Mahesabu ya Kianga na Tofauti za Mi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mahesabu ya Kianga na Tofauti za Miandamo

Question

 Nini kuhusu suala la mahesabu ya Kianga na tofauti za miandamano?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Tumesoma utafiti uitwao: (Majadiliano ya kielimu kati ya wataalamu wa anga na wanazuoni wa Sharia kuhusu mwanzo na mwisho wa miezi ya kalenda ya kiislamu), na mwandishi wake Bwana ni Abdus-Salaam Muhajir Khalifa Qari R.A., utafiti ulio sajiliwa kwa nambari 31, kwa mwaka wa 2011, na tukaukuta unazungumzia masuala mbali mbali, miongoni mwake ni:
- Suala la tofauti kati ya wanazuoni wa elimu ya anga na wanazuoni wa Sharia.
- Suala la kuyazingatia mahesabu ya elimu ya kianga katika kuthibitisha miandamo ya miezi ya: Ramadhani, Shawali, na Dhulhijja, kuzingatia kuwa ni muhimu kati ya miezi ya kalenda ya kiislamu.
- Suala la tofauti ya miandamo, na athari yake katika kuthibitisha kuingia mwezi.
- Suala la kuchomoza kwa jua na kuandama kwa mwezi, na kuzama kwa Jua na mwezi katika hesabu ya elimu ya anga na katika Qur`ani Tukufu.
- Suala la Saumu na Hija na ibada zinazoambatana nazo.
- Suala la vituo vya kianga na kutofautiana vigezo vyake.
- Suala la kuzaliwa na kuonekena kwa Mwezi mwandamo.
- Suala la vyombo vya kisayansi vya kisasa katika kuchunguza mwezi mwandamo mwanzoni mwa miezi ya kiislamu, ikiwemo Satalaiti na uwezekano wa kurusha sura ya Mwezi mwandamo kupitia satilite, baada ya machweo ya Jua ya siku ya ishirini na tisa ya kila mwezi, ili waislamu wote duniani kote waweze kuutazama.
- Suala la hitilafu kati ya elimu ya anga na unajimu, na Suala la umoja wa mwanzo wa miezi ya kiislamu kwa waislamu wote duniani.
Baada ya kusoma sana masuala haya yaliyotajwa katika utafiti huu, na kuomba ushauri wa wabobezi wa Elimu ya anga wa Taasisi ya taifa ya tafiti za anga na Elimu ya Fizikia ya dunia, tunajibu yafuatayo:
Suala la kwanza: linalohusu uzingatiaji wa mahesabu ya kianga: Tunaona kuwa Sharia tukufu imefanya suala la kujua mwanzo wa kila mwezi wa kiislamu kwa kuonekana mwezi mwandamo wake baada ya machweo ya Jua ni jukumu la lazima, kwa sababu mjumuiko wa ibada mbali mbali kama vile: kufunga na kufungua saumu, kutoa zaka, kuhiji, na kukaa eda n.k, unaambatana na wakati wake uliokadiriwa kisharia, na ikawa hivyo, ni katika mambo ambayo wajibu haukamiliki isipokuwa kwayo, na kanuni ya Sharia inasema: “Kitu ambacho wajibu hautimii isipokuwa kwa kitu hicho nacho ni wajibu”.
Na Mwenyezi Mungu alisema: {Wanakuuliza juu ya miezi. Sema: “Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili (ya mambo) ya watu (mengine) na ya Hija (zao)}. [AL BAQARAH: 189]; Imamu Al-Baidhawiy katika tafsiri yake [1/474-475, Ch. ya dar Al-Fikr] anasema: “waliuliza hekima ya mabadiliko ya hali ya Mwezi na kugeukageuka kwake, Mwenyezi Mungu akamuamuru ajibu kawamba: hekima ilio wazi katika hili ni: mabadiliko ni vipimo kwa watu ili wapime mambo yao, na vipimo vya ibada zinazoainishwa kwa wakati, ili wajue nyakati zake”. [Mwisho].
Uthibitishaji wa kuonekana au kutoonekana kwa mwezi mwandamo baada ya machweo ya jua unaweza kupatikana kwa macho au kwa hesabu ya kianga, na uzingatiaji wa kuona kwa macho hauna tatizo lolote, nayo ni kama ilivyopokokelewa katika matini ya sharia, na Imamu Bukhariy na Muslim wamepokea katika vitabu vyao - na tamko hili ni la Muslim- kutoka kwa Abu Hurairah R.A., kuwa Mtume S.A.W., alisema: “Fungeni kwa kuuona , na fungueni kwa kuuona, na ukifunikwa na mawingu, fungeni siku thelethini”.
Na muradi wa kuuona mwezi kisharia ni kuuona kwake kwa macho, baada ya machweo ya Jua ya siku ishirini na tisa ya mwezi uliopita, kwa mtu ambaye kauli yake inasadikika, na ushahidi wake unakubalika, na kuingia kwa mwezi kunathibiti kwa kuuona kwake.
Kuhusu hesabu ya kianga ndiyo inatambuliwa na wanazuoni wengi wa zamani na wa sasa; ama kwa upande wa ubora au kwa upande wa kutambulika, na miongoni mwao ni:
Tabii mtukufu Mutarrif Ibn Abdillahi Ibn Ash-Shikhiir (Aliyefariki Mwaka, 95 H.); Imamu Al-Qurtwubiy katika tafsiri yake [2/293, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Masriyah] na Imamu Abu Bakr Ibn Qutaibah walisema kuwa maana ya kauli yake S.A.W,: “Pangeni kadiri ya hesabu yake”, yaani; “jueni hali ya mwezi kwa vituo vyake, na pangeni siku za mwezi kwa hisabu yake”, na imenukuliwa na Ad-Dawuudiy kuwa maana yake ni: “Pimeni vituo vya Mwezi”, na Imamu Abul-Waliid Ibn Rushd alinukulu katika kitabu cha [Bidayat Al-mujtahid: 1/228, Ch. ya Dar Al-Fikr] kutoka kwa Al-mutarrif ibn Ash-Shikhiir kuwa alisema: “Na kama Mwezi hauonekani, basi hesabu ya mwendo wa Jua na Mwezi itumike”.
Al-Hafidh Al-A’ainiym mfuasi wa madhehebu ya Hanafiy katika kitabu cha [U’umdat Al-Qariy; 10/387, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah] alinukulu madhehebu hii kutoka kwa Ibn Qutaibah Ad-Dinawariy (Aliyefariki Mwaka, 276 H.), na hii pia ni kauli ya Imamu Najm Ad-Diin Az-Zahidiy Al-Khuwarizmiy (Aliyefariki Mwaka, 658 H.), mwandishi wa kitabu cha Al-Qunyah, naye ni katika wanazuoni wakubwa wa madhehebu ya Hanafiy, ambapo alisema [Uk. 68, Ch. ya Matbaa’at Al-Mahanand]: “Si vibaya kutegemea kauli za wanajimu. Na kutoka kwa Muhammad Ibn Muqatil- naye ni Ar-Raaziy, miongoni mwa wafuasi wa Imamu Muhammad Ibn Al-Hassan- kuwa yeye alikuwa akiwauliza wanajimu na anazitegemea kauli zao, baada ya kukubaliana juu ya hilo kundi miongoni mwao". [Mwisho].
Imamu Al-Qarafiy, mfuasi wa madhehebu ya Malik katika kitabu cha Al-Furuuq [2/178, Ch. ya A’alam Al-Kutub] alitaja kuwa: Kuna kauli mbili katika madhehebu ya Imamu Malik juu ya kuthibitisha Miezi kwa njia ya hisabu. Na hiyo pia ni kauli moja ya madhehebu ya Shafi, ambapo mtu mmoja akijua kwa njia ya hisabu ya vituo kuwa kesho ni mwanzo wa Ramadhani, basi analazimika kufunga saumu, kwa sababu yeye alijua mwezi kwa njia ya dalili na sababu ya nguvu, na hiyo ni mfano wa hoja, kama akiambiwa hivyo na mtu mwaminifu mwenye kuona.
Na kauli hii pia ni ya wafuasi wengi wa madhehebu ya Shafi, nao ni: Imamu Abul-Abbas Ibn Suraij Al-Baghdadiy (aliyefariki Mwaka, 306 H.), Imamu Abu Bakr Al-Qaffal Ash-Shashiy (Aliyefariki Mwaka 365 H.), na Kadhi Abut-Taiyb At-Tabariy (Aliyefariki Mwaka, 450 H.). [Tazama: Al-Majmuua’: 6/289-290, Ch. ya Al-Munitiyah], na [Raudat At-Talibiin: 2/211, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyyah].
Na Imamu mwenye jitihada Qadhi Al-Qudhah Taqiy-diin As-Subkiy wa Kishafiy (Aliyefariki Mwaka 756 H.)- ambaye alisifiwa na wanazuoni wa wakati wake kuwa amefikia ngazi ya jitihada- kuwa: ushahidi wa kuona Mwezi kwa macho ukipingana na hesabu ya kweli utakataliwa, na hisabu imezingatiwa; na alitaja hivyo katika Risala ya [Al-A’alam Al-Manshuur Fi Ithbaat Ash-Shuhuur], na akasema katika fatwa zake [1/209, Ch. ya Dar Al-Maarif]: “ na hapa kuna sura nyingine: nayo ni hesabu inaonesha kuwa kutokuona kwake, kutokana na dalili nguvu, ambapo Mwezi huwa karibu sana na Jua, na katika hali hii haiwezekani kuonwa kwa macho, kwa hiyo mtu akituambia katika hali hii kuwa aliona Mwezi, basi maneno yake hayakubaliki, na habari yake ni ya uongo na ya kosa.
Na kama mashahidi wawili wakisema hivi, basi ushahidi wao haukubaliki; kwa sababu hesabu ni thabiti, lakini ushahidi na habari ni dhana, na dhana haiupingi ukweli, na wala haitangulii. Na sharti ya hoja ili ikubaliki iwe kwa njia ya hisia, akili, na sharia, na hisabu ikionyesha kuwa kuona mwezi ni kutoweza, basi Sharia inakubali hivi wala haipingi, kutokana na kutoweza kuhakikishwa, na Sharia haileti magumu, na hakuna dalili katika Sharia inayosema inaweza kukubaliwa ushahidi wa mashahidi wawili wowote iwe ushahidi wao ni sahihi au batili, kwa hiyo uwajibikaji wa saumu na hukumu ya Mwezi haufungamana na habari au ushahidi tu, basi tunasema kuwa: msingi hapa ni kauli ya Mwenye Sharia: (Fungeni saumu mtakapoambiwa na mwenye habari), na kama ikiwepo hivi tunaikubali vilivyo, lakini kanuni kama hii haijapokelewa katika Sharia, kwa hiyo inapaswa kuchunguza hivi mpaka tujue ukweli wake kwanza.
Hakuna shaka kuwa baadhi ya wanaoshuhudia kuona mwezi huenda hakuuona, na huenda akadhani kuwa ameuona Mwezi na hakika yake si Mwezi, au macho yake yakamuonesha kile ambacho hajakiona, au akatoa ushahidi baada ya siku kadhaa bila ya kuainisha usiku aliouona Mwezi ndani yake, au huwa na ujinga sana ambapo hufikiri kuwa saumu ya watu hupelekea thawabu kwa ajili yake, au huenda anakusudia kuwa na uadilifu na kusifiwa mbele ya mahakimu, na kwa kweli, tumeona na kusikia hayo yote.
Na hakimu akijaribu hivi na kujua mwenyewe au kwa njia ya habari ya mtu mwaninifu kuwa hesabu inaonyesha kuwa kuona mwezi hakuwezekani, basi asiukubali ushahidi huu wala athibitishe, na hatoi hukumu kwa mujibu wake, na hufuata msingi wa kukamilisha siku za mwezi, kutokana na dalili nguvu ya kisharia, mpaka ionekane kinyume chake”. [Mwisho].
Imamu mwenye jitihada Abul-Fat-h Ibn Daqiiq Al-I’id katika kitabu cha Sharh Al-U’umdah [2/8] anasema: “Nisemayo kuwa: haijuzu kutegemezwa kwa hisabu katika saumu, kwa sababu ya kutengana na Mwezi na Jua kwa mtazamo wa wanajimu kuwa Mwezi wa hisabu hutangulia Mwezi wa kuona muda wa siku moja au wa siku mbili; na kufanya hivi ni kutegemea sababu ambayo Mwenyezi Mungu hajaiweka.
Na kama mahesabu yakionesha kuwa Mwezi mwandamo ulichomoza katika upeo pamoja na kuweza kuonwa- kama siyo kuwepo kizuizi kama vile mawingu- basi ni wajibu kutokana na dalili ya kisharia, na katika hali hii kuona kwa macho si sharti; kama kwamba mtu aliyefungwa shimoni akijua kukamilika kwa mwezi, au kwa kufanya jitihada kutokana na alama kuwa leo ni mwanzo wa Ramadhani, basi analazimika afunge saumu, bila ya yeye kuuona Mwezi mwandamo wala kuambiwa na mtu aliyeuona”. [Mwisho].
Na Mtaalamu Al-Qalyubiy katika kitabu cha: [Hashiya Ala Sharh Al-Muhalla Ala Al-Minhaj: 2/63] alinukulu kutoka kwa Mtaalamu Ibn Qasim Al-A’abbadiy (Aliyefariki Mwaka, 994 H.) kauli yake: “Kama hesabu ya kweli inaonesha kutoonekana Mwezi mwandamo, hapo haitakubalika kauli ya waaminifu kwa kuona, na ushahidi wao utakataliwa”, kisha Al-Qalyubiy akaongeza: “Hii ni dhahiri sana, na haijuzu hapo kufunga saumu, na kupinga hivi ni inadi na kiburi”. [Mwisho].
Na hivi ndivyo ilivyoamuliwa na Sheikh mkubwa Muhiy-Diin Ibn Al-Arabiy Al-Andalusiy (Aliyefariki Mwaka, 638 H.) ambapo akisema katika [Al-Futuhaat Al-makkiyah; 1/606, Ch. ya Al-Maimaniyah]:
“Wanazuoni walihitilafiana juu ya Mwezi uliofunikwa na mawingu, wengi wao walisema: kukamilisha siku za mwezi ziwe thelathini; na kama Mwezi uliofunikwa ni wa mwanzo wa mwezi, basi mwezi uliopita utakamilishwa thelathini, na mwanzo wa Ramadhai utakuwa siku ya thelathini na moja, na kama Mwezi uliofichwa ni wa mwisho wa mwezi- yaani mwezi wa Ramadhani- watu watafunga saumu siku thelathini, na baadhi yao wanasema kuwa: ikiwa Mwezi uliofinkwa ni wa mwanzo wa mwezi watafunga saumu siku ya ishirini na nane, nayo ni siku ya shaka, na wengine wanasema kuwa: hesabu itumike kutokana na mwendo wa mwezi na Jua, nayo ni madhehebu ya Ibn Ash-Shikhiir, na hii ni kauli yangu pia”. [Mwisho].
Wengi wa wanazuoni wa sasa wanapendelea kutegemea mahesabu ya kianga katika kuthibitisha Miezi miandamo, miongoni mwao ni: Mtaalamu Shihabudin Al-marjani At-Tatariy Al-Qazaniy (aliyefariki Mwaka, 1889) katika kitabu chake [Nadhuratul-Haq Fi Fardhiyat Al-Ishaa Waillam Yaghib Ash-Shafaq: Uk. 44-45, Ch. ya Qazan] akisema:
“Aina zote za hesabu ni mambo thabiti na yenye hoja na hakuna njia ya kuyapinga, lakini baada ya kuyafahamu na kuyajua… na wanazuoni na wengine hurejea kwa wenye uzoefu kuhusu masuala yote kutokana na utaalamu wao; wanaichukua kauli ya wanazuoni wa lugha ya maana za maneno ya Qur`ani na Hadithi, na kauli ya Mganga / Daktari ya kufungua saumu kupitia mwezi wa Ramadhani, n.k., hapo basi, kitu gani kinachozuia kutumia hesabu katika kukamilisha mwezi wa Shabani na miezi mengine ingawa ni thabiti na inakwenda sambamba na maelezo ya Mwenye Sharia?”. [Mwisho].
Na miongoni mwao pia ni: Sheikh Muhammad jamalu-din Al-Qasimiy Ad-Dimishqiy (Aliyefariki Mwaka, 1914), kama ilivyofahamika kutoka kwa utangulizi wake wa kitabu cha [Al-Alam Al-manshuur, na Imamu Taqiiy-Din As-Subkiy].
Na miongoni mwao pia ni: Sheikh Muhammad Rasiid Ridha (Aliyefariki Mwaka 1935) ambapo alisema katika [Tafsiir Al-manaar: 2/151, Ch. ya Al-hjaiah Al-Masriyah Al-A’amah Lilkitaab]: “Hisabu inayojulikana katika wakati wetu huu hupelekea elimu thabiti… na viongozi wa waislamu na mahakimu wao ambao wana yakini ya hivi, wanaweza kutoa amri ya kuitekeleza, ili iwe hoja kwa watu wote”. [Mwisho].
Na miongomi mwao pia ni: Mkuu wa wanazuoni wa zamani yake, Mufti wa Nchi ya Misri wa zamani, Mtaalamu Mhakiki Sheikh Muhammada Bakhiit Al-Mut’iiy (Aliyefariki Mwaka, 1936) katika kitabu chake [Irshaad Ahlil-Millah Ila Ithbaat Al-Ahillah; Uk. 256-257, Ch. ya Matbaat Kurditaan Al-ilmiyah] amesema: “Watu wote, nchi zote na zamani zote, siku zote wanategemea kuainisha nyakati kwa njia ya hesabu ya kutumia mchanga au maji, n.k., kama ukisia mizunguko ya sayari, bali ni bora zaidi na anaweza kulazimika kujua mwanzo wake na kuona sayari na mfano wake, na akajengea hoja yake, na hayo yote hayawezekani ila kwa elimu na hisabu”. [Mwisho].
Na miongoni mwao pia ni: Sheikh Mtaalamu Tantawiy Jawhariy, mwenye anayefahamika kama (Mwanahekima wa Uislamu) (Aliyefariki Mwaka, 1940 ) katika kitabu chake [Al-Hilaal: Uk. 30] amesema: “Hesabu… ni kitu kizuri kinachotakiwa; ili iwe kinga inayozuia kosa la hisia, kusudio la kusema uongo, na kutaka kutoa shahada kwa ajili ya kupata thawabu tu, n.k.,”. [Mwisho].
Na miongoni mwao pia Imamu mkubwa Sheikh wa Uislamu Muhammad Mustafa Al-Maraghiy (Aliyefariki Mwaka, 1945), ambapo Sheikh Ahmad Shakir katika Risala yake: [Awail Ash-Shuhuur: Uk. 15] alisema: “Sheikh Al-Maraghiy alikuwa na rai tangu zaidi ya miaka kumi, wakati alipokuwa Mkuu wa Mahakama ya juu ya kisharia, kurudi ushahidi wa mashahidi ikiwa hesabu inathibitisha kutowezekana Mwezi”. [Mwisho], na vivyo hivyo alisema Sheikh wa Uislamu Abdu-Rahman Taj, Mwenyezi Mungu amrehemu.
Na miongoni mwao pia: Sheikh Ahmad Muhammad Shakir (aliyefariki Mwaka, 1958) aliyeandika Risala pekee iitwayo: [Awail Ash-Shuhuur Al-Araniyah, Je, inajuzu kuithbitisha kwa njia ya mahesabu ya kianga? Amesema katika UK. 14]: “Ikiwa italazimika kurejea katika hesabu peke yake, kwa kutokuwepo sababu ya kuizuia, basi itawajibika kurejea hesabu ya kweli ya Miezi miandamo, na kuepusha suala la kuweza au kutokuweza kuona, na mwanzo wa kweli wa mwezi unakuwa usiku ambao Mwezi mwandamo unapotea baada ya machweo ya Jua, hata punde kidogo”, kisha akasema [Uk. 15] baada ya kunukulu rai iliyotangulia ya Sheikh Al-Maraghiy:
“Mimi, baba yangu na baadhi ya wenzangu tulikuwa miongoni mwa walioipinga rai ya Mwalimu Mkuu, lakini sasa natangaza kuwa yeye alikuwa sawa, nami naongeza kuwa inawajibika kuthibitisha Miezi kwa njia ya hesabu katika hali zote, isipokuwa kwa wale wanaopata ugumu kufanya hivi”. [Mwisho].
Na miongoni mwao pia Imamu Al-Hafidh As-Saiyd Ahmad Ibn As-Siddiq Al-Ghumariy Al-Hasaniy (Aliyefariki Mwaka, 1960) katika utafiti wake: [Tawjih Al-Andhar Li Tawhiid Al-Muslimiin fi As-Saum Wal Iftaar].
Na miongoni mwao pia mwanafiqhi Sheikh Mustafa Ibn Ahmad Az-Zarqa Al-Halabiy (Aliyefariki Mwaka, 1999) katika utafiti wake: [Kwa nini kuna tofauti juu ya mahesabu ya kianga?], na miongoni mwa kauli zake ni: “Amri ya Sharia ya kutegemea kuona Mwezi mwandamo si kwa sababu kuwa kuona kwake ni ibada, au ndani yake kuna maana ya ibada, bali ni kwa kuwa hiyo ni njia nyepesi katika wakati huu ili kujua mwanzo wa mwezi wa kiislamu na mwisho wake kwa watu ambao hawana elimu ya kusoma na kuandika na mahesabu ya kianga.
Kutokana na maana ya matini ya kisharia ni kwamba: Mtume S.A.W., na watu wake Waarabu katika wakati huo kama wangelikuwa wanajua kuandika na wanajua mahesabu ambapo wanaweza kuzichunguza sayari na kuzidhibiti kwa njia ya kuandika na kuhesabu mwendo wake wa mzunguko uliopangiliwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mjuzi na Muweza kwa njia isiyo na kasoro wala tofauti, mpaka wakaweza kujua mapema kwa njia ya mahesabu lini utaandama Mwezi mpya? ambapo ni alama ya kuisha mwezi uliopita na kuanza mwezi ujao, wangeliweza kutegemea mahesabu ya kianga. Vile vile wote wanaoweza kufikia ngazi madhubuti ya kutumia elimu hii kwa hali ya kuaminika usahihi wake. Hapo basi bila shaka ni afadhali na bora katika kuthibitisha Mwezi kuliko kutegemea mashahidi wawili ambao hawana kinga ya wasiwasi na udanganyifu wa macho, au uongo kwa ajili ya haja au masilahi binafsi yasiyofichikana, hata tukijaribu kuchunguza uadilifu wao, ili tuweze kuthibitisha ukweli wao.
Kwa njia ya ma hesabu ya kianga ni afadhali na bora zaidi kuliko kumtegemea shahidi mmoja wakati wa hali ya anga ni ya mawingu na kuwa kuona ni kugumu, na hii ni kama ilivyo kwa baadhi ya madhehebu yanayotegemewa katika hali hii”. [Mwisho].
Kuna jumla ya dalili ya dalili nyingi zinazoonesha kutegemea mahesabu ya kianga, baadhi yake zimechukuliwa kutoka katika Qur`ani Tukufu, na baadhi yake kutoka katika Sunna Tukufu, na baadhi yake kutoka katika maoni sahihi.
Kuhusu Qur`ani Tukufu, kauli yake Mwenyezi Mungu: {(Mwezi huo mlioambiwa mfunge) ni Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huo hii Qurani ili iwe uwongozi kwa watu, na hoja zilizo wazi wa uwongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili). Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge}. [AL BAQARAH; 185], kuuona Mwezi ima kuwe kuwepo ndani yake na kutosafiri, au kwa kujua kuwepo kwake, na maana hii ya pili ni ndiyo inayofahamika na Aya hii; kwa sababu kushuhudia mwezi kwa maana ya kujua ni sababu ya kweli ya kuwajibika saumu, na kauli yake Mwenyezi Mungu: {afunge} maana yake: kila mmoja kati yenu akijua kuwa mwezi upo, yaani Mwezi wa Ramadhani, basi atawajibika kuufunga, na kuwepo kwa mwezi kisharia ni kuwepo kwa Mwezi mwandamo wake baada ya mchweo Jua; kwa namna ambayo muonaji anauona, kwa hiyo atakayejua kuwepo kwa Mwezi mwandamo baada ya mchweo kwa njia yo yote miongoni mwa njia za kujua hata ikiwa kwa dhana yenye nguvu, na ikiwa kujua ni kwa njia ya kuona kwa yeye mwenyewe, au kuambiwa na mtu mwaminifu, au kwa amri ya kadhi, au kwa njia ya mahesabu ya kianga ambayo yanayoonyesha kuwa kuwepo kwake na uwezekano wa kuonekana kwake bila ya ugumu wowote, kama hakuna kizuizi chochote, basi atawajibika kufunga. Na kuambatanisha kufunga na kufungua kwa kuuona Mwezi hakupingani mahesabu ya kianga, kwa sababu kuona hakulazimiki kuwa kwa kitendo, bali inatosha katika kuuona Mwezi wazi wazi pawepo na dalili ya kuwa anaweza kuona kama hakuna kizuizi. Tazama: [Irshaad Ahl Al-Millah, na Mtaalamu sheikh Muhammad Bakhiit Al-Mutii’iy: Uk.: 259-261].
Kuhusu Sunna Tukufu: imepokewa na Bukariy na Muslim, kutoka kwa Ibn Omar R.A, kuwa Mtume S.A.W., alisema: “Mkiuona Mwezi fungeni, na mkiuona tena fungueni, na kama ukifunikwa kwenu na mawingu, basi kadirieni”, na Hadithi hii inaonesha asili ya hukumu ya kutegemea mahesabu ya kianga, kwa mtazamo wa pande mbali mbali:
Kwanza: Hadithi hii imeambatanisha kufunga na kufungua kwa kuona Mwezi mwandamo, yaani kwa macho, na kuhusisha kuona kwa macho makusudio yake ni rehema kwa wenye kukalifishwa na kurahisishia kwao, waambiwa wao kwa amri iliyo wazi ambayo kila mmoja anaijua na wala hawezi kuikosea, kinyume na hesabu ambayo hawajui isipokuwa wachache, kadhalika kuona kwa macho ni rahisi kuliko njia zingine, kwa kuwa kwake inawezekana kwa kila mtu, lakini vyombo vya kuchunguza sayari havipatikani kwa kila mmoja, na njia hizi mbili ni dalili na alama zinazotumika kujua nyakati za ibada, ingawa mwenye Sheria hajaufanya mzunguko wa elimu kwa nyakati hizo kwa elimu ya hesabu, isipokuwa hakuzuia kutoa dalili ya nyakati hizo kwa anayezijua, kwani hesabu ni dalili pia.
Kwa hiyo, Imamu Abul-Abbas Ibn Suraij- aliyekuwa akijulikana kama Shafiy Mdogo- alitaja kuwa: katika Hadithi hii kuna aina mbili za amri, kwani kauli yake S.A.W.,: “Kamilisheni idadi za siku” inaelekezwa kwa watu wote ambao hawakuona Mwezi mwandamo, na hawajui kukadiria vituo vyake wala mahesabu ya kianga; na kauli yake: “ukadirieni” inaelekezwa kwa wale waliopewa na Mwenyezi Mungu elimu ya mahesabu ya kianga na wanaojua elimu ya anga, kwa kuwahimiza kujua mahesabu ya kituo cha mwandamo.
Mtaalamu Abu-Mansuur Al-Azhariy katika kitabu chake [Az-Zahir Fi Ghariib Alfadh Ash-Shafiy: Uk. 113-0114, Ch. Ya Dar At-Talai’] anasema: “Nilimsikia Abul-Hassan As-singaniy akisema: Nilimsikia Abul-Abbas Ibn Suraij akisema katika kuelekeza habari hizi mbili kuwa: hitilafu ya amri za Mtume S.A.W, ndiyo kutokana na tofauti ya akili za wenye kuambiwa:
- Akamuelekeza yule asiyejua kukadiria vituo vya Mwezi akamilishe idadi ya siku za mwezi aliokuwa nao, mpaka aingie katika mwingine kwa yakini.
- Na akawaelekezea wale wanaojua elimu ya mahesabu ya vituo, miongoni mwa wapiga mahesabu bingwa- nao ni wachache- wapige mahesabu na wakadirie, hata iwadhihirikie ukamilifu wa idadi ya siku za mwezi ishirini na tisa au thelathini, watauingia mwezi ujao kwa yakini iliyowadhihirikia.
Abul-Abbas anasema: kulingana na haya kuwa: inaruhusiwa kwa watu wa kawaida kuwafuata wanazuoni kwa yale wanayoyatolea Fatwa, lakini wanazuoni na wanajitihada wanalazimika kujilinda na kutokufuata ila Qur`ani na Sunna. Na kila moja ya kauli ya hizi mbili ina mwelekeo wake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa yote” [mwisho].
Pili: Hadithi ilitaja kuwa kuuona Mwezi ni sababu ya kufunga na kufungua, na hukumu kama hii ikiambatanishwa na sababu, na ikajulikana maana ya sababu, kisha ikipatikana katika wasifu mwingine, hapo inajuzu kuitekeleza sababu hiyo; na suala hili linajulikana katika elimu ya Usuli ya Fiqhi kuwa: (Kipimo cha Sababu), na hukumu iliyochaguliwa na wanazuoni wengi wa Misingi ya Fiqhi, miongoni mwao:
Hojjatul-Islam Al-Ghazaliy (Aliyefariki Mwaka: 505 H.), Imamul-Kiya A-Harasiy (Aliyefariki Mwaka: 504 H.) kuwa: inajuzu. Imamu Az-Zarkashiy, mfuasi wa madhehebu ya Shafiy katika kitabu chake [Al-Bahr Al-Muhiit: 7/85, Ch. Ya Dar Al-Kutbiy] anasema: “Hukumu iliyoinukuliwa kutoka kwa wanachuoni wetu wa madhehebu ya Shafi kuwa ni: Inajuzu”. [Mwisho], na kwa mujibu wa hayo: Hakika mambo yalivyo kuona kwa macho kunambatanishwa na sababu zingine zinazolifikia lengo la kuona kwa kuthibitisha kuingia kwa mwezi au kutoka kwake kama vile mahesabu ya kianga.
Tatu: kauli yake (ukadirieni) inafasiriwa kuwa ni ukadiriaji wa mahesabu ya vituo vya mwezi; kwa sababu haya ndiyo yaliyoelezwa na Qur`ani Tukufu katika kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na mwezi (kadhalika ni alama kwao); Tumeupumia vituo, (hiki baada ya hiki); mpaka unakuwa (mwembamba) kama chaparare la mtende kuukuu (lililonywea)}. [YASIIN: 39], na kauli yake Mwenyezi Mungu: {Yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye aliyelifanya jua kuwa muanga, na mwezi kuwa nuru, na akaupimia vituo (huu mwezi) ili mjue idadi ya miaka na hisabu (nyinginezo)}. [YUNUS: 5], kwa hiyo Mtume SAW, anaashiria kwa kauli yake hiyo jinsi Mwenyezi Mungu alivyokadirina vituo vya Mwezi na mwendo wake ndani ya vituo hivyo.
Imamu Abu Jaafar At-Twahawiy katika kitabu chake [Sharh Mushkil Al-Athaar: 9/385, Ch. Ya Muassasat Ar-Risalah] anasema: “tumezingatia kauli yake SAW, (ukadirieni) nini makusudio yake S.A.W? Tumesikia mazuri zaidi tuliyoyasikia katika kauli hiyo- na mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi- kuwa Allah Mtukufu alisema katika kitabu chake: {Na mwezi (kadhalika ni alama kwao); Tumeupumia vituo, (hiki baada ya hiki); mpaka unakuwa (mwembamba) kama chaparare la mtende kuukuu (lililonywea)},
Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema kwamba Yeye ameukadiria Mwezi vituo vyake vya kupitia, ikawa hivyo kwamba Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu akaupitisha Mwezi na kuufanya upite kila usiku mmoja mpaka kituo kimoja kikamalizika, nacho ni sehemu ya sita juu ya saba ya saa moja, kwa sababu vituo vya usiku viko kumi na nne, na masaa yake ni kumi na nne, na upeo wa kila kituo ni sehemu sita juu ya saba ya saa moja.
Kwa hivyo, Mwezi unapita katika nyusiku ishirini na nane na unajificha, na ikiwa mwezi una siku thelathini unajificha nyusiku mbili, na ikiwa mwezi una siku ishirini na tisa, unajificha usiku mmoja tu. Kwa hivyo, kilichoamrishwa katika Hadithi ya Ibn Omar R.A., ni kwamba Mwezi utakapofunikwa na mawingi kisha ukachomoza, tutaangalia unavyozama, na ikiwa ni kwa ajili kituo kimoja, tutajua kuwa huo ni usiku wake, na ikiwa ni kwa vituo viwili, tutajua kuwa ni kwa nyusiku mbili, na tutatambua kwa hivyo kwamba kati yake kuna siku moja, na kwamba sisi tunalazimika kuilipa siku hii, ikiwa ni ya Mwezi Mtuku wa Ramadhani”. [Mwisho].
Pia miongoni mwa dalili: ilivyopokelewa na Muslim, kutoka kwa Abu Hurairah R.A., alisema kuwa: Mtume S.A.W., alitaja Mwezi mwandamo akisema: “Mkiuona fungeni, na mkiuona fungueni, na kama ukifunikwa na mawingu, basi hesabuni siku thelethini”, pia kuna suala la kuunganisha hukumu ya kuona Mwezi, bila ya kuusia suala la kukadiria wakati wa Mwezi kufunikwa na mawingu, na kitenzi (ona) kina maana mbili katika Kiarabu: kuona kwa macho, na kuona kwa moyo, kwa mfano: nilimwona ndege mtini, maana yake nilimtazama; na niliyaona maoni ya fulani; maana yake niliyaelewa na kuyaamini.
Maana hizi mbili zinafaa kuwemo katika Hadithi, na kutumia tamko moja kwa na maana isiyo halisi kwa pamoja kunakubalika na wengi wa wanazuoni wa elimu ya Misingi ya Fiqhi, miongoni mwao; Imamu Shafi na wengi wa wafuasi wake; kwa mfano kauli yake mwenyezi Mungu:
{Enyi mlioamini! Mnaposimama ili mkasali, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpaka vichwa vyenu, na (osheni) miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi kusudieni (tayamamuni) udongo (mchanga) ulio safi na kuupaka nyuso zenu na mikono yenu}. [AL MAIDAH: 6], hapa (mmeingiliana na wanawake), neno kugusa katika Qur`ani lina maana halisi ya kugusa kwa mkono, na maana isiyo halisi ya kukutana kimwili.
Kwa mujibu wa hayo Hadithi ni kutaka ujumla kwa kuelewa, na dalili ya hayo kuwa: Tuchukulie kuwa watu wa mji fulani ni vipofu isipokuwa wachache, na wachache wangeuona Mwezi mwandamo, au wanazijua nyakati zake kwa kuziona alama zake, kisha wanawaambia vipofu, wakiwa waadilifu, maelezo yao yatalazimika kukubalika.
Vile vile wabobezi wa mahesabu ya kianga wanazijua alama kwa mahesabu ya kianga, kisha wanawaeleza wasioyajua na maelezo ya, maelezo yao yanakubalika, iwapo uadilifu wao utakuwepo.
Kwa upande wa maoni ya akili: kipimo cha kuthibitisha mianzo ya miezi ya kiislamu kwa njia ya mahesabu, ni kipimo cha kuthibitisha nyakati za Swala kwa njia hiyo hiyo; kwa sababu hakuna tofauti kati yake, hivi sasa Swala duniani kote, imekuwa inategemea mahesabu, bila ya kukanushwa na mtu yeyoye, na hakuna mtu yeyote anayesema kuwa hili ni kosa, na kwamba ni kuliona Jua kwa macho ili azione alama za kuingia kwa nyakati za Swala, vile vile inajuzu kutumia mahesabu ya kianga ili kujua mwanzo na mwisho wa miezi.
Ama kutumia Hadithi iliyopokelewa na Maimamu wawili, kutoka kwa Ibn Omar R.A., kuwa Mtume S.A.W, alisema:
“Sisi ni umma usiojua kusoma na kuandika; hatuandiki wala hatupigi mahesabu, mwezi wetu upo hivi na hivi”, yaani siku ishirini na tisa, au siku thelathini- kuwa ni dalili ya kutotumia mahesabu ya kianga katika kuthibitisha Miezi miandamo, hakika maneno haya si sahihi, kwa sababu Hadithi hii haikukataza kutumia kuandika wala kuhisabu, wala haikupunguza umuhimu wake, wala haikuashiria kuvunja elimu ya anga, isipokuwa inawaelezea waislamu wa zama za Mtume S.A.W., ambao hii ilikuwa sifa ya wengi wao, na hii haimaanishi kuwa sifa ya (kutojua kusoma na kuandika) ni sifa inayoambatana na umma wa kiislamu kwa zama kwa zama na nchi zote.
Al-Hafidh Ibn Hajar Al-A’asqalaniy kayika kitabu chake [Fath Al-Bariy: 4/127, Ch. Ya Dar Al-Ma’rifah] anasema: “Kauli yake Mtume S.A.W, (Hatuandiki wala hatupigi mahesabu) muradi wake wale waislamu waliohudhuria kikao chake wakati wa usemi huu, na huu unasemwa kwa wengi wao, na miongoni mwao ni Yeye Mwenyewe S.A.W… pia hii ni tafsiri ya hali yao, na Waarabu walijulikana kuwa (Ummiyun) kwa sababu uandishi ulikuwa nadra kwao, na Mwenyezi Mungu anasema:
{Yeye ndiye aliyeleta Mtume katika watu wsiojua kusoma, anayetokana na wao, awasomee Aya zake na kuwatakasa na kuwafunza Kitabu na Hikima, (ilimu nyiginezo). Na kabla ya haya walikuwa katika upotofu (upotevu) ulio dhahiri}. [AL JUMA'A: 2], na hii haipingi kuwa kuna miongoni mwao anayejua kuandika na kupiga mahesabu kwani uandishi ulikuwa nadra kwao, na maana ya mahesabu hapa ni: Mahesabu ya mwendo wa nyota, na pia walikuwa hawayajui haya isipokuwa kwa uchache tu, imeambatana hukumu ya kufunga na ibada zingine kwa kuona Mwezi kwa ajili ya kuepusha taabu kwao kwa kutumia maahesabu, na ikaendelea hukumu ya kufunga, hata akija baadaye anyejua hivyo, lakini ni dhahiri kuwa muktadha wa jumla unakanusha kuambatana hukumu na mahesabu kimsingi”. [Mwisho].
Hii inamaanisha kuwa: amri ya kutegemea kuona Mwezi si kwa sababu kuwa kuuona huko kunamaanisha ibada, lakini kwa sababu ni mbinu rahisi ya kujua mwanzo wa mwezi wa kiislamu na mwisho wake kwa watu ambao hawana na elimu ya kusoma na kuandika na mahesabu ya kianga.
Inawajibisha kutokana na hayo kuwa: Mtume SAW, na watu wake Waarabu katika wakati huo kama wangelikuwa wanajua kuandika na wanajua mahesabu ambapo wanaweza kuzichunguza sayari na kuzidhibiti kwa njia ya kuandika na kuhesabu mwendo wake wa mzunguko uliopangiliwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mjuzi na Muweza kwa njia isiyo na kasoro wala hitilafu, mpaka wakaweza kujua mapema kwa njia ya mahesabu lini utaandama Mwezi mpya? ambapo ni alama ya kuisha mwezi uliopita na kuanza mwezi ujao, wangeliweza kuyategemea mahesabu ya kianga.
Vile vile wote wanaoweza kufikia ngazi madhubuti ya kutumia elimu hii kwa hali ya kuaminika usahihi wake; kwa sababu amri ya kutegemea kuuona Mwezi peke yake imeambatana na sababu yake katika matini, nayo umma ni usiojua kuandika wala kupiga mahesabu, na sababu inaambatana na hukumu yake ya kuwepo au kutokuwepo.
Na pindi umma wa kiislamu utakapoepukana na kutojua kusoma na kuandika, ukawa ukaandika na kuhesabu, yaani wengi wa watu watakapopata elimu ya hivi, na wakaweza kufikia ngazi ya yakini katika kuhisabu mwanzo wa mwezi, ambapo hali hii italingana na kuuona Mwezi au zaidi, hapo basi wana haki ya kutegemea kuthibitisha Miezi kwa njia ya mahesabu ya kianga, bila ya uzito wowote.
Hapo basi bila shaka mahesabu ya kianga ni afadhali na bora katika kuthibitisha Mwezi kuliko kutegemea mashahidi wawili ambao hawana kinga ya wasiwasi na udanganyifu wa macho, au uongo kwa ajili ya haja au masilahi binafsi yasiyofichikana, hata tukijaribu kuchunguza uadilifu wao, ili tuweze kuthibitisha ukweli wao.
Kuhusu kauli ya baadhi ya wanazuoni kuwa kuzingatia mahesabu ni madhehebu batili, kwa sababu inategemea elimu ya nyota, na kuwa sharia imeonya na mfano wa haya, kama ilivyopokelewa na Muslim kuwa Mtume S.A.W., alisema: “Yeyote atakayemwendea mpiga ramli akamuulizia kitu, Swala yake kwa muda wa usiku arobaini haitakubaliwa”, na ilivyopokelewa na At-Tabaraniy katika Al-Mu’jam Al-Kabiir kuwa Mtume S.A.W, alisema: “Pindi Masahaba wangu wanapotajwa jizueni na maneno, na nyota zikitajwa jizueni na maneno pia, na Kadari ikitajwa vile vile jizueni na maneno”. Pia elimu ya utabiri wa nyota ni dhana na kubahatisha, na haina yakini wala dhana yenye nguvu, kwa hiyo haitegemewi kwa mambo yafuatayo:
Kwanza: Maneno haya ni mchanganyiko kati ya kupiga ramli, utabiri wa nyota na ukuhani, kwa upande mmoja, na elimu ya mahesabu ya nyota, nayo ni elimu ya anga, kwa upande mwingine.
Na elimu ya anga hata ikachanganyika na kazi za kupiga ramli na ukuhani kwa wahusika wake, lakini hivi sasa imetengana nazo kikamilifu, na ikawa inaambatana na vituo vya kisasa vya kuchunguza, na vyombo vya kuchunguza sayari na miendo yake kwa umbali unaokadiriwa kwa mamilioni ya miaka ya mwanga, na iliyojengeka kwa milinganyo ya kihisabati na kanuni za ulimwengu, na hisabati madhubuti zenye uhakika ndizo zinzopambanua miendo hii kwa sekunde na sehemu za sekunde.
Hivi sasa elimu ya anga iko mbali na shubha ya kutabiri nyota inayomaanisha kutabiri mambo, na elimu ya anga imejengeka kwa elimu za fizikia, hisabati, na kimia katika ngazi zake za juu za kiakademia. Bali Elimu ya Viumbe hai (Biolojia) imeungia katika mitaala yake na tafiti zake, baada ya kujitenga Elimu ya kuchunguza Staarabu zilizoendelea, elimu ambayo inashughulikia sura za uhai ulio nje ya Mfumo wa Jua na Sayari zake.
Pili: elimu ya nyota ya zamani si mbaya kabisa, Mtaalamu Al-Mirghinaniy, mfuasi wa madhehebu ya hanafi na wandishi wa kitabu cha Al-Hidayah anasema katika (Masuala yaliyochaguliwa) kuwa: “Elimu ya nyota yenyewe ni nzuri na si mbaya, nayo ni aina mbili: ya hesabu, nayo ni kweli, kutokana na kauli ya Qur`ani Tukufu, na Mwenyezi Mungu alisema: {Jua na mwezi (hwenda) kwa hisabu (yake)}. [Ar RAHMAN: 5], Yaani miendo yake kwa hisabu madhubuti, na aina ya pili ni: ya kutoa dalili, kwa mwendo wa nyota na harakati za sayari, na kutazamia matokeo kutokana na hivi, kwa mujibu wa uamuzi wa Mwenyezi Mungu na kadari yake, na hii inajuzu; kama vile daktari anapochunguza hali ya afya na maradhi kwa mujibu wa mapigo ya moyo, hata kama hakuamini kadha ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, au akadai elimu ya mambo yasiyojulikana, hapo ni kafiri”. [Mwisho, imenukuliwa na: Hashiytat Mtaalamu Ibn Abdiin: 1/43-44, Ch. Ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]
Tatu: Kusemwa vibaya kwa elimu ya nyota ya zamani ilikuwa kwa sababu ambazo hazikuwepo katika elimu ya anga ya kisasa, na Hujatul Islam Al-ghazaliy katika [Al-Ihiyaa; 1/29-30, Ch. Ya dar Al-Maarifah] anasema: “Hakika imezuiwa kwa sababu tatu:
kwanza: inawadhuru watu wengi; kwa sababu watu wakiamini kuwa matokeo wnayoyakabili kutokana na mwendo wa sayari, wataamini kuwa sayari hizi ndizo zenye kuathiri na ni miungu inayoendesha mambo; na kwa sababu sayari hizi ni viumbe vitukufu vya mbinguni, kwa hiyo vinatukuka katika nyoyo za watu, na hii hupelekea kuwa moyo kuambatana nazo, na kutazamia heri na shari kuwepo au kutokuwepo kwa upande wake.
Pili: kanuni za utabiri wa nyota ni dhana tu, hazifikiwi na yeyote si kwa njia ya yakini au njia ya dhana, kwa hiyo hukumu yake ni ujinga, basi kulaumiwa kwake kwa sababu ni ujinga na wala si kwa kuwa elimu, na inavyosimuliwa kuwa kazi hii ilikuwa muujiza kwa Mtume Idrisi A.S., na hakika imetoweka , na yanayoafikiana na utabiri wa najimu kwa nadra ni usadifu tu, lakini ni kwa bahati tu, kwa sababu huenda anatazamia baadhi ya sababu bila ya kuwepo matokeo yake, isipokuwa baada ya masharti mengi ambayo bianadamu hawezi kujua hakika zake, na kama Mwenyezi Mungu akileta sababu zote, basi matokeo yapo, na kama asipoleta, basi matokeo hayapo, na sura ya hii ni kama vile:
Mtu kukisia kwamba leo mvua itanyesha kwa sababu ya kuona mawingu mengi juu ya milima, na yeye akaamini hivyo, na huenda joto la jua likazidi, na mawingu yakatoweka, au huenda matokeo yakawa kinyume, hapo kuwepo kwa mawingu tu hakutoshi kunyesha mvua, pamoja na kutoelewa mabaki ya sababu, kwa hiyo inakatazwa kuzungumzia nyota kwa hii sababu.
Tatu: kuwa haina faida; kwa sababu ni kazi bure na kupoteza umri, ambao ni kitu ghali kuliko vitu vyote bila ya faida, na hiki kiwango cha juu cha hasara”. [Mwisho kwa maelezo machache].
Na kitu kama hiki hakipo katika elimu ya kianga ya kisasa, nayo si sababu ya kuwa watu wanaamini katika kuathiri sayari zenyewe katika uliumwengu, au wanaamini kuwa hii ni miungu, bali hakika mambo yalivyo ni sababu ya kumjua Mwenyezi Mungu na kuujua mfumo wa ulimwengu ambao ni dalili ya uwepo wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anasema:
{Hakika katika mfuatano (wa daima) wa usiku na mchana; na katika alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi; ziko dalili (dhahiri za kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja tu) kwa watu wnaoogopa}. [YUNUS: 6], na haijengeki na dhana, bali ni yakini kwa sababu inajengeka kwa kanuni za yakini, na kutokana na elimu hii na kanuni zake zimejengeka vituo vya anga vinavyozunguka ardhini, na kurushwa satalaiti kwa angani, na zikaandaliwa safari za anganikuelekea katika maeneo ambayo ni vigumu kwa mwanadamu kuyafikia kwa sababu za kimaumbile, na mitambo hii inatayarishwa kwa ajili ya kushughulika kazi maalum katika wakati maalum na mahali maalum.
Pia elimu hii haifikiriwi kuwa haina faida, bali ni katika fardhi za kutoshelezeana, ambayo umma wote utapata dhambi katika hali ya kutokuwepo anayeijua elimu hii, kwa kuwa inategemezwa nayo jumla ya masilahi ya dini na dunia ambayo hayatimizwi isipokuwa kwa kuijifunza na kuijua.
Na sisi tunaona kuwa suala la kutegemea mahesabu ya kianga- kwa maana ya kukanusha kuona mwezi kwa macho, hali ya hesabu ya kifalaki ikisisistiza kuwa ni kosa; au kwa maana nyingine: kutegemea kuona kwa macho katika hali ya kukanusha tu, bila ya kuthibitisha - suala hili halisihi kuwa maudhui ya tofauti; kwa sababu yameamuliwa kisharia kuwa dalili ya yakini inatanguliza mbele ya dalili ya dhana; yaani mahesabu ya yakini hayawezi kupingana na kuonekana sahihi, kwa hiyo Imamu Mujtahid At-Taqiy As-Subkiy katika [Al-Fatawa; 1/209,217] anasema:

“Hatusemi kuwa: Sharia imetengua kauli ya mahesabu kwa uwazi, na kuwa wanazuoni wa Fiqhi wanasema: elimu ya mahesabu ya kianga (haitegemewi); hakika mambo yalivyo wamelisema kinyume chake, na suala hili lililotangulia ambalo tumelizungumzia lina hitilafu, ama suala hili la sasa halina tofauti yoyote.
Na haiamniki kuwa Sharia ilitengua kauli ya mahesabu kwa uwazi, hii haikuwepo, iweje! Wakati mahesabu unategemewa katika mirathi na mambo mengine, na ilivyotajwa katika Hadithi ni kuandika na kuhesabu, na ikiwa kuandika hakukatazwi, basi mahesabu ni hivyo hivyo, na muradi hapa ni kudhibiti hukumu ya kisheria kuhusu mwezi kwa njia mbili zinazodhihiri kwa uwazi, nazo ni: kuona Mwezi mwandamo au kutimiza siku thelathini, na kuwa mwezi huwa na siku ishirini na tisa au siku thelathini, kwa hiyo mwezi si muda wa wakati unaodhibitiwa kwa hisabu, kama walivyosema wanazuoni wa elimu ya anga.
Pia mwanazuoni haamini kuwa suala hili ni lile lile ambalo wanazuoni walisema katika kitabu cha kufunga kuwa: Rai sahihi ni kutotekeleza hesabu; kwa sababu hii ni kweli kama mahesabu yakikanusha utazamaji, na suala hili ni kinyume chake. Na hakuna shaka kuwa: anayesema katika suala la kwanza kuwa: saumu ni kujuzu au wajibu, anasema katika suala hili: Haijuzu kwa uwazi zaidi; na anayesema kule: Haijuzu, hapa hasemi kitu.
Lakini maoni yetu hasa kuwa: Haijuzu, na kutokujuzu hapa ni kauli ya yakini, na sisi hatuoni suala hili ndani ya vitabu, lakini tulijitahidi juu yake, na kwa hiyo ni miongoni mwa masuala ya yakini na si mwa masuala ya dhana, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi”.
Kisha akasema: “Huenda baadhi ya watu ambao hawana akili na wajinga wakawa na wasiwasi tuliyoyasema, na wakakanusha kutegemea mahesabu kwa uwazi, na husimama kwenye kila lililoshuhudiwa na mashahidi wawili linathibiti; na watu kama hao hatuna mazungumzo nao, na sisi hakika tunazungumza na mwenye akili, ama mjinga kumzungumzia hapana”. [Mwisho}.
Mfano wa hayo, ilivyonukuliwa na Mtaalamu Al-Qalyubiy katika kitabu cha: [Hashiya Ala Sharh Al-Muhalla Ala Al-Minhaj: 2/63] kutoka kwa Mtaalamu Ibn Qasim Al-A’abbadiy (Aliyefariki Mwaka, 994 H.) kauli yake: “Kama mahesabu ya kweli huonyesha kutoweza kuona Mwezi, hapo haitakubalika kauli ya waaminifu kwa kuona, na shahada yao itakataliwa”, kisha Al-Qalyubiy akaongeza: “Hii ni dhahiri sana, na haijuzu hapo kufunga saumu, na kupinga hivi ni ukaidi na kiburi”. [Mwisho].
Hakika, hakuna upingano wa kweli kati ya ushahidi wenyewe na mahesabu ya kianga katika jambo hili, na ushahidi utakataliwa katika hali ya kupinga mahesabu ya kianga- hata kama mahesabu hayakuwa ya yakini, bali ni yalikuwa karibu ya yakini- kwa sababu katika ushahidi kuna kinachotengua, nacho ni dhana yenye nguvu kuwa shahidi hakudhibiti alivyoiona; kwa hiyo shahidi akipinga hesabu ya kweli ni dalili ya kutoelewa kwake tabia ya kitu anavyokishuhudia. Na katika hivi Imamu Mtaalamu Sheikh Muhammad Bakhiit Al-Muti’iy katika kitabu cha [Irshad Ahlil Millah; Uk. 290, Ch. ya Matbaat Kurdistaan Al-Ilmiyah] anasema:
“Kama ushihadi utakataliwa kwa sababu ya upekee unaopelekea kosa au uongo, wanapouona Mwezi watu wachache na si wengi- na haya yameandikwa na vigogo wa madhehebu ya Hanafi na Maliki, kama itakavyotajwa baadaye- iweje hakuna wa kurudi ikiwepo dalili ya nguvu au karibu ya nguvu kuwa kuona Mwezi mwandamo hakuwezekani! Bila shaka kuwa kutokubali ushihadi hapa ni bora;
Hakika mambo yalivyo wachache wakiona na wengi wakawa hawakuuona, basi kutokuuona Mwezi mwandamo wengi wao kunawajibisha dhana ya wachache kukosea au kusema uongo katika madai yao ya kuuona Mwezi, kuhusu mahesabu hapa, dalili yake ni yenye yakini au karibu na hiyo; kwa hiyo walijaalia miongoni mwa masharti ya habari yenye uhakika zaidi ili kuleta elimu kwa msikilizaji kuwa msikilizaji asiwe mwenye kuamini kinyume na maudhui ya habari hiyo; ima kwa shubha, kuiga, au kuitakidi.
Kama ikiwa hii ni hali ya habari yenye uhakika zaidi, itakuwaje kwa isiyokuwa hiyo! Hapo, kadhi akikubali shahada ya anayeshuhudia mbele yake kuona Mwezi mwandamo, pamoja na kuwa mahesabu ya yakini au karibu na yakini ya kutokuwepo uwezekano wa kuona, basi hiyo itakuwa kinyume na anavyoitakidi, kwa hiyo, As-Subkiy anasema: yeye ni mjinga, na hii si aina ya kupingana na mahesabu na ushahidia mpaka ikasemwa: unatumika ushahidi bila ya kutumika mahesabu, bali hakika hayo ni upande wa kuwepo dalili mbele ya kadhi ambaye ushahidi unatolewa mbele yake, ambayo aliamini kuwa ushahidi huu kuwa shahidi amekosea au mwongo; kwa kuwa mahesabu ya muadilifu, mwenye kubobea katika elimu yake ikionesha kuwa kuona Mwezi ni kutoweza, hapo dhana nguvu yake kuwa shahidi ni mwenye kosa au mwongo, bila ya shubha, hapo basi vipi kadhi anaweza kukubali ushahidi wa shahidi huyo?”. [Mwisho].
Suala la kurudi ushahidi kwa dhana ya kuwa ni kosa walilitaja wafuasi wa madhahebu ya Hanafi na Maliki, bila ya kujali idadi ya mashahidi. Imamu Al-Hafidh Mtaalamu Muhammda Ibn Tolon Al-Hanafiy katika baadhi ya Risala zake anasema: “wanazuoni hawakusudii kwa (upekee) ni kuwa mtu mmoja, na kama si hivyo wangekubalika wawili hawa, na hili limekanushwa, lakini maana ya (upekee) kama ilivyotajwa katika (Al-Fat-h) na vitabu vingine ni: Watu wachache wanaoshuhudia pamoja na kuwepo wengine wengi”. [Mwisho].
Na kwa kueleza maneno haya, tunataja kauli ya Imamu Abu Hanifa R.A., katika kitabu cha: [Al-Mabsuut: 3/140] akisema: “pasipokuwa mawingu mbinguni, basi haikubaliki ushahidi wa mtu mmoja wala watu wawili, bali mbele ya watu wengi kwa uwazi kuhusu Mwezi wa Ramadhani, na mfano wake Mwezi wa kufungua katika mapokezi ya kitabu hiki. Na katika mapokezi ya Al-Hasan, kutoka kwa Abi Hanifa- Mwenyezi Mungu awarehemu- anasema: “Kuhusu kuona Mwezi, imekubalika ushahidi wa wanaume wawili au mwanamume mmoja na wanawake wawili, kulingana na haki za watu.
Na rai sahihi ni iliyotajwa hapa, na kuhusu haki za watu ushahidi wa watu wawili umekubalika hali ya kutowepo jambo dhahiri linaliwakadhibisha, na hapo jambo dhahiri linawakadhibisha katika Mwezi wa Ramadhani na pia wa Shawali sawa sawa; wao wawili ni kigezo cha watu wote katika mahali, kuuona, ukali wa macho, na kituo cha Mwezi, kwa hiyo, haukubaliki ushahidi isipokuwa katika jambo wazi tana dhahiri”. [Mwisho].
Sasa hivi ushahidia unayopinga mahesabu ya kianga ni ushahidi wa jambo lisilowezekana kihisia, kwa sababu mahesabu ya kianga yenye uhakika yamekuwa jambo- kama ilivyotajwa katika (Al-kawakib Ad-Durriyah) na kunukuliwa na Sheikh Muhammad Bakhiit Al-Mutii’y katika (irshad Ahl Al-Millah)- linajengeka na kuasisiwa kwa vyombo vya kuchunguza vinavyoonekana ambavyo hupelekea kujua makadirio ya miendo ya sayari na maumbile mengineyo, na umbali wa sayari zenyewe kwa zenyewe, na kupakana kwake, na kuainisha mahali pake kwa kuona na kwa kushuhudia.
Na hii inavyoashiria maneno ya Mtaalamu Ash-Shihab Ibn Hajar Al-Haitamiy katika [Tuhfat Al-Muhtaj: 3/ 282-283, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy] kuwa: “inavyopendelewa katika hivi kuwa wataalamu wa mahesabu wakikubali kuwa utangulizi wake ni wa kweli, na watoaji wa habari ni wengi, basi ushahidi wa kuuona Mwezi utakataliwa, na kama si hivyo basi hautakataliwa, na hii ni bora kuliko kauli huru ya As-Subkiy kutengua ushahidi iwapo mahesabu ya uhakika yataonesha kutowezekana kuuona Mwezi mwandamo, au kauli huru ya wengine kuwa ushahidi umekubalika, na kila upande umerefusha maneno yake ambayo ndani yake kuna mtazamo kwa mwenye kuzingatia”.
Kwa hakika Mtaalamu At-Taqiy As-Subkiy alisema kuwa ushahidi utakataliwa kwa mtazamo mwingine usio ambao kwa ajili yake Mtaalamu Ibn hajar alirudi ushahidi; As-Subkiy aliurudi ushahidi kutokana na kuwepo dalili mbele ya kadhi ambaye ushahidi unatolewa mbele yake akiamini kwa mujibu wake kuwa shahidi huyo ni mwenye kosa au mwongo- kutokana na kutotofautisha kati ya mahesabu yenye ukweli na yanayo karibu na kweli- na hii ikawa kutia kasoro ya ushahidi wa shahidi, wakati ambao Ash-Shihab Ibn Hajar akarudi ushahidi shahada kwa sababu ya kutokuwepo kitu kilichoshuhudiwa nacho, kutokana na mahesabu yenye ukweli ni thabiti kwa njia yenye uhakika zaidi.
Kuhusu kauli ya Mtaalamu Ibn Qasim katika Hashiya yake ya [Tuhfat Al-Muhtaj Fi Sharh Al-Minhaj: 3/383, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy] kuwa: “Hakika kutoa habari kutoka kwa watu wengi kunaonesha uhakika usio na shaka, ikiwa habari hizi zinambatana na kitu kinachoonekena, basi hizi zinategemea uhisi wa tangulizi hizi na maneno yanayoambatana nazo”. [Mwisho].
Mtaalamu Sheikh Muhammad Bakhit Al-muti’iy katika [Irshad Ahl Al-Millah: Uk. 291-292] alieleza kauli hii akisema: “Muradi wake ukimaanisha kupinga kuwa maneno ya watu wengi hapa hayawezekani kwa sababu kutokuwepo kitu kinachoonekana- kama walivyofahamu baadhi ya wanazuoni maneno yake, na kunukuliwa na Ibn Abidiin katika Risala yake [Tanbiih Al-Ghafil wal Wasnaan]- basi muradi wake si sahihi..; kwa sababu inaonekana kuwa tangulizi hizi ni kihisi; lakini kama muradi wake ukimaanisha yale yale aliyoyasema Ibn Hajar kuwa: tangulizi hizi ni kihisi, na hapo kutoa habari juu yake ni kwa uhakika usio na shaka, basi muradi wake ni sahihi, na yalazima kuyafahamu yale yale, na kama imekwishjuliwa kuwa: si sharti la kurudi ushahidi kuwa idadi ya watoaji habari ni wengi, bali inatosha kuwa maneno yao huonyesha dhana yenye nguvu inayokaribia yakini kuwa kuona Mwezi hakuwezekani, na kwa kadiri hiyo ushahidi wao utakuwa mwwenye dhana ya kosa au uwongo basi utakataliwa”. [Mwisho].
Wanazuoni wa Madhehebu ya Kihanafiy walieleza kuwa ushahidi hata ungekuwa katika haki za watu ukiambatana na kitu kisicho weza kiakili au kikawaida au ukapinga uwazi basi haukubaliki, mfano wa kupokea Hadithi sawasawa, na Mtaalamu As-Sarkhsiy katika kitabu cha: [Al-Mabsuut; 3/64, Ch. ya Dar Al-Maarifah] akizungumzia shahidi: “naye ni mtoa habari inayohusu jambo la kidini, nalo ni uwajibikaji wa kuitekeleza saumu kwa watu, hapo inalazimika kukubali habari yake isipokuwa uwazi unamkadhibisha, mfano wa aliyepokea Hadithi”. [mwisho].
Na kauli ya pamoja inaonyesha kuwa ushahidi wa mwenye kushuku ushahidi wake haukubaliki, na wanazuoni wana masuala mengi ya hivyo ya kuwa: Hakika mambo yalivyo ushahidi hali ya kutowezekana kitu kinachoshuhudiwa nacho ni nguvu kwa kurudi ushahidi kuliko hali ya mashaka; basi kurudi ushahidi katika hali hii ni boR.A., na hii ni dhahiri sana na haihitaji kuinukuliwa na yeyote, Na Mtaalamu Muhammad Bakhiit Al-Muti’iy alitanabahisha hivyo katika [Irshad Ahl Al-Millah].
Na uwezekano ni kinyume na muhali, nao ni sharti la kukubali ushahidi, na wanazuoni wa fiqhi waliuhisabia sharti la kukiri. Na Imamu At-Taqiy As-Subkiy, Mola Amrehemu, anasema katika [Al-Alam Al-Manshuur; Uk. 23]; “Kadhi anaangalia hali ya mashahidi baada ya kuchunguza uadilifu wao, uelekevu wao, kutokuwa na mashaka na tuhuma, uzima wa viungo na ukali wa macho yao, na usafi wa upeo wa hewa, na mahali pa Mwezi namna ambayo inashawishi kuona, na kujua kituo cha Mwezi ambamo huchomoza, na mapimo ya mahesabu kwa njia ya uwezekano wa kuuona au unashindikana, kwa sababu kinachoshuhudiwa nacho ni sharti la uwezekano; na uwezekano ikiwa ni sharti la kukiri, na mwenye kukiri ni mtoa habari juu ya nafsi yake na pia mlinzi kwake, iweje iwepo dhana yako ya ushahidi! kwa hiyo, ni muhimu kuwa hivyo vyote vinapatikana mbele ya kadhi”. [Mwisho].
Hakika ushahidi ni muhimu katika Sharia- ingekuwa ni habari inayoweza kuambia ukweli au uongo- kwa sababu unaambatana na dalili zinazoimarisha ukweli juu ya uongo, kama vile uadilifu wa mashahidi, muafaka wa maana ya kila ushahidi kwa nyingine, muafaka wa ushahidi wao kwa madai, na kama ushahidi ukiambatana na kisichokuweza kiakili au kikawaida, au ukipinga kitu mashuhuri na wazi, basi kipo kinachoimarisha uongo juu ya ukweli, au kinaleta uhakika kuwa uongo, hapo ushahidi huu utakataliwa.
Na imetajwa katika [Al-Walwalijiyah] kuwa: “dalili ya ukweli- nayo ni uadilifu wa ushahidi wa mtu mwaminifu- inapingana na dalili ya kurudi ushahidi- nayo ni kupinga uwazi- hapo dalili ya kurudi ushahidi ni kipaumbile, kwa kauli sahihi, na dlili ya makubaliano”, kama ilivyonukuliwa na Mtaalamu Sheikh Muhammad Bakhiit Al-Muti’iy, na kigezo cha kurudi ushahidi kuwa ni dhana ya kosa au uongo bila ya tofauti kati ya mmoja au wengi, na katika hali ya kuyapinga mahesabu ya yakini ushahidi utakuwa vile vile dhana ya uongo na kosa, kwa hiyo ni bora utakataliwa.
Baadhi ya wanazuoni wa fiqhi waliandikia umuhimu wa kupatikana kipengele cha kuangalia Mwezi kwa shahidi, na wakajaalia hilo ni jambo muhimu, kwa kiwango ambacho wafuasi wa madhehebu ya Maliki, katika kauli yao, wanakubali ushahidi wa watu wawili waaminifu wakati wa usafi wa mbingu, kwa sharti la kuwa wao wawili wana ujuzi wa jambo la Mwezi, ingawa msingi wa jambo hili kwao kutokubali ushahidi isipokuwa kutoka kwa wengi; kwa sababu ujuzi wa jambo la Mwezi unakusanya kwa kawaida elimu ya mahesabu, na hii ni dalili inayoimarisha makubaliano.
Imamu Sahnuun anasema: “Ushahidi wa watu wawili waaminifu utakataliwa wakidai kuuona Mwezi hali ya usafi wa mbingu ndani ya nchi kubwa”. [Mwisho]. Na hivyo hivyo pia waliielekea wafuasi wa madhehebu ya Hanafi, kwa kutokuwepo kizuizi na kupatikana sababu za kuuona.
Kwa hiyo, mikutano ya kifiqhi, mfano wa mkutano wa Jeddah, ilikubali kufaidika na mahesabu ya yakini ya kianga, pamoja na kutegemea kuona sahihi kwa macho, na hii inamaanisha kuwa mahesabu yanakanusha na hayathibitishi, na inafikiriwa kuwa ni tuhuma kwa mwenye kuona anayedai kinyume chake.
Na hiyo hiyo iliyopendekezwa na Baraza la Tafiti za Kiislamu, Cairo katika mkutano wake wa tatu, uliofanyika kutoka kwa 30 Septemba hadi 27 Oktoba, Mwaka 1966 kuhusu kuainisha mwanzo wa Miezi ya kiislamu kuwa: “Kuuona Mwezi ni msingi kwa ajili ya kujua kuingia mwezi wa kiislamu, kwa mujibu wa Hadithi Sharifu, yaani kuona ni msingi, lakini hakutegemewi hali ya kuwepo wasiwasi nguvu juu yake. Na kuwa kuthibitisha kuuona Mwezi mwandamo ni kwa njia ya habari zenye uhakika zaidi na idadi ya watu wengi, na inaweza kuwa kwa habari ya mtu mmoja, mwanamume au mwanamke, isipokuwa inaambatana na habari yake tuhuma kwa sababu yo yoye iwayo, miongoni mwake kupinga mahesabu ya kianga yanayotolewa na mawaminifu”.
Kwa mujibu wa hayo: Mahesabu ya kianga yanatekelezwa nayo katika hali ya kukanusha na si katika hali ya kuthibitisha; yaani kuuona Mwezi kwa macho ndiko kunatambuliwa, isipokuwa katika hali ya kuyapinga mahesabu ya yakini ya kianga, na ingeliyapinga isingelitambuliwa, hapo ushahidi wa aliyeshuhudia kuona Mwezi mwandamo hautambuliwi kwa sababu ya kuyapinga mahesabu, kwa mbinu hii tunajumlisha kati ya msingi, nao ni kuuona mwezi kwa macho tunayoamriwa nayo kama msingi wa suala, na kati ya mahesabu ya yakini ya kianga yanayojuliwa kwa udhibiti katika wakati wetu.
Kuhusu suala linaloambatana na miandamo: wanazuoni walitofautiana juu ya kuizingatia au kutoizingatia, kwa upande wa matokeo ya kuuona Mwezi mwandamo katika nchi moja, ambapo saumu itakuwa wajibu juu ya watu hawa, au kufungua juu ya nchi nyingine ambayo Mwezi mwandamo haukuchomoza ndani yake, kama yatakayotajwa baadaye.
Wafuasi wa madhehebu ya Hanafi- kama alivyotaja Imamu An-Nasafi katika [Kanz Ad-Daqaiq: 1/321, Sharh Tabiin Al-Haqaaiq na Az-Zailai’iy, Ch. ya Dar Al-Kitaab Al-Islamiy; na Mtaalamu Iibn Abidiin katika: Tanbiih Al-Ghafil wal Wasnaan Ala Ahkaam Hilaal Ramadhan: Uk. 27-28, Ch. ya Maarif, Damascus]- kuwa: tofauti za miandamo haizingatiwi; yaani kama watu wa nchi moja wakiona Mwezi mwandamo, na watu wa nchi nyingine hawakuuona, basi saumu ni wajibu kwa wote kwa njia yo yote iwayo.
Wafuasi wa madhehebu ya Maliki walielekea kuwa: kuuona Mwezi mwandamo kwa upande wa jumla ya watu wengi wa nchi moja kunalazimisha nchi nyingine kwa uwazi, Saiydiy Khalil katika Mukhtasar wake anasema: “(Itaenezwa, kama ikipokelewa nao)”. [Mwisho], yaani: uwajibikaji wa saumu utaenezwa kwa nchi zote, zilizo karibu na zilizo mbali, kama kuuona Mwezi kukipokelewa na watu wawili waaminifu, kutoka kwa wawili waminifu, au idadi ya watu wengi kutoka kwa kwa idadi ya watu wengi, na kama Mwezi mwandamo ukionwa na kuthibitishwa mahali po pote, basi kuuona huku kutaenezwa nchi zote”. [Tazama: Sharh Mukhtasar Khalil na Al-Khirshiy: 2/236, Ch. ya Dar Al-Fikr; Hashiyat Ad-Disuuqiy: 1/510, Ch. ya Dar Ihiyaa Al-Kutub Al-Arabiyah].
Kwa wafuasi wa madhehebu ya Hanbal pia: haizingatiwi tofauti za miandamo. Mtaalamu Ibn Muflih katika [Al-Furu’: 3/12, Ch. ya Alam Al-Kutub] anasema: “(Kama watu wa nchi moja wakiona Mwezi mwandamo, basi saumu ni lazima kwa watu wote) na hakuna tofauti kati ya waliouona na wasiouona, na ikiwa miandamo ni mamoja, saumu inawalazimu, na kama iko tofauti basi rai sahihi ya madhehebu ni: saumu inawalazimu wote pia”. [Mwisho]., na hivyo hivyo katika [al-Insaf na al-Mirdawiy: 3/273, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy].
Na dalili yao ni: walivyopokea Imamu Bukhariy na Muslim- na tamko hili ni la Muslim- kutoka kwa Abi Hurairah R.A., kuwa Mtume S.A.W., alisema: “Fungeni kwa kuuona na fungueni kwa kuuona”, naye anazungumzia watu wote wa nchi zote, na hakuainisha watu wa nchi maalum peke yao, na kama kuuona kwa watu wa nchi moja kukizingatiwa katika kufunga na kufungua, vile vile kuuona kwa wengineo kunazingatiwa pia.
Mtaalamu Al-Bahutiy katika [Sharh Muntaha Al-Iraadaat: 1/471, Ch. ya Alam Al-Kutub] anasema: “(Ikithibitishwa kuuona) yaani Mwezi mwandamo wa Ramadhani (katika nchi moja, saumu inawalazimu watu wote) kwa Hadithi ya “fungeni kwa kuuona” nao ni uzungumzaji kwa umma wote”. [Mwisho].
Kuhusu wafuasi wa madhehebu ya Shafi walielekea kuwa: Kama Mwezi mwandamo ukionwa katika nchi moja na haukuonwa nchi nyingine, basi kama nchi hizi mbili zinakaribiana, zikawa kama nchi moja, na saumu inawalazimu watu wa nchi zote, lakini zikiwa mbali, basi saumu haiwalazimu watu wa nchi nyingine.
Sheikh wa Uislamu Zakaria Al-Ansariy katika [Al-Manhaj na Sharh yake; 2/308-309, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “(Kama ukionwa) yaani Mwezi mwandamo (katika mahali, hukumu yake inalazimu mahali karibu) napo (na huku) kuwepo (mwandamo ni mmoja) kinyume na mbali napo, na huku kuwepo tofauti za miandamo au kuna mashaka nao, kama alivyoeleza katika [Ar-Raudhah], kwa kuangalia asili yake na si kwa kuangalia masafa ya kupunguza Sala”. [Mwisho].
Ibn Al-Mundhir alinukulu kuwa: kuuona Mwezi mwandamo hakulazimu ila watu wa nchi ya kuuona, na hizi ni kauli za Ikrimah, Al-Qasim, Salim, na Is-haaq Ibn Rahawaih, kama ilivyotajwa katika [Al-Majmuu’ na Imamu An-Nawawiy; 6/282, Ch. ya Al-Muniriyah].
Na dalili yao ni: alivyopokea Muslim, kutoka kwa Kuraib Ibn Abi Muslim, naye ni huru wa Ibn Abbas R.A, kuwa: Ummul Fadhl Bint Al-Harith alimtuma kwa Mua’awiyah huko Sham, akisema: nilifikia Sham, nikatimiza haja yake, ikafika Ramadhani nami nipo Sham, nikaona Mwezi mwandamo usiku wa Ijumaa, kisha nilikuja Madinah mwishoni mwa mwezi huu, hapo Abdullhi Ibn Abbas R.A, aliniuliza kisha akataja Mwezi mwandamo, akisema: lini mliuona Mwezi mwandamo? Nikajibu; tuliuona usiku wa Ijumaa, akasema; wewe uliuona? Nikajibu: naam, na watu waliuona pia, wakafunga saumu, na Mua’awiyah akafunga saumu pia, akasema: lakini sisi tuliuona usiku wa Jumamosi, na tutaendelea saumu mpaka tumalize thelathini au tuuone, nikasema: huridhii kwa kuona kwa Muaawiyah na saumu yake? Akasema: la, na hivyo hivyo Mtume S.A.W., alituamuru.
Hadithi hii ni wazi ya kuwa: kila watu wanatekelezwa kwa kuona kwao.
Na mahali pa kupokea Hadithi hii ni Sham na Hijaz, na masafa kati yake ni masafa ya kupunguza Sala, tofauti ya jimbo, tofauti ya miandamo, na kutoweza kuona.
Kuhusu kutoweza kuona ni jambo mbali; kwa sababu Ibn Abbas R.A, alisema kwa Kuraib: wewe uliuuona? Na Kuraib akajibu: naam, na watu wliuuona pia, wakafunga saumu na Mua’awiyh akafunga saumu pia.
Na kuhusu masafa ya kupunguza Swala, na tofauti ya jimbo, ndivyo si kitu muhimu, kama alivyohakikisha Mtaalamu Imamu Muhammad Bakhiit Al-Muti’iy katika [Irshaad Ahl Al-Millah: Uk. 279, ch.ya Matbaat Kurdietan Al-Ilmiyah] kwa kauli yake: “Tukirudi uhalisia, tunaona kuwa hakuna uhusiano kati ya kuona Mwezi mwandamo baada ya machweo, na masafa ya kupunguza Sala wala tofauti ya jimbo, bali umuhimu hapa ni tofauti za miandamo, na muradi wa kuwa watu wanahitilafiana katika kuona haumaanishi kuwa: huyu anaona na yule haoni, bali muradi ni kuona Mwezi mwandamo baada ya machweo hakuzingatiwi kuona kwa mwengine; kwa sababu hakuna machweo wala Mwezi mwandamo katika nchi yake, kutokana na tofauti za miandamo, na hii ndiyo sababu inayotegemewa”. [Mwisho].
Kuhusu dalili ya wale wakwanza kuwa uzungumzaji unaambatana na kuona kwa uwazi katika Hadithi ya: “Fungeni kwa kuuona, na fungueni kwa kuuona”, ni dalili sahihi, lakini haihusu ila hawa walioleta kuona Mwezi baada ya machweo, ama wale wasiopata kuona baada ya machweo; hali ya kuwa wakati wa machweo kwao ni wakati wa kupambazuka kwa wengine, haiwajibika saumu kwao, kwa kutokuwepo sababu ya uwajibikaji, nao ni kuuona Mwezi mwandamo baada ya machweo. Na Hadithi hii si dalili ya kutozingatia miandamo.
Iliyopendekezwa na Baraza laTafiti za Kiislamu, Cairo katika mkutano wake wa tatu kutoka kwa 30 Septemba hadi 27 Oktoba, Mwaka 1966, kuhusu kuainisha mwanzo ya miezi ya Kiislamu kuwa: “tofauti za miandamo haizingatiwi, hata nchi zilikuwa mbali, hali zikishirikiana katika sehemu ya usiku wa kuuona Mwezi, hata ikiwa sehemu ndogo, lakini tofauti za miandamo inazingatiwa hali ya kuwa nchi hazishirikiani katika sehemu ya usiku huu”. [Mwisho].
Na hii imesisitizwa katika pendekezo lake nambari ya 42, katika kikao chake cha pili, baraza lake la kawaida ya ishirini na nane, liliofanyika tarehe ya 23 Mfunguo saba, Mwaka 1412 H., sawa na 31 Oktoba, Mwaka 1991, kuhusu kuuona Mwezi mwandamo, na matini yake ni: “ikiwepo tatizo la kuingia mwezi wa kiislamu, na kuthibitika kuona katika nchi nyingine ambayo inashirikiana na jimbo katika sehemu ya usiku, na wapigaji mahesabu ya kianga walisema kuwa: Mwezi itakaa muda wa dakika kumi au zaidi baada ya machweo, basi kuingia mwezi wa kiislamu ni upo”. [Mwisho].
Na kwa mujibu wa yaliyotangulia, na yaliyotajwa katika utafiti ulioashiriwa hapo juu, na kwa ajili ya kusahihisha baadhi ya makosa ya kielimu yaliyomo ndani yake, na kuyaeleza mambo yanayojiri hapa Jamhuri ya kiarabu ya Misri katika uwanja huu, twaweza kubainisha yafuatayo:

Kwanza: Baadhi ya dhana za msingi
(Mashariki na Magharibi): maneno ya umoja hapa yanaonesha kuelekea upande wa mashariki na upande wa magharibi. Na haipo mashariki moja wala magharibi moja tu kwa Mwenyezi Mungu.
Kwa hakika machweo wa Jua yanabadilika siku hadi nyingine karibu na robo ya digrii kwa kwenda upande wa kaskazini, kuanzia punde ya Ikwinoksi ya masika (kuingia kwa majira ya masika) karibu na siku ya 21 Machi, mpaka punde ya Solistasi ya kiangazi (kuingia kwa majira ya kiangazi) karibu na siku ya 22 Juni; na kwa kurudi upande wa kusini kuanzia Solistasi ya kiangazi (kuingia kwa majira ya kiangazi) , mpaka punde ya Ikwinoksi ya vuli (kuingia kwa majira ya vuli) karibu na siku 21 septemba, kisha punde ya Solistasi ya kipupwe (juingia kwa majira ya kipupwe) karibu na siku ya 22 Desemba, kisha kurudi tena kwa punde ya ikwinoksi ya masika.
Kwa hiyo, Jua lina mahali pa machweo 365, na mahali pa machweo 365, na halirudi kupambazuka tena kutoka kwa mahali penyewe isipokuwa katika mwaka ujao, na kwa hivyo, Jua halipambazuki kutoka kwa nukta yenyewe katika mwaka ujao, kwa sababu pambazuko linabadilika kutoka mwaka hadi mwingine kadiri ya mwendo wa ardhi katika muda wa masaa 5, na dakika 48, na sekunde 46, na kadiri hii ni ziada ya urefu wa mwaka kuliko siku 365. Kwa hiyo, mahali pa macheo na machweo hapana mwisho, na kwa hiyo pia, Mwenyezi Mungu hana mashariki moja wala magharibi moja, kwa kujibu kwa maswali ya Mayahudi kuwa: Je, Mwenyezi Mungu ana mashariki moja na magharibi moja?
Na upande wa mashariki na magharibi ndio unaoainisha pande za msingi, nzo ni msingi wa pande za mahali, ambazo kutokana nazo upande wa Qibla unaainishwa, na sharti la kuuainisha Qibla ni kuwepo masafa fupi sana kuliko zote, kwa sababu kuelekea Kaaba kunapelekea masafa mbili, moja yao ni fupi sana kufikia Kaaba, nayo ni kutegemewa, na nyingine masafa ndegu sana kufikia nayo.
Kwa mujibu wa hayo, kuna nukta iliyopo katika uso wa dunia, katika nusu ya kusini mwa dunia, katika upande unaokabili Kaaba, nayo mbali na Kaaba kwa masafa hiyo hiyo kutoka kwa pande zote, Iitwayo: Mfanano wa Qibla (Latitudo: 23 digree ya kusini; Longitudo: 131 digriiya magharibi), unapoelekea uso wako kutoka kwa nukta hii, basi wewe upo katika upande wa Qibla, kama ilivyotajwa katika Aya tukufu:
{Basi mahala popote mgeukiapo (alikokuamrisheni Mwenyezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu}. [AL BAQARAH: 115], na ndani ya nukta hii mwenye kuasli hahitaji kutafuta upande wa Qibla, bali anatawadha na kuswali, na upande wowote anapouelekea basi ni upande wa Qibla.
(Mashariki mbili na Magharibi mbili): kama ilivyotajwa katika Aya mbili za Suratuz- Zukhruf: 142, na Suratur Rahman: 17. Na vitu viwili hapa vinakubaliana na hakika ya kisayansi inayoashiria kuwa: kila nukta ya mwendo wa Jua wa mwaka ina mashariki mbili, ambapo jua linapambazuka mara mbili za kila nukta katika mwendo wake wa mwaka, kutoka kwa upande wa mashariki mpaka kaskazini ya mashariki. Kisha linarudi tena kutoka kwa kaskazini ya mashariki mpaka nukta ya mashariki, kisha mpaka kusini ya mashariki. Kisha linarudi tena mpaka nukta ya mashariki, n.k… kwa muda maalum kati ya kila mashariki mbili za nukta moja inayopata kati ya miezi 6 na siku moja au chini ya siku moja, juu ya miendo miwili ya kuchomoza na machweo.
(Mashariki zote na magharibi zote za dunia) kwa wingi unaokubaliana na hakika ya kianga ya kuwa: Jua linabadilisha mahali pake pa kuchomoza na machweo kadiri ya robo ya digrii kila siku, kama ilivyotajwa katika kipengele cha Umoja cha hapo juu.
(Mabadiliko ya usiku na mchana), kama ilivotajwa katika Aya mbili za Suratul Baqarah: 164, na Surat Yunus: 5; ambapo huenda kumaanisha ufuatano wa usiku na mchana, au mabadiliko ya usiku na mchana katika sifa zake, kutokana na urefu, ufupi, au usawa.
Na inajulikana kuwa mabadiliko na tofauti haipiti kwa njia ile ile katika urefu wa mwaka, au katika kila mwaka, isipokuwa katika hali ya kubadilika ardhi mahali pake wakati wa kulizunguka Jua (inaenda), na kubadilisha umbali wake na Jua ( yaani mzunguko wake ni wa yai na mahali pa Jua ni katika moja ya sehemu zake mbili), na kubadilisha haraka ya mwendo wake kulizunguka Jua, ambapo haraka yake ni kubwa kwenye ukaribu, na polepole kwenye umbali (mabadiliko ya eneo linalofunikwa kwa Jua wakati hadi wakati), hata ardhi ingezunguka kwa Jua na haitengi eneo lake.
Na mabadiliko ya urefu wa usiku na mchana inaonesha kuwa umbo la ardhi haulingani kikamilifu, ambapo picha zilizopigwa kwa anga zimethibitisha kuwa ardhi si mviringo kamili wala umbo la mpiR.A., kwa sababu ya haraka yake ya kujizunguka (kadiri yake 20 km kwa sekunde), na tofauti ya athari ya kani pewa katika mkanda wa ikweta na eneo la ncha mbili, na hii ndiyo husababisha (utambarare) ambao unajaalia kipenyo cha ikweta kikubwa kadiri ya 43 km kuliko kipenyo cha ncha. Na urefu wa majira za mwaka hayabadiliki kutoka kwa mahali hadi nyingine, na kaskazini hadi kusini, isipokuwa jira lake limemili na kiwango cha mzunguko wake.
Na hizi ni Aya ambazo Mwenyezi Mungu hakuzungumzia nazo isipokuwa watu wenye akili.
(Kuziumba mbingu na ardhi): kama ilivyotajwa katika Aya mbili, Surat Ali Imran: 190-191. Kuumba mbingu na ardhi ni muujiza ambao ni upeo wa miujiza yote, na tukichunguza mbingu na ardhi, hasa kwa kutumia darubini kubwa kabisa na za kiangani ambazo zinaizunguka ardhi, tutaona sayari, Miezi, makundi ya nyota, magalaksia, na maumbo yanayogunduliwa sasa hivi kama vile: matundu meusi, mifanano ya nyota (Quasars), nyota zinzotoa mwanga wa vipindi, nyota za neutroni, na nyota zinazomeremeta sana (Blazars); na hivi inavyovielezea Aya tukufu:
{Kwa yakini umbo la mbingu na ardhi ni kubwa kuliko umbo la wanaadamu. (Basi mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi ndiyo kutamshinda kuwafufua akawapa umbo jingine na uhai mwengine Binaadamu?) Lakini watu wengi hawajui (ila wanajisemea tu}. [AL MUMINUN: 57], na hawajui ishara za ulimwengu huu wa ajabu, na kuzitafakari juu yake ila watu wenye akili.
(Mwanga na nuru): kama ipo katika kauli yake Mtukufu: {Yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye aliyelifanya jua kuwa muanga, na mwezi kuwa nuru, na akaupimia vituo (huu mwezi) ili mjue idadi ya miaka na hisabu (nyinginezo)}. [YUNUS: 5], na mwanga hautolewi ila kwa nyota yenye joto, na hii ni sifa ya Jua, na nuru haitolewi ila kwa sayari yenye baridi, kwa njia ya kuakisi n.k., na hii ni sifa ya Mwezi. Na Mola aliupimia vituo huu mwezi, navyo ni mahala pa nyota ambapo mwezi ulitua ndani yake kila usiku,.
Na Waarabu kabla ya Uislamu walikuwa wakifikiri kuwa Mwezi unatua kama mgeni kwa nyota ya usiku huu. Kwa hiyo, kundi la nyota la usiku huu huitwa (kituo). Na idadi ya vituo hivi ni 28; na vinajulikana na majina yake ya wakati huu, nayo ni:
1- Ash-Sharatan (au An-Nat-h).
2- Al-Butain.
3- Ath-Thutaya.
4- Ad-Dabaran.
5- Al-Haqa’h.
6- Al-Hana’h.
7- Adh-Dhiaa’ (au Dhiraa’), (auAd-Dhhiraa’ Al-Maqbudah), (au Adh-Dhiaa’ Al-Mabsytah).
8- An-Nathrah.
9- At-Tarf.
10- Al-Jabhah.
11- Az-Zubrah (au Al-Khartan).
12- As-Sarfah.
13- Al-A’waa.
14- As-Simak (au As-Simak Al-Aa’zal).
15- Al-Ghafr.
16- Az-Zubalah.
17- Al-Iklil.
18- Al-Qab.
19- Ash-Shawlah (au Al-Ibrah), (au Ibrat Al-A’qrab).
20- An-Naa’aim, ni makundi mawili, kila kundi ni nyota 4; nayo ni Al-Qaws, na Al-Wasl, zinazogawanya kati ya makundi haya mawili.
21- Al-Baldah: ni eneo tupo katika nyota, ni kati ya vituo vya 20, 22.
22- Saad Adh-Dhabiih (au Saad Dhabih).
23- Saad Balaa’.
24- Saad As-Suu’ud.
25- Saad Al-Akhbiyah.
26- Al-Fara’ Al-Muqadam (au Al-Fara’ Al-Awal.
27- Al-Fara’ Al-Muakhar (au Al-Fara’ Ath-Thaniy.
28- Batn Al-Huut (au Ar-Rasha).
Baada ya vituo hivi, kuna kituo cha Ufifiaji wa nuru ya Mwezi, na wakati wake ni jioni la siku ya ishirini na tisa, nao ni wakati wa kuchunguza Mwezi mwandamo wa mwezi mpya, au wakati wake ni jioni la siku ya thelathini, ambapo mwezi wa kiarabu hauzidi kuliko hivi.
(Tofauti kati ya kuzaliwa Mwezi mwandamo na kuuona Mwezi mwandamo): Kuzaliwa kwa Mwezi mwandamo ni punde ambayo Mwezi unapita mstari wa makutano; nao ni msatari unaounganisha kati ya kitovo cha ardhi na jua, na punde hii inaambatana na kitovu cha ardhi kama kanuni ya kidunia. Na inatofautiana kidogo kwa wakazi wa uso wa ardhi, bila ya athari kubwa kati ya wale walio karibu au walio mbali na punde hii.
Na punde hii ipo kati ya nusu ya usiku wa ishirini na tisa na asubuhi ya siku ya thelathini ya mwezi wa kiarabu. Na punde hii haionwi wala kuchunguzwi kwa chombo cho chote, isipokuwa wakati wa kupatwa Jua, kwenye upeo wa kupatwa (kitovu cha kupatwa), wakati tunapoona kivuli cha Mwezi sawa na mduara wa Jua, au ipo juu ya mstari wa makutano.
Na mstari huu hauzingatiwi kama kipimo cha kuona Mwezi, wala hautegemewi katika hukumu ya kuingia mwezi mpya, kwa njia ya kianga au kisharia.
Na kuhusu kuuona Mwezi mwandamo ni punde ambayo nuru ya Mwezi unaweza kuonwa kutoka kwa uso wa ardhi, baada ya kuwa mbali na mstari wa makutano kadiri ya digrii 8. Na punde hii ikitokea baada ya machweo wa Jua, na hali ya hewa ni safi, na Mwezi utakaa muda haupunguzi dakika 10, hapo inawezekana kuuona Mwezi mwandamo . Na kuona huku kunategemewa katika hukumu ya kuingia mwezi mpya, na hakutegemewi na miadi ya kuzaliwa Mwezi mwandamo, kama yatatajwa baadaye.
(Kushirikiana katika sehemu ya usiku): katika mikutano mengi na vikao, ibara hii imesemwa, na kwa kweli ni yenye udanganyifu, kwa sababu nchi zote za ulimwengu zinashirikiana kati yao katika sehemu ya usiku; kwa mfano: Japani inashirikiana na India na China katika sehemu ya usiku, na China inashirikiana na Irani katika sehemu ya usiku, na Irani inashirikiana na Saudia, , Misri, Libya, Tunis, Algeria, Moroco, na lingananisha nchi zote zinazoshirikiana na hizi zilizotajwa, ambazo zipo katika Longitudo, kaskazini na kusini.
(Kupatwa Jua na Mwezi): kupatwa Jua kunatokea katika muda unaogawanya kati ya mwezi uliopita na mwezi mpya, katika Kiingereza (Solar eclipse); na kupatwa Mwezi kunatokea wakati mwezi ukawa kamili, katika nusu ya mwezi wa Kiarabu, katika Kiingereza (Lunar eclipse).

Pili: Hadithi zinazohusu kuona Mwezi:
Hadithi Tukufu inasema: “Fungeni kwa kuuona na fungueni kwa kuuona, na kama ukifunikwa”.
Mabaki ya Hadithi yamepokelewa kwa ibara mbali mbali, kama ifuatavyo: “kamilisheni idadi ya thelathini”, “Kamilisheni idadi ya Shabani thelathini”, Kamilisheni thelathini”, “mpaka mkiuona Mwezi mwandamo au mkamilishe idadi”, “basi fungeni saumu thelathini”, “Hesabuni idadi ya Shaabani kwa Ramadhani”, “Kamilisheni hesabu thelathini”’, “kamilisheni idadi thelathini, na hii haifunikwi kwenu”, “Hesabuni thelathini”, “kamilisheni idadi”, ‘kamilisheni idadi ya Shabani siku thelathini”, “fungeni saumu siku thelathini”, “Hesabuni siku thelathini”, “ukadirieni kwake thelathini”, “ukadirieni’.
Katika makundi mengine ya Hadithi tunaona:
Hadithi ya Abu hurairah R.A., alisema: Mtume S.A.W, alisema: “Mkiuona Mwezi mwandamo fungeni, na mkiuona fungueni, na kama ukifunikwa na mawingu, fungeni siku thelathini’. [wameipokea Imamu Bukariy na Muslim].
Na katika tamko lingine kutoka kwake pia: “Mwezi ni ishirini na tisa au thelathini, na kama mkiuona fungeni, na mkiuona fungueni, na kama ukifunikwa kamilisheni idadi”.
Na Hadithi ya Ibn Omar R.A., kuwa Mtume S.A.W, alisema: “kama mkiuona fungeni, na mkiuona fungueni, na kama ukifunikwa kwenu ukadirieni”. Ameipokea Imamu Bukhariy, na tamko la Muslim kuwa “Mtume S.A.W., aliutaja Ramadhani, akapiga mikono yake miwili, akasema: mwezi ni haya na haya, kisha alikunja kidole chake cha gumba mara ya tatu: fungeni kwa kuuona, na fungueni kwa kuuona, na kama ukifunikwa kwenu, kadirieni thelathini’, na katika tamko lingine: “ukadirieni”.
Na Hadithi ya Ibn Abbas R.A, kuwa: “Mtume S.A.W, aliutaja Ramadhani akisema: msifunge mpaka mnauona Mwezi mwandamo, na msifungue mpaka mnauona, na kama ukifunikwa kwenu, kamilisheni idadi thelathini”, na katika tamko la Abu Dawud: “msitangulie mwezi kwa kufunga siku moja au siku mbili, na msifunge mpaka mnauona, kisha fungeni mpaka mnauona…”. [mpaka mwisho wa Hadithi].
Na kutoka kwa Ibn Omar R.A, kuwa Mtume S.A.W, alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu aliijaalia Miezi miandamo kama nyakati, na kama mkiuona fungeni, na mkiuona fungueni, na kama ukifunikwa kwenu ukadirieni… kamilisheni thelathini”. Wameipokea Al-Hakim katika Al-Mustadrak, na Al-Baihaqiy kwa Isnadi Sahihi.
Na Hadithi ya Aisha R.A., alisema: “Mtume S.A.W., alikuwa akijihadhari katika Shaabani kuliko mwingine, kisha akafunga kwa kuuona Mwezi wa Ramadhani, na kama ukifunikwa kwake anazihesabu siku thelathini kisha akafunga”. Ameipokea Abu Dawud.
Na kama ilivyotangulia kutajwa baadhi ya matini za wanazuoni, kama vile: Mutarrif na Ibn Qutaibah, zinazonesha kuwa maana ya kauli yake S.A.W,: “ukadirieni” yaani: ainisheni mahala pake kupitia vituo vyake, na kadirini ukamilifu wa mwezi kwa mahesabu yake.
Pia ilivyotangulia, kutoka kwa Imamu Abul-Abbas Ibn Suraij kuwa: kuna aina mbili za uzungumzaji katika Hadithi, basi kauli yake S.A.W., : “kamilisheni idadi” ni kuzungumzia watu ambao hawakuona Mwezi kwa jumla, na hawajui kupimia vituo na mahesabu ya kianga; na kauli yake S.A.W,: “ukadirieni”, ni kuzungumzia wajuzi, miongoni mwao, wa elimu ya anga, kwa ajili ya kuwahimiza wahesabu mahali pake.
Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu alimuongoza Mtume wake S.A.W, katika maneno yake yanayohusu hivyo haja ya waislamu kwa kurefusha suala hili, na ilivyo ndani yake ya matata, majadiliano, na mabadiliko yanayosababishwa kwa tabia ya mwendo wa Mwezi ya kuizunguka ardhi, na tofauti za miandamo yake kwa nchi hadi nyingine, na mabadiliko ya haraka yake kwa nukta hadi nyingine katika mzunguko wake, na migogoro ambayo Mwezi unayoyakabili katika wakati wa mwendo wake katika mzunguko, na mabadiliko ya mahali pa vizingo vinavokwenda juu na chini angani… na vigezo mbali mbali vinavyodhibiti mwendo wa Mwezi.
Vile vile, Qur`ani Tukufu kwa mujibu wa alivyowekea Mwenyezi Mungu ndani yake ya ijazi ya kutamka, balagha ya maana, na sauti ya muziki, vyote vinapelekea kuelezea suala hili kwa njia ya muhtasari, bila ya upambanuzi, na kwa jumla bila ya kurefusha, na maneno yanayokamilisha maana yalikuwa yanalingana na viwango vyote vya mawazo inavyopitia akili ya binadamu, na maendeleo yake ya mawazo na ustaarabu, tangu kuteremshwa Qur`ani mpaka Siku ya Qiyama.
Tatu: Kuuona Mwezi: Misingi yake na fuatano zake:
Kwa njia ya kurahisishia watu, Mwenyezi Mungu aliyajaalia matokeo ya kawaida ya kianga ishara zinazongozwa nazo katika nyakati za Swala, kufunga, kufungua, na kuingia miezi ya kiislamu ya kisharia.
Kuna njia mbili Kwa kujua kuingia mwezi wa kiislamu:
Njia ya kwanza: Njia ya kuona, ambapo Mwezi mwandamo unaonwa katika upeo wa magharibi, baada ya machweo ya Jua la siku ya ishirini na tisa ya mwezi uliopita, na karibu na mahali pa machweo yake, na hali hii ni mfano wa alama za kuingia nyakati a sala, zinazoambatana na mwendo dhahiri wa Jua kuizunguka ardhi. Alama ya kuingia wakati wa Adhuhuri kuwa: Jua linamili kidogo kwa mstari wa Jua utosini:
{Simamisha Sala jua linapoopinduka (likenda magharibi) mpaka giza la usiku; na (msiache) Qurani ya (sala ya) alfajiri. Hakika (kusoma) Qurani katika (kusali Sala ya) alfajiri kunahudhuriwa (na Malaika). [AL ISRAA: 78], na wakati wa Alasiri: ikiwa kivuli cha kitu cho chote ni mfano wake, na Magharibi: kwenye kufichwa ncha ya juu ya Jua chini ya ncha ya upeo, na Isha: kwenye mwisho wa ukungu mwekundu wa jioni, na Alfajiri: mwanzoni mwa nuru ya kweli ya asubuhi.
Njia ya pili: njia ya mahesabu: katika hali ya ugumu wa kuuona Mwezi, baada ya macweo ya jua la siku ya ishirini na tisa, kwa sababu ya kizuizi cha hewa kama vile; mawingi, ukungu, moshi, nuru kali ya hewa, na Mwezi mwandamo kuwa karibu na nukta ya machweo ya Jua.
Na njia hii ina mbinu mbili: ima mahesabu ya idadi kwa kukamilisha mwezi siku thelathini, katika hali ya kufunikwa; au mahesabu ya vituo vya Mwezi. Na kama mahesabu yakionyesha kuwa kuwepo kwa Mwezi mwandamo juu ya upeo , baada ya machweo ya Jua, pamoja na kizuizi cha mabadiliko ya hewa na mengineyo, basi saumu inalazimika; kutokana na kuwepo sababu yake, nayo ni kujua kuwa Mwezi mwandamo ulichomoza juu ya upeo.
Lakini mahesabu yakionesha, pamoja na kuwepo mawingu, kuwa kutowepo Mwezi mwandamo juu ya upeo, baada ya machweo ya Jua, kwa sababu Mwezi mwandamo ulitangilia Jua katika machweo, basi mwezi itakamilishwa thelathini, na hivi haijuzu saumu ya siku ya mawingu, mwishoni mwa Shaabani, kama haijuzu kufungua kwake mwishoni mwa Ramadhani; kwa ajili ya kuwepo dhana yenye nguvu kuwa kutowepo Mwezi mwandamo nyuma ya mawingu.
Na hii anayoisema Imamu Abul Fat-h Muhammad Ibn Ali Al-Qushairiy Al-Manfalutiy Al-Malikiy Shafiy ajulikaye Ibn Daqiiq Al-I’id, naye amefikia ngazi ya jitihada, na akazaliwa katika Sahil Yanbu’, Hijaz, mwaka wa 625 H., na akafariki Kairo, mwaka wa 702 H., ambapo anasema katika [sharh Al-Umdah; 2/8]: “Na kama mahesabu yakionesha kuwa Mwezi mwandamo ulichomoza katika upeo pamoja na kuweza kuonwa- kama siyo kuwepo kizuizi kama vile mawingu- basi ni wajibu kutokana na dalili ya kisheria, na katika hali hii kuona kwa macho si sharti; kama kwamba mtu aliyefungwa shimoni akijua kukamilika kwa mwezi, au kwa kufanya jitihada kutokana na alama kuwa leo ni mwanzo wa Ramadhani, basi analazimika afunge saumu, bila ya yeye kuuona Mwezi mwandamo wala kuambiwa na mtu aliyeuona”. [Mwisho].
Wanazuoni wana ithibati nyingi ktika kuimarisha madhehebu hii, na hakuna cho chote katika Hadithi Tukufu kinachojibu wanaosema: Inajuzu kufunga saumu kwa kutegemea mahesabu; kwa sababu mahesabu hayakubadilika mwezi kuwa siku ishirini na tisa, na thelathini, kama alivyoitoa fatwa Sheikh As-Subkiy katika Fatwa zake.
Na kama sisi katika wakati huu tunategemea nyakati za sala zilizotayarishwa kipaumbile, na tukatumia saa za mikono na za ukuta bila ya kutazama kwa mahali pa Jua moja kwa moja mbinguni, na bila ya kuangalia matokeo ya kianga ambayo yanaashiria mwanzo wa nyakati za Swala, kisha tukatangaza adhana, kadhalika twaweza kujua kuwa Mwezi mwandamo upo au haupo kupitia mahesabu ya yakini, ambayo wanayafanya wapigaji wa mahesabu waaminifu.
Nne: Misingi ya mahesabu ya kuuona Mwezi mwandamo:
1- Kutokana na mwendo wa ardhi wa kujizunguka mara moja kila saa 24 kutoka kwa magharibi mpaka mashariki, hakika Jua na Mwezi zinachomoza kutoka kwa upande wa mashariki na zikazama katika upande wa magharibi.
2- Mzunguko wa Mwezi kwa ardhi unamili kuliko mzunguko wa ardhi kwa Jua kadiri ya digrii 5 na dakika nane ya katikati, kupata digrii 5 na dakika 20, na digrii 4 na dakika 48; na matokeo ya hivi ni:
- Si sharti kuwa kupatwa Mwezi hutokea mwanzoni mwa kila mwezi wa kiarabu, na vile vile kutokea kupatwa Jua kwenye nusu ya kila mwezi wa kiarabu.
- Mizunguko ya Jua na Mwezi inakaribiana katika uso wa mbingu kutoka kwa nukta ya macheo hadi nukta ya machweo, ambapo zinazokaribiana na zinazo mbali isiyozidi kupata digrii 5 au 6 kwa kiasi kikubwa sana.
3- Tukizingatia mwendo wa ardhi kulizunguka Jua, na kiasi chake ni kidogo kuliko digrii moja kila siku (59.14 dakika za kitao) tutaona kuwa Mwezi unakwenda kuelekea mashariki karibu digrii ya kitao 13 kila siku, yaani digrii moja kila saa mbili takriban, kwa hiyo Mwezi ni katika shindano la mbio na Jua siku zote, ukalifikiana kulivuka mara moja kila mwezi, na mara kumi na mbili kila mwaka, yaani idadi ya miezi ya mwaka.
4- Haraka ya mwendo wa Mwezi kuzunguka kwa ardhi (1 km\S takriban) kwa hiyo unamaliza mzunguko wake kwa ardhi katika siku 27, saa 7, dakika 43, na sekundu 11.6, katika hali ya kuwa ardhi ni thabiti katika mahali pake na Jua, lakini ardhi na Mwezi zinakwenda kuzunguka kwa Jua, basi Mwezi haurudi tena mahali pake palipoanza mwendo isipokuwa baada ya siku 29, saa 12, dakika 44, na sekundu 2.9 ya kaikati, na hii ianjulikana kwa mwezi wa makutano, kwa kiingereza: Synodic Month.
5- Tunapima mwezi wa kiarabu kwa idadi ya siku, kuanzia machweo wa Jua mpaka siku ifuatayo; kwa hiyo mwezi ima siku 29, au 30, na mwezi kuwa 30,
Kwa sababu ya wakati unaozidi na siku 29, saa 12, dakika 44, na sekundu 2.9 ya kila mwezi, pamoja na mabadiliko mengine yanayoambatana na mwendo usio mpangilio kwa mzunguko wake, kati ya Perigi na Apogi, (kwa Kiingereza; Perigee & Apogee).
6- Kutokana na yote yaliyotangulia, machweo ya Mwezi inachelewa kwa machweo ya Jua kutoka kwa dakika 40 mpaka 50 kuliko siku iliyopita, kutokana na mistari ya Longitudo na duara za Latitudo.
7- Katika siku ya ishirini na tisa ya mwezi wa kiarabu: machweo wa mwezi huenda yanatokea kabla ya machweo wa jua, basi Mwezi hauonekani, na huenda kutokea baada ya machweo wa Jua, basi inaweza kuonekana; pengine inasemwa kuwa; kukaa kwa mwezi ni hasi, na pengine ni chanya, kutokana na hali maalum, zinazotajwa baadaye. (muda wa kukaa ni mkubwa katika nchi zilizopo katika upande wa magharibi, kama vile: Libya, Tunis, Algeria, Morocco, n.k.)
8- Kwa kutumia milinganyo ya machweo ya sayari, inafanyika mahesabu ya wakati wa machweo ya Jua na mwezi katika siku ya ishirini na tisa ya kila mwezi wa kiarabu, na hii ni ile ile ya milingano ya nyakati za Swala ya Magharibi; na sisi tunatangaza Adhana kwa kuzitegemea nyakati zinazoandikwa katika kalenda kipaumbile, na bila ya kuona moja kwa moja ncha ya juu ya Jua inapoficha chini ya upeo wa mahali tunapoutangaza Adhana ndani yake; au Swala ya Adhuhuri, wakati wa Jua linapovuka mstari wa katikati ya mchana ya mahali, au duara ya kufikirika inayounga kati ya nukta za kaskazini na kusini, kupitia kipeo cha anga.
Tano: Hali za kuuona Mwezi kutokana na mahesabu ya kianga:
Kutokana na mahesabu ya kianga tunaona kuwa hali za kuona Mwezi wa mwezi wa kiarabu ni tano: Nne miongoni mwake haziathiriwi kwa tofauti za miandamo, na ya tano inaathiriwa nayo.
- Hali ya kwanza ni: Mwezi unazama kabla ya machweo wa Jua, yaani kukaa kwake ni hasi, katika nchi zote za Kiarabu na Kiislamu, kwa hiyo kuona Mwezi hakuwezekani, na hukumu yake ni kukamilishwa idadi ya mwezi siku thelathini, na hapo ushahidi wa shahidi yeyote utakataliwa, hata ikiwa utashuhudiwa kwa Taqwa na uchamungu; kwa sababu yeye hujidai kuona kifikira.
- Hali ya pili: Mwezi unazama baada ya machweo wa Jua , yaani kukaa kwake ni halisi, katika nchi zote za Kiarabi na Kiislamu, na kuona kwake itawezekana kwa mujibu wa muda wa kukaa kwake katika kila nchi, na hukumu ya hali hii ni kuwa: Siku ijayo ni mwanzo wa mwezi mpya, na ushahidi wa shahidi ye yote mwaminifu, mwanamume au mwanamke itatekelezwa, katika nchi yoyote ya kiislamu.
- Hali ya tatu: Kuzaliwa kwa Mwezi au makutano yake ni baada ya machweo wa Jua, na hii inamaanisha kuwa mzunguko wa kianga kwa mwezi wa kiarabu haujaanza, kwa hiyo Mwezi hauonekani, na kama ukionwa baada ya machweo na kabla ya makutano, hali ya kuchelewa makutano karibu nusu ya usiku- na hii ni hali adimu isiyo ya kawaida- basi uatazamaji huu ni wa Mwezi wa mwisho wa mwezi, ambao huonekana na ncha zake mbili ziko chini kuelekea upande wa magharibi, na utazamaji huu hautegemewi, na matokeo ya hayo kuwa: siku ijayo ni mwisho wa mwezi, kama anavyosema Ibn Taimiyah na Ibn Al-Qaiym; “Hakuna utazamaji kabla ya makutano”, na hapo ushahidi wa mashahidi utakataliwa, hata wakiuona Mwezi mwandamo, na hukumu ya hali hii ni kukamilisha mwezi siku thelathini.
- Hali ya nne: Jua linazama hali ya kupatwa, na hii inamaanisha kuwa hali ya makutano inafanyika wakati wa machweo, kwa hiyo haiwezekani kuona mwezi, kwa sababu muwale wa Jua ni wima katika uso wa ardhi, na karudi tena kwa uso wa Jua katika sura ya kivuli juu ya uso wa Jua, na hauakisi upande wa ardhi, hapo haiwezekani kuonwa athari yo yote ya Mwezi mwandamo, na matokeo ya hayo kuwa: siku ijayo ni mwisho wa mwezi, kama alivyotaja Sheikh Muhammad Rashid Rida kuwa: “Jua likizama siku ya ishirni na tisa ya Shaabani kwenye kupatwa, kisha shahidi mwenye uaminifu na utawa akishuhudia kuwa ameona Mwezi mwandamo, basi tutarudi ushahidi wake, kwa sababu alijidai kuona Mwezi kifikira”.
- Hali ya tano: Ni hali inayosababisha tatizo na mchafuko, hasa katika mwezi wa Saumu na Haji, nayo ni hali si thabiti, na kuuona kwa Mwezi mwandamo hubadilika kwa tofauti za miandamo, na kadiri yake kama 24% ya jumla ya miezi ya mwaka, yaani kutokea kwake mwanzoni mwa Ramadhani kadiri yake ni 2% tu kutoka kwa hali za kuona Mwezi, yaani hutokea katika Ramadhani kadiri ya mara mbili mwanzoni mwake, na mara mbili mwishoni mwake, hivi kila miaka minane.
Katika hali hii, tofauti za miandamo ina umuhimu sana. Na hii ni hakika ya kielimu kutokana na tabia ya mzunguko wa Mwezi kwa ardhi, na lazima itekelezwe kwenye kutoa hukumu yoyote, na kugawanywa kwa hali tatu kuu;
1- Mwezi unazama baada ya machweo wa Jua katika nchi nyingi za Kiarabu na Kiislamu, na unazama katika baadhi ya nchi kabla ya machweo wa Jua . Na katika hali hii kila nchi ina mahali pake pa kuchomoza, ambapo huainisha mwanzoni mwa mwezi au sio, na hii inajuzu kisheria. Na dalili ya hayo walivyoipokea Imamu Muslim katika kitabu chake, Imamu At-Tirmidhiy katika kitabu chake, na Imamu Ahmad katika Musnad yake, kutoka kwa Kuraib, huru wa Ibn Abbas R.A., ambayo imetajwa hapo juu.
2- Mwezi unazama kabla ya machweo wa Jua katika nchi nyingi za Kiarabu na Kiislamu, na huzama katika baadhi yake baada ya machweo wa Jua.
3- Mwezi huzama kabla ya machweo wa Jua katika nusu ya nchi hizi takriban, na huzama baada ya machweo ya jua katika nusu yake nyingine, na katika hali mbili zilizotangulia- pili na tatu- huenda kanuni ya tofauti za miandamo itekelezwe kama katika hali ya kwanza, au haitekelezwi, kutokana na maamuzi ya wenye madaraka juu ya jambo hili.
Sita: Shahidi mwaminifu:
Inapasa kupatikana masharti ya kisheria na kifalaki juu ya shahidi mwaminifu, ambayo yangalizingatiwa na kutekelezwa kwa nchi zote za Kiislamu, mwanzo ya miezi ya kiarabu uangelikuwa moja katika nchi zote za Kiislamu, kwa kiasi kisichopungua 80%. Na tatizo hili ni jiwe la pembe la suala la umoja wa mwanzo wa miezi ya kiarabu katika nchi za Kiislamu, kwa kuwa hakuna mapigano kati ya utazamaji sahihi ambao huletwa na shahidi mwaminifu na mahesabu sahihi yanayoletwa siku hizi kwa teknolojia ya kisasa, na vyombo vikubwa vya hesabati, ambapo matokeo yake ni karibu ya mia kwa mia, kutokana na ujuzi kamili wa tabia ya mizunguko ya Ardhi na Mwezi. Kwa hiyo lazima kuwepo masharti manne juu ya shahidi mwaminifu:
1- Awe na mwili mzima na akili nzuri.
2- Awe na macho yenye uzima, na ukali wa macho si sharti kama vile kengeza, ili hukumu ikusanye watu wote.
3- Awe na Taqwa na uchamungu.
4- Awe na elimu ya mahali, zamani, na sura ya mwezi wakati wa kuuona.
Na wenye madaraka, wanaotoa maamuzi ya Saumu na Futari wanatakiwa kuwatahini wenye uwezo wa kimwili, kinafsi, na kielimu kwa shahidi, kutokana na matokeo ya mahesabu ya kianga juu ya hali za kuuona Mwezi, na hali ya Mwezi mwandamo wakati wa kuuona.
Na shahidi mwaminifu kama huyu akiwepo katika nchi zote za kiislamu, basi matokeo ya mahesabu ya kianga hayatabadilika kwa utazamaji wa macho utakaofanyika na mashahidi waaminifu, isipokuwa hali za tofauti za miandamo zilizoamuliwa na Mtume S.A.W, kama ilivyopokelewa katika Hadithi ya Ibn Abbas R.A.,
Saba: Mahali na zama za kuangalia Mwezi:
Hali zinazolazimika kupatikana katika kuangalia Mwezi mwandamo wa mwanzo wa miezi ya Kiarabu zinaambatana na vigezo vifuatavyo:
1- Mahali na zamani za kuangalia Mwezi mwandamo na sura yake katika uso wa anga:
Kwa mtazamo wa kiwango cha mzunguko wa Mwezi kinamili kuliko kiwango cha mzunguko wa Ardhi kwa Jua kupata digrii tano na dakika nane ya katikati, kwa hiyo nukta ya kuzama mwezi ipo kwa kushoto kwa nukta ya machweo wa Jua, au kwa kulia kwake kupata 5 ya digrii za kitao- kipenyo cha mduara wa Jua na Mwezi kinafunika nusu ya digrii ya kitao katika uso wa anga takriban- na haya yanajulikana kwa tofauti kati ya vipeo viwili vya Mwezi na Jua katika wakati wa machweo. Kuhusu kupanda kwa Mwezi kuliko upeo, hakika kunategemea kadiri ya kukaa kwake, na kila Mwezi ulipokaa basi pembe ya kupanda juu ilizidi kuliko upeo.
Na kuhusu wakati wa kuangalia Mwezi mwandamo: ni punde ya machweo mpaka mwisho wa muda wa kukaa, na unaangaliwa kuzunguka eneo la machweo ya jua ipatayo digrii tano kulia kwake, na digrii 5 kushoto (ambapo duara ya Jua hufunika nusu ya digrii).
- Na mahali panapofaa kwa kuangalia Mwezi mwandamo ni mahali pa juu ya uso wa bahari ambapo upeo wake ni upande wa magharibi na upo wazi, na mbali na majengo, minaR.A., majengo yanayokwenda juu sana, na viwanda vinavyotoa moshi. Na mahali palipo mbali na miangaza ya miji, mbali na barabaR.A., ambapo miangaza mikali ya magari haiakisi katika upeo wake wa magharibi.
- Mwezi wa mwanzo wa mwezi kwenye kuuangalia ncha zake mbili zinaelekea juu upande wa mashariki, lakini ncha zake zilikuwa chini upande wa magharibi, basi ni Mwezi wa mwisho wa mwezi, na utazamaji wake hautegemewi, na hali hii ni adimu na kutokea, wakati makutano yanapotokea baada ya machweo kwa muda mrefu usiopungua masaa saba.
2- Umri wa Mwezi na uhusiano wake na sehemu yenye nuru ya uso wake:
Umri wa Mwezi si kigezo cha kukaa kwake, na huenda umri wake ni mkubwa na kukaa kwake ni kudogo, au bila ya kukaa, au kukaa kwake ni hasi, na maana ya umri wa Mwezi katika kitambo maalum ni wakati unaopita tangu kuzaliwa kwake mpaka kitambo maalum, punde hii kwa kawaida ni machweo ya Jua la siku ya utazamaji, au machweo ya Jua la siku ijayo, ikiwa kuzaa kwake baada ya machweo ya jua la siku ya ishirini na tisa ya mwezi wa Kiarabu.
- Sehemu yenye nuru ya uso wa Mwezi inayorahisisha kuonwa kutoka kwa ardhi, baada ya umbali wake na mstari wa makutano ni: 0.01, ikiwa Mwezi ni mbali na ardhi kadiri ya masafa ya katikati ya ardhi na mwezi, nayo ni: 384400 km., na kadiri hii itapungua kutokana na masafa inapungua, na itazidi kutokana na masafa itazidi, na hayo yote yategemea kuwepo hali ya hewa ya kufaa.

- Umri wa Mwezi, ukizidi ukipungua, si kigezo cha kukaa kwake, na kitu kinachodhibiti kuuona ni kuinama kiwango cha mzunguko wake kuliko kiwango cha mzunguko wa Ardhi, pamoja na hitilafu ya kung’aa kwa maeneo ya uso wa Mwezi ambamo muale wa Jua unaakisi kutoka kwake (kwa Kiingereza; Albedo).

3- Hali za kupatwa na maelezo yake:
Hali za kupatwa ni dalili nguvu za mwisho wa mwezi wa Kiarabu kianga, au kwa kweli alama yake ni kitovu cha kupatwa, ikiwa kupatwa ni kamili, sehemu, duaR.A., au mchanganyiko. Na kama kupatwa kunapotokea siku ya ishirini na tisa, basi hii ni dalili thabiti kuwa haiwezekeni kuuona Mwezi, na hukumu yake ni kukamilisha mwezi siku thelathini.
Siku hizi elimu imefikia ngazi ya juu katika (Nadharia ya Mizunguko; Theory of Orbits) ambapo hupelekea kujua nyakati za kupatwa Jua na Mwezi iwe na kiwango cha juu cha udhibiti kifikacho sehemu moja ya elfu ya sekunde moja.
Kwa hiyo wanazuoni wahakiki miongoni mwa wanazuoni wa fiqhi wa kisasa wanaona uthabiti wa mahesabu ya kianga na umuhimu wa kuutekeleza katika siku hizi; ktokana na urahisi wa kuifanya, udhibiti wa matokeo, na kuisajili katika diski zinazohifadhi idadi kubwa ya taarifa katika kipimo kidogo.
Na vyombo vya hesabati kama hivi havikupatika zamani, pamoja na juhudi za waislamu katika mahali mbali mbali pa kaskazini na kusini kwa dunia ambapo haiwezekani kuleta utazamaji, na alama za kianga za Mwezi na nyakati za Swala haziptikani; kama vile urefu wa usiku, ufupisho wa mchana, au kinyume ya hivi, au kuendelea macheo ya Jua au machweo yake muda wa miezi sita.
Nane: Njia ya Idara ya kutoa Fatwa ya Misri kuhusu kuthibitisha kuingia mwezi wa Kiarabu:
Idara ya kutoa Fatwa ta Misri inashughulika kupitia imani yake kwa umuhimu wa kuifuata sunna Tukufu katika Hadithi ya Mtume S.A.W,: “Fungeni kwa kuuona…” kujenga komiti mbalimbali zinazoshughlikia kuangalia Mwezi katika mahali kumi ndani ya Jamhuri ya kiarabu ya Misri: Hilwan, Kattamiya, Oktoba 6, As-salum, Qina, Aswan, Al-Wahat, Toshka, Marsa Alam, Sant katrin.
Na kila komiti inakusanya; mhusika wa falaki katika Taasisi ya taifa ya tafiti za kifalaki, mhusika wa elimu ya kisharia ya Idara ya kutoa Fatwa, au miongoni mwa Maimamu wa misikiti ambao wajuzi wa mahali pa kuangalia mwezi, mwanachama wa Idara ya upimaji wa ardhi.
Pengine wanashirikana na kamati hizi baadhi ya wanazuoni wa anga katika Idara ya Anga, kitivo cha Sayansi, Chuo kikuu cha Cairo na Alazhar, ili kuleta vipengee vinne vya shahidi mwaminifu, ambaye anaongozwa kwa mahesabu ya kianga, ambazo zikwa thabiti katika enzi yetu ya teknolojia ya kisasa.
Kuhusu utazamaji kwa macho ukawa dhania sasa hivi; kwa mtazamo wa hali ya hewa chafu ambayo ikawa sifa kuu ya mbingu za nchi mbali mbali za dunia; hasa maeneo ya upeo wa magharibi, na upeo mwenye mawingu, pamoja na matendo mabaya ya kutumia vyombo vya starehe ambavyo husababisha kuvunja Tabaka la Ozoni linaloumbwa na Mwenyezi Mungu ili kulinda binadamu na viumbe vyote kwa hatari ya muale wa Ultraviolet unaotolewa na Jua.
Kwa hivi tulikuwa tukifuata Sunna Tukufu kwa mtindo na utaratibu wa kisasa kimaendeleo, ambao husaidia kutumia vyombo hivi vya teknolojia, ili kuleta kutekeleza sababu za kisayansi kwa Waislamu, kwa ajili ya kusimamisha Hukumu sahihi za kisharia.
Tisa: Satalaiti ya Kiarabu na kiislamu Inayopendekezwa kwa ajili ya kuchunguza Mwezi mwandamo wa mwanzo wa miezi ya kalenda ya kiislamu:
Ni mradi ulikwenda hatua kubwa ya hatua za kuujenga, ambapo machunguzi ya kweli yamefanyika kwake, na imekwisha kubaliwa mambo mengi yanayouhusu. Sasa hivi mchango wa fedha unafanyika mpaka kupatikana ugharamiaji unaotakiwa kwa ajili ya kurusha aina mbali mbali za satalaiti hizi.
Satalaiti inachunguza Mwezi mwandamo kwa njia ya darubini iliyopo katika mgongo wake, na katika siku ya ishirini na tisa ya mwezi wa Kiarabu, darubini inaelekezwa kwa upeo wa kuona, ambao ni lazima kulingana na upeo wa mwenye kuona kutoka kwa uso wa ardhi, mbali na mawingu na vizuizi mbali mbali vya hewa, Na hali ya kuwepo Mwezi mwandamo juu ya upeo, sura yake ipelekwe kwa monita za TV za kawaida, na hapo watazamaji wote wanauona kwa macho yao.
Satalaiti hii inakwenda duara yake kuzunguka kwa ardhi katika muda wa karibu ya saa na nusu, na sehemu ya muda huu ikiwemo ndani ya upeo wa nchi nyingi za kiarabu na kiislamu, baada ya machweo wa Jua, na hii inaleta fursa ya kuuona Mwezi mwandamo mwenyewe katika monita za TV zake.
Kuna sababu mbili zinazoahirisha kuutekeleza mradi huu:
Kwanza: Ni ya kielimu; nayo ni kutotatua tatizo la tofauti za miandamo.
Pili: Ni ya ndani; ambapo baadhi ya wanaojidai utungaji wa sharia wanashikamana na kutotumia mbinu za teknolojia ya kisasa, na wakatia maanani ya kuuona moja kwa moja kwa macho, na hii ni ufa katika ukuta wa kuunganisha maneno ya Waislamu.
Tumuomba Mwenyezi Mungu ajumuishe maneno ya Waislamu na kuunganisha jumuiya yao katika haki.
Kumi: Kalenda ya Jua na ya Mwezi:
Kalenda ya Mwezi inakuwa ikiainishwa sana na kudhibiti; kwa sababu inatumia mifumo ya kianga dhahiri mbele ya watu wote. Na siku inaanza na machweo ya jua, na mwaka unaanza na machweo ya siku nyingine ya Mfunguo Tatu, na katikati ya urefu wa mwezi ndani yake ni: siku 29, saa 12, dakika 44, na sekunde 2.9; na idadi ya miezi ya mwaka wa kalenda ya Mwezi ni: miezi kumi na mbili, kama alivyosema Mwenyezi Mungu:
{Idadi ya mezi (ya mwaka mmoja) mbele ya Mwenyezi Mungu ni mezi kumi na mbili katika ilimu ya Mwenyezi Mungu (Mwenyewe tangu) siku alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo imo minne iliyo mitukufu kabisa nayo ni Rajabu, Mfunguo Pili, Mfunguo Tatu, na Mfunguo Nne)}. [AT TAWBAH: 36].
Na Aya hii Tukufu ndiyo inatekelezwa katika kalenda zote za dunia, kwenye mila na dini zote. Na kalenda hizi zote zinathibiti kuwa urefu wa mwaka ni miezi kumi na mbili.
Kuhusu urefu wa mwaka wa kalenda ya kiislamu ni: siku 354.3670556, sawa na: siku 354, saa 8, dakika 48, na sekunde 33.6. Na kiti kinachoainisha mwanzo wa mwaka huu ni uwazi wa mwanzo na mwisho wake, nao ni punde ya kwanza ya machweo ya Jua ya siku ya mwisho wa ya Mfunguo Tatu. Na kuhusu mwaka wa kalenda ya Jua ndio mwanzo wake usiainishwa kila mwaka, ambapo urefu wake ni siku: 365.24189814, sawa na: siku 365, saa 5, dakika 48, na sekunde 45.2. Na urefu wa mwaka wa kalenda ya Jua ni mrefu kuliko mwaka wa kalenda ya kiislamu muda wa; siku 10, saa 20, dakika 59, na sekunde 46.4.
Na kwa kuwa mwanzo wa kweli wa mwaka wa kalenda ya Jua ambao unaainishwa kwa kumalizika kwa duara moja kuzunguka kwa Jua, kwa sababu mwaka wa kalenda ya Jua unaanza mwanzo mbali mbali kila mara; kwa dharura ya kuingizana miaka yenywe kwa yenyewe, ili iwe miaka mifupi, Februari wake ni siku 28, na miaka mirefu, Februari wake ni 29.
Na ingawa kuwepo kuingizana lakini kipande kilichokatwa hakiongezwi, kwa sababu kipande hiki ni chini kuliko robo, kwa hiyo tunapasa kuongeza kipande hiki kwa kuifanya miaka ya karne ambayo haiwezi kuigawanywa kwa 400 ndiyo miaka mifupi, na ile inayoweza kuigawanywa kwa 400 ndiyo miaka mirefu. Na hata hivyo kipande hiki si kamili, na inapasa kukibadilisha baada ya miaka elfu tatu.
Kumi na moja: Vigezo sanifu vya kujenga vituo vya uangalizi vya kianga:
Vituo vya uangalizi vya kianga ni taasisi za serikali ambazo zilijengwa kwa dola kwa mujibu wa maamuzi rasmi, na zinakusanya kati ya kuta zake vyombo, vifaa vya kianga vikuukuu au vya kisasa vya maendeleo, miongoni mwake ni; darubini ambazo zinatumia katika kazi za uangalizi mbali mbali, zikiwemo uangalizi wa Mwezi, sayari zingine za kianga. Wafanya kazi wa vyombo hivi ni wanaanga wanaopata digrii ya kwanza ya B.A, ya elimu ya anga, na wakafanya kazi ya kutayarisha tafiti za kianga, kwa ajili ya kupata digrii ya uzamili ya elimu ya anga, na hii inawapelekea wawe wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Elimu ya Anga, ambayo ni shirika la kwanza la elimu ya Anga kati ya mashirika haya duniani.
Na Mashirika ya kianga ya kiarabu ambayo yana sifa hizi ni machache sana, na miongoni mwake:
- Taasisi ya taifa ya tafiti za kianga na Fizikia ya Dunia, Jamhuri ya Misri ya Kiarabu, ambayo imejengwa Mwaka 1903, nayo ina viti vitatu katika Jumuiya ya kimataifa ya Elimu ya Anga, sawa na Ufaransa, na kila kiti kinakubali kushirikiana na wanachama23 ndani yake, na idadi ya Wamisri waliojiandikisha ndani yake 65, na wanachama wote ni wanaanga waliomaliza masomo katika Idara za Elimu ya Anga, Vyuo vikuu vua Cairo na Alazhar, na wengi wanapata digrii ya Profesa.

- Taasisi ya elimu ya Anga na Fizika ya Dunia, Mji wa Mfalme Abdulaziz, ya Sayansi na Teknolojia, Ufalme wa Saudi wa Kiarabu, ndani yake ni wanaanga , wanachamama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Elimu ya Anga, waliomaliza masomo katika Idara za Elimu ya Anga, Vyuo vikuu vya Mfalme Saud, Riadh, na Mfalme Abdulaziz, Jeddah.

- Kuna vituo vingine vingi vya kianga katika ulimwengu wa Kiarabu na kiislamu, kama vile: Libya, Aljeria, Morocco, Kuwait, Jordan, Syria, Iraq, Lebanon, Yemen, Imarat. Na nchi za Kiislamu zisizo za Kiarabu ambazo zina vituo vya uangalizi mbali mbali na vinavyoendelea: Indonesia, na Malysia.
Na hii ni tone la bahari la kuwepo hapa Misri, ambayo wanazuoni wa anga na wa sharia wanaijua sana, kuhusu maudhui hii ya uhai na muhimu, ambayo inashughulika na maisha ya waislamu katika upande muhimu sana kwa ibada zao, mahusiano yao wenyewe kwa wenyewe, pamoja na wengineo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

 

Share this:

Related Fatwas