Hukumu ya Kuuza Mwanamke na Kununua...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kuuza Mwanamke na Kununua wakati wa Swala ya Ijumaa

Question

 Ni ipi hukumu ya mwanamke kuuza na kununua wakati wa Swala ya Ijumaa?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Kuuza ni mabadilishano ya pesa kwa pesa, au mbadala wa kitu kwa kitu chengine, au kulipa mbadala na kuchukua kitu fulani kwa mbadala. Na Swala ya Ijumaa ni lazima kwa mwanamume aliye baleghe, aliye huru, mzima wa afya njema na mkazi. Wala hakuna ulazima wa kuiswali Swala hiyo ya Ijumaa, kwa mwanamke wala mtoto mdogo, wala kwa mtumwa, wala kwa mgonjwa na msafiri, amepokea Ad-Darqutniy na Al- Baihaqiy Hadithi kutoka kwa Jabir Ibn Abdillah R.A. amesema: Amesema Mtume S.A.W.: “Mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi analazimika kuswali Swala ya Ijumaa siku ya Ijumaa, isipokuwa mgonjwa au msafiri au mwanamke au mtoto mdogo au mtumwa, na mwenye kujitenga na Swala ya Ijumaa kwa michezo au biashara, basi Mwenyezi Mungu Anajitenga naye, kwani Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, si muhitaji, naye ni Msifiwa kwa kila sifa njema”.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu Ametoa amri ya kuacha kuuza wakati wa adhana ya Swala ya Ijumaa, Amesema Mola Mtukufu: {Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua} [AL JUMAA, 9].
Ni haramu kufanya biashara kwa yule anayewajibikiwa na Swala ya Ijumaa. Amesema Sheikh wa Uislamu Zakaria Al-Ansariy kwenye kitabu [Hashiyat Al-Jamal ala Sharh Al-Manhaj: 2/54 chapa ya Dar Al-Fikr]: “Imeharamishwa kwa mwenye kuwajibikiwa na Swala ya Ijumaa kujishughulisha na kazi za kuuza, na utengenezaji bidhaa na nyinginezo, katika kazi ambazo zinashughulisha na kumweka mbali mtu na Swala ya Ijumaa, baada ya kuanza adhana ya hotuba, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ikiadhiniwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara} kwa maana ya wacheni, na amri hapa ni ya lazima, basi ni haramu kukifanya kitendo hicho. Na linganisha kazi za kuuza na zenginezo katika zile zilizotajwa”.
Ama kuuza kwa mwanamke na kununua wakati wa Swala ya Ijumaa hakuna uharamu wowote, bali hilo kwake linafaa, kwa kuwa kwake hakuna ulazima wa kuiswali Swala hiyo ya Ijumaa. Amesema Al-Bahutiy Al-Hanbaliy: “Ni haramu kuuza na kununua kidogo au kingi isipokuwa kwa dharura kama yule mtu aliyetenzwa nguvu ambaye anawajibika kuswali Swala ya Ijumaa, hata akiwa huyu ambaye anawajibika kuswali Swala ya Ijumaa ni mmoja wa wenye makubaliano ya biashara, na mwengine akawa hana makubaliano hayo.
Na inachukiza kuuza na kununua na mtu mwengine ambaye hana ulazima wa kuiswali swala ya Ijumaa kutokana na kuonekana ndani yake kuwa kuna usaidizi wa kutenda dhambi, au akawa amekutana na mtu mwovu kwenye kuuza na kujibiwa au kukubaliwa na mtu anayelazimika kuiswali Swala ya Ijumaa baada ya kuingia kwa wakati wa adhana, kwa maana adhana ya pili ya Ijumaa ambayo inafuatana na hotuba, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara} kukatazwa kuuza ni baada ya kuingia adhana ya Swala, nayo ipo wazi katika uharamu, kwa sababu ni kitendo kinachoweza kuishughulisha Swala, na kinakuwa hatarishi na kinaweza kumfanya mtu akapitwa na Swala au sehemu ya Swala hiyo. Na imehusishwa adhana ya pili ambayo Imamu anakuwa kwenye mimbari, kwa sababu ilikuwa ikifanyika hivyo katika zama za Mtume S.A.W, na kutokea kwa hukumu ya hilo. [Kitabu cha Kashaf Al-Iqnaa: 3/180, chapa ya Dar Al-Fikr].
Na akasema Ibn Qudama: “kuharamishwa kuuza, na wajibu wa kufanya haraka kwenda msikitini, kunawahusu wale wenye ulazima kwao wa kuiswali Sala ya Ijumaa, ama wale wengine wasio kuwa na ulazima huo kama vile wanawake, watoto wadogo na wasafiri, halijathibiti hilo katika haki yao. Na akazitaja Ibn Abu Mussa kwa wasiokuwa na wajibu wa kuswali Ijumaa kauli mbili.
Na iliyo sahihi ni ile tuliyoitaja, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu Amekataza kuuza kwa amri yake ili kufanya haraka kwenda kwenye Swala ya Ijumaa, na kwa wasioambiwa kufanya haraka kwenda kwenye Swala ya Ijumaa hawahusiki na katazo hili, na kuharamishwa kuuza kuna sababu ikiwa ni kushughulishwa na kuwekwa mbali na Swala ya Ijumaa, na hili halipo kwenye haki yao. Mtu anapokuwa msafiri ambaye si mkazi, au ni mkazi kwenye kijiji ambacho hakuna ndani yake Sala ya Ijumaa kwa wakazi wake, basi haiharamishiwi kwake kuuza kwa kauli moja, na wala haichukizi, na ikiwa mmoja wa wanaouziana ni mwenye kulazimika na Saala ya Ijumaa na mwingine akawa hana ulazima, uharamu ni kwa yule mwenye ulazima wa Ijumaa. Na inachukiza kwa mwingine asiye na ulazima wa Ijumaa, ikiwa kufanya hivyo ni uwepo wa usaidizi katika dhambi. [Kitabu cha Al-Mughniy: 2/146 chapa ya Al-Kitab Al-Arabiy].
Na kutokana na maelezo haya: kuuza na kununua kwa mwanamke inafaa bila ya kuchukiza vyovyote iwavyo, kwa kuwa tu mwanamke huyo hanunui au kumuuzia mtu mwenye ulazima wa kuswali Swala ya Ijumaa, na kama itakuwa kinyume na hivyo basi inachukiza kwa mwanamke kufanya hivyo.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

Share this:

Related Fatwas