Damu ya Mtume S.A.W

Egypt's Dar Al-Ifta

Damu ya Mtume S.A.W

Question

Imepokelewa kutoka kwa baadhi ya Masahaba wakarimu kuwa walikunywa damu ya Mtume, S.A.W, je, damu ya Mtume S.A.W. ni twahara na inaruhusiwa kuinywa? Na kama haiwezekani, basi nini mwongozo wa kisheria kwa kitendo hiki kinachotendwa na Masahaba? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu..
Hadithi ya kunywa baadhi ya Masahaba damu ya Mtume S.A.W, kwa makusudi ilitajwa katika mapokezi kadhaa kwenye vitabu vya Hadithi, mapokezi haya yalielezwa katika vitabu vya Fiqhi kwenye mlango wa twahara, As-Suyutiy ameyakusanya katika kitabu cha Al-Khasais, akisema: “mlango wa kuhusika kwake S.A.W kwa utwahara wa damu yake, mkojo wake, na choo chake”:
Imepokelewa kutoka kwa Al-Ghitrif katika sehemu yake, At-Twabaraniy na Abu Naim kutoka kwa Salman Al-Faris kuwa aliingia Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., wakati Abdullah Ibn Al-Zubair alipokuwa na sahani anakunywa yaliyo ndani yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia, S.A.W,: "Unafanyaje" akasema: nilipenda iwe damu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., iwe ndani ya kinywa changu! Mtume S.A.W., akasema: "Ole wako kutokana na watu na ole wao wale watu kutokana na wewe, wala moto haukugusii ila kwa kula kiapo cha kutokukugusa".
Na imepokelewa kutoka kwa Ibn Hibbaan katika kitabu cha Al-Dhuafaa kutoka kwa Ibn Abbas alisema: Mtume S.A.W., alifanywa uumikaji na mvulana mmoja wa Maquraish, yule mvulana alipomaliza kufanya hivyo alichukua damu ya Mtume S.A.W. akaenda na kunywa kisha akarudi Mtume S.A.W. akamtazama na kusema: "Ole wako umefanya nini kwa damu yangu" alisema: Ewe Mtume wa Allah sitaki kumwaga damu yako katika ardhi kwa hivyo, damu iko katika tumbo langu, alisema: "Nenda, tayari umeshajihifadhi nafsi yako kutokana na moto".
Na imepokelewa kutoka kwa Al-Daraqutwniy katika Sunan yake kutoka kwa Asmaa binti yake Abu Bakr alisema: Mtume, S.A.W. alifanya uumikaji akampa damu yake mwanangu akainywa akamjia Jibril alimwambia, akasema: "umefanya nini" akasema: nilichukia kumwaga damu yako! Mtume, S.A.W. akasema: "moto haukugusi" na akamfuta juu ya kichwa chake na kusema: "Ole wako kutokana na watu na ole wao wale watu kutokana na wewe".
Vile vile imepokelewa kutoka kwa Al-Bazzar na Abu Yaala na Ibn Abi Khaithamh na Al-Baihaqiy katika Sunan, na At-Twabaraniy kutoka kwa Safinah alisema : Mtume, S.A.W. alifanya uumikaji akaniambia: "uifiche damu hii" nikaenda na kuinywa kisha nilikuja, akasema: "umefanya nini": nikasema nimeificha! Akasema: "umekunywa" Nilisema: Ndiyo. akatabasamu.
Pia imepokelewa kutoka kwa Al-Bazzar, At-Twabaraniy, Al-Hakim na Al-Baihaqiy katika Sunan na kwa mapokezi mazuri kutoka kwa Abdullah Ibn Al-Zubayr alisema : Mtume, S.A.W. alifanya uumikaji, akanipa damu, alisema: "Nenda uifiche". Basi nikaenda na kuinywa kisha nilimjia Mtume S.A.W akaniambia: "Ulifanya nini" Nilisema: nimeificha. Akasema: "Labda umekunywa" Nilisema: Nimeinywa.
Na imepokelewa kutoka kwa Al-Hakim kutoka kwa Abu Said alisema : Mtume S.A.W., alijeruhiwa katika siku ya Uhud baba yangu akamfuta damu kutoka uso mpaka mdomo wake, Mtume S.A.W. alisema : "Anayependa kumwangalia mtu aliyechanganya damu yangu na damu yake amwangalie Malik Ibin Sinan".
Na imepokelewa kutoka kwa Ibn Sikin na Al-Tabarani katika kitabu cha Al-Awsat kuwa alisema: "Damu yake na damu yangu imechanganywa na moto haumgusi".
Na imepokelewa kutoka kwa Abu Yaala, Al-Hakim, Al-Daraqutwniy, Al-Tabarani na Abu Naim kutoka kwa Ummu Ayman alisema: Mtume S.A.W. aliamka katika usiku akakojolea chombo maalumu, nikaamka usiku nilipokuwa na kiu nikanywa yaliyomo ndani ya chombo hicho, na wakati alipoamka asubuhi nikamwambia akatabasamu na kusema: "Tumbo lako halitaumwa kamwe". Na kutoka kwa Abu Yaala akasema: "Hutalalamika kwa tumbo lako baada ya siku hii kamwe".
Na imepokelewa kutoka kwa Al-Tabarani na Al-Baihaqiy kwa mapokezi mazuri kutoka kwa Hakimah binti yake Umaimah kutoka kwa mama yake akasema : alikuwa ni Mtume S.A.W alikuwa na kombe anakojoa ndani yake na kuiweka chini ya kitanda chake, hivyo akaamka akakitafuta, lakini hakukikuta, akakiulizia akisema: "kombe liko wapi?" aliambiwa kuwa: kijakazi wa Ummu Salamah aliyekuja pamoja naye kutoka nchi ya Uhabeshi na anayeitwa Burah alikunywa. Mtume, S.A.W. alisema: "amejihifadhi nafsi yake na moto". [Al-Khasais Al-Kubra 2/440, 441, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Na mwenye kuangalia mapokezi haya yaliyopokelewa kutoka kwa Imam Al-Suyuti ataona kwamba baadhi ya mapokezi haya ni sahihi na mengine ni dhaifu, na mapokezi haya yanaweza kuzingatia kunywa Masahaba hawa damu yake Mtume S.A.W, kunaruhusiwa na katika Sunna iliyokubaliwa na Mtume S.A.W.
Lakini nini kuhusu mtazamo wa kufanya hivyo kutoka kwa Masahaba? Hakuna shaka kwamba waliona kuwepo kwa sifa za kimwili na kiroho zinazowafanya kushughulikia kwa njia hii, na kwa hiyo hawakunywa damu yake tu, lakini walifanya hivyo katika mambo mengine, kama vile kunywa mkojo kama yalivyotajwa na katika mambo mengi yanayohitaji muda mrefu ili kuyataja.
Sifa hizi zilikuwa katika mawazo ya Masahaba, na zilionekana katika mazungumzo yao pamoja na Mtume S.A.W katika nyakati kadhaa, zikiwemo :
Imepokewa kutoka kwa Aisha, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alikuwa kama akiwaamuru, aliwaamuru kufanya vitendo wanavyoweza tu, walisema: Sisi sio kama wewe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amekusamehe madhambi yako yaliyotangulia na yaliyochelewa, Mtume S.A.W. alikuwa akikasirika hata hasira zake zinaonekana katika uso wake, kisha anasema: "Hakika mimi ninamcha Mwenyezi Mungu zaidi kuliko nyinyi na ninamjua zaidi kuliko nyinyi". [Imepokelewa kutoka kwa AL-Bukhariy].
Imepokelewa kutoka kwa Umar Ibn Abi Salamah, kuwa alimwuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W akisema: Funga inakubaliwa? Mtume wa Allah akamwambia, A.S: "Mwulize yule" anakusudia Umm Salamah, akamwambia kuwa Mtume, S.A.W. alikuwa akifanya hivyo, alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amekusamehe madhambi yako yaliyopita na yajayo, Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia, A.S: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu, mimi ninamcha Mwenyezi Mungu zaidi kuliko nyinyi na ninamwogopa zaidi kuliko nyinyi" [Imepokelewa kutoka kwa Muslim].
Na imepokelewa kutoka kwa Aisha, kwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume, S.A.W. anamwuliza kuhusu Fatwa moja, naye Aisha anawasikia kutoka nyuma ya mlango, mtu yule alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unafika wakati wa Swala nami ninajanaba, inaruhusiwa kwangu kufunga ? Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alisema: "Hata mimi unafika wakati wa Swala nami nana janaba na ninafunga", mtu yule alisema: wewe si kama sisi, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tayari Mwenyezi Mungu ameshakusamehe madhambi yako yaliyopita na yajayo, Mtume S.A.W. akasema: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu, kwamba Mimi ninamwogopa Mwenyezi Mungu zaidi kuliko nyinyi, na ninajua vipi kumcha zaidi kuliko nyinyi". [Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Muslim].
Imepokewa kutoka kwa Al-Mughirah Ibn Shubah alisema kuwa Mtume S.A.W. alisimama kuswali tahajud mpaka ikivimba miguu yake. Akaambiwa kuwa taabu yote hiyo unachukua ya nini na hali Mola wako ameshakusamehe madhambi yako yaliyotangulia na yajayo, akasema: "Basi siwi mimi mja mwenye kushukuru ?". [Bukhariy na Muslim].
Na imepokewa kutoka kwa Aisha, alisema: kama Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W akisimama kuswali tahajud mpaka hupasuka miguu yake, Aisha akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unafanya hivyo na hali yako umeshasamehewa madhambi yako yaliyotangulia na yajayo, alisema: "((Ewe Aisha, Basi siwi mimi mja mwenye kushukuru?" [Bukhariy na Muslim]
Na imepokewa kutoka kwa Aisha, R.A, alisema: Mtume S.A.W. aliwakataza Masahaba zake kufunga bila ya kula daku kwa ajili ya kuwahurumia, walisema: hakika wewe huli daku, akasema: "Mimi hali yangu si kama hali yenu, Mola wangu ananilisha na ananinywesha". [Bukhariy na Muslim].
Na imepokewa kutoka kwa Anas: kwamba mamake Ummu Sulaymmi alikuwa akimtandikia Mtume S.A.W. Busati la Ngozi akilala Bwana Mtume S.A.W. kisha alikua akichukua Jasho la Mtume S.A.W. na Nywele zake akizikusanya katika Kichupa kisha huziweka katika Mafuta mazuri, akasema : siku akifa babu yangu Anas bin Malik R.A alinipa Wasiya ziwekwe hizo Nywele na jasho lake Mtume S.A.W. katika zile vitu anavyowekewa Maiti akifa katika Mafuta mazuri na vitu vingine zikienezewa katika Sanda. [Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Al-Bukhari].
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah, au kutoka kwa Abu Sa'id -Shak Al-Aamash- alisema: Katika siku ya vita vya Tabuk Waislamu walikuwa na njaa sana hivyo walimuuliza Mtume, S.A.W. : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., lau ungetupa ruhusa kuchinjwa ngamia wetu na kula nyama zao na kutumia mafuta yao? 'Mtume S.A.W., akawapa ruhusa. Kwa mujibu huo huo Omar alisema: 'Ewe Mtume S.A.W., kama tukifanya hili, usafiri wetu utakuwa wa tabu. Lakini mwite kila mtu kuleta chochote alichonacho kisha mwombe Mwenyezi Mungu kuwabariki, labda Mwenyezi Mungu awahifadhi baraka zao. Mtume, S.A.W. alikubali, kisha akaomba busati la ngozi akaliweka. Kisha aliwataka Maswahaba zake kuleta chochote walichokuwanacho, na hivyo walifanya. Mmoja wao kaleta baadhi ya maharage, mwingine kaleta baadhi ya tende, wa tatu kaleta kipande cha mkate mpaka vitu hivi vikawekwa juu ya busati. Kisha Mtume, S.A.W. aliwaombea baraka. Kisha alisema: Chukueni mabakuli yenu, basi wakachukua mabakuli yao, na halikubaki bakuli moja tupu katika kambi nzima. Alisema : walikula mpaka wakashiba, na bado kuna baadhi ya mabakuli! Mtume, S.A.W., alisema: 'Ninashuhudia kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, na kwamba mimi ni Mtume wake. Hakuna mja ambaye hukutana na Mwenyezi Mungu kwa yakini hii, kisha azuiliwe na peponi. [Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Muslim].
Na imepokewa kutoka kwa Iyaas ibn Salamah, kutoka kwa baba yake, alisema: tulitoka pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W katika vita, tukachoka sana hivyo tukaamua kuchinja baadhi ya ngamia wetu, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W aliamuru tukusanye vitu vya ziada, tukaweka busati la ngozi, vitu hivi viliwekwa juu ya busati hili, alisema: nikaamua kuvihisabu ni vingapi? Nikavihisabu kama zizi la kondoo, na idadi yetu ilikuwa Elfu moja na mianne alisema: tulikula mpaka tulishiba sote, kisha tulijaza mikoba yetu, Mtume wa Allah S.A.W alisema: "Je, kuna yeyote ana maji ili kutia udhu ?" Akasema: mtu akaleta maji machache akayaweka ndani ya bakuli, tukatia udhu sote, alisema, kisha wakaja watu wanane, wakasema: Je, kuna maji mengine? Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W akasema: "Kutawadha kumemaliza" [Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Muslim].
Imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdullah, R.A. alisema: Nilikuwa pamoja na Mtume S.A.W wakati wa swala ya Al-asiri ulifika na hatuna maji ila machache tu, maji haya yaliwekwa kwenye bakuli, kisha lililetwa kwa Mtume S.A.W. akaingiza mkono wake ndani yake na kufungua vidole vyake akisema: "Njooni kwa ajili ya udhu, baraka kutoka Mwenyezi Mungu", nimeona maji yanapasuka kutoka kati ya vidole vyake, watu wakatawadha na kunywa, nikamuuliza Jabir: Mlikuwa wangapi siku hiyo? Alisema: tulikuwa elfu na mia nne. [Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Al-Bukhari].
Katika Hadithi ya Ummu Ma’bad, Mtume S.A.W akamkama yule mbuzi aliyekonda sana, na akawanywesha waliokuwa ndani ya nyumba kisha akaacha chombo kilijazwa maziwa, na katika Hadithi hii: wakati Mtume S.A.W. alipoondoka, Abu Ma’abad alirudi akiwaswaga kondoo waliokonda, akaona kuwa yako maziwa nyumbani, akasema: umepata haya kutoka wapi? Ummu Ma’bad akasema: alipita kwetu mwanamume mwenye baraka”. [Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Al-Baghawi katika kueleza kwa Sunna, Ibn Abd Al-Barr katika kitabu cha Al-Istiaab, na Ibn Al-jawzi katika kitabul Wafaa, na Hadithi hii ina kisa.
Na imepokewa kutoka kwa Harith ibn Amr As-sahmi alisema: "Nilimjia Mtume S.A.W, wakati alipokuwa kwenye Mina Au Arafaat ambapo watu walimzunguka, Harith ibn Amr As-sahmi alisema: mabedui wakimjia na kuona uso wake Mtume S.A.W wakisema: Huu ni uso wenye Baraka" [Imepokewa kutoka kwa Abu Daawud].
Na imepokewa kutoka kwa Aisha, R.A. kwamba "Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alikuwa kama akilalamika alijisomea Suratul Falaq na Suratun Naas, wakati ugonjwa wake ulipozidi nilikuwa nikimsomea, na kumfuta kwa mkono wake wa kulia nikitarajia baraka zake". [Bukhariy na Muslim]
Na imepokewa kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah, R.A akasema: "Wakati wa kuchimba Handaki niliona Mtume S.A.W. ana njaa kali, nikarudia kwa mke wangu haraka nikimwuliza: Je, unacho chakula chochote? Kwani niliona Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. ana njaa kali, naye akanitolea mfuko wa ngozi ndani yake kuna pishi ya shairi (nafaka kama ngano), na tulikuwa na mnyama wa kufugwa nyumbani nikamchinja, na mke wangu akasaga shairi, akamaliza kusaga nilipomaliza kuchinja, nikakata nyama, kisha nikaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W, mke wangu aliniambia: usinifedheheshe mbele ya Mtume wa Allah S.A.W, na Masahaba zake ambao ni pamoja naye, nikamjia nikamfurahisha, nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tulimchinja mnyama wetu na tukasaga pishi ya shairi tuliyokuwa nayo, basi uje wewe na watu wawili au watatu tu pamoja nawe, Mtume S.A.W. akaita akisema: Enyi watu wa handaki, Jabra ametayarisha chakula, basi njooni, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akasema: msiweke sufuria, wala msipike mkate mpaka nifike, nikafika pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W akitanguliza Masahaba zake, nilipofika kwa mke wangu akanilaumu, nikamwambia kuwa nilifanya kama ulivyo niambia, mke wangu akaniletea baadhi ya unga naye Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W akatema mate katika unga huu na akauombea baraka, kisha akatema mate katika nyama pia na akaiombea baraka, halafu akasema: mwite mpishi ili apike pamoja nawe, na ulete nyama kidogo kidogo tu, na idadi ya Masahaba siku ile ni elfu, akaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa: walikula hadi wakaondoka na nyama yetu ilikuwa kama ilivyo, na unga wetu ulikuwa kama ulivyo" [Bukhariy na Muslim].
Na imepokewa kutoka kwa Qatada, alisema: tumehadithiwa na Anas Ibn Malik akisema: "Mtume S.A.W. alikuwa akiwatembelea wake zake wakati wa mchana na usiku, nao walikuwa kumi na moja, nikamwambia Anas. Alikuwa akiwaweza? Alisema: Tulikuwa tukisema kwamba alipewa Nguvu ya wanaume thelathini". [imepokewa kutoka kwa Al-Bukhariy].
Imepokewa na imethibitika kutabaruku kwa athari zake katika maisha yake:
Imepokewa kutoka kwa Aisha, R.A: "kuwa Mtume S.A.W alikuwa akiletewa watoto wadogo, basi akiwaombea baraka na akiwafanyia tahniik (kumtafunia mtoto tende na kumlisha". [Imepokewa kutoka kwa Muslim].
Katika Hadithi ya mkataba wa Al-Hudaibiya kuwa: "Urwah alirudia wenzake, akasema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu nilikuwa na wafalme; nilikuwa na Kaisari, Kisra na Al-Najashi, naapa kwa Mwenyezi Mungu, sikumwona mfalme kamwe kuheshimiwa na wenzake kama Masahaba wanavyomhishimu Muhammad S.A.W., naapa kwa Mwenyezi Mungu kama Mtume S.A.W. akitema mate, basi mate haya yanaangukia kiganjani mwa mmoja wao akipaka kwake uso wake na ngozi zake, na kama akiwaamuru wanashindana katika kutekeleza amri yake, na kama akitawadha wanakaribia kupambana kwa ajili ya kutabaruku kwa maji ya udhu wake, na kama akizungumza, wanaangusha sauti zao mbele yake, wala hawamwangalii vibaya kwa ajili ya kumhishimu". [Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhariy].
Imepokelewa kutoka kwa Muhammad Ibn Sereen kutoka kwa Anas, alisema: "Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. aliponyoa nywele zake kwenye Mina, alichukua nusu ya nywele zake kwa mkono wake wa kulia, alipomaliza akanipa nywele hizi na akaniambia: Ewe Anas, uende kwa nywele hizi kwa Ummu Sulaim, Masahaba walipoona hivi walishindana katika nusu nyingine ya nywele zake, mmoja wao akichukua baadhi ya nywele na mwengine akichukua baadhi nyingine", Mohammed alisema: nilimuhadithia Obeida Al-Salmani Hadithi hii, akasema: kama nikiwa na nywele moja kutokana na nywele zake ni bora kwangu zaidi kuliko chochote duniani". [Imepokewa kutoka kwa Ahmad, na asili yake katika vitabu viwili vya sahihi].
Maswahaba wanaendelea kutabaruku kwa athari zake tukufu baada ya kifo chake:
Imepokewa kutoka kwa Aisha, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., amekufa, na tunayo baadhi ya shairi, tukala kutoka shairi hii muda mrefu, kisha nikamwambia kijakazi kuipima, akaipima, shairi hii haikubaki muda ila ilikwisha, Aisha akasema: kama hatukuipima tukala zaidi. [Imepokewa kutoka kwa Al-Tirmidhi: Na akasema: Hadithi hii ni sahihi. Na asili yake katika vitabu viwili vya sahihi].
Na imepokewa kutoka kwa Othman Ibn Abdullah Ibn Mohab, alisema: nilitumwa kwa Umm Salamah, mke yake Mtume S.A.W., kwa chombo cha maji ndani yake baadhi ya nywele za Mtume S.A.W. kama mtu yeyote akipatikana na Hasada (jicho) au Ugonjwa, akamtumia chombo chake, nikaangalia, nikaona baadhi ya nywele zake za rangi nyekundu. [Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari].
Katika Hadithi ya Al-Baihaqiy: imepokelwa kutoka kwa Othman Ibn Abdullah Ibn Mohab, alisema: Umm Salamah alikuwa na chombo kikubwa cha fedha, ambapo nywele zake Mtume S.A.W., zilihifadhiwa ndani yake, kama mtu yeyote akipatikana na homa, akamtumia chombo chake, akatia Unywele wake Mtume S.A.W. katika chombo kikiwa na maji, kisha akakisukasuka kisha akatolewa Unywele wake Mtume S.A.W. kisha mgonjwa anapaka uso wake kwa maji hayo, Othman Ibn Abdullah alisema: nikatumwa kwa Umm Salamah nikaangalia, nikaona baadhi ya nywele zake za rangi nyekundu. [Dalail Al-Nubuwah kwa Al-Baihaqiy 1/237].
Na imepokewa kutoka kwa Asmaa alisema: Hili ni juba la Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. na akaniletea juba lenye Dibaaj (aina ya hariri), alisema: Hili lilikuwa pamoja na Aisha mpaka akafariki, na wakati alipofariki nikalichukua juba hili, na Mtume, S.A.W. alikuwa akilivaa, basi tunaliosha kwa wagonjwa ili kutibiwa kwake. [Imepokelewa kutoka kwa Muslim].
Imepokewa kutoka kwa Hamid, kutoka kwa Anas kuwa alifanywa ndani ya sanda yake mkwiji wa miski au miski ndani yake baadhi ya nywele zake Mtume S.A.W. [Imepokewa kutoka kwa Ibn Abi Shaybah].
Bado kutabaruku kunaendelea baada ya zama za Masahaba:
Al-Qadhi Ibn Iyadh alisema: "Tuliambiwa na Al-Qadhi Abu Ali kutoka kwa Sheikh wake Abu Al-Qasim Ibn Al-Ma’mun, alisema: (Tumekuwa na bakuli ya miongoni mwa mabakuli ya Mtume S.A.W … basi tulikuwa tukiliwekea maji kwa ajili ya wagonjwa ili watibiwe kwake". [Al-Shifa Bitarif Huquq Al-Mustafa 1/638, Dar Al-Fayhaa]
Wanavyuoni wengi wa Fiqhi wametaja mengi miongoni mwa tulivyotaja kuhusu suala hili:
Al-Khatib El-Sherbini alisema: "Kinyesi hichi cha Mtume S.A.W. ni twahara na hakina najisi kama ilivyoelezwa na Al-Baghawi na wengine, na imesahihishwa na Al-Qadhi na wengine, na ilitolewa Fatwa na Sheikh wangu kinyume na yale yaliyo kwenye [Al-Sharhu Al-Saghiir wa Al-Tahqiiq], kwa sababu Barakah wa mhebeshi alikunywa mkojo wake S.A.W. akasema: "Tumbo lako halitaingiwa na moto". imesahihishwa na Al-Daraqutni. Abu Jaafar Al-Tirmidhi alisema: damu ya Mtume S.A.W. ni twahara kwa sababu Abu Taibah aliikunywa, na Ibn Al-Zubair alifanya hivyo alipokuwa mvulana wakati Mtume S.A.W alipompa damu ya uumikaji ili aizike, basi akaikunywa. Mtume S.A.W alisema: “Mwenye kuchanganywa damu yake na damu yangu moto haukumgusia”. [Mughni Al-Muhtaj 1/233, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Al-Bahuatiy alisema: "na vitu vya najisi kutoka kwetu ni twahara kutoka kwake S.A.W", na Manabii wengine, na inaruhusiwa kutibiwa kwa mkojo wake na damu yake S.A.W.; kufuatana na iliyopokelewa kutoka kwa Al-Daraqutwniy kuwa Umm Ayman amekunywa mkojo wake, S.A.W Mtume akasema: "Tumbo lako halitaingia motoni", lakini Hadithi hii ni dhaifu. Na kufuatana na iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Hibban katika kitabu cha Al-Dhuafaa kwamba mvulana akamfanyia Mtume S.A.W. uumikaji, alipomaliza akanywa damu yake akasema: "Ole wako umefanyaje kwa damu?" alisema: nimeificha katika tumbo langu. Mtume S.A.W. akasema: "Nenda, tayari umeshajihifadhi nafsi yako kutokana na moto". Al-Haafidh Ibn Hajar alisema: Kana kwamba siri ni katika hili walilofanya Malaika kutokana na kuosha kifua chake. [Kashaaf Al-Qinaa 5/31, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kusema hivyo kwa Manabii wote pia ilielezwa na Al-Bajirmi katika maelezo yake katika kitabu cha: [Al-Qinaa 1/314, Dar Al-Fikr].
Sheikh Zakaria Al-Ansari alisema: "Masahaba walikuwa wakitabaruku na kutibiwa kwa mkojo wake na damu yake S.A.W" imepokelewa kutoka kwa Al-Daraqutni kuwa Umm Ayman amekunywa mkojo wake, Mtume S.A.W. akasema: "Tumbo lako hataingia motoni)), lakini Hadithi hii ni dhaifu. Na kufuatana na iliyopokewa kutoka kwa Ibn Hibban katika kitabu cha Ad-Dhuafaa kwamba mvulana akamfanyia Mtume S.A.W. uumikaji, alipomaliza akanywa damu yake akasema: "Ole wako umefanyaje kwa damu?" alisema: nimeificha katika tumbo langu. Mtume S.A.W. akasema: "Nenda, tayari umeshajihifadhi nafsi yako kutokana na moto", Sheikh wetu alisema: Kana kwamba siri ni katika hili walilofanya Malaika kutokana na kuosha kifua chake. [Asna Al-Matwalib 3/106, Dar Al-Kitab Al-Islamiy].
Kutokan na yaliyotangulia hapo juu, inaonekana kuthibitishwa kwa utwahara wa damu ya Mtume S.A.W. na sababu za imani ndizo zilizowafanya Masahaba kunywa na kuiingia katika matumbo yao na kuichanganya na damu yao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas