Ahadi ya Masufi.

Egypt's Dar Al-Ifta

Ahadi ya Masufi.

Question

 Tunasikia kwamba kuna kitu kinachoitwa ahadi kwa Masufi. Wanakusudia nini kwa ahadi hiyo? na je, ahadi hiyo ina msingi gani wa kisheria? Au ahadi hii ni uzushi usio na asili katika sheria?

Answer

 Bismillahi na sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu na sala na salamu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na aali zake na masahaba wake na wanaoufuata mwongozo wake, ama baada.
Kwa hakika kuna Istilahi nyingi zilizoenea miongoni mwa Masufi ambazo zina dalili ya uzito wa uhusiano baina ya shekhe na mfuasi wake, na wamekiita chanzo cha kuungana kwao kwa majina kama “Ahadi, ahadi ya utiifu, Uamuzi, Tahkimu, kuvisha kitambaa, na njia”, na maneno haya yana dalili za kimalezi ya kimaadili yenye uzito wake, kwa maana ya wazi ni mwanzo wa uhusiano baina ya mfuasi wa njia na shekhe wake kikamilifu, na kwa mujibu wa hakika na undani wake ni kiunganishi cha mfuasi anaejulikana kwa jina muridi kwa Anayetakiwa na Mwenyezi Mungu.
Na ahadi katika lugha ina maana nyingi, na miongoni mwa maana hizo ni: Wasia, Dhamana, Amri, Mwono, Maono na Shaani, au Pahala. Kwa hivyo kila linaloahidiwa na Mwenyezi Mungu na kila makubaliano au mikataba baina ya waja ni Ahadi, na jambo la yatima pia ni kutokana na Ahadi, na kadhalika kila jambo linaloamriwa au kuharamishwa na Mwenyezi Mungu ni Ahadi, na dalili ya hayo ni katika Sahihi Muslim kwenye dua ya Sayid Al-Istighfar: “Na mimi niko katika Ahadi yako na ulazimu wake kiasi ninavyoweza” [Imetolewa na Al-Bukhariy].
Ama Ahadi katika ufahamu wa wasufi, shekhe As-Sahrudiy amesema kwamba Ahadi ni uhusiano, au kiunganishi baina ya shekhe na mfuasi wake, na ufuasi wa maamuzi ya mfuasi kutoka kwa shekhe wake katika nafsi yake kwa ajili ya masilahi ya dini na dunia yake. Inamuongoza na kumnyoosha na kumtahadharisha na maafa ya nafsi na ufisadi wa amali na malengo ya maadui [Aawaref Al-Maaref Lil Sahrudiy, Ku 251-260].
Au kwa maana nyingine Ahadi ni ufuasi endelevu wa ukaribu wa kidini kama ufuasi wa Ansari wa Madina wanalivyomlinda Mtume S.A.W. pamoja na ulinzi wa wanawake na watoto wao, na ni lazima kutumia lafudhi au neno lenye dalili juu ya maagano. [Aadhab Al-Masalek Al-Mahmoudiyah Lil Sheikh Mahmoud Katwab Al-Sobkiy 2\245, Ch. Al-Maktabah Al-Mahmoudiyah].
Na ulinzi wa ahadi ni kuilinda mipaka ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake bila kuacha amri zake, na kuhifadhi ahadi ya Mwenyezi Mungu na uwaja wake ni kutonasibisha ukamilifu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu tu, na upungufu wa vitu ni kwa mwanadamu tu. [Al-Muajam Al-Sufi, Dkt. Muhamad Abdelmoneem Al-Hefniy, Uk. 190, Ch. Dar Al-Masirah- Bairut].
Na miongoni mwa maana ya ahadi pia ni Kiapo cha utiifu, ni yeye utangulizi wa usuhuba wenye baraka baina ya shekhe mwongozaji na mfuasi wake ambaye ni muridi, anayetaka kuyafikia maarifa ya kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu S.W. na kwa Kiapo cha utiifu, athari ya shekhe huwa inaendelea kwa mfuasi au muridi kwa hali zake zote, na kwa hiyo kuutimiza muungano mkuu kwa ajili ya kuisafisha nafsi ya kibinadamu na usalama wa moyo na roho, kwani haitoshi katika tabia ya Wasufi wa njia ya Mwenyezi Mungu kwa elimu tu, kwani kusoma vitabu vya kisufi bila ya tabu kunaleta furaha ya kiakili, na utamaduni wa kiakili, na jambo hili labda huwenda likawa kwa kushirikiana na nafsi inayojiamrisha mabaya, na kwa hivyo inakuwa njia ya upotovu, ama zawadi ya kiroho kutoka kwa Mwenyezi Mungu inakuwa ni matokeo ya juhudi na kazi, kwani Masufi wana hali zao za kiutendaji na sio maneno tu, na wana kauli isemayo ((Anayeacha kufanya kazi kwa bidii hawezi kuona matunda yake)).
Anayekwenda katika njia ya Mwenyezi Mungu lazima ajiepushe na mambo yanayompamba na yanayompendezesha na lazima awe na zadi ya uchamungu, na silaha ya uchamungu ni dhikri ili aweze kupambana na shetani ambaye ni adui wa mwanadamu, na anahitaji pia chombo cha kupanda kinachomwezesha na kumsaidia katika safari zake, na chombo hicho ni hima au jitihada yake.
Na jambo hili halikuwa sahihi ila kwa dalili na mwongozo, na mwongozo huo ni mwalimu wa kiroho mkamilifu anayeweza kumlea na kumwongoa mwengine, na masufi wana kauli mashuhuri inayosema “asiye na shekhe basi shetani ni shekhe wake”. Anayetaka kwenda katika njia ya Mwenyezi Mungu juu ya mikono ya baadhi ya wanachuoni waliokaribu ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu analazimika kuwa na anayemwongoza jambo hilo, basi yapasa kuilazimisha nafsi yake kumtii na kuwa chini ya amri zake na makatazo yake. [Al-Fatawa Al-Hadithah Lil-Haytamiy, Uk. 77, Chapishwa katika Chapishaji cha Al- Halabiy].
Kwa hakika kiongozi wa sufi anamwongoza mfuasi wake anayeelekea kwa Mwenyezi Mungu na kuelekea katika njia ya haki, na anamwangazia njia yake kwa nuru ya imani pahala pa giza palipoizunguka nafsi yake, ili amwabudu Mwenyezi Mungu kwa uangalifu, na kwa mwongozo wenye yakini. Kwa hivyo mfuasi anamwahidi kiongozi wake kwenda naye juu kwa kuyaacha mabaya na kuzishikilia sifa njema na kuhakikisha utekelezaji kamili ya nguzo ya ihsani mpaka daraja la juu. Na kuihifadhi ahadi ni kuzifuata amri za Mwenyezi Mungu na kuifuata mipaka yote ya Mwenyezi Mungu.
Kwa hakika ahadi ni ahadi ya Mwenyezi Mungu na mkono ni mkono wa Mwenyezi Mungu: {Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao.} [AL-FATH: 10]. Kutoka hapa Mwenyezi Mungu anatahadharisha uvunjifu wa ahadi au kufanya kinyume cha ahadi hiyo: {Basi avunjaye ahadi hizi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake}. [AL-FATH:10], maana ya hayo ni kuwa ahadi ya dhahiri ni ahadi ya shekhe kiongozi, na ahadi ya ndani ni ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu S.W.
Ikidhihiri maana ya ahadi ya masufi katika lugha na desturi ya masufi, tutajikuta mbele ya swali muhimu: Je kuna msingi wowote wa kisheria kwa ahadi ya masufi na dalili zilizoleta maafikiano ya misingi ya sheria tukufu?
Jawabu: Ndio. Ahadi ina dalili katika Qur`ani na Sunna: katika Qur`ani ni kama katika kauli yake Mwenyezi Mungu:{ Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Basi avunjaye ahadi hizi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake; na anaye tekeleza aliyomuahidi Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa.} [AL-FATH: 10].
Mwenye tafsiri ya kitabu cha: [Roho Al-Bayan 9\21 Ch. Dar Al-Fikr]
Kutoka kwa sheikh Ismaiel Ibn Sudken kauli yake: “Wanaofungamana ni watatu :Mitume, Mashekhe wanaorithi na Masultani, na anayefungamaniwa kwa kweli hapa ni mwenyezi Mungu, na hawa watatu ni mashahidi tu kwa Mwenyezi Mungu juu ya mfungamano wa hawa wanaofuata. Na hawa watatu mashahidi wanalazimisha kufuata amri za Mwenyezi Mungu, na vilevile wanaofuatwa na wanafungamana lazima kufuata amri za Mwenyezi Mungu.
Ama Mitume na Masheikh hawaamrishi kufanya maasi asilani, kwani Mitume wanajitenga na shetani na hawafanyi maasi, na Mashekhe wanahifadhiwa, na masultani wanayeungana na Mashekhe miongoni mwao anahifadhiwa, na sultani akiamrisha maasi hakuna kumtii. Na muungano ni lazima mpaka unapofika wakati wa kukutana na Mwenyezi Mungu”.
Na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa} [Israa’i (Bani Israil: 34]. Maana ya mfungamano hapa ni ile inayoambatana na na aina zote tatu za mifungamano zilizotajwa hapo juu, na miongoni mwazo ni mfungamano baina ya shekhe mlezi na mtu anayemlea.
Na kuchukua ahadi na kuungana katika Sunna ya Mtume S.A.W. hakuchukuwi sura moja tu kutoka kwa mapokezi au kuhusisha kikundi kimoja cha waislamu, bali ahadi katika Sunna ni ahadi kamili baina ya muungano wa wanaume, mapokezi ya vikundi na watu binafsi kwa upande mmoja na baina ya muungano wa wanawake na hata vijana ambao bado hawajabaleghe. [Tazama: Ahadi ya Masufi kwa Ustadh Ashraf Saad, Gazeti la Al-Buhuth wa Ad-Derasat As-Swufiyah, Jalada la Pili, Uk. 458]
Na katika vitabu viwili vya Swahihi kutoka kwa Ubaadah bin As-Ssamit R.A. kwamba Mtume S.W.A alisema: “Niahidini kuwa: Hamtamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hamtaiba, wala hamtazini, wala hamtaua watoto wenu, wala hamtamzulia mtu wala kumtangazia uzushi (kwa kupita huku na kule); wala hamtaniasi kwa kukataa kufanya kheri. Basi yoyote miongoni mwenu atakayetekeleza ahadi hizo basi ujira wake uko kwa Mwenyezi Mungu, na atakayefanya lolote katika hayo na akapewa adhabu duniani basi hiyo itakuwa ndiyo kafara yake, na atakayefanya lolote katika hayo na Mwenyezi Mungu akamsitiri basi itakuwa juu yake Mwenyezi Mungu akipenda atamsamehe au akitaka atampa adhabu huko Akhera” Tukampa ahadi ya utiifu kwa hayo”.
Ama kwa upande wa kuchukuwa ahadi kutoka kwa watu katika kundi ama jamaah, Ahmad katika kitabu chake na Al-Tabaraniyy katika kamusi yake kikubwa na Al-Hakim katika kielelezo chake, wote walitaja kutoka kwa Yaala bin Shaddad alisema kwamba “Babangu R.A. alinizungumzia na Ubaada bin al-Ssamit yuko miongoni mwetu anayemsadikisha alisema: Tulikuwa pamoja na Mtume S.A.W. ambaye alisema: Je, kuna mgeni miongoni mwenu? -Yaani kutoka kwa Watu wa kitabu-tukasema: hakuna, Mtume aliwaamuru maswahaba wake kufunga mlango na akasema: Inuweni mikono yenu na semeni: Hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, basi tukainua mikono yetu na tukasema: Hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, kisha Mtume S.A.W. alishusha mkono wake chini na alisema: Al-Hamdu lilahi ulinituma kwa neno hilo, na uliniamuru kwa neno hilo na uliniahidi upepo kwa sababu ya neno hilo na kwa hakika wewe hauendi kinyume na ahadi yako. Kisha alisema; Mbashirieni kwa furaha Mwenyezi Mungu atakusameheni madhambi yenu nyote”. Al-Hafedh Al- Hayathamiy alisema katika kitabu chake: [Majma’ Al-Zawaed 1\191, Ch. Dar Al-Maamun Lil Turath: Rejaluhu Mawthoqun].
Na miongoni mwa ahadi za binafsi za kibinadamu ni ile inayotolewa na Ahmad katika kitabu chake na Al-Twabaraniy katika kitabu cha: [Al-Kabiir na Al-Awsat, na Al-Hakim Katika Kitabu Chake cha Kielelezo, na Al-Baihaqiy katika kitabu chake kinachoitwa: [Sunanuh] kutoka kwa Besher Bin Al-Khasasiyah R.A. alisema: “Nilimwendea Mtume S.A.W. ili nimpe ahadi ya utiifu, naye akasema: Basi Mtume alinishurutisha kwanza shahada ya kuwa hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Muhamad ni Mja na Mtume wake, na ninasimamisha Swala, na ninatoa Zaka, na ninahiji, na ninafunga mwezi wa Ramadhani, na najiunga katika Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ama mambo mawili ni magumu sana juu yangu: Jihadi na Sadaka, kwani Jihadi siwezi na Sadaka sina mali yatosha ili kutoa sadaka. Bishri alisema: Mtume (s.a.w) aliharakisha mikono yake na kunyamaza kitambo kisha alisema: Mbona unataka kuingia peponi na bila Jihadi ama Sadaka?! Alisema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ninakuahidi juu ya hizo zote. Alisema: Niliziahidi zote)). [Alisema Al-Hayitahmiy katika Majma’ Al-Zawaed 1\294: Rejal Ahmad Mawthuqun].
Na kutoka kwa Jarer ibin Abdullahi R.A. katika kitabu cha Ahmad na Al-Nasaiy alisema: Nilisema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unipe sharti kwani unajua sharti zaidi kuliko mimi. Alisema: Nikuahidia juu ya unamwabudu Mwenyezi Mungu pekee na usimshirikie, kusimamisha Sala, kutoa Zaka, kumnasihi mwislamu na kujiepushana sherki”.
Na katika Sahihi ya Al-Bukhariy pia kutoka kwa Jarir alisema: Nilimpa ahadi ya utiifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kwa kusimamisha Sala (za faradhi), kutoa Zaka,na kumpa Nasaha kila Mwislamu itakayomfaa katika mambo ya Dunia na ya Akhera.
Na katika kitabu cha At-Termiziy na Al-Nisaiy kutoka kwa Umaimah binti Raqiqah alisema: “Nilimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. na baadhi ya akina mama ili wampe ahadi walisema: Tunakupa ahadi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu juu ya tusimshiriki Mwenyezi Mungu, wala tusiiba wala tusifanyi uzini wala tusiwaui watoto wetu wala tufanyi uwongo miongoni mwa mikono yetu wala miguu yetu wala tusikuasi katika mambo mema, Mtume S.A.W. alisema: ahidieni katika unavyowezikanavyo.Wakasema; Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake ni wenye rehema juu yetu zaidi kuliko nafsi zetu, haya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu tukupe ahadi. Mtume S.A.W. akasema: Kwa hakika nisiwape mikono ya wanawake bali kauli yangu kwa wanawake mia ni kama kauli yangu kwa mwanamke mmoja”.
Baada ya Aya za Qur`ani na Hadithi za Mtume S.A.W. zilizotajwa hapo juu kuhusu ahadi, tunaweza kusema kwamba ahadi ya kisufi inayotajwa inaweza kufuata misingi ya kisheria,kwani inaambatana na ufahamu wa maana ya ushirikiano miongoni mwa watu katika wema na uchamungu, kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na saidianeni katika wema na uchamungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu}. [ AL MAIDAH: 2].
Vile vile kiongozi wa Sufi anafuata njia ya Mtume S.A.W. katika kupokea ama kuchukuwa Ahadi katika wakati wote. Sheikhi Abu Al-Hasan An-Nadwiy alitaja katika kitabu chake [Rejal Al-Fikr wa Ad-Dawah Fi Al-Islam, 1\209, Ch. Maktabat Nezar Mostafa Al-Baz]: Kwamba sheikh Abdulqader Al-Jelany alifungua mlango wa Ahadi na Tawba kwa upana sana kwa waislamu wote wa pande zote za ulimwengu wa kislamu ili kurejea mara kwa mara kumpa Mwenyezi Mungu Ahadi na miadi tena, na kumpa Ahadi Mwenyezi Mungu ni kutomshirikisha au kumkufuru Mwenyezi Mungu, kutofanya maovu, kuzuia uzushi, kutowadhuluma watu, kutohalalisha yaliyoharimishwa na Mwenyezi Mungu, kutoziacha faradhi za Mwenyezi Mungu, na kutoyafuata mambo ya Dunia tu na kuisahau Akhera. Na kutokana na hayo ya Sheikh Al-Jelany watu wengi sana wanaingia katika mlango huu na hali zao zimesuluhiswa na Uislamu wao unabadilika na kuwa bora zaidi. Na sheikh Al-Jelany anaendelea kuwaelimisha na kuwachunga pamoja na kuyasimamia maendeleo yao. Kwa hivyo wanafunzi hawa wa kiroho wanalihisi jukumu lao baada ya Ahadi na Toba pamoja na kuzirekebisha imani zao tena.
Ahadi na maagano haya yanaathari njema sana katika usafi wa nafsi na mtengemao binafsi na wa kijumla zaidi kuliko mambo mengine.
Na namna ya Ahadi kwa wanaume ni mfuasi kuketi mbele ya Sheikhe wake akiwa na usafi wa kimwili na kiroho, ni kama usafi wa kwenda kusali, na wakati huo Sheikhe anampa maneno ya toba, na baadaye anamwambia: Uniahidi kuacha maasi na kufanya mema unavyoweza ili Mwenyezi Mungu asikuone katika jambo lolote baya. Pia unapaswa kutimiza wajibu wako kwa upande wa Ulinganiaji kwa njia maalumu ya Masufi. Akikubali haya atauweka mkono wake katika mkono wa mfuasi na kusoma Aya ya Ahadi ya utiifu: {Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Basi avunjaye ahadi hizi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake; na anayetekeleza aliyomuahadi Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa}. [AL FAT-H'I: 10].
Kisha anamwambia aseme: Hii ni Ahadi ya Mwenyezi Mungu juu ya kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na njia yetu kwake S.W. hatubadiliki wala kughairi katika Dini, Ahadi ni Ahadi ya Mwenyezi Mungu na Mkono ni Mkono wa Mwenyezi Mungu, na mnaitimiza Ahadi ya Mwenyezi Mungu mkiahidiana, na timizeni Ahadi kwani Ahadi itaulizwa, sisi sote tunakwenda kwa Baraka ya Mwenyezi Mungu katika mambo yaliyofaulu, na Shekhe na maulana wetu Fulani, kisha anamwita Shekhe wake na Shekhe wa shekhe wake mpaka kwenye njia yao inayoridhisha kuifuata, kisha kwa bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. [Rejelea katika Tafswel ya Bai na Ahadi kutoka kwa mfuasi mpaka Sheikh katika kitabu: [Al-Nafahat Al-Iilahiyah fi Kayfiyat Suluk At-Twariqah Al-Muhamadiyah kwa Sheikh/ Muhamad Abdul-Karem Al-Qurashiy Al-Madaniy anaye maarufu kwa jina la As-Saman, Uk.14, Ch. Maktabat Al-Adab wa Muayad Misr].
Akikubali hayo anampa jina la Jalali la Mwenyezi Mungu na siri yake katika masikio yake mara tatu pamoja na maelezo ya Mashekhe wake mpaka kuunganisha roho za mioyo yao miwili juu ya mafunzo ya maelezo haya, na baadaye anamwamuru kuyakariri hayo mara tatu – Jambo hilo ni kama katika Hadithi mashuhuri ya Mtume S.A.W. ni kwamba siku moja Mtume alifunga mlango na na hali ya kuwa ana kundi fulani na analiapisha kundi hili kuwa Hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, mara tatu, hasa baada ya kujua hakuna mtu yeyote mgeni miongoni mwao kama ilivyotajwa hapo juu – na baadaye akamwamuru kuyafuata mafunzo na ubora wa maadili na kuhudhuria masomo ya Dhikiri na kusoma uradi wake daima na kila wakati.
Ama kwa upande wa wanawake wakati wa Ahadi, lazima ifuate mfumo na njia ya kisheria kwa mujibu wa ilivyo, na hairuhusiwi kuweka mkono katika mkono wala kukaribiana na masikio ya wanawake wakati wa kuwapa jina la Jalali, wala kulihudhuria baraza la wanaume, wala mambo yote yasiyoruhusiwa katika sheria kwa wanawake, ama baraza la elimu wanawake wanaweza kuhudhuria na kukaa katika mahali pao mahususi mbali na pahala pa wanaume.
Kutokana na yaliyotangulia kuelezwa hapo juu, tunaweza kusema kwamba Ahadi ya Masufi haina uhalifu wa sheria, wala haina upingaji wa mizizi ya sheria kwa mujibu wa matini ya Qur`ani na Sunna.Tunaomba Mwenyezi Mungu atufaulishe kwa utii wetu kwake katika hali ya siri na ya dhahiri.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas