Kuhiji kwa Manabii na Watu wao

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhiji kwa Manabii na Watu wao

Question

Je. Manabii waliotangulia walihiji? Na je, Manabii hao waliwaamrisha Watu wao kuhiji? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafaradhishia viumbe wote kumtii yeye; kwani wao wote wameumbwa kwa lengo hilo, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi} [ADH-DHARIYAAT 56]. Na akawatuma mitume hao watukufu kwa ajili ya jambo hilo hilo, na mitume hiyo mitukufu S.A.W., hawakuhitilafiana katika mambo thabiti kama vile; Upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutomshirikisha. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipokuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.} [AL-ANBIYAA 25]. Na Kauli Yake: {Na waulize Mitume wetu tulio watuma kabla yako: Je! Tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rah'mani?{ [AZ-ZUKHRUF 45]
Ama katika matawi ya sharia, pengine hukumu zinahitilafiana baina ya sheria na sharia nyingine; kama Alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake.} [AL-MAIDAH 48]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Basi kwa dhulma yao Mayahudi tuliwaharimishia vitu vizuri walivyo halalishiwa. Na kwa sababu ya kuwazuilia kwao watu wengi na Njia ya Mwenyezi Mungu,} [AN-NISAA 160]. Na Akatutajia kauli ya Issa kwa Bani Israi’l katika mambo hayo: {Na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale mlioharimishiwa} [AAL-IMRAAN 50], na nyingineyo kama ilivyojulikana.
Na Mitume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu wao ndio akuowazungumzia Mwenyezi Mungu aliposema: {Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaahidi. Basi fuata hidaya yao. Sema: Mimi sikuombeni ujira. Haya hayakuwa ila ni mawaidha kwa walimwengu wote} [.AL-ANAAM 90].
Basi hakuna shaka kwamba manabii wote ni wa kwanza kuuitikia wito wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hadithi nyingi zinazolisiaitizia jambo hili zimetajwa, na zinayaelezea hayo kwa ujumla na kwa kusambaza.
Basi At-Tarmiziy aliitoa Hadithi kutoka kwa Amru Bin Shuaib, kutoka kwa babake, kutoka kwa babu yake; kwamba Mtume S.A.W., anasema: “Dua ya heri zaidi kuliko dua zote ni ile dua ya siku ya Arafah, na kauli ya heri niliyoisemea mimi na manabii waliokuja kabla yangu ni kwamba Hakuna Mungu yoyote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, hana mshiriki wake, Ufalme wote ni wake na Sifa zote njema ni zake na Hakika Yeye Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.”
Na Hadithi inayoielezea simulizi huyo ni ile iliyopokelewa na Al-Baihaqiy katika kitabu chake cha Sunan kutoka kwa Ali Bin Abi Twalib R.A. alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. anasema: “Isome kwa wingi Dua yangu na dua za manabii waliokuja kabla yangu katika eneo la Arafah; nayo ni: Hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.” Na akaitaja hadithi hiyo.
Na athari zimekuja pia kutoka kwa wema waliotangulia mfano wa hayo: kutoka kwa Abdullah Bin Dhamrah As-Sluliy alisema: Sehemu iliyopo baina ya Kona na Kisimamo cha Ibrahim mpaka katika kisima cha Zamzam kuna kaburi la manabii tisini na tisa waliokuja kuhiji, wakafa na wakazikwa hapo”.
Na kutoka kwa Mujahid amesema: “Manabii sabini na tano walihiji, na wote walitufa Kaabah, na wakaswali katika msikiti wa Minna, na ikiwa utaweza kutopitwa na swala katika Msikiti wa Minnah basi uswali ndani yake!
Na kutoka kwa Abdullah Bin Abbas R.A, alikuwa akisema: “Manabii sabini waliipita njia ya Ar-Rawhaa-u kama mahujaji, walikuwa wakivaa nguo za sufu, huku wakiwapitishia puani ngamia kwa kamba zilizotengenezwa kwa majani, na hakika Manabii sabini walisali katika msikiti wa Al-Khiif. (Al-Azraqiy akayapokelea hayo yote katika kitabu cha: Akbaar Makka; nambari ya 68/69/72, Ch. Al-Andalus).
Basi hayo ni baadhi tu ya yaliyotajwa kuhusu hija za Manabii kwa ujumla, ama yaliyotajwa kwa kirefu zaidi, basi katika hayo ni yale yaliyokuja katika matini ya baadhi yao kwa kuwataja wakuu wao, kama katika kitabu cha: [Sahihi Ibn Khuzaimah] kutoka kwa Ibn Abbas R.A., kutoka kwa Mtume S.A.W, anasema: “Hakika Nabii Adam alikuja kuhiji Makkah mara elfu moja, kamwe hajawahi kupanda kipando chochote katika safari zake hizo alfu moja kutoka India bali alitembea kwa miguu yake tu,”.
Na katika kitabu cha: [Sahih Muslim] kutoka kwa Ibn Abbas: “Kwamba Mtume S.A.W., alipita katika bonde la Al-Azraq, na akasema: hili ni bonde gani? wakasema: hili ni bonde la Al-Azraq, Mtume S.A.W., akasema: Kama vile mimi ninamwona Musa amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, akiteremka kutoka katika njia ya majabalini huku akiwa na waatu kwa kuuitikia wito wa Mwenyezi Mungu kwa Talbiah, halafu Mtume S.A.W., akaja kwa njia ya Harshi, na akasema: ni njia gani hii? Wakasema: hii ni njia ya Harshi, na, Mtume S.A.W. akasema: Kama vile mimi ninamwona Yunus Bin Matta amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, akiwa juu ya ngamia mwekundu na yeye amevaa vazi la manyoya ya ngamia, na akitoa Talbia. Na katika kitabu cha: [Sahih Muslim], kutoka kwa Abi Hurairah R.A., kutoka kwa Mtume S.A.W. akasema: Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko katika mikono wake, Ibn Maryam lazima aje kuhiji au kufanya Umrah, au kuzifanya zote mbili kwa Njia Ar-Rawhaa”.
Basi hayo ndiyo yanayohusiana na Manabii. Ama kuhusu watu wao; Inajulikana kwamba siyo watu zote waliwamini Mitume wao, basi, miongoni mwao wapo walioamini, na miongoni mwao wapo ambao hawakuwaamini. Ama kuhusu wale watu waliokufuru; huwenda ikawa Nabii wao aliwalingania waenda kuhiji, lakini wakakataa kusikiliza matawi (hija) kwani wao walilikanusha Shina (Nabii) au inawezekana ikawa Nabii huyo hakuwalingania kuhiji mpaka waamini kwanza. Kama ilivyokuja mfano wa hayo katika hadithi iliyoafikiwa na wanazuoni wa Hadithi kutoka kwa Ibn Abbas R.A., alisema: Mtume S.A.W., amesema kwa Muaaz Bin Jabal alipomtuma Yemeni: “Hakika wewe utawaendea watu wa kitabu, na ikiwa utawaendea watu hao basi uwalinganie Shahada nayo ni: "hakuna mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na, kama wao watakutii wewe kwa hayo, basi waambie kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu Amewafaradhishia Sala tano kila siku mchana na usiku. Na kama wao wakikutii katika hayo, basi waambie kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafaradhishia Zakkah inayochukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurejeshwa kwa mafakiri wao. Na kama wao wakikutii katika hayo, basi tahadhari mali zao za halali!
Na ni bora kuiogopa dua ya aliyedhulumiwa, kwani hakuna kizuio baina ya dua hiyo na Mwenyezi Mungu”. Na walipoendelea katika ubishi wao basi yeye hakuwalazimisha kufanya hivyo, basi Nabii alikuwa akihiji yeye mwenyewe pamoja na waliomwamini wakati huo, na wengine waliokufuru wakangamizwa. Na hadithi hiyo ya mwisho imewekwa kama dalili kwa kutolewa na Al-Azraq, katika kitabu cha: [Akbaar Makka, juzu ya 68], kutoka kwa Muhammad Bin Sabit, kutoka kwa Mtume S.A.W, akasema: “Hakika Nabii miongoni mwa Manabii alikuwa ukiangamizwa umma wake alikwenda Makka yeye na kaumu yake walioamini, na wakakaa Makka hadi wakafariki dunia na kuzikwa hukohuko. Basi Manabii; Nuhu, Hud, Swaleh na Shuaib walifia Makka na makaburi yao yako katika eneo la baina ya Zamzam Na Hijri”.
Ama walioamini kama Bani Israel, huwenda ikawa waliamrishwa kuhiji na wao wakakana, na hili haliko mbali nao, kwani waliowaua Manabii na wakamwabudu ibilisi siyo mbali na hao, kwamba wakatae jambo maalumu na wakampinga Nabii wao. Au walikuwa umma miongoni mwao waliomwitikia Nabii wao, kama Alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yao: {Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno.} [AL MAIDAH 66], Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wote hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu walio simama baraabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu.} [AAL IMRAA 113].
Na pia, kuna dalili ya hayo kutokana na maelezo yaliyotajwa na As-Swalihiy katika kitabu cha: [Subul Al-Huda Wa Ar-Rashad 212/1, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], (Kuhiji kwa Bani Israel na Wengineo): Abu Nuaim alipokea kutoka kwa Mujahed, rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: “Watu laki moja walikuwa wakihiji kila mwaka, na walikuwa pindi wanapofika katika mipaka ya Kaaba huvua viatu vyao kisha huingia Eneo takatifu bila ya viatu”.
Na Ibn Abi Shaibaha na Al-Azraqiy wamepokea kutoka kwa Abdullah Bin Az-Zubair radhi za Mwenyezi Mungu ziwafikie wote wawili, amesema: “Ulikuwa huo Umma wa Bani Israel ukienda Makkah, na walikuwa pindi wanapofika Dah Twuwa huvua viatu vyao wakilitukuzia Eneo takatifu. Na Al-Azraqiy nq Ibn Asaker wamepokelea kutoka kwa Ibn Abaas, radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziwafikie wote wawili, akasema: “Wanafunzi wa Nabii Issa (Al-Hawareyun) pia walihiji, na walipoingia Eneo takatifu walitembea bila ya viatu wakilitukuza eneo hilo.
Na hakika mambo yalivyo sisi hatukuweza kufikia uamuzi wa mwisho kwa hayo yaliyotajwa katika haya yaliyopokelewa kwa kutokutajwa kitu katika hayo kutoka kwa Mtume S.A.W mwenye kukingwa na makosa, na kwa uwezekano wa watu hawa waliotajwa kuyapokea mambo hayo kutoka kwa Watu wa Kitabu, na hiyo ni kama itasihi Isnadi kwa hao wema waliotangulia.
Na kama tungekubaliana – kwa hali yoyote - kwamba wao Mitume walikuwa wanahiji lakini hawakuamrishwa Kuhiji, basi hiyo isingekuwa vyema kwao, bali ingelikuwa vibaya kwao, kwani wangekuwa wamenyimwa utukufu mkubwa wa ibada hii muhimu.
Basi kama Hija ilikuwa haifanywi isipokuwa na Manabii, na wafuasi wa umma huo wakaitekeleza, basi hiyo ilikuwa ni miongoni mwa sifa zao, na walikuwa na haki zaidi kwa Mtume wao na watu wake.
Na Qura’ani tukufu iliwachambua watu wa Kitabu wasiohijii nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika kauli yake: { Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote.(96) Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewawajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo tukufu, kwa yule mwenye kumudu gharama za kwenda kuhiji. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu simhitaji kwa walimwengu (97)}. [AAL-IMRAAN 96, 97] Ambapo mayahudi na wakristo walijidai kuwa wafuata mila ya Mtume Ibrahiim A.S. basi Mwenyezi Mungu Mtukufu Akabainisha wongo wao, kwani kuhiji Al-Kaaba ilikuwa ni mila ya Ibrahiim A.S., na mayahudi na wakristo hawakuwa wakihiji, basi hiyo ni dalili ya wongo wao. Kama ilivyotajwa na Al-Fakhr Ar-Raziy katika tafsiri yake: [295/8, Ch. Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy].
Na kutokana na maelezo hayo yaliyotangulia: Hakika Manabii waliotangulia kuhiji, na huwenda wafuasi wao wakawa waliamirishwa kuhiji, na pengine hawakuamrishwa kuhiji.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas