Kuosha Macho Katika Twahara.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuosha Macho Katika Twahara.

Question

Je, ni wajibu kuosha macho katika twahara kisharia, kwani mimi navaa lensi ya macho, je, ni wajibu kuiondoa lensi wakati wa twahara kisharia?  

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu..
Macho ni kiungo cha ndani mahali pake usoni, na ni faradhi kwa makubaliano ya wanachuoni kuoshwa katika twahara ndogo au twahara kubwa,kwa hivyo baadhi ya wanachuoni wa Fiqhi waliona ni wajibu kuliosha jicho katika twahara.Kutokana, na hayo ni wajibu kuiondoa lensi ya macho wakati wa twahara hata pasiwepo kizuizi cha maji kwa baadhi ya sehemu ya macho wakati wa udhu.Kwani sharti la udhu sahihi ni maji lazima yaoshe sehemu zote za faradhi za kutawadha kwa mujibu wa rai hii.
Na rai sahihi katika suala hili ni kwamba hakuna sharti la kuosha ndani ya jicho bali wala hata sharia ya kuharamisha kuvaa lensi ya jicho katika twahara ya kisharia, ikiwa ni lensi ya kimatibabu au lensi ya pambo.
Na dalili ya hayo ni kwamba Mtume (S.A.W) hakusema kwa kulazimisha kuingia maji ndani ya macho wakati wa twahara kwa kauli au kitendo na pia kuna ugumu wa kufanya hivyo kwani kuosha ndani ya macho kunasababisha madhara juu ya macho na tunaamrishwa kujiepusha kufanya jambo hili. Na hatuwi mbali kulitaja jambo hilo kuwa ni kukalifisha jambo la ziada juu ya mambo ya sharia na hiyo ni mambo yasiyofaa Kisharia.
Na tulivyotaja hapo ni madhehebu ya jumuhuri ya wanachuoni wa zamani na wa sasa na hii ni rai ya sahihi katika madhehebu manne ya kiislamu.Na zaidi ya hayo,Al-Serkhesiyy alisema katika kitabu cha: [Al-Mabsout] na hiki ni miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Al-Hanafiyah [1\6 Ch, Dar Al-Maarifah]: “Halafu anasha uso wake mara tatu”, na mipaka ya uso ni kutoka sehemu ya nywele mpaka chini ya kidevu na masikio mawili ;kwani uso ni jina kwa vile inavyoviangalia,na kuingia maji katika macho mawili haikuwa ni sharti katika twahara;kwani macho ni kama mafuta hayakubali maji,na pia ni vigumu,na aliyejikalifisha jambo hili miongoni mwa swahaba za Mtume S.A.W., hatoweza kuona kwa macho yake mwisho mwa umri wake kama Ibn Omar na Ibn Abbas R.A..
Na Al-Qadhi Sanad Al-Malikiy alisema: “Viongozi wote wa madhehebu waliafiki juu ya kutokuwa na haja ya kuosha ndani ya macho mawili,na Ibn Omar alifanya jambo hili mpaka (akawa kipofu) hakuona mwishoni mwa maisha yake”. [Mawaheb Al-Jalil Fi Sharh Mukhtaswer Khalil 1\191.Ch. Dar Al-Fikr].
Na Al-Khatweb Al-Sherbiniy alisema katika kitabu chake cha: [Mughni Al-Muhtaaj] na hiki ni miongoni mwa vitabu vya Al-Shafiyah [1\172. Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah): “Uso mahali pake ni mbele na macho katika sehemu hii ya mbele,na anasema kwa dhahiri ya ufahamu wake,kwa maana kuosha ndani ya mdomo , pua na macho,kwani hakupendelewi kuosha ndani ya macho, bali baadhi walisema kuwa ni karaha ya kuosha ila ikiwa hakuna madhara”.
Na Al-Bahutiy alisema katika kitabu chake cha [Kashaf Al-Qinaa] na hiki ni miongoni mwa vitabu vya Kihanbali (1\96, Ch. Dar Al-Fikr]: “(Si wajibu) kuosha ndani ya jicho (bali haikuwa sunna kuosha ndani ya jicho kwa mwenye hadathi dogo au kubwa. Alisema hivyo katika kitabu cha: [Al-Sharh] na kinginecho; kwani Mtume S.A.W., hakulifanya jambo hili wala kuliamuru litedwe (Hata ikiwa hakuna madhara,bali ni makruhu) kwani kuna madhara yake. Na ilisimuliwa kwamba Ibn Omar alipoteza nuru ya macho yake kwa sababu ya kuingia maji mengi ndani ya macho yake”.
Na kwa upande mwingine kuna wanachuoni wachache wamependelea kuosha ndani ya macho, na baadhi yao walisema kuwa ni wajibu, na baadhi walisema kuwa ni wajibu wakati wa janaba tu.
Al-Emraniy alisema: “Ama kuingiza maji ndani ya macho :sio wajibu….na miongoni mwa rafiki zetu walisema :inapendeza kwa ilivyopokelewa kutokana na kusemwa kwamba Ibn Omar alikuwa akiyaosha macho yake mpaka akapofuka. Na rai ya kwanza ni sahihi zaidi” [Al Bayan 1\118, Ch. Dar Al-Menhaj, Jedah].
Na Al-Medawiy alisema: “Dhahiri ya maneno ya Al-Moswanef: Ni wajibu kuosha ndani ya macho,na usimulizi huu kutoka kwa Ahmad kwa sharti la kutokuwepo madhara… na usahihi miongoni mwa madhehebu ya wengi miongoni mwa wanachuoni wa jamhuri ya maswahaba na wengi wao walisema kwamba: Si lazima kuyaosha macho ndani yake kamwe,hata ikiwa kwa sababu ya janaba.Na kwa hivyo kuosha ni wajibu kwa twahara kubwa ….na rai ya madhehebu nyingine inasema:Haipendezwi kuosha ndani ya macho,hata ikiwa hakuna madhara juu ya macho,bali ni makruhi ya kuosha ndani ya macho…na wengine walisema kuwa: Inapendezwa kuyaosha macho ikiwa hakuna madhara…na wengine walisema kwa kupendeza kuosha ndani ya macho katika janaba tu,ama udhu yasioshwe”. [Al-Inswaf 1\155, Ch. Dar Ihyaa At-Tutath Al-Arabiy).
Na watu hawa hawakutaja hoja yao yoyote na ikiwa tutalifuatilia hilo kwao hatutakuta kwao isipokuwa ujumla wa tamko tu.
Na rai yetu ni kwamba yaliyojificha si katika uso;kwani hakuelekeani nako nayo ni kama ndani ya mdomo na pua kwa wale wanaosema kutowajibika kuyaosha katika twahara,ama watu wakiwa na dalili ya kitendo cha Swahabu wa Mtume S.A.W., Ibn Omar R.A., jamhuri ya wanachuoni hawakukichukua kitendo hicho kama ni hoja ya kutenda. Pia anasema kwa rai hii pekee kama yalivyoandikwa na kutajwa katika vitabu vya wanachuoni wa Hadithi na Fikhi.Kwa hivyo Malik alisema: Si lazima kufanya jambo hilo na yapasa kupeleleza watu wa Madina katika kazi zao kwa wawezavyo.
Na Abdulrazeq alisema kutoka kwa Abdulahi Ibn Moammar kutoka kwa Nafea kutoka kwa Ibn Omar alisema: Alikuwa akiosha kutokana na Janaba anaweka maji katika macho yake na juu ya kidevu chake .Alisema; Abdullahi alisema: “Sijui hata mtu mmoja ameweka maji machoni ila Ibn Omar. [Al-Moswanef 1\259, Ch. Al-Majles Al-Elmiy, India).
Muhamad Ibn Al-Hassan alisema katika riwaya yake katika kitabu cha: [Al-Mowatwa] cha Imam Malik kwa urefu, halafu Muhamad alisema: “Tunazichukuwa rai zote ila rai ya kuweka maji machoni, kwani kuweka maji machoni si wajibu juu ya watu katika Janaba,na rai hii ni rai ya Abu Hanifah na Malik Ibn Anas na Jamhuri ya Wanachuoni. [Al-Mowatwa, Uk 45, Ch. Al-Maktabah Al-Elmiyah].
Na Al-Baihaqiy alitaja katika kitabu chake kutoka kwa Ashafiy, Malik alisema kutoka kwa Nafea kutoka kwa Ibn Omar alkuwa: “Akiosha kutokana na Janaba aliingiza maji machoni . Malik alisema: Si lazima kufanya hivyo na Ashafiy alisema pia: “Si lazima kuweka maji machoni, kwani macho si dhahiri juu ya mwili wake”.
Na kutokana na dalili zilizotajwa hapo juu pamoja na upinzani wa jamhuri ya wanachuoni wa zamani na wa sasa kuhusu karaha ya kuosha ndani ya macho, imekuwa ndio dalili ya uteuzi wetu sahihi , kwa hivyo Ibn Qudamah alisema juu ya ukaraha wake; anaposema: Rai sahihi si lazima kuosha ndani ya macho katika udhu au kuoga;kwani Mtume S.A.W., hakulifanya, wala kuliamuru kwayo, na lina madhara, na lililotajwa juu ya Ibn Omar ni dalili ya karaha yake; kwani jambo hili lilisababisha kumpofua; na kitendo kinachohofiwa kuondoa nuru ya macho au upungufu wake katika kisichofuata sharia isipokuwa ni haramu hakiwi chini ya kuwa makuruhu. (Al-Mughniy 1\80, Ch. Maktabet Al-Qahirah].
Na kutokana na yaliyotangulia ni wazi sana si lazima kuosha ndani ya macho katika twahara zote mbili kubwa na ndogo- yaani kuoga na udhu-na hii ni rai sahihi ya miongoni mwa madhehebu ya jamhuri ya wanachuoni,kama ambavyo rai sahihi ni makuruhu ikisababisha madhara kwa macho japo kidogo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas