Kununua Bidhaa za Ushuru wa Forodha...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kununua Bidhaa za Ushuru wa Forodha

Question

 Ni ipi kuhumu ya kushiriki katika mnada wa vitu vilivyotaifishwa na mamlaka ya mapato?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Wakati mwengine mamlaka ya mapato hutangaza kuuza vitu na bidhaa ambazo zipo chini yake, na vitu hivi vinavyopigwa mnada kwa asili si miliki ya mamlaka ya mapato, lakini imevichukua kutoka kwa wamiliki wake, ambapo wamiliki hao wanafahamika, na mamlaka ya mapato inavichukua vitu hivyo kwa sababu mbalimbali, na inafahamika hatua hiyo ya kuchukuliwa bidhaa hizi na mamlaka ya mapato kupitia sheria ya ushuru wa forodha namba 66 ya mwaka 1963, na mada zilizomo ndani ya sheria hiyo kuhusiana na swali letu, ni kutoka katika kipengele cha 121 mpaka 129, na katika yale yaliyoelezwa ndani ya vipengele hivyo ni aina za makosa ya uhalifu yaliyopitishwa na sheria hii, pamoja na adhabu zilizoainishwa, ni pamoja na mamlaka ya mapato kuwa na haki ya kuuza bidhaa ambazo zimeshikiliwa na mamlaka hiyo baada ya kupita muda uliopangwa na sheria hii.
Mamlaka ya mapato, huwa inachukua kodi ya bidhaa zilizoingia kutoka nchi nyengine. Na hii ni aina moja kati ya aina za kodi, nayo huwekwa kodi hii kwa mwenye kumiliki mali, mfanya kazi na mapato mengine kwa ajili ya taifa, hutofautiana kwa tofauti ya sheria na mazingira, kama ilivyo kwenye kamusi ya Al-Wasit, 1/537.
Maelezo kuhusu hukumu ya suala hili yanahitaji kwanza maelezo ya hukumu ya ulipaji kodi, kisha hukumu ya uuzaji wa bidhaa zilizotaifishwa, na mwishowe ni hukumu ya upigaji mnada.
Kwanza: Hukumu ya kodi kwa wananchi:
Inafaa kwa serikali au mtawala kulazimisha kodi kwa wananchi ikiwa serikali inahitaji fedha za kodi kwa lengo la kuzitumia kwenye masilahi ya taifa, kwa sharti la kutokuwepo kiwango cha kutosha kwenye mfuko mkuu wa mapato.
Na dalili ya hilo ni kuwa dharura huhalalisha yaliyozuiliwa. Ikiwa matumizi ya nchi yamekuwa mengi lakini wakati huo huo mfuko mkuu wa mapato ya taifa hautoshi, basi ni lazima Waislamu kukamilisha kilichopungua ili kukidhi mahitaji, lakini kwa wale wenye vigezo au uwezo wa kufanya hivyo, kwa sababu jambo la lazima lisipo kamilika ila kwa kitu fulani basi kitu hiko huwa kinakuwa ni lazima pia.
Masuala haya yanafungamana na kile kinachofahamika kwenye Fiqhi kama ni masuala yanayosema: Je kwenye mali ya umma kuna haki nyengine zaidi ya zaka au hakuna? Kauli yenye nguvu ni kuwa, ni lazima ikiwa Waislamu wana hiyajio kubwa katika hilo kama tulivyoeleza, na dalili katika hilo zitakuja kwenye maelezo ya Imamu Al-Qurtwubiy. Na kiongozi wa nchi anatakiwa kukusanya kodi kutoka kwa wananchi, lakini hata hivyo nafsi hailazimishwi kwenye jambo lililo nje ya uwezo wake. Na mfano wa kauli yetu hii umeelezwa pia na jopo kubwa la wanachuoni:
Imamu Al-Qurtwubiy amesema kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na anawapa mali, kwa kupenda kwake} [AL BAQARAH 177]. Imechukuliwa aya hii kuwa ni dalili kwa wale wenye kusema: Katika mali kuna haki zengine mbali na Zaka, na kwa haki hizo ndio ukamilifu wa kufanya wema unapatikana. Na ikasemwa: Kusudio hapa kwenye hii aya ni Zaka ya Mali, na kauli ya kwanza ndio sahihi zaidi, kutokana na yaliyopokelewa na Fatuma Bint Qais amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W: “Hakika kwenye mali kuna haki nyengine isiyokuwa zaka” kisha akasoma Aya hii: {Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu...} mpaka mwisho wa Aya hii ya 177 ya Surat AL BAQARAH.
Na imepokewa kutoka kwa Ibn Majah katika kitabu cha Tirmidhy, na amesema: Hadithi hii hailikusudii suala hilo, na Abu Hamza Maimuun ameifanya kuwa ni Hadithi dhaifu. Na yamepatikana maelezo ya Ismail Ibn Salim kwenye Hadithi hii kauli yake: Nayo ni kauli sahihi zaidi. Nikasema: Hadithi hii hata kama itakuwa na maelezo ndani yake lakini inaonesha usahihi wake kwa maana iliyopo kwenye Aya hiyo ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka} imetajwa zaka pamoja na swala, na hiyo ni dalili ya kusudio la Mwenyezi Mungu kwenye kauli yake: {na anawapa mali, kwa kupenda kwake} kwa maana sio mali ya zaka tu. Naye Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi Zaidi.
Wanachuoni wamekubaliana kuwa: Ikiwa kwa Waislamu kumekuwa na hitajio kubwa la mali baada ya kukusanywa mali ya zaka, basi ni lazima itumike mali kwenye mahitaji hayo. Amesema Malik –Mwenyezi Mungu Amrehemu– watu wanalazimika kuwalipia fidia mateka wao hata kama hilo litawagharimu mali zao, na kauli hii ya wanachuoni, nayo inayapa nguvu yale tuliyoyaeleza na ambayo yanakubaliana na kauli ya Mola. [Kitabu Al-Jamii li Ahkam Al-Qurani, 2/242 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Araby].
Amesema Ibn Abideen, kwenye kitabu cha Al-Qaniya, na amesema Abu Jaafar Al-Balkhiy: Kile kinachoamrishwa na Mfalme kwa wananchi wake na kikawa na masilahi kwao hicho ndicho kinachokuwa deni na ni lazima, pia ni haki inayopaswa kutolewa kama vile mali ya kuokotwa chini ya ardhi. Na wamesema Masheikh wetu: Kila kinacholazimishwa kwao na Imamu kwa masilahi yao basi jibu lake ni hili, hata ikiwa kwenye malipo ya walinzi, kwa ajili ya kulinda barabara, wezi, waporaji na wavunja milango, hili linafahamika, lakini haufahamiki wasi wasi wa fitina. Kisha akasema: Katika hili kuchukuliwa mali za kwenye mifuko ya watu kwa lengo la kuleta mabadiliko kwenye masilahi ya umma ni jambo la lazima na wala haifai kulikwepa na wala sio dhuluma, lakini jibu hili linafundisha kuifanyia kazi amri ya mtawala na kuzuia kuomba kwa Sultani katika juhudi zake, na wala kusiwe kwa lengo la kupata umaarufu ili kuepusha kukusanywa mali zaidi ya kiwango kinachopaswa kukusanywa, nikasema: Inapaswa kufungamanishwa hilo ikiwa kwenye mfuko mkuu wa mapato hakuna mali inayotosheleza kwa ajili ya mahitaji hayo, kama ilivyokuja kwenye amri ya kupambana jihadi kuwa inachukiza kukusanya fedha za malipo ikiwa kipo chenye kutosha”. [Kitabu Radd Al-Muhtar ala Dur Al-Mukhtar, 2/57, chapa ya Ihyaa Al-Turath].
Na amesema Abu Ya’aly Al-Hanbaliy: “Aina ya pili ni kuwa, matumizi yake yanatekelezwa kwa njia ya masilahi ya umma na si vinginevyo, kulazimika kwake kunazingatiwa kuwepo sio kukosekana. Ikiwa mali zipo ndani ya mfuko mkuu wa mapato ni lazima itumike na ulazima wa kutoa kwa Waislamu utaondoka. Na ikiwa kwenye mfuko mkuu wa mapato ya nchi hakuna fedha basi utakosekana ulazima wa kutumika mfuko huo. Na ikiwa – madhara yake yataenea – kwa Waislamu wote, kwa ulazima wa kutosheleza, basi baadhi yao watatosheleza kutelekeza kama vile jihadi.
Na ikiwa madhara yake si yenye kuenea kwa wote kama vile uharibifu wa barabara ya karibu lakini kukawa na barabara nyingine ya mbali, au kukatika kwa maji ya kunywa lakini watu wengine wanapata huduma ya maji, ikiwa utaondoka ulazima wa kutumika mfuko mkuu wa pato la taifa kwa kukosekana mali basi ulazima unaondoka pia kwa wote kwa kuwepo huduma mbadala. Ikiwa kwenye mali ya umma kutakuwa na haki mbili, moja ikakosa fedha, nyengine ikapata fedha basi fedha hiyo itatumika katika haki ambayo itakuwa ndani yake kuna deni. Na ikiwa haki zote mbili zimekosa fedha, basi inapaswa kwa Mkuu wa mambo ya nchi ikiwa atahofia madhara na uharibifu kukopa kwenye mfuko mkuu wa mapato kiwango kitakacho kidhi mahitaji pasi na kuongeza.
Na ikiwa mali kwenye mfuko mkuu wa fedha za umma imezidi zaidi ya matumizi yake, hapo imesemwa: Itahifadhiwa kwenye mfuko mkuu wa mapato kiwango kitakacho walazimu Waislamu kwenye tukio, na ikasemwa: Itatenganishwa ile itakayo simamia masilahi ya Waislamu wote na wala haitahifadhiwa, kwa sababu kile kinacholazimu kitalazimishwa kwa Waislamu pale litakapotokea jambo. Vigawanyo hivi vinne vimewekwa kwenye kanuni. [Kitabu Al-Ahkam Al-Sutwaniya cha Aby Ya’alaa, uk. 253, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya].
Pili: Kuhusu hukumu ya forodha:
Kiasili hukumu ya forodha ni sehemu ya kodi, lakini yenyewe huwa zaidi ya kodi kwa kuwa ndani yake kuna sehemu inayochukuliwa kwa njia ya kuimarisha mapato ya nchi, kama ilivyotangulia kuelezea masuala haya, na suala la kuimarisha mapato linafaa, kutokana na kuwepo matamshi mengi katika hili, na kufanyiwa kazi pia na baadhi ya Makhalifa, na kuelezewa pia na baadhi ya wanachuoni. Yametajwa yote haya kwa dalili zake:
Ibn Al-Qayyim amesema: “Ama kuweka adhabu za mali, ni jambo la kisheria kwenye maeneo maalumu ndani ya madhehebu ya Imamu Malik na Ahmad, na kauli ya Imamu Shafi, imekuja Hadithi toka kwa Mtume S.A.W, na Masahaba wake sehemu mbalimbali: Miongoni mwazo: Ni kuhalalisha kwake Mtume S.A.W, kuchukua mali kwa ambaye atakutwa anawinda katika mji wa Madina. Pia mfano wa amri yake Mtume S.A.W, ya kuvunja vyombo vilivyohifadhiwa pombe na kuyabana mazingira yake.
Mfano wa amri ya Mtume S.A.W, kwa Abdillah Ibn Umar ya kuzichoma moto nguo zilizo na chapa ya mmea ambao maua yake hutumika kwenye kutengenezea ladha ya chakula. Mfano pia amri ya Mtume S.A.W, siku ya Khaibar ya kuvunjwa vyombo ambavyo vilitumika kupikia nyama ya nguruwe au visafishwe, hapa imeonesha kufaa kwa mambo mawili, kwa sababu adhabu haikuwa lazima itekelezwe kwa kuvunja. Mfano wa kuvunja kwake Msikiti wa Al-Dhirar, mfano pia wa kuchoma vitu vya thamani, mfano mwengine wa kuongeza gharama kwa mwizi ambaye hakuingia kwenye hukumu ya kukatwa mkono, mfano wa kuongeza kwake Mtume S.A.W, gharama kwa mfichaji aliyepotoka, mfano pia wa kuchukua fungu la mali kwa mwenye kuzuia Zaka, ni dhamira katika dhamira za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na mfano wa amri yake Mtume kwa mwenye kuvaa pete ya dhahabu kuivua na akaivua hakuna aliyepinga, mfano wa Nabii Musa A.S. kuamrisha kuchomwa moto ndama wa dhahabu aliyekuwa anaabudiwa na Waisraeli na kutupwa masalio yake kwenye kisanduku, mfano wa Wayahudi kukata mitende kwa chuki zao, mfano wa Umar R.A. kuchoma moto sehemu ambayo inauzwa pombe, mfano wa Umar pia kuchoma moto hekalu la Sa’ad Ibn Aby Wiqaasw, pindi alipowazuia raia ndani yake. Mambo haya ni sahihi na yanafahamika, si jambo jepesi kutoa wito wa kuondoshwa kwa adhabu hizi. Na mwenye kusema kuwa: Adhabu za mali zimefutwa, hakika atakuwa amekosea kwenye madhehebu ya Maimamu, kwa nukuu na dalili. Masuala haya yamefafanuliwa sana kwenye madhehebu ya Imamu Ahmad na wanazuoni wengine, na maelezo mengine mengi yameelezwa na Imamu Malik, na vitendo vya Makhalifa Waongofu pamoja na Masahaba wakubwa baada ya kufariki kwa Mtume S.A.W, vimeonesha pia ubatilifu wa wito wa kuondoa adhabu za mali, na wale wenye kulingania kuondoshwa kwa adhabu ya mali kwa kweli hawana Kitabu (Qurani) wala Hadithi, lakini pia hawana hata kauli za wanachuoni zinazoruhusu madai yao”.
[Kitabu: Al-Turuk Al-Hukumiya cha Ibn Al-Qayyim uk. 207 – 209, chapa ya Al-Kutub Al-Elmiya].
Tatu: Kuhusu hukumu ya kuuza kwa njia ya mnada:
Mauzo kwa njia ya mnada kwa kauli yenye nguvu ni kwamba yanafaa. masuala haya yametujia bila kutegemea kwa fatwa inayojitegemea, basi na airudie fatwa hiyo kwa mwenye kutaka.
Ufupisho: ni kuwa inafaa kununua vitu vinavyotangazwa kuuzwa kwa kupigwa mnada na mamlaka za mapato ya forodha ikiwa njia ya kumiliki hivyo vitu kwa mamlaka hizo hazipingani na Sheria.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu Ni Mjuzi Zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas