Swala ya Maamkizi ya Msikiti Baada ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Swala ya Maamkizi ya Msikiti Baada ya Swala ya Al-Asiri.

Question

 Ninapoingia msikitini baada ya Swala ya Alasiri je naweza kuswali Sala ya maamkizi ya msikiti au hapana?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Ama baada ya hayo:
Swala ya kuuamkia msikiti: ni rakaa mbili anazoziswali yule mwenye kuingia msikitini tofauti na msikiti Al-Haram akiwa ametawadha na anataka kukaa msikitini na wala siyo kupita tu, kabla ya kukaa. Na swala hii ni Sunna. Imepokelewa na Imamu Bukhari na Muslim kutoka katika Hadithi ya Qatada R.A, kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Pindi anapoingia mmoja wenu msikitini, basi wala asikae mpaka aswali rakaa mbili”.
Na katika mapokezi ya Muslim kuna Hadithi inayotoka kwa Jabir R.A. amesema: “Aliingia Saliik Al-Ghatfaniy, na Mtume S.A.W. alikuwa anatoa hotuba, Akasema: Ewe Saliik simama na uswali rakaa mbili”, na Swala ya Sunna imekatazwa kabisa katazo ambalo ni la kuchukiza ndani yake kuiswali baada ya Swala ya Al-Asiri, kwa Hadithi ya Maimamu wawili kutoka kwa Abu Said Al-Khudriy R.A, amasema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, anasema “Hakuna Swala baada ya Swala ya Al-Asiri”. Wafuasi wa Imamu Shafi wakazitenga na hukumu hiyo Swala za Sunna ambazo husaliwa kwa sababu za dharura, kama vile Swala ya kukamatwa kwa jua, Swala ya kuomba mvua na Swala ya kuingia msikitini, kwa sababu Swala za Sunna zinaweza kuswaliwa kwa sababu za kuzuka, kwa muda na kwa wakati maalumu.
Amesema Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha Raudhat Al-Talibin: “Swala za Sunna zimegawika sehemu mbili; sehemu ya kwanza: ni ile isiyofungamana na wakati, isipokuwa hutekelezwa kwa sababu zinazojitokeza, kama vile Swala ya kukamatwa kwa jua na mwezi, Swala ya kuomba mvua na Swala ya kuuamkia msikiti. Sehemu ya pili: ni ile inayoendana na wakati, kama vile Swala ya Idd mbili na Swala ya Dhuha. (Kitabu cha Raudhat Al-Talibin cha An-Nawawiy, 1/337, chapa ya Al-Maktab Al-Islamiy).
Na akasema Al-Khatib Al-Shafiy: “Nyakati ambazo zinachukiza kuswali ndani yake isipokuwa Swala zenye sababu si za kuchelewa, kwa maana ya sababu yake ni baada ya Swala na wala siyo kabla yake kama vile Ihram, yenyewe hutekelezwa baada ya Swala, inafaa kama vile Swala iliyokupita, na Swala ya kukamatwa kwa jua na ile ya kuomba mvua na kutufu, pamoja na Sunna ya Maamkizi ya Msikiti na Swala ya Sunna ya kutawadha, kusujudu kwa ajili ya kisomo na kushukuru pamoja na Sala ya Jeneza”.
Kisha akahesabu hizi nyakati na akasema: “Baada ya Swala ya Al-Asiri mpaka kuzama kwa jua, zote hizo ni nyakati ziliokatazwa kwa Hadithi zilizopokelewa na Maimamu wawili” [Kitabu cha Al-Iqna’a fi hal Alfadh Abi Shuja’, 2/116, chapa ya Dar Al-Fikr].
Kutokana na maelezo haya: Swala ya Maamkizi ya msikiti baada ya Swala ya Al-Asiri inafaa kuiswali, kwa sababu ni katika Swala za Sunna zenye sababu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

 

 

Share this:

Related Fatwas