Kuiainisha Nia katika Saumu Wakati ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuiainisha Nia katika Saumu Wakati wa Hitilafu ya Namna ya Saumu.

Question

Je, ni yapi masharti ya kuiainisha nia katika saumu wakati wa hitilafu namna ya saumu kama katika Nadhiri na kulipa, au kulipa siku badala ya siku za Swaumu ya faradhi na kadhalika, wakati wa kufunga siku sita za shawali?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu:
Nia: Ni ile anayeinuia mtu, kwa lengo la kubadilisha sehemu kwa nyingine [Rejea mada ya: N.W.Y., katika kamusi ya kiarabu ya Al-Mesbah Al-Muner kwa Al-Fayumy, Uk. 631, cha, Al-Maktabah Al-Ilmiyah, na Al-Muajam Al-Waset, uku, 965, Ch. Dar Al-Dawah].
Na maana ya Nia katika Istilahi: Ni makusudio ya mwanadamu kwa moyo wake, anavyotaka kwa kitendo chake. [Al-Zakherah kwa Al-Qurafy 1\240, Ch. Dar Al-Gharb Al-Islamy].
Na makusudio ya nia katika sharia ni kupambanua baina ya Ibada na mambo ya kawaida, na kutenganisha daraja za Ibada, Al-Bukhariy alisimulia kutoka kwa Umar Ibn Al-Khatwab R.A. alisema: "Hakika vitendo huzingatiwa kwa nia, na kwa hakika kila mtu atalipwa kwa nia yake. Mtu ambaye kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na ambaye kuhama kwake ni kwa ajili ya kuupata Ulimwengu au mwanamke wa kumuoa, basi kuhama kwake ni kwa lile alilolihama". Basi Hadithi hii ilionesha kuwa thawabu ya vitendo na malipo yake vinasimama kwa nia.
Ibn Najeem alisema: "Makusudio ya nia ni kuzipambanua kati ya Ibada na Ada, na kuzipambanua baadhi ya Ibada na nyingine, ni kama aliyejizuia na vyakula labda kwa ajili ya kuupunguza uzito wa mwili wake au kwa ajili ya tiba, kwa maana ya dawa, na kukaa msikitini labda ni kwa ajili ya kustarehi au kwa ajili ya kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa sala ya fardhi au sunna, kwa hivyo nia imewekwa ili kuzipambanua hizo zote". [Al-Ashbah wa Al-Nadhaer Uk. 25, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Nia ni sharti ya kusihi saumu kama katika Ibada zote, kwa hivyo asiyenuia nia yake kabla ya Al-Fajiri basi saumu yake ni batili; kwa kauli ya Mtume S.A.W., katika Hadithi moja iliyosimuliwa na Al-Baihakiy kutoka kwa Anas Ibn Malek R.A alisema: Mtume S.A.W., alisema: "Hakuna kazi kwa mtu asiyenuia kwa nia ya kazi hiyo".
Al-Nawawiy alisema: "Haisihi saumu ila kwa nia". [Rawdhat Al-Talebeen kwa Nawawy 2\350, Ch. Al-Maktab Al-Islamy].
Na Al-Shiekh Ad-Dardir: "Na sharti ya kusihi saumu kwa ujumla, iwe saumu hiyo ni ya faradhi au ya sunna ni nia ya saumu wakati wa usiku". [Hashiyat Al-Desouky juu ya Al-Sharh Al-Kabeer 1\250, Ch. Dar Al-Fikr], na Ad-Desouky alieleza juu yake akasema: Kwa ujumla wa Hadithi ya wenye vitabu vinne vya Sunanu kutoka katika Hadithi ya Hafsa R.A, alisema: Mtume S.A.W., alisema: "asiyenuia nia ya saumu kabla ya sala ya Al-Fajiri haisihi saumu yake".
Na ni wajibu kuiainisha nia katika Saumu ya Faradhi, yaani Saumu ya Ramadhani, au kulipa saumu iliyoachwa, au nadhiri au katika ibada zingine; kwani nia imewekwa kwa ajili ya kupambanua kati ya daraja za Ibada miongoni mwao, kwa hivyo kuna tofauti kubwa baina ya saumu ya wajibu na saumu ya sunna, na kwa sababu ya kuwa ni ibada ya kuongeza kwa wakati kama Swala, basi nia ni wajibu ili kupambanua baina ya faradhi na sunna.
Al-Khatweb Al-Sherbeniy alisema: "Na kuiainisha nia katika saumu ya faradhi ni kuinuia kuwa ni kufunga mwezi wa Ramadhani au saumu yake ni nadhiri au ya kafara; kwani ibada ni ya kuongeza kwa wakati, kwa hivyo ni wajibu kuiainisha nia yake kama inavyoainishwa katika Sala Tano za Faradhi". [Al-Iqnaa 2\327, Ch. Mostafa Al-Halaby]
Na katika jambo hilo pia, Al-Nawawiy alisema: "Ni wajibu kuiainishia Nia katika saumu iwapo itakuwa ya Ramadhani, saumu ya nadhiri, saumu ya kafara au nyingine". [Rawdhat Al-Talebeen 2\350].
Na Ibn Qudamah amesema: "Saumu bila ya nia haikubaliki, iwapo itakuwa ni ya saumu ya Faradhi au katika saumu ya Sunna ya nadhiri au kafara; kwani saumu ni ibada kama ibada ya sala, na wanazuoni wa Madhehebu ya Maliki na ya Shafii pamoja na Imam Abu-Hanifa wameafikiana juu ya Nia katika jambo hili". [Al-Mughny kwa Ibn Qodamah 3\22, Ch. Al-Kitab Al-Arabiy].
Na An-Nawawiy alisema pia katika kitabu cha: [Al-Majmuu] haisihi saumu ya faradhi ila kwa nia ya saumu hiyo. Ama kwa upande wa saumu za Sunna yawezekana mtu akaifunga bila ya kuiainisha namna ya saumu, kwani namna ya sunna ni moja. [Al-Majmuu' 6\295, Ch. Dar Al-Fekr]
Na Jalal Al-Din Al-Mahaliy alisema: "Saumu ya nawafili yaweza kuwa kwa nia ya saumu kwa ujumla". [Sharh Al-Menhaj kwa Al-Mahaly 2\53, Ch. Isa Al-Halabiy].
Na kutokana na maelezo haya yote yaliyotangulia, tunaweza kusema kwamba: Sharti ya kusihi saumu ni nia, na pia kuiainishia nia ya saumu ya faradhi, na bila ya kuiainisha niya hiyo katika saumu ya Sunna.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas