Sharti katika Mkataba wa Ndoa.

Egypt's Dar Al-Ifta

Sharti katika Mkataba wa Ndoa.

Question

  Mtoto wangu alioa na kipengele kifuatacho kilikuwa ni moja ya masharti ya kufungwa ndoa hiyo: “Awe mke peke yake ndiye mwenye haki ya kunufaika na makazi ya wanandoa katika hali mbili; hali ya kwanza ni ya talaka, na ya pili ni ya kifo". Kwa hivyo basi, sharti kama hili lina hukumu gani ya kisheria? Na je, ina maana mwanangu akifariki mke huyu atamiliki makazi ya ndoa?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Ilitajwa katika Hadithi tukufu kwamba: “Hakika masharti yenye haki ya kutekelezwa ni yale ambayo kwayo mmehalalishia tupu”. imepokewa na watu wengi kutoka kwa Oqbah Bin Amir kutoka kwa Mtume S.A.W.
Na maana ya sharti lililopo katika swali kwamba mke wa mwanao atakapoachwa au kufiwa na mume wake ataendelea kuishi katika nyumba ya ndoa na ambayo alikuwa akiishi na mtalaka wake au mume wake (mwanao) kabla ya kufa kwake na ataishi bure bila ya kulipa chochote katika kipindi chote cha uhai wake sio kwa sababu yeye ni mmiliki wa upande wa nyumba ya ndoa. Isipokuwa kama mmiliki tu kwa ajili ya haki ya kunufaika nayo: na anaweza kunufaika na nyumba hiyo yeye mwenyewe au mtu mwingine yeyote kwa njia zake zote; miongoni mwa manufaa hayo, ni makazi, kupangisha, kukopea kwa muda na mengineyo, lakini katika muda wa maisha yake tu, na haitakuwa mirathi kwa watu wengine.
Na atajizoesha hivyo kama hiyo ni zawadi kutoka kwake kwa ajili ya kunufaika na upande wa nyumba yake anayoimiliki, au tuzo kwa ajili ya manufaa ya upande wa nyumba ambayo anaikodisha kwa ajili ya mke wake katika kipindi chote cha maisha yake baada ya talaka, na wasia wake kwa mke wake baada ya mauti yake.
Na katika mazingira ya kuwa upande wa nyumba unamilikiwa naye basi atakapokufa atarithiwa na warithi wake kwa kupokonywa manufaa kwa muda wote wa maisha ya ndoa, na katika hali ya kuwa nyumba hiyo ni upande wa nyumba iliyokodishwa basi itakatwa kutoka kwa kile kitakachotosha ujira wake katika kiwango kisichozidi theluthi moja.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas