Kumshurutisha Mwanamke Aache Haki y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumshurutisha Mwanamke Aache Haki yake ya Matumizi

Question

 Mwamume mmoja aliomba kumposa mwanamke mmoja, lakini ameshurutisha kuwa mwanamke aache haki yake ya matumizi katika mazingira ya kuwepo maisha ya ndoa, basi, je, sharti hilo linajuzu kisheria au linatofautiana na hukumu za kisheria?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Miongono mwa haki zinazomuwajibikia mume kwa mke wake kwa mkataba wa ndoa na mwanamke kujisalimisha nafsi yake kwa mumewe ni matumizi kama mfano: vyakula, vinywaji, nguo, nyumba na matumizi ya dawa na mengineyo, na mfano wa hayo ambayo yanafaa kwa wema. Na kwa hayo walisema wanavyuoni wa madhehebu manne, na Al-Kassaiy wa kihanafi na Ibn Rushd wa kimaliki na wengineo waliyanukuu hayo makubaliano juu ya jambo hilo. [Tazama: Bada’i Aswana’i 15/4, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah, na Bidayatu Al-Mujtahed 76/3, Ch. Dar Al-Hadiith]. Na asili katika kuwajibika kwa matumizi tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na mwenye dhiki atoe katika alichompa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alichompa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraji} [ATWALAAQ 7]
Na dalili juu ya kuwajibika matumizi ni tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Najuu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake} [AL-BAQARAH 233]. Na anayemkusudia kwa kuzaliwa kwake ni mume, basi Aya Tukufu imetoa dalili kwa amri ya kumpa matumizi kwa mke.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Wawekeni humo humo mnamo kaa nyinyi kwa kadiri yapato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwadhiki. Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwengine.} [ATWALAAQ 6]
Na amri ya makazi na matumizi ingawa inarejea kwa walioachwa isipokuwa wake ni bora zaidi kwa uwajibu wake, na aliyeachwa ni wajibu kumpa makazi kwani alikuwa mke, na ana baadhi ya hukumu za ndoa zinazobaki miongoni mwake ni makazi, kwa hiyo matumizi ni wajibu kwake akiwa mwenye mimba, kwa hiyo wajibu kwa mke ni bora zaidi.
Na Mtume S.A.W. alisema katika Hadithi ya Jabir inayojulikana katika hutuba ya kuaga: “…Basi mcheni Mwenyezi Mungu Mtukufu katika wanawake kwani hakika nyinyi mmewachukua kwa amana ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na mkazihalalisha tupu zao kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu, na nyinyi mna juu yao kuhakikisha hakuna yoyote anayeingia nyumbani kwenu katika wale mnaowachukia na iwapo watafanya hivyo basi wapigeni kipigo kisichoumiza, na ni wana juu yenu kuwalisha na kuwavalisha nguo kwa wema…” [Imepokelewa na Muslim].
Basi, mwanamke kwa kufunga ndoa tu, anastahiki kupewa matumizi, na iwapo mwanaume atamshurutisha kuondosha matumizi hayo wakati wa kufunga ndoa, basi inajuzu kufunga ndoa na kubatilisha sharti kwa mujibu wa Madhehebu manne, na kwa hayo wakasema wanazuoni wa Kihanafi, wa Kishafi na wa Kihambali. Na wanazuoni wa Madhehebu ya Malik wanahusisha usahihi wa mkataba wa ndoa na ubatilifu wa sharti baada ya kuingia, ama kabla ya kuingia basi mkataba na sharti ni batilifu. [Rejea: Radu Al-Mukhtaar 586/3, Ch. Dar Al-Fikr, na Sharhu Al-Kharashiy 195/3, Ch. Dar Al-Fikr, na Hashiyatu Adisoqiy 238/2, Ch. Dar Al-Fikr, na Al-Umm 79/5, Ch. Dar Al-Maarifah, na Hashiyat Qaliyobiy Ala Sharhi Al-Minhaaj 22/4, Ch. Dar Ihyaa Aturaath Al-Arabiy, na Hashiyat Al-Bigirmiy Ala Al-Khatweb 86/4, Ch. Dar Al_Fikr, na Al-Inswaaf 165,166 /8, Ch. Dar Ihyaa Aturaath Al-Arabiy].
Na wameweka dalili ya Kusihi kufunga ndoa kwa kuwa sharti la kutotoa matumizi linarejea katika maana iliyoongezeka katika ufungaji ndoa ambayo haishurutishwi kutajwa kwake na wala haina madhara kuipuuzia kwake, na wala haibatilishi msingi wa ndoa kama vile angeweka sharti la kufunga ndoa kwa kutoa sadaka iliyoharamishwa. Kama ambavyo ndoa inasihi pamoja na kutokujua malipo mbadala, basi imejuzu pia kufungwa pamoja na sharti baya kama vile kumwachia huru mtumwa. Ukiongezea katika hayo, sharti la kuondosha matumizi halivurugi lengo la kufunga ndoa ambalo ni kumwingilia mke, kwa hiyo ufungaji ndoa huo unasihi.
Ama kuhusu kubatilika kwa sharti, wao wameweka dalili yake kutokana na tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana.} [AN NISAA 3]
Imamu Shafiy amesema kwamba: “Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu kimetoa dalili ya kwamba mwanamume lazima ampe mke wake matumizi katika maisha yake. Na kadhalika Sunna imeweka dalili. Na iwapo atamshurutisha asimpe matumizi yake basi, sharti hilo litakuwa limebatilishwa, na ameamrishwa kumtendea wema. [Al-Umm 79/5]
Vile vile sharti la kutotoa matumizi linakwenda kinyume cha mazingira ya ufungaji ndoa, na kwa hivyo linabatilika, vile vile sharti hilo lina ndani yake uondoshaji wa haki kwa kufungwa ndoa kabla ya kufungika kwake na kwa ajili hiyo halifai, vile vile kama mwombezi anapoondosha uombezi wake kabla ya kuuza au mnunuzi akamwepusha muuzaji na kasoro. [Rejea: Al-Mughniy 94/7, Ch. Maktabat Al-Qahirah, na Kashaafu Al-Qenaa’ 98/5, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Na yapo matamko mengine katika suala hilo, kama vile, tamko la kusihi mkataba wa ndoa na sharti, au tamko la ubatilifu wa mkataba na sharti, na yote mawili yanapelekewa na Imamu Ahmad. [Al-nsaafu 165- 166/8]
Na kanuni ya Maisha ya Familia ya Misri haikutaja katika mada zake suala hilo, lakini ilitaja maana iliyo karibu na jambo hili. Basi, katika mada ya pili kutoka katika kanuni namba mia moja ya mwaka elfu moja mia tisa themanini na tano; tamko hili: “Matumizi ya mke yanazingatiwa kuwa ni deni kwa mume kuanzia tarehe ya yeye kuacha kutoa matumizi hayo pamoja na kuwa wajibu wake na deni hilo halifutiki isipokuwa kwa kulilipa au kufutiwa na muhusika”.
Kwa hivyo, kanuni imetaja kuwa matumizi ya mke yanazingatiwa kuwa ni deni lililo mikononi mwa mume pale anapoacha kutoa matumizi hayo na huhesabika tangu pale mume anapoacha kutekeleza, na katika vitu vinavyo ondosha deni baada ya kuthibitika uwepo wake ni kusamehewa, kwa hiyo sheria imejuzisha kufutiwa deni la matumizi yaliyopita. Kwa upande wa matumizi yajayo - nayo ni yale ambayo yamo ndani ya swali - hakuyagusia, isipokuwa Fiqhi ya Sheria inatumika katika hili kwa madhehebu ya Jamhuri ya wanazuoni. [Tazama: Mawsu’at ya Fiqhi na Uqadhi katika Maisha ya Familia kwa Mshauri Muhammad Azmiy Al-Bakriy 339-340/2, Ch. Dar Mahmoud].
Na imetaja katika Ukurasa wa Kielezo kwa maboresho ya Kanuni ya Maisha ya Familia ya Kimisri namba ya mia moja ya mwaka elfu moja mia tisa thamanini na tano, Kwamba hukumu maalumu za kikanuni za maisha ya familia hata kama hazikuzungumzia jambo hili hakika ni kwamba patatolewa maamuzi ndani yake kwa kauli zinazokubalika kutoka katika madhehebu ya Imamu Abu Hanifa isipokuwa zile zilizotengwa kuhusu jambo hili.
Na katika madhehebu ya Hanafi, ni kwamba haisihi kufuta matumizi yajayo katika ndoa mikononi mwa mume iwe kwa kuridhiana au kwa maamuzi ya kadhi, na hiyo ni kwa muda mmoja katika muda ambao pameamuliwa kutolewa matumizi ndani yake kwa sharti la kuwa muda huo umekwishaanza, na kwa mfano, akimpa jukumu la matumizi kadhaa kila mwezi, na mwezi maalum umeanza, basi inajuzu kwa mke amsamehe matumizi ya mwezi huohuo tu, pasipo miezi inayobaki ijayo. [Al-Bahru Ara’iq 192/4, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy, na Radu Al-Mehtaar 586/3].
Na yanayothibitisha katika suala hilo kwamba kusamehe kwa mwanamke kwa baadhi ya haki zake – miongoni mwake ni matumizi – Inajuzu kiujumla, na asili ya hayo ni yale yaliyotolewa na Imamu Al-Bukhariy katika usahihi wake, katika sababu ya kuteremka Aya ya Suratu AN NISAA, {Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa namumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu.Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamchamungu basi hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayoyatenda.} [AN NISAA 128]
Kutoka kwa Mama wa Wanaumini Bibi Aisha R.A. alisema: “Mwanamume ambaye mwanamke anakuwa kwake si mwenye kumwongezea na anataka kuachana naye, na mwanamke akasema: ninakufanyia jambo langu kuwa ndio suluhisho”, basi Aya hiyo imeteremka katika jambo hilo. Na kadhalika kusamehe kwa mke mmoja wa Mtume S.A.W. usiku wake kwa Bibi Aisha ili asimwache, kama ilivyotajwa katika vitabu viwili vya Swahihu.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia; Kwa hiyo sharti la kusamehe matumizi linaishia kuwepo kwake pamoja na kufungwa ndoa lakini linabatilika baada ya kufungwa ndoa na hii ni kwa upande wa kisheria, ama kwa upande wa hatua iwapo zitaafikiana juu ya hili basi hakuna chochote kinachozuia na mwanamke anakuwa na haki ya kudai matumizi wakati wowote atakapo kufanya hivyo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas