Mchumba Kuamua Kuachia Haki yake ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mchumba Kuamua Kuachia Haki yake ya Vito Vyote au Baadhi yake

Question

 Mwanaume mmoja alikuwa tayari ameshamchumbia mwanamke na akwamwasi Mwenyezi Mungu Mtukufu na mchumba huyo kisha akavunja uchumba wake kwa Mwanamke huyo na kuchumbia mwingine kisha akarejea kwa wa kwanza kwa msukumo wa kusutwa na dhamira yake, pindi yule mchumba wa pili na wazazi wake walipojua alichokifanya mchumba wake huyo na wakaangalia mapana na marefu pamoja na misukumo ya hatua hiyo waliamua kuuvunja uchumba huo kwa kutotulizana nafsi zao kutokana na maadili ya huyo mchumba na wakamtaarifu kwa uamuzi huo na pande mbili zikakubaliana tena kwa kuridhiana kuwa parejeshwe nusu ya vito vya uchumba kwa mwanaume huyo ambavyo alimpa mchumba wake, na yeye mwanamke aliyevunja, uchumba aendelee kuwa na nusu iliyobaki ya vito dhahabu. Je, uwafikiano huo una jambo la kudhulumu kwa mwanamume? Au una jambo kinyume na sharia kwa upande wowote?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Uchumba, kupokea mahari na vito vya dhahabu, vinazingatiwa kuwa ni utangulizi wa ndoa na ni kama ahadi ya ndoa hiyo kwa muda wa kuwa ndoa haijafungwa kwa kukamilika nguzo na masharti yake ya kisheria, na iwapo mmoja wao ataamua kutoazimia kukamilisha ufungaji wa ndoa basi mchumbiaji atarejeshewa Mahari alioitoa na mchumbiwa hastahiki chochote katika mahari hiyo.
Na vile vile vito; kwa kuzoeleka kwake kuwa ni sehemu ya mahari ambapo watu hukubaliana watu kuhusu vito hivyo pale mtu anapotaka kufunga ndoa, ambapo mchumbiaji huvitoa vito hivyo kama zawadi na baadaye kufuatiwa na mahari; na mazoea yana nafasi yake katika sharia ya Kiislamu. Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, najitenge na majaahili} [AL-AARAF 199]. Kwani kila kilichoshuhudiwa na mazoea hupitishwa maamuzi kwa kitu hicho, kama alivyosema Imamu Al-Qarafiy katika kitabu cha: [Al-Fruoq 185/3, Ch. Alam Al-Kutub]
Kwa hiyo, vito vilivyotangulizwa kutolewa na mchumbiaji kwa mchumbiwa huwa ni vya mchumbiaji katika hali ya mmoja wao kuamua kuuvunja huo uchumba na mchumbiwa hana haki ya kitu chochote katika vito hivyo na wala haiathiri chochote iwapo aliyevunja uchumba huo ni mwanamke au mwanaume. Isipokuwa atakapoamua kuachia haki yake ya vito kwa aliyekuwa mchumba wake au baadhi ya vito hivyo, kwa hivyo hakuna ubaya wowote kwa Mwanamke kubaki na chochote katika vito alivyoamua mwanamume kuachia haki yake kwa Mwanamke huyo avimiliki; kwani hicho ni kitendo cha mwanaume yeye mwenyewe kwa anachokimiliki na hatua hiyo imechukuliwa kwa ridhaa yake mwenyewe na kwa kukubali kwake kwa hiyo hicho ni kitendo kinachokubalika na kutekelezwa.
Na Ad-Darqatwniy alipokea kutoka kwa Habaan Bin Abi Jabalah R.A., kutoka kwa Mtume S.A.W., amesema: “Kila mtu ana haki zaidi katika mali yake kuliko mzazi na mtoto wake na watu wengine wote”. Kwa hiyo Hadithi hii inaamua msingi wa uhuru wa mtu kufanya atakavyo katika mali yake.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia kuhusu suala hilo: Sio vibaya kwa mchumba wa pili ambaye ameamua kubadili msimamo wake wa uchumba, ahifadhi nusu ya vito vya ndoa vilivyotolewa na mchumbiaji aliyetajwa, kwa kuwepo maridhiano juu ya hili na makubaliano na ndugu wa mchumbiwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas