, hata ikiwa maneno yanahitilafiana, ni mbali na akili kufikiria kuwa Tajwidi ambayo ni aina ya ziada ni lazima, kama tulivyowahi kubainisha.
Licha ya hayo, vipi ilikuwa lazima, wakati wa kuwepo tofauti za wasomaji Qur`ani katika wingi wa hivi, na kwa mifano yake ni:
Ibn Al-Jazriy anasema: “Kuhusu (Idhihaar) inakuwa pamoja na herufi sita, nazo ni herufi zinazotamkwa katika koo, miongoni mwake herufi nne zisizo na tofauti, nazo ni: Hamza, Haa, Ain, na 3 aa… kuhusu harufi mbili ambazo zina tofauti, nazo ni: Ghain na Khaa… Abu-Jaafar alizisoma kwa Ikhfaa, na mabaki ya wasomaji walisoma kwa Idhihaar”. [An-Nashr: 2/22, Ch. Ya Al-Matbaah At-Tijariyah Al-Kubra].
Pia anasema: “Kuhusu hukumu ya pili, nayo ni (Idghamu) inakuwa na herufi sita, nazo ni herufi za neno la (Ya-R-ma-l-u-n), na herufi mbili miongoni mwa hizi hutumika bila ya (Ghuna), nazo ni (Lam- Raa), kwa mfano: (Fain- Lam- Tafa’alu), (Hudan-Lil-Muttaqin), (Min- Rabbihim), na (Thamaratin-Rizqa). Hii ni madhehebu ya wataalamu wengi wa wasomaji Qur`ani, na wengi wa maimamu wa Tajwidi, na kanuni inayotekelezwa na maimamu wa miji katika nyakati zote, na wasomaji wa nchi za magharibi za kiarabu, na wengine pia, wote hawakutaja isipokuwa hii… Na wengi wa wasomaji walielekea kutumia (Idghamu) pamoja na (ghuna), wakapokelea hivi kutoka kwa wengi wa maimamu wa usomaji, kama vile: Nafii’, Ibn Kathir, Abi-Amr, Ibn Amir, Asim, Abi-Jaafar, yaa’qub, na wengineo…
Nasema: “kutumia ghuna pamoja na Lam-Raa na wasomaji wote, ambayo pia ni sahihi kwa njia ya waandishi na wsomaji kutoka kwa watu wa Hijaz, Sham, Basrah, pamoja na Hafs.
Na nikisoma kisomo hiki kutoka kwa mapokezi ya: Qalun, Ibn Kathir, Hisham, Issa Ibn Wardan, Rauh, na wengineo. Kuhusu herufi nne za neno la (Yarmalun), nazo ni Nun, Mim, Waw, yaa- yaani herfi za neno la (Ya-n-m-u), ambazo hutamkwa kwa Idghamu na Ghuna… na kuna tofauti inayohusu Waw-Yaa, ambapo hutamkwa kwa Idghamu bila ya Ghuna katika kisomo cha Khalaf, kutoka kwa Hamza. Namna hivi, kuna tofauti kwa Ad-Duriy, kutoka kwa Al-Kisaiy, inayohusu Yaa, ambapo hutamkwa na Au-Uthman Ad-Dariir kwa Idghamu bila ya Ghuna, mfano wa mapokezi ya Khalaf, kutoka kwa Hamza. Na Jaafar Ibn Muhammad alipokela kutamka kwa Ghuna, na mtungaji wa kitabu cha Al-Mubhij alitaja visomo hivi viwili, na hivi viwili ni sahihi, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa yote”. [An-Nashr: 2/ 23, 24].
Pia anasema: “Inajulikana kuwa katika madhehebu za wasomaji wa Misri, na wa Magharibi, hawa waliopokea mapokezi ya Warsh, kwa njia ya Al-Azraq, kuwa herufi ya Raa- kutokana na kuitamka- ina sehemu nne: ya kwanza: hutamkwa kwa Tafkhim, ya pili: kwa Tarqiq, ya tatu: walihitilafiana wote kwa, ya nne: walihitilaffiana baadhi kwa baadhi”. [An-Nashr: 2/91].
Kwa hiyo, kundi la wanachuoni walieleza, kama alivyotaja mtungaji wa (Sharhul-Qaul Al-Mufiid), kuwa : “Wajibu katika elimu ya Tajwidi umegawanyika katika: Wajibu wa kisheria, nao ni ukitekelezwa kuna thawabu, na ukiachwa kuna adhabu; na wajibu wa kimapokeo, nao ni kuutekeleza ni kuzuri, na kuuacha ni kubaya, pamoja na kuadhibisha aliyeuacha namna ya kuainishwa na wahusika. Basi wajibu wa kisheria ni: unavyohifadhi herufi na mabadiliko ya maneno na kuvunja maana, kwa hiyo, mwenye kuuacha ni mwenye dhambi. Na wajibu wa kimapokeo ni: waliutaja wanachuoni katika vitabu vya elimu ya Tajwid, kama vile: Idghamu, Ikhfaa, Iqlaab, Tarqiq, Tafkhim; na mwenye kuuacha si mwenye dhambi, kwa maoni ya baadhi ya wanachuoni”. [Nihayat Alqaul Al-Mufiid, na Sh. Muhammad makkiy Nasr Al-Jarisiy, Uk. 26, Ch. Ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Lakini kuna baadhi ya wanachuoni wanaona kinyume cha hivi, kama alivyotaja Ibn Al-Jazriy katika utangulizi wake akisema:
Kusoma kwa Tajwidi ni dharura na lazima
Na anayeisoma bila Tajwidi analaumika
Katika maelezo ya hayo: “kuwa Tajwidi ni wajibu wa kisheria, ambapo mtu akiuacha basi huwa menye dhambi, na rai hii ni ya wengi wa wanachuoni mafaqihi, kwa sababu Qur`ani imeteremshwa kitajwidi, na Mtume S.A.W, amepatiwa na Jibrili vilivyo, na akawasomesha masahaba, kwa hiyo, ni Sunna ya kinabii. Na miongoni mwa dalili zao kuwa ni wajibu, kauli yake Mwenyezi Mungu: {na soma Qur`ani vilivyo}. [AL MUZAMMIL: 4], na Ali Ibn Abi-Talib RA, anasema: At-Tartiil ni kudhibiti herufi na kujua vituo”. [Qawaid At-Tajwiid, na Abdul-Aziz Ibn Abdil-Fattah Al-Qariy, Uk. 40, Ch. Ya Muassasat Ar-Risalah].
Ibn Al-Jzriy alitoa dalili ya hayo kwa mfano (Mad): kutandaza herufi, akitaja Hadithi ya mlango huu, akisema: “ni lazima kutofikiriwa kuwa inajuzu kuizembea (Mad) kwa msomaji ye yote, ni kuchunguza hivi sikukuta katika kisomo sahihi wala kisicho cha kawaida, bali nimekuta ithbati ya kuitekeleza (Mad); na hii imepokewa na Ibn Masu’ud R.A, akafikisha kwa Mtume S.A.W, katika alivyoniambia Al-hassan Ibn Muhammad As-Salihiy, miongoni mwa mapokezi ya mdomo, kutoka kwa Ali Ibn Ahmad Al-Maqdisi, alituambia Muhammad Ibn Abi-Zaid Alkaraniy katika kitabu chake, Akatuambia Mahmud Ibn Ismail As-sairafiy, akatuambia Ahmad ibn Muhammad Ibn Al-Hussain Al-Asbahaniy, akatuambia Suleiman Ibn Ahmad Al-Hafidh, akatuzungumzia Muhammad Ibn Ali As-saigh Al-Makkiy, akatuzungumzia Said Ibn Mansur, akatuzungumzia Shihab Ibn Khirash, akanizungumzia Masu’ud Ibn Yazid Al-kindiy, akisema : Ibn Masu’ud alikuwa akisomesha mtu, na mtu akasoma: {Sadaka hupewa (watu hawa):− Mafakiri na Maskini}, yaani bila ya kutumia (Mad), na Ibn Masu’ud akasema: si kwa njia hii Mtume S.A.W, alinisomesha Aya, na mtu akasema: Vipi Mtume akakusomesha, ewe akina Abdur-Rahman? Akasema: akanisomesha: {Sadaka hupewa (watu hawa):− Mafakiri na Maskini}, yaani kwa kutumia (Mad). Na hii ni Hadithi tukufu ambayo ni hoja na dalili katika mlango huu, na wapokezi wa Isnad yake ni waminifu.
Na At-Tabaraniy ameipokelea katika kitabu chake: Al-Mu’jam Al-Kabiir”. [An-Nashr: 1/316], na amekubali Isnad hii Al-haithamiy katika [Majma’ Az-zawaid: 7/155, Ch. Ya Maktabat Al-Qudsiy; na S-sayutiy katika Al-Itqan; 1/333, Ch. Ya Al-haiah Al-Masriyah Al-A’amah Lil-Kitab].
Lakini dalili yao ya kuwa wajibu si nguvu, na maana ya (Tartiil) ni kupanga kwa uzuri, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: {Na wakasema walewaliokufuru: “Mbona hakuteremshiwa Qur`ani yote mara moja?” Kama hivi (unavyoona tumeiteremsha kidogo kidogo kwa mpango mzuri) ili tuuthibitishe, (tuutie nguvu) moyo wako (kwa hizo Aya mpya mpya zinazoteremka wakati baada ya wakati), na tumeipanga kwa uzuri}. [AL FURQAAN: 32].
Na washirikina wakitamani Qur`ani iteremshwe mara moja, jibu lilikuja kuashiria hekima ya kuiteremsha kidogo kidogo, na Ibn Al-Jawziy anasema: “Kauli yake Mwenyezi Mungu: {“Mbona hakuteremshiwa Qur`ani yote mara moja?”}, yaani kama zilivyoteremshwa Taurati, Injili, na Zaburi, na Mwenyezi Mungu alisema: {namna hivi}, yaani: tumeiteremsha namna hivi kidogo kidogo, kwa sababu maana ya walivyosema ni: je, mbona hakuteremshiwa Qur`ani yote mara moja? Kwa hiyo, isemwe: tumeiteremsha namna hivi {ili tuuthibitishe moyo wako}, yaani: tuutie nguvu moyo wako hata uwe na busara, kwa sababu, Wahyi ulikuwa ukija kwa Mtume kutokana na tukio na mnasaba, na hali hii ya kuiteremshwa ina nguvu zaidi kwa moyo, na nuru kwa busara, na kuepusha kungoja kwake, na {tumeipanga kwa uzuri}.Yaani: tumeiteremsha kwa njia ya Tartiil, nayo ni polepole bila ya haraka”. [Zad Al-Masiir: 3/320, Ch. Ya Dar Al-Kitaab Al-Arabiy].
Tafsiri hii ya maimamu wa Tafsiri, miongoni mwa Salaf kuhusu kauli yake Mwernyezi Mungu Mtukufu: {na soma Qur`ani vilivyo}. [AL MUZZAMMIL; 4]; Ibn Abbas anasema: ibainishe kwa uwazi. Na Al-Hassan anasema: isome kwa usomaji wazi. Na Mujahid anasema: isome polepole.
Na Qatadah anasema: ithibitishe kithibitisho. Pia kutoka kwa Ibn Abbas: isome polepole, Aya tatu au Aya nne, au Aya tano, kama ipo katika [Tafsiri ya Al-Baghawiy: 5/165, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy]. Na Al-Baidawiy katika [Tafsiri yake: 5/255, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy] anasema: “Isome polepole na kudhihirisha herufi, ambapo msikilizaji anaweza kuziendeleza”.
Kuhusu mapokezi ya Ali R.A, katika tafsiri ya Aya, hatukuikuta kwa Isnad, lakini wanachuoni wa Tajwidi wanaisimulia katika vitabu vyao. Na hata ikiwa ni sahihi, basi kudhibiti herufi hakumaanishi vlivyoongezeka nazo kama vile: (Mad) au (ghuna), na ilivyotilia nguvu rai hii kuwa alisema katika mapokezi: (kujua vituo), na matumizi ya vituo kupitia maana ya istilahi huenda kufahamisha kuwa wajibu, lakini hii si makusudi hapa, kama ilivyotumiwa.Na Ibn Al-Jazriy anasema: “Zinduzi: (kwanza) kauli ya maimamu: Haijuzu kuachana, katika kusoma, kati ya majina mawili yanayoambatana, kitenzi na mtendaji wake, mtendaji na mtendwa, kiima na prediketa, n.k., na hii haimaanishi kuwa ni haramu au makuruhu, bali wanakusudia kituo katika hali ya hiari.
Pia hawakusudii kukataza kituo hata kidogo, lakini inajuzu katika hali ya dharura, kama vile hali ya kufunza, kutahini, isipokuwa hali ya kusudi kubadilisha maana na mwelekeo wake, kinyume cha maana anayeitaka Mwenyezi Mungu, hapo basi ni haramu, na ni lazima kumkataza kwa mujibu wa kanuni za Sheria inayotakasika, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa yote”. [An-Nashr: 1/230]. Hapo ni wazi kuwa dalili hii haisaidii katika dai la wajibu.
Kuhusu mapokezi ya Ibn Masuud, aliitaja Said Ibn Mansur katika tafsiri yake, na Said alisema: akatuzungumzia Shihab Ibn Khirash, akanizungumzia Musa Ibn Yazid Al-kindiy, akisema : Ibn Masu’ud alikuwa akisomesha mtu, na mtu akasoma: {Sadaka hupewa (watu hawa):− Mafakiri na Maskini},yaani bila ya kutumia (Mad), na Ibn Masu’ud akasema: si kwa njia hii Mtume S.A.W, alinisomesha Aya, na mtu akasema: Vipi Mtume akakusomesha, ewe akina Abdur-Rahman? Akasema: akanisomesha: {Sadaka hupewa (watu hawa):− Mafakiri na Maskini}, [AT TAWBAH:60] yaani kwa kutumia (Mad). [Tafsiir said ibn Mansuur: 5/257, Ch. ya As-Sumaiiy lin-Nashr wat-Tawzii].
At-Twabaraniy ameipokea, akisema: Muhammad Ibn Ali As-Saiygh, alituzungumzia Said Ibn Mansur, akatuzungumzia Shihab Ibn Khirash, akanizungumzia Musa Ibn Yazid Al-kindiy, akisema : Ibn Masuud alikuwa akisomesha mtu, na mtu akasoma: {Sadaka hupewa (watu hawa):− Mafakiri na Maskini}, [AT TAWBAH: 60], yaani bila ya kutumia (Mad), na Ibn Masuud akasema: si kwa njia hii Mtume SAW, alinisomesha Aya, akanisomesha: {Sadaka hupewa (watu hawa):− Mafakiri na Maskini}, [AT TAWBAH: 60] yaani kwa kutumia (Mad). [Al-Mu’jam Al-kabiir: 9/137, Ch. ya Maktabat Ibn Taimiyyah, Cairo].
Tumetaja mapokezi mawili kwa Isnad yake, kwa kuwepo tofauti katika Isnad, iliyotajwa katika (An-Nashr) ni Masuud Ibn Yazid, na katika (At-Tafsiir na Mu’jam At-Tabaraniy) ni Musa ibn yazid, ambaye ni sawa. Kuhusu Musa, mhakiki wa (Tafsiir Said Ibn Mansuur anasema: kuwa yeye ni hajulikani. Hata akiwa yeye aliyetajwa katika wapokeji wa Ibn Hibban, lakini, kutokana na sira yake hakuna ishara kuwa akutane na Ibn Masu’ud.
Huenda hii ni sababu ya kusema kwa wanasunna kuwa: wapokeaji wake ni waaminifu, bila ya kusema kuwa: Isnadi yake ni sahihi kwa uwazi, na kama inajulikana kuwa wapokeaji ni waaminifu haimaanishi kuwa: Isnadi ni sahihi, kwa sababu huenda kuwepo baadhi ya kizuizi katika Isnad.
Kuhusu matini ya mapokezi: hatuwezi kufahamu zaidi isipokuwa namna ya kusoma kwa njia hii ni kujuzu au kitu kizuri tu.
Twaweza kuangalia katika mlango huu, ilivyotolewa na Al-Hafidh Ibn Hajar, katika muktadha wa maelezo ya baadhi ya masuala ya Tajwidi, yale yanayostahiki kuandikwa kwa maji ya dhahabu, ambapo akisema: “Imeenezwa katika enzi yetu kuwa kundi la wasomaji Qur`ani wanakanusha hivi, hata baadhi yao waeleze kuwa ni haramu, kwa hiyo, baadhi ya wanachuoni walidhani kuwa wao wana dalili, na kwa ajili ya hayo waliwafuata, na wakasema: wahusika wa kila fani ni wajuzi wa fani yao! Lakini hii ni upotovu kwa aliyeisema, kwa kuwa elimu ya halali na haramu hakika ichukuliwe na wanachuoni tu”. [Fath Al-Bariy: 9/38].
Kwa mujibu wa yale yaliyotangulia, inabainika kuwa tekelezo la msomaji Qur`ani na hukumu za Tajwidi zinazozidi asili ya kutamka maneno ya kiarabu, ambapo kuziacha hazibadilishi maana ya maneno ya asili, si wajibu, katika rai yenye nguvu zaidi, lakini ni jambo la hiari. Hakika wajibu ni: kutamka maneno namna anavyoyatamka mwarabu, kadiri iwezekanavyo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas