Mkristo Kumswalia Mtume Muhammad.

Egypt's Dar Al-Ifta

Mkristo Kumswalia Mtume Muhammad.

Question

Ugomvi wa maneno ulijitokeza baina ya wakristo wawili, mmoja wao ni mwenye nyumba na mwingine ni fundi mwashi wake, basi, yule fundi akamwambia mwenye nyumba: “Mswalie Mtume ewe ami yangu, sisi tutatengeneza kila kitu”. Basi mwenye nyumba akamtukana Mtume S.A.W, na akamshutumu huyo fundi aliyeyasema maneno hayo. Na wanakijiji wakaamua kumfukuza mtu huyo aliemtukana Mtume S.A.W, na wakamlazimisha auze mali zake alizozimiliki ili ashindwe kurudi tena kijijini hapo. Na pia wakaamua kumweka mbali ya kijiji hicho fundi yule aliyesema tamko hilo ingawa fundi huyo ana watu na ukoo hapo kijijini, na hapo baadaye wanakijiji walimwombea ruhusa ya kurejea kijijini hapo, kwani fundi huyo hakuwa na kosa lolote, na pia fundi hakukubaliana na tabia mbaya na makosa ya mwenye nyumba. Kwa hivyo basi, maoni ya watu wa kijiji walikubaliana kulipeleka tukio hilo kwa wanazuoni wa kisharia. Na ni ipi hukumu ya tamko la fundi kwa mwenye nyumba: “Mswalia Mtume amu yangu”? Na ni ipi hukumu ya fundi kukubaliwa kurejea kijijini?  

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Ama kuhusu huyo fundi mkristo ambaye alimwambia mkristo mwenzake mwingine: Mswalie Mtume”, basi mkristo huyo hakufanya kosa lolote, kwani katika manenao yake hapakuwepo kitu chochote kinachoonesha kuwa alimpuuza Mtume S.A.W., lakini alisema maneno ambayo labda ulimi wake ulikuwa umezoea kuyatamka katika jamii yake, hasa katika hali ya kunyamazisha. Na yalitokea mambo kama hayo kwa maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziwafikie wao wote, katika zama ya Mtume S.A.W. Kwa hivyo, katika kitabu cha Sahihi ya Al-Bukhariy, kutoka kwa Abi Hurairah R.A, amesema: Mtume S.A.W. amesema: “Mtu yeyote anapo apa na akasema katika kiapo chake: ‘Wallaata Waluzah’ basi aseme; Hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu”.
Na dalili inayotokana na Hadithi hiyo ni kuwa: Maswahaba wote R.A, pamoja na uangalifu wao kwa kwenda mbali kutoka katika ukafiri, alikuwa mmoja wao anasahau baadhi ya nyakati na kuapa kwa matwaghuti. Ama asiye muislamu anayeishi na jirani zake waislamu, labda anaweza kuwa ametamka tamko ambalo yeye hakulikusudia, au halitaki, na kama tamko hilo linakuwa ni la shari, basi inakuwaje dhana katika maneno yanye heri ndani yake!
Na katika Hadithi kama hizo ambazo zina maneno kama vile; ‘Thakalatka Umuka’ yaani: mama yako amekupoteza, au maneno kama; ‘Tarebat Yamenuka’ yaani: mkono wako wa kulia umeangukia ardhini; kuwa ni dalili ya ufakiri. Wakasema kwamba hayo ni maneno yanayotamkwa na ndimi za waarabu, na hayakusudiwi kuwa na maana yake ya wazi.
Kwa hivyo, inadhihirika kutokana na maelezo tuliyoyataja kwamba labda ulimi huwa unatamka maneno ya shari lakini yasiyokusudiwa hivyo, na mwanadamu hahisabiwi kwa maneno hayo, na kutamkwa maneno hayo kwa ajili ya heri hata kama bila ya nia, hakuna ubaya wowote kwa aliyetamkiwa.
Na lipo kundi kubwa la watu wasio waislamu na wanaishi na waislamu, wanadhani kwamba Bwana wetu Muhammad S.A.W, ni Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu lakini alitumwa kwa waarabu tu. Au inadhaniwa kuwa yeye ni Mtume lakini Watu wa Kitabu hawalazimiki kumfuata, kwani wao ni wafuasi dini nyingine, na wao ni tofauti na watu wengine.
Kama ambavyo yamepokelewa mfano wa haya kwa yale yalikuja katika riwaya ya Tirimidhiy kutoka kwa Swafwan Bin Assaal R.A. amesema: Myahudi mmoja alimwambia mwenzake: Twende kwa Mtume huyu, na mwenzake akasema: usiseme Mtume! Hakika yeye akikusikia atakuwa na macho manne. Na wakafika kwa Mtume S.A.W, na wakamuuliza Aya tisa zilizo bainifu. Basi Mtume S.A.W. akawaambia: “Msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na msiibe, na msizini, na msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameiharamisha ila kwa haki, msimpeleke mtu asiye na hatia, kwa mwenye madaraka ili amuue, na msiloge, na msile riba, na msimsingizie uzinifu mwanamke mwenye mume, na msikimbie katika siku ya vita, na juu yenu – Mayahudi hasa – msifanye kazi siku ya Jumaamosi”. Akasema: basi wakambusu mikono na miguu yake, na wakasema: tunashuhudia kuwa wewe ni Mtume. Mtume S.A.W, akasema: Na ni kipi kinachokuzuieni kunifuata? Wakasema: hakika Mtume Daudi alimwomba Mola wake kwamba Mtume aendelee kutoka katika kizazi chake. Na sisi tunaogopa kwamba tukiamua kukufuata basi mayahudi watatuua”.
Na mfano wa watu kama hao wanamtukuza Mtume S.A.W. wazi na kwa kificho, na hasa kwa yale wanayoyasikia kivitendo jinsi waislamu wanavyomtukuza Mtume Issa A.S. na mama yake Mariamu msema kweli aliye kigori.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia na katika hali ya swali lililoulizwa; ni kwamba mtu asiye muislamu hakufanya kosa lolote la kumfanya astahiki kuadhibiwa, na kwa hivyo haijuzu kumfukuza mtu na kumtoa kijiji kwake bila ya mtu huyo kufanya dhambi yoyote.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas