Kusamehe Mirathi Kabla ya Kufa.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusamehe Mirathi Kabla ya Kufa.

Question

Ninataka kumwoa mwanamke kwa sharti la kumwandikia kila mmoja wetu kwa mwingine kuacha na kusamehe urithi kutoka kwake atakapofariki. Basi, jambo hilo linajuzu? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Kuna watu wanaotaka kuoa ndoa ya pili, na wala hawataki kushirikisha isipokuwa familia yake ya kwanza katika urithi; mpaka wasije wakashitushwa na ndoa baada ya kufariki kwake katika hali ya kuwa ndoa ya pili haijulikani kwa familia ya kwanza, au hata isije kuwa kizuizi cha kukubaliwa na familia yake ya kwanza kama wanaijua, na huwenda pakawepo sura nyingine zinazowasukuma baadhi ya watu kufanya kitendo hicho ambacho mtu analibeba jukumu lake.
Na katika hali hii inazingatiwa kuwa ni uondoshaji wa haki kabla ya uwepo wa sababu ya kuwepo haki hiyo; kwani mrithi haki yake ya kurithi inatoweka kabla ya mrithiwa kufariki. Na hukumu iliyopo kwa hali hii inakuwa ni kutojuzu; na kwa kutohesabika kwa kusamehe huku.
Na dalili ya hayo ni mauti ya mrithiwa ni sababu ya kwenda mirathi kwa mrithi. Na inaeleweka kuwa sababu ndio iliyofanywa na sheria ya Kiislamu kuwa kama alama ya msababishaji na mfungamano wa kuwepo msababishaji au kutokuwepo kwake. Na kwa hivyo kuwepo kwa sababu kunalazimisha kuwepo kwa msababishaji na kutokuwepo kwake pia kunasababisha kutokuwepo sababu,. Na hilo ni jambo dhahiri na thabiti, sheria ya Kiislamu ililijaalia jambo hilo ni alama juu ya hukumu ya kisheria nao ni msababishaji, kuwepo kwa sababu kunawajibisha uwepo wa msababishaji, na kukosekana kwake ni kutokuwepo kwa msababishaji, na hili ni jambo la wazi lenye kushikika na limewekwa na sheria kama alama ya maamuzi ya kisheria.
Ibn An-Najaar amesema: “Kuzungumziwa hali maalumu ni maelezo” kwa Istilahi ya wanazuoni wa ‘Usuul (Mizizi ya Elimu) ambayo sio Insha.
Ni kama vile mirathi inaingia kwenye mikono (dhima) ya warithi kwa nguvu kwa maana ya ulazima ambao hawezi kuukwepa na wala sio kwa kuchagua kama vile zawadi au wasia kwa mfano mwenye kupewa zawadi na mwenye kuusiwa anamiliki uwezo wa kuitoa mali yake au kutoikubali.
Na kwa mfano wa hayo walieleza baadhi ya wanazuoni, basi, katika kitabu cha: [Radu Al-Mukhtaar 758/6, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]; “Tamko lake au kwa dharurah” yaani mirathi, na uchaguzi kama vile, kuuza au kununua, na kukabidhi zawadi au wasia”.
Na suala kama hilo lilikuja wakati wa mheshimiwa Mufti wa Misri Sheikh Bakriy Aswadafiy, katika mwezi wa mfunguo saba, mwaka wa 1331 wa Hijra, na matini ya swali ilikuwa ni: “Mwanamume mkristu anaitwa Waswef, alimwoa mwanamke mkristu anaita Roma, Wamekubaliana wote wawili hawa wakati wa mahudhurio ya uchumba kabla ya kuwafungisha ndoa sharti la kimaandishi linalotolewa kwa kopi mbili za maandishi yake: anapokufa mmoja wao kabla ya mwingine basi aliye hai hawezi kumrithi aliyekufa kati yao, kwa hiyo sharti la mwanamke ni mirathi yake inakuwa kwa ndugu zake baada ya kufa kwake kama hapatakuja kizazi baadaye bila ya kuingia mume wake aliyotajwa kwenye mirathi.
Na sharti la mwanamume ni atakapokufa kabla ya mwanamke mirathi yake itakuwa kwa watoto wake ambao atakufa na kuwaacha, iwe ni kwa mke wake aliyefariki au kwa mke wake aliye hai bila ya kumwingiza kwenye mirathi ya mume wake. Na je sharti hili kombozi kati yao linatumika ikiwa hali itahitajia kupitishwa maamuzi ya mmoja wao baada ya kufa mwingine mbele ya sheria au hapana? Nipe jawabu! Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akuhifadhini na nyinyi mna ujira na thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mheshimiwa Mufti wa Misri akajibu kuwa: mirathi ni lazima, haifutwi (haiondoki) kwa kuondoshwa kamwe, kama inavyotajwa katika matini za kisheria, na kutokana na hayo; basi masharti yanayotajwa baina ya mume na mke kwa hawa katika tukio la swali hilo, hayategemei juu yake (masharti mabatilifu}, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi.
Na baadhi ya wanazuoni wakasemea katika ubatilifu wa suala hilo ikitajwa kama sharti katika mkataba wa ndoa. Al-Khatweb Asherbiniy akasema: “Na Iwapo sharti litapotosha kwa makusudio asili ya ndoa, (kama vile) akimwekea sharti la (kutomwingilia kabisa) mume, na asimwingilie isipokuwa mara moja kwa mwaka kwa mfano, au asimwingilie isipokuwa usiku tu, au isipokuwa mchana tu, (au) kwamba (amwache) hata ikiwa baada ya kumwingilia, (ndoa hiyo itabatilika) kwa sababu inapingana na lengo la ndoa na hivyo kuibatilisha.
Na mume akiweka sharti kuwa asimrithi mke wake, au mke hatamrithi mume wake, au hawarithiani wote wawili, au kwamba matumizi yatakuwa juu ya mtu mwengine pasipo mume, basi sharti hilo litakuwa batili pia, kama alivyosema katika kitabu cha: [ASwlu Ar-Rawdhah] kutoka kwa Al-Khanatwiy, na akamfuata Ibn Al-Mughriy, na Al-Balqiniy akasahihisha usahihi mkataba na ubatilisho wa sharti. [Mughniy Al-Muhtaaj 226/3, Ch. Dar Al-Fikr]
Na Sheikh Adardiriy akasema: “(Na) ilivunjwa kabla ya kukutana kimwili kama ni wajibu (ambao) una maana ya kuharibika kwa mahari, inaweza kuwa kwa kuwa kwake hamiliki kisheria kama vile pombe, nguruwe au akawa anamiliki na wala haisihi kukiuza anachokimiliki kama vile Mtumwa aliyetoroka (au) alijikuta katika (sharti linalokwenda kinyume) na kilichokusudiwa katika ndoa (kama vile (asimgawie) katika malazi na mke mwingine au sharti linalomfadhilishia mwingine ni kama vile, anajaalia kwa mke wa pili siku mbili, na ana usiku mmoja, au sharti kuwa wasirithiane, au matumizi maalumu kila mwezi au siku au kwamba matumizi yake yatakuwa juu yake au juu ya babake. Au alimpa masharti atoe matumizi kwa mtoto wake au juu ya kwamba jambo lake liko mikononi mwake, au alimshurutisha mke mdogo au mtu mchafu au mtumwa kwamba matumizi yake yako juu ya Walii wake au bwana hakika ndoa inaharibika kwa wote kabla ya kukutana kimwili na itathibiti baada ya hapo kwa mahari inayofanana na ile ya dada zake na kufutwa sharti kama alivyosema (limefutwa) sharti lenye ukinzani baada kukutana kimwili katika yote yaliyopita. [Asharhu Al-Kabiir pamoja na Hashiyat Adosoqiy 238/2, Ch. Dar Al Fikr]
Na kutokana na yaliyotanguliza inajulikana kwamba kutokujuzu kuweka sharti la kutokurithi baina ya pande mbili katika kufunga ndoa na kwamba inayofaa yakiafikiwa makubaliano juu ya sharti la kupata kusihi ufunguja ndoa na kubatilika sharti, na kwa hivyo urithi utafanyika baina ya wanandoa wawili kwa mujibu wa kinachotambulika kisheria na kinatambulika katika dini ya kiislamu iliyosafi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas