Ubora wa Mji Mtakatifu wa Makkah na Utukufu wa Kaburi la Mtume S.A.W.
Question
Je, Mtume S.A.W, aliposifu Mji mtakatifu wa Makkah kwamba mji huo ni ((Ardhi bora zaidi kuliko ardhi nyingine yoyote ulimwenguni na pia ni upendeleo wa ardhi ya Mwenyezi Mungu ulimwenguni)) ni dalili ya ubora wa Makkah zaidi kuliko Madina na Msikiti Mtakatifu ni bora zaidi kuliko Msikiti wa Mtume S.A.W, na Al-kaaba ni bora zaidi kuliko mahala palipozikiwa mwili Mtakatifu wa Mtume S.A.W?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Makkah takatifu ni jina la mji maarufu ambao una Nyumba Takatifu ya Mwenyezi Mungu, na kuna hitilafu katika sababu za jina lake kuitwa Makkah, ilisemwa kwamba: Maana yake ni kujiepusha na kila mtu mbaya au kuwasukuma watu wote jeuri, na pia una majina mengi mengine kati ya hayo ni: Bakkah, Umulqura na mengine. [Tazama: Ielam Alsajed Biahkam Al-Masajed Lilzarkashiyy, uku: 78,Cha, Al-Majles Al-Aala Lilshuun Al-Islamiyah].
Na yapasa kuutukuza mji wa Makkah kwa kauli ya ALBUKHARY na MUSLIM kutoka katika Hadithi ya Abi Shurah Al-Adawiy kwamba Mtume S.A.W, amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameutukuza Mji wa Makkah na wala sio watu walioutukuza Mji huo. Kwa hivyo, si halali kwa anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kumwaga damu huko Makkah wala kukata mti. Na kama mtu yeyote anaruhusiwa kupigana na Mtume S.A.W, - basi mwambieni: Kwa hakika Mwenyezi Mungu amemruhusu Mtume wake S.A.W tu, na hakukuruhusuni nyinyi, bali Mwenyezi Mungu alinilihalalishia kipindi kichache cha mchana, na umesharudishwa utakatifu wake leo, tena kama utukuzwaji wake jana, na kwa hivyo yampasa anayeshuhudia kumfikishia ujumbe yule asiyehudhuria". [Tazama: Fathu lbary Libn Hajar 4\41, Ch. Dar Al-Maarifah] Na Jamhuri ya Maulamaa ilisema kwamba mji wa Makkah ni bora zaidi kuliko mji wa Madinah, na dalili yao juu ya hayo ni ile iliyosimuliwa na Tirmidhi kutoka kwa Abdullahi Ibn Adeyy Ibn Hamraa –Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake– alisema: nilimwona Mtume S.A.W., akiwa amesimama juu ya mahala pa Hazuorah katika mji wa Makkah na huku akisema: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Wewe ni ardhi ya Mwenyezi Mungu iliyo njema zaidi, na ni ardhi ya Mwenyezi Mungu ninayoipenda zaidi, na lau watu wako hawangenitoa basi nisingetoka", na Hadithi iliyosimuliwa na Tirmidhiy kutoka kwa Abdulahi Ibn Abas – R.A, alisema: Mtume S.A.W, alisema kuhusu Makkahh: "una ubora kwangu na ni nchi ninayoipenda zaidi, na lau watu wangu hawakunitoa nisingetoka na nisingekaa mji mwengine", basi Hadithi hizi mbili ni dalili za wazi juu ya ubora wa mji wa Makkah juu ya miji mingine yote na miongoni mwao ni Madinah, na dalili yao juu ya ubora wa Msikiti Mtakatifu wa Makkah ina nguvu zaidi kuliko Msikiti Mtakatifu wa Mtume, kutokana na Hadithi ya Bukhary na Muslim kutoka kwa Abuhurairah –R.A – kuwa Mtume S.A.W, amesema: "Sala katika Msikiti wangu huu ni bora mara elfu kwa thawabu kuliko katika Msikiti mwingine isipokuwa Msikiti wa Makkah”, na pia kwa Hadithi iliyotoka kwa Ahmad katika (kitabu chake) kutoka kwa Abdulah Ibn Al-Zubair -R.A – kuna ziada ya hayo: "Na Sala katika Msikiti wa Makkah ni bora zaidi kuliko Sala mara mia katika Msikiti wangu huu".
Wanazuoni wote waliafikiana juu ya kuwa eneo la pahala pa kuweka mwili mtukufu wa Mtume S.A.W, ni eneo lilo bora zaidi juu ya ardhi hii. Kadhi Ayyadh alisema: Hakuna hitilafu juu ya kuwa eneo la pahala pa kaburi lake Mtume S.A.W, ni eneo bora la ardhi) [Al-Shefa Betaareef Huquq Al-Mustafa Lilqadhi Ayyadh 2\91, Cha, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah].
Al-samhudiy alisema katika kitabu chake cha: [Wafaa Al-Wafa Bi-akhbar Dar Al-Mustafa]: "Wanazuoni wote walikiri juu ya ubora wa eneo lililovihifadhi viungo vya mwili wa Mtume S.A.W, hata juu ya Kaabah, na simulizi ya ijimaa ya wanazuoni juu ya ubora wa pahala pa kaburi la Mtume S.A.W, ilinakiliwa na Al-Kadhi Ayyadh, Al-Kadhi Abu-Walid Al-Bajiy, Al-Khateeb Ibn Jumlah, Abu-Al-Yaman Ibn Asaker na wengine wote waliuzungumzia ubora wa pahala palipozikwa mwili wa Mtume juu ya pahala pengine hata pahala pa Arshi)).
Kisha alisema: "Na Al-Taj ll-Fakihiy alisema: Walisema: Hakuna hitilafu baina ya wanazuoni juu ya ubora wa eneo lililovihifadhi viungo vya mwili wa Mtume S.A.W, juu ya pahala popote pa ulimwengu wote hata pahala pa Kaabah na Zarkashiy alisema kuwa na ubora wa pahala palipo na mwili wa Mtume S.A.W, ni kutokana na ukaribu wake, na dalili ya hayo ni kama vile kuharamishwa kuligusa jalada la Msahafu kwa mtu mwenye janaba". Kisha akasema kwamba: (Rehema na Baraka zinazoteremshwa juu ya kaburi la Mtume S.A.W, nuru zake zimeenea kwa Umma wote wa Mtume S.A.W, bila ya kikomo; kutokana na kuendelea kuongezeka kwa daraja lake Mtume S.A.W, na kwa hivyo, umma wake umekuwa bora kwa sababu ya kuwa Nabii wake ni mbora wa Manabii, na kwanini basi kaburi lake Tukufu lisiwe katika eneo bora pamoja na kuwa kwake ni chanzo cha kheri nyingi yote?
Kisha alisema: "Ibn Al-Juziy alisimulia katika kitabu chake cha: [Al-Wafaa] kutoka kwa mama yetu Aisha alisema: Mtume S.A.W, alipofishwa, masahaba walihitilafiana katika pahala pa kumzika; wakasema: wapi tumzike Mtume S.A.W.? Aly R.A. akasema: hakuna pahala pazuri kuliko pahala alipofia Mtume ni bora zaidi yeye kuzikiwa, na Abu-Bakr R.A. akaisema pia rai kama hii pale aliposema: Mtume azikwe mahala alipofia, kwani Mwenyezi Mungu hakuifisha roho ya Nabii wake ila katika pahala pazuri. Rai hii ilisimuliwa na Termidhiy katika kitabu chake [Al-Shamael] na Al-Nassaiy katika kitabu chake [Al-Kubra], na Hadithi hii ni sahihi, na Abu-Yaala Al-Mawseleiy aliisimulia kwa maana hiyo hiyo na tamko lake ni: nilimsikia Mtume S.A.W, anasema: Mtume hafii ila katika mahala pa anapopapenda)), na nikasema: Na upendo wake kwake ni upendo wake kwa Mola wake; kwani upendo wake umefuata upendo wa Mola wake S.W. [Wafaa Al-Wafa 1\28-33, Cha, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]. Katika jambo hili, Al-Haskafiy alisema katika kitabu chake” Al-durr Al-Mukhtar”: "Makkah ni bora na patukufu zaidi kuliko Madinah, isipokuwa mahala palipo na viungo vya mwili wa Mtume S.A.W, ambapo ni pahala bora ulimwengoni". [Al-Durr Al-Mukhtar na juu yake Hashiyat Ibn Abdeen 2\257, Cha, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Na Sheikh Muhammad Ibn Ahmad Elesh Al-Malikiy alisema katika maneno yake kuhusu hitilafu ya wanazuoni juu ya ubora wa Makkah au Madinah: "Wanazuoni wote wanaafikiana juu ya utukufu wa mahala pa kaburi la Mtume juu ya pahala pengine popote ulimwenguni katika ardhi na mbingu". [Manh Al-Jalel Sharh Mukhtasar khalel 3\133, Cha, Dar Al-Fekri]. Na pia Al-Ruhaibaniy alisema katika jambo hili: "Mahala pa kaburi lake Mtume S.A.W ni mahala bora zaidi ulimwengu kote kwani yeye Mtume S.A.W, aliumbwa kutokana na udongo wake, na udongo wake huo ni bora kuliko udongo wowote ardhini". Kisha akasema: "Na Abu-Al-Wafaa Aly Ibn Akel alisema katika kitabu chake: [Al-Funun]: Al-Kaabah Tukufu ni bora zaidi kuliko chumba cha kaburi la Mtume S.A.W, tu, lakini utukufu wa kaburi na chumba chake ni kwa sababu ya uwepo wa mwili wa Mtume S.A.W, ndani yake, na kwa hivyo ni bora zaidi kuliko mahala pa Al-Arshi na malaika waibebao Arshi hiyo pamoja na Pepo; kwani ndani ya chumba hicho kuna mwili wa Mtume S.A.W”. [Mataleb Auly Al-Nuha 2\384, Cha, Al-Maktab Al-Islamy].
Hadithi ya Tirmidhiy juu ya kauli ya Mtume S.A.W, juu ya Mji Mtakatifu wa Makkahh: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Wewe ni ardhi ya Mwenyezi Mungu iliyo njema zaidi, na ni ardhi ya Mwenyezi Mungu ninayo ipenda zaidi, na lau watu wako wangenitoa basi nisingetoka". Hadithi hii ni dalili ya wazi juu ya ubora wa Makkah ulimwenguni kote kuliko miji mingine, na pia ina dalili ya wazi juu ya kwamba Msikiti Mtakatifu ni bora zaidi kuliko Msikiti wa Mtume S.A.W, lakini kaburi lake Mtume S.A.W, linazingatiwa kuwa ni bora zaidi kwani ndani yake kuna mwili wa Mtume S.A.W, na mwili wake S.A.W, ni bora zaidi kuliko miili mingine yote ardhini na mbinguni, na kwa hivyo basi makazi ya mwili wake ni eneo bora zaidi kuliko maeneo mengine yote ulimwenguni kwa Ijimai ya wanazuoni wote.
Kwa hivyo: kwa hakika Hadithi iliyotajwa katika swali ina dalili juu ya ubora zaidi wa Makkah kuliko Madina, na Msikiti Mtakatifu ni bora zaidi kuliko Msikiti wa Mtume S.A.W, na eneo la ulipozikwa mwili wa Mtume S.A.W, ni bora zaidi kuliko maeneo mengine yoyote, hata kama ni Kaaba kwa Ijimai ya wanazuoni.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.