Uchaguzi wa Rai kwa Ajili ya Kuchu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uchaguzi wa Rai kwa Ajili ya Kuchunga Masilahi.

Question

Mwanachuoni huenda akatoa fatwa kwa rai na kujenga hoja ya kile alichokitolea fatwa ni kwa sababu ya masilahi au kuwa fatwa hiyo italeta maslahi, basi ni nini vigezo vya maslahi ambavyo yafaa kuipa nguvu kauli yake? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Maana ya Masilahi katika lugha ni: manufaa ni neno linalotokana na neno “nufaika” au faida ya jambo fulani, na neno masilahi ni kinyume cha neno ufisadi, na inasemwa: amefanya marekebisho, kinyume na neno ameharibu, amekifanyia marekebisho kitu ni baada ya kuharibika kwake, kwa maana ya kukisimamia na kukirekebisha kinyume na uharibifu, na masilahi: pia ni manufaa. Na neno masilahi lina maana mbili katika lugha:
Maana ya Kwanza: Ni manufaa kwa uwiyano na kwa maana.
Maana ya Pili: Ni kitendo ambacho ndani yake kuna maslahi na manufaa, kwa maana ya kunufaika nacho [Tazama: Lisan Al-Arab: 2\516, Mada: S.L.H, Ch. Dar Swader, na Mukhtar As-Swahah Uk. 178, Mada: S.L.H. na Al-Muswbah Al-Muneer 1\345, Mada: S.L.H. Al-Maktabah Al-Elmiyah, na Al-Muo’jam Al-Waswet Uk. 520, Ch. Dar Al-Dawuah].
Na neno maslahi katika maana ya Istilahi ya kisharia halipishani na maana ile ya kilugha, lakini maana yake katika Istilahi lina maana ya kina zaidi kuliko maana ya kilugha, kwa hivyo inawezekana kuelezewa dhana ya masilahi katika Istilahi kuwa: ni manufaa yanayokusudiwa na Mwenyezi Mungu Mwingi wa hekima kwa waja wake katika kuhifadhi Dini yao, nafsi zao, akili zao, kizazi chao na mali zao kwa mujibu wa taratibu maalum kati yao, kwa hivyo kila kinachohifadhi vyanzo hivi vitano basi hicho kinaitwa ni masilahi, na kila kinachokuwa kinyume na vyanzo hivi hicho ni kiharibifu (uharibifu/ufisadi) na kukiondoa ni maslahi au manufaa [Al-Mustaswfa Lil Ghzadliy: 1\174, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] na kutokana na hayo tunaweza kusema kwamba kila kitu chenye manufaa ni sawa sawa kikiwa ni chenye kuleta manufaa au kwa kuondoa na kuepusha madhara basi pia kinastahiki kuitwa masilahi [ Rejea kitabu cha: Resalah Fi Re’ayat Al-Maswelaha Lil Twfiy: Uk, 25, CH. Ad-Dar Al-Masweriyah Al-Lubnaniyah, na Dhawabetw Al-Maswelaha Fi As-Shariah Al-Islamiyah kwa Dakt./ Al-Butwiy, Uk. 23,Ch. Muasaset Ar-Resalah].
Na Wanachuoni wa Usuul wamegawanya masilahi kwa namna nyingi mbali mbali, lakini muhimu kwetu ni aina mbili:
Ya kwanza ni: kugawanyika kwake kwa kuzingatia nguvu yake yenyewe.
Ya pili ni: kugawanyika kwake kwa kuzingatia msingi wa sharia yake.
Hugawanyika masilahi kwa msingi wa kwanza kuna sehemu tatu:
1) Masilahi ya lazima: nayo ndio ambayo lazima yawepo katika kuimarisha maslahi ya Dini na dunia kwani pindi yakikosekana masilahi ya dunia hayotosimama imara isipokuwa yatasimama kwenye misingi ya uharibifu na kukosa maisha yaliyo na mafanikio, na siku ya mwisho pia kukosa kuokoka kwa neema na kupata hasara.
2) Masilahi ya haja: nayo ni yale yanayokosekana kwa upana wake kuondoa shida ambazo mara nyingi zinapelekea kwenye matatizo kwa kukosa kinachohitajika, ni kama vile wepesi wa safari, maradhi, uhalali wa kuwinda, kustarehe na yaliyo mazuri miogoni mwa yale yaliyohalali katika kula kunywa kuvaa na makazi.
3) Masilahi ya kimaendeleo: nayo ni kuchukuwa yanayolingana miongoni mwa desturi nzuri na kuepuka hali za uchafu wa mambo ambayo hayakubaliki na akili za watu wenye akili, yote yanakusanyika katika sehemu ya maadili mema kama vile usafi, kustiri uchi, kujipamba vizuri, kujiweka karibu na ibada za hiyari, adabu za kula, kunywa na kuvaa, kutofanya ubadhilifu katika kula kunywa na kuvaa. [AL-MUWAFAKAT Lil Shatwebiy 8-12, Ch. Dar Al-Marifah].
Msingi wa pili wa masilahi umegawanyika sehemu tatu:
1) Masilahi yanayozingatiwa kisharia: nayo ni yale yamezingatiwa na sharia na kuwepo kwa dalili na tamko au makubaliano ya wanachuoni juu ya kusimamiwa kwake na sharia, mfano ni kama vile kuhifadhi akili kunako kusudio la kuharamishwa kunywa mvinyo, na kuhifadhi nafsi kunako kusudiwa uwepo wa sharia ya kulipa kisasi kwa uuaji wa makusudi, na pia uhalali wa sharia ya dhamana ya kuhifadhi mali ambayo ndio makusudio yanayozingatiwa kisharia. Sharia inapotamka juu ya hukumu fulani na kuongoza kuonesha uwepo wa kasoro ambayo inafungamana na hukumu hiyo, ikiwa kufungamana huku kunapelekea kufikiwa kwa masilahi yanayokusudiwa na sharia basi masilahi haya ni yenye kuzingatiwa, na kila tukio tumekuta ndani yake kuna kasoro hii au ila hii imethibiti basi yafaa kuitia kasoro hukumu hiyo, na kufaa kwa hukumu katika tukio la mfano wa hili ni kutokana na kasoro au ila iliyopo na wala si kwa upande wa masilahi.
2) Masilahi yanayofutwa na sharia: nayo ni yale sharia imeona ubatili wake na kutoyazingatia kwa tamko au makubaliano ya wanachuoni, na baadhi ya Wanachuoni wa Usuul wanayaita “Mnasaba mgeni” na mfano wa aina hii ni kusema kuwepo usawa kati ya ndugu wa kiume na wa kike katika mirathi, kwa sababu ya kuwepo undugu unaowakutanisha kati yao, basi maana hii imefutwa kwa kauli yake Mola Mtukufu: {Na wakiwa ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamume atapata sehemu iliyo sawa na ya wanawake wawili. Mwenyezi Mungu anakubainishieni ili msipotee, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu} [AN-NISAA: 176].
Na katika mgawanyo huu unahusisha kila kinachodhaniwa ndani yake kina masilahi isipokuwa ikiwa sharia imetamka au kauli ya wanachuoni wamekubaliana kutozingatiwa kwake.
3) Masilahi yaliyonyamaziwa: ambayo sharia haijayazingatia au kuyafuta lakini yanakubaliana na makusudio ya sharia katika kuleta masilahi au kuondoa madhara, nayo yanaitwa kwa jina la Masilahi ya kupelekea.
Na sehemu hii ya tatu ya masilahi inazingatiwa kuwa ni sehemu yenye tofauti kwa Wanachuoni wa Usuul, baadhi yao wanasema usahihi wa hoja yake na wengine wanakataa, na baadhi yao wapo kati ya hawa na wale, wale wa kati ya hawa na wale wametaja vigezo vya kuzingatiwa kwa masilahi ya kupelekea ndio sahihi kwa kuzingatia hukumu zilizopatikana kupitia masilahi hayo, ambapo hayawi yenye kuzingatiwa isipokuwa pale yanapokuwa yamefungamanishwa na vigezo, na yafaa pia kuyawekea vigezo vya kupewa kipaumbele kwani kipaumbele ni sehemu ya kuzingatiwa.
Miongoni mwa vigezo hivi: ni kuwa masilahi yanaendana na makusudio ya Mweka sharia [At-Taqrir wa Al-Tahbiir; 3\153, Ch. Al-Matwba’ha Al-Amiriyah, wa Al-Muwafqat 3\47] na makusudio ya sharia yanakusanya mambo yaliyo muhimu haja na uboreshaji, Az-Zinjaniy anasema: “Shafiy -Mwenyezi Mungu Amrehemu– alisitiza kuwa kushikamana na masilahi yanayofuata sharia nzima hata kama masilahi hayo hayakuegezwa sehemu maalumu ya sharia basi yafaa” [Takhriij Al- Furuue Ala Al- Uswul: Uk: 320 Ch. Muasasat Ar- Resalah] na baadhi ya Wanachuoni wa Usuul kama Ibn Al-Hajeb anaita masilahi ya kupelekea yanayokubaliana na hayo makusudio ya sharia kuwa ni: “Masilahi ya kupelekea yanayokubaliana” ili kutenganisha na Masilahi ya kupelekea mageni ambayo ni yenye kukataliwa kabisa kwa makubaliano ya wote [Bayan Al-Mukhtaswer Lil- Aswfahaniy: 3\126 Ch. Kuliyat As-Sharia’h wa Ad-Derasat Al-Islamiyah Bi Jame’at Ummu Al-Quraa. Na Al-Taqrir wa At-Tahiyer Li Ibn Amiir Al- Haajji 3\153. Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]. Maana ni kuwa: sharti za kukubaliana kati ya masilahi ya kupelekea na makusudio ya sharia kwenye jumla ambapo haikataani katika msingi miongoni mwa misingi yake wala dalili katika dalili zake, ambapo masilahi yanakuwa katika jumla ya masilahi mapama ambayo Mwana sharia amekusudia kupatikana kwake, au kufikia karibu nayo, na wala sio mageni japokuwa yatakuwa hayana dalili maalumu ya kuzingatiwa.
Na miongoni mwake: ni kwamba masilahi yasipishane na tamko kutoka ndani ya Qur`ani Sunna Makubaliano ya Wanachuoni au kipimo na ulinganisho ulio sahihi: tamko la maandiko kutokana na kupokelewa kwake na dalili zake lina maana mbili: tamko la moja kwa moja, na tamko la udhanifu.
La Kwanza: ni tamko la moja kwa moja kuthibiti kwake na dalili zake, na masilahi yanayojengewa hoja na mwenye kujitahidi haifai kupingana na tamko la wazi la moja kwa moja, hii ni kwa sababu ya masilahi kwa maana hii inajengeka kwa misingi ya dhana ni sawa sawa masilahi ya mbali yenye dalili au hayana dalili, yakiwa ni ya dhana na yakawa na ushahidi au dalili ya kuwa kwake ya mbali basi yenye hayatokuwa na nguvu juu ya kupingana na tamko la wazi, hii ni kwa sababu ya kutowezekana kukutana sehemu moja kati ya kufahamika kitu na kukidhania, kwani masilahi yanayotegemea dhana yanaitwa masilahi yasiyo kweli hivyo tamko linapewa nafasi zaidi bila ya shaka yeyote, mfano wa hilo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu {Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba} [AL-BAQARAH: 275.]
Tamko hapa la wazi na la moja kwa moja limethibiti, na lenye dalili ya wazi juu ya tofauti kati ya kuuza na riba katika uharamu, hakuna athari kwa masilahi yeyote ya dhana inayokwenda kinyuma na andiko hili.
La Pili: ni andiko la dhani na hatua zake, nalo ndio ambalo linaonesha maana zaidi ya moja, kazi ya mwenye kujitahidi ni kukusanya maana hizo ambazo zinachukuliwa na andiko, kisha kuzifanyia kazi ya kuangalia maana iliyokaribu zaidi na masilahi halali, wala hakuna tatizo hapa kupingana masilahi katika hali fulani tofauti na hiyo maana iliyochukuliwa sawa na masilahi, lakini kilichozuiliwa hapa ni kupingana masilahi na dalili zote za andiko kidhana, kwa sababu kupingana na dalili zote za andiko za kidhana ni kama kupingana kwa andiko la wazi la moja kwa moja, masilahi yanapopingana na dalili zaote za kidhana basi hukumu yake ni kama hukumu ya kupinga dalili ya wazi iliyothibiti, na katika hilo kwa mfano haifai kupingana na dalili hedhi na muda wa utohara kwa kauli ya tatu, kwa lengo la kuleta masilahi kwa mwanamke au mwanaume.
Na pia haifai kupishana maana mbili za ugusaji zilizokuja katika aya ya kugusa au kuingilia, haifai kuja na mtazamo wa tatu, na yasiyokuwa hayo katika maana zinazo chukuliwa kwenye andiko la kidhana ambalo haifai kulijengea hoja nyingine kwa sababu tu ya kudhaniwa masilahi au kudhaniwa kwa dhana dhaifu.
Ama kauli za wanachuoni zilizokubaliwa zinagawanyika kwa kuzingatia nguvu yake kuwa kauli ya wazi ya moja kwa moja na kauli ya dhana.
Kauli ya Kwanza: ni mfano wa makubalianao ya Masahaba yaliyopokelewa kwa idadi kubwa ya wapokezi, na kauli ya wanachuoni kwa yale yanayofahamika katika Dini kuwa ni muhimu, aina hii ya kauli ya wanachuoni haibadiliki kwa sababu ya masilahi hata yawe ni masilahi halali kwa aina gani na hata yakiwa masilahi hayo yanaingia akilini namna gani, kwani kauli ya wazi ya wanachuoni ni kama andiko la wazi la moja kwa moja.
Kauli ya pili: ni kama kauli ya wanachuoni ya kunyamaza ambayo dhana kubwa iliyopo ni kukubaliana kwao wote, ikiwa kauli ya wanachuoni inasimama kwa hukumu ya yenye kubadilika badilika kwa kubadilika hali au mazingira au kauli iliyojengewa juu ya msingi wa masilahi ya wakati na wala haijathibiti kubakia na kuendelea kwake, kauli hiyo inakubali kufanyiwa marekebisho kwa mujibu wa masilahi yanayo ibuka, na kwa mujibu wa makubaliano mengine pia ya kuwa ni ya kuendelea na wala si ya kubadilika.
Ama kiasi: ni usawa wa sehemu ya asili katika kasoro ya hukumu yake, na kasoro hii inakubaliana na hukumu iliyowekwa kwa ajili yake, ambayo Wanachuoni wa wanaita “kukubaliana” na inatofautiana viwango vyake kwa tofauti ya mazingatio yake au kufutwa kwake kisharia, ambapo kuna wasifu umezingatiwa na Mweka sharia, na wasifu uliofutwa, na wasifu mwingine haujazingatiwa wala kufutwa, katika hali ambayo wasifu unazingatiwa na sharia, basi mazingatio yanakuwa na sura tofauti, wakati mwingine wasifu unakuwa ni wenye kukubaliana wenye andiko la wazi.Na makusudio ya kuelezea mgawanyiko huu unaokubaliana ni kufahamu yanayokubalika kutoka yale mengine yasiyokubalika, na kufanya kiasi “uwiano” na kuupa nguvu kati ya uwiano na masilahi pale panapo tofautiana, nakuonesha tofauti ya masilahi katika mtazamo wa sharia kwa tofauti ya mazingatio ya kisharia, na kutokana na hayo ikiwa masilahi ya kupelekea yanapingana na kiasi au uwiano uliojengeka juu ya msingi wa kasoro na kukusanya wasifu wa masilahi basi masilahi yatakuwa ni sahihi kupingana na kiasi, au kupingana na masilahi mengine yenye uzito zaidi.
Na miongoni mwake: ni kuwa kuyafanyia kazi katika mambo yasiyokuwa ya ibada, kwani amri za kisharia zipo aina mbili: ibada na desturi, na asili katika ibada kwa mtu aliyepewa amri ya kutekeleza ni kufuata bila ya kuangalia maana ya amri hiyo – kwa maana kasoro - na asili ya mambo ya desturi ni kuangalia maana zake [Al-Muwafaqat :1\285] na sehemu ya kufanyiwa kazi masilahi ya kupelekea ni katika mambo ya desturi na yanayofungamana na namna ya kushirikiana na watu wao wenyewe kwa wenyewe, na wala si katika ibada ambazo hazina sehemu ya kuingiza rai, na inazingatiwa ibada ni kila kilicho na maana ambayo akili haina njia wala upenyo wa kufahamu masilahi yatokanayo, kama vile makadirio ya mipaka ya Mwenyezi Mungu amri za miradhi na yanayo fanana na hayo, lakini huenda mtu anaweza kuwa na rai katika baadhi ya njia ama vitendo vinavyosaidia mtu ili kufika kwenye matakwa na amri za Mwenyezi Mungu kwa mfano kutumia baadhi ya vyombo vya kisasa ili kujua upande wa Qibla na wakati wa Swala.
Na miongoni mwake pia ni: yasipingane masilahi mengine muhimu zaidi, katika nguvu au upendeleo, ama yakipingana na yakawa ni yenye kuhifadhi masilahi haya mawili katika tofauti ya mtazamo, kama vile ikihifadhiwa moja wapo kwa umuhimu wake na nyingine kwa hitajio lake, basi hutangulizwa lile lenye kuhifadhi umuhimu, na vile vile hutangulizwa lile lenye kuhifadhi mahitajio ikiwa usawa wa hilo ni kuhifadhi maendeleo, ama yakiwa ni sawa sawa bila ya tofauti kati yao katika kiwango cha umuhimu wake basi yataangaliwa mambo mawili: kiwango cha kuenea kwake, kwani masilahi ya umma yanatangulizwa zaidi kuliko masilahi binafsi, na katika kusisitiza upande wa kutoka matokeo yake, masilahi ya uhakika yanatangulizwa zaidi kuliko masilahi ya kudhaniwa.
Kwa kuchunga vigezo hivi ni kuepukana mwanachuoni na kupotea katika hukumu zake juu ya matendo, haingii kwenye batili isipokuwa pale anapopuuza katika kufuata vigezo hivi, au kutoviangalia kwa undani zaidi katika usahihi wake, hivyo basi kuteua masilahi kwa sura hii si kazi nyepesi, na huzingatiwa hilo ni katika sehemu zinazo ibua tofauti katika baadhi ya maswala, ama yule aliyefikia kuwepo kwa masilahi na akahukumu kwa upendeleo wake atakuwa ametoa Fatwa ya kufaa, na asiye ona hivyo atakuwa amezungumza kinyume.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas