Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa Jina Mo...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa Jina Moja.

Question

Ni nini maana ya Dhikiri (Kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu) Na Je, inajuzu tumtaje Mwenyezi Mungu kwa jina moja tu kati ya majina yake? Kwa mfano kama tukisema: Allahu Allahu au Arahman Arahman?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Utajo kilugha maana yake ni kukitaja kitu, anakitaja kutaja, alisema Bin Faris: nimekikumbuka kitu, kinyume na kukisahau, kisha ikabebwa maana ya kutaja kwa ulimi, na wanasema: ijaalie kutoka kwako kutaja, kwa maana ya usimsahau. [Mojam Maqayiis Al-Lughah 358/2, Kidahizo cha Dh-K-R, Ch. Dar Al-Fikr]
Mtunzaji wa kitabu cha: [Mukhtaar Al-Swhah 112/1,Ch. Al-Maktabah Al-Aswriyah] akasema: “Utajo (dhikiri) na kukumbuka na ukumbusho: ni kinyume cha kusahau. Na maana ya dhikiri ni kusifu na kutukuza, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na Qur`ani yenye utajo} yaani yenye Utukufu”.
Na katika lugha, neno utajo huja kwa maana mbili: ya kwanza: Ni kitu kinachopita katika ulimi, kwa maana ya kinachotamkwa. Inasemekana: nimekitaja kitu, ninakitaja utajo: unapotamka jina lake au ukakizungumzia. Na miongoni mwake ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Huu ni Ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwamja wake, Zakariya} [MARIAMU 2] Na maana ya pili: Ni kulileta jambo moyoni bila ya kulipitisha katika ulimi, kinyume cha kusahau. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika kisa cha kijana wa Musa A.S. {Na hapana aliye nisahaulisha nisimkumbuke ila Shet'ani tu} [AL-KAHF 63}.
Ar-Ragheb alisema katika kitabu cha: [Al-Mufradat 328/1, Ch. Dar Al-Qalam] “Utajo katika baadhi ya nyakati hukusudiwa hali ya nafsi ambayo kwayo mtu huweza kulinda kile anachokipata katika maarifa, nayo ni kama kuhifadhi isipokuwa kwamba kulinda husemwa kwa kuzingatia kufanyika kwake, na utajo husemwa kwa kuzingatia kuuleta kwake, na mara nyingine husemwa kwa kuhudhurisha jambo moyoni au kwa kusema. Na kwa hivyo: utajo uko wa aina mbili: utajo kwa njia ya moyo, na utajo kwa njia ya ulimi, na kila moja kati ya aina hizi mbili za utajo zina namna mbili: utajo kutokana na kusahau, na utajo usiotokana na kusahau, bali kuendelea kuhifadhi. Na kila kauli isemwayo ni utajo (dhikiri)”
Kwa upande wa Istilahi: utajo hutumika kwa maana ya mja kumtaja Mola wake Mtukufu aliyetukuka zaidi, iwe kwa kuelezea dhati yake yenyewe, au kwa sifa zake, vitendo vyake, hukumu zake, usomaji wa kitabu chake, au kwa maswala yake na dua zake, au kwa kuanzisha utajo wa sifa njema za utakatifu wake na kumtukuza pamoja na kumpwekesha na kumsifu kwa sifa njema na kumshukuru na kumtukuza yeye.
Na dhikri katika istilahi hutumika kwa maana maalumu kuliko lilivyo neno hili; na ikawa kwa maana ya kuanzisha utajo wa sifa njema kama ilivyotangulia bila ya maana zingine zilizotajwa. Na kinachoashiria matumizi ya maana hii ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Swala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa.} [AL-ANKABUUT 45]
Na kauli ya Mtume S.A.W, katika aliyoyapokea kutoka Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Mtu yeyote atakayeshughulishwa na Qur`ani pamoja na kunitaja mimi kuliko kuniomba nitampa kilicho bora zaidi katika ninavyowapa wanaoomba”, imetolewa na At-Twabaraniy katika Dua. Na Aya ikaifanya dhikiri kuwa sio swala kwa tafsiri kwamba Mwenyezi Mungu amezuia kumtaja yeye katika mambo machafu na yanayochukiza na kukatazwa zaidi kuliko kuzuia kufanya hivyo katika swala, na Hadithi imeufanya utajo kuwa sio katika usomaji wa Qur`ani, na wala sio kuomba ambako ni Dua.
Na utajo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa aina zote za matamshi ni dawa ya magonjwa ya moyo na matatizo ya nafsi, na matamshi ya nyiradi ni mengi na ya aina mbali mbali miongoni mwake yamekuja kutoka kwa Mtume S.A.W. na miongoni mwake yamekuja kutoka kwa Maswahaba, wafuasi, wanazuoni na wajuzi zaidi, na kila moja lina athari maalumu moyoni na utendaji mzuri katika nafsi maalum. Na miongoni mwa utajo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni: kumtaja kwa jina moja miongoni mwa majina yake; kama vile tukisema: Allahu Allahu, au Latwifu Latwifu, na kadhalika utajo wake kwa tamko lenye kiwakilishi (yeye), na utajo kwa kauli hizo inajuzu na siyo Bidaa.
Ama kwa upande wa utajo wa Mwenyezi Mungu kwa tamko moja lenye kiwakilishi jina: wanazuoni wanaligawa jina kwa aina ya lisilo maalumu na lililo maalumu linalojulikana, na wanaligawa maalumu linalojulikana kwa migawanyiko vya aina saba, kikiwemo kiwakilishi jina, na wanazuoni wa sarufi ya lugha; wanasema kuwa: kiwakilishi jina kinatambulisha zaidi, majina maalumu yote yamejengeka kwa uainisho na umaalumu, na kiwakilishi jina kina nguvu zaidi ya kuainisha nacho ni maalumu na kinatambulika zaidi ya jina maalumu.
Kwa hiyo majina Maalumu hayako katika kiwango kimoja, miongoni mwake yamo yanayohamishika, na miongoni mwake yamo mazito, na yamo yaliyo maalumu ya maumbile, ama kwa upande wa kiwakilishi jina kuna ngazi moja tu inayoziba majina kama ni utatuzi wa kifupi.
Wanazuoni wa lugha wanakiona kiwakilishi jina kuwa kinatambulisha zaidi kuliko jina maalumu, wanakusudia kwayo majina maalumu ambayo yanatolewa kwa viumbe, na katika hayo, jina la Mwenyezi Mungu haliingii; kwani lenyewe linatambulika zaidi na zaidi. Na jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu "Allah" ni moja na maalumu, limewekwa kwa lengo la kuonesha mwambatano wa wajibu wa uwepo wa Mwenyezi Mungu, na lina sifika kwa sifa zinazolitakasa na kila aina ya maana mbaya, Mwenyezi Mungu ambaye hana mshirika katika viumbe vyake, na jina ambalo ni maalumu ni lile lililowekwa kwa kitu maalumu, kwa hivyo mwenye kutaja anaikusudia maana hii kwa jina maalumu moja.
Na kiwakilishi jina si chochote isipokuwa ishara inayomuainisha mtu anayeashiriwa, kwa sharti pasiwazike katika akili ya mwenye kudhikiri kitu kingine isipokuwa hicho hicho kilichoashiriwa, na atakayemtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutumia (yeye) kwa maana kiwakilishi jina lake hakika mambo yalivyo, anamkusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu (Allah), na huku akijua kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwangalia na anajua yaliyomo ndani ya nafsi ya mja wake.
Kwa upande wa kulitaja kwa tamko moja la dhahiri jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu (Allah) au Mwenye rehema kubwa kubwa (Arrahmaan), hakika yake ni neno linaloitwa ambalo neno lake la kuitia limeondoshwa. Na neno linaloitwa ni katika migawanyiko ya maneno yenye maana kamili kwani wao wamelitafsiri neno la kuitia kwa maana ya "ninakuomba" na kuondosha neno la kuitia kunajuzu na kunajulikana katika lugha ya Kiarabu. Kwamba neno linalotumika katika kuitia wito huletwa kwa ajili ya kutanabahisha, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye kuepukana na utanabahisho, na maneno mengi yatumikayo katika kuitia yamewekwa kwa ajili ya kumwitia aliye mbali, kama neno (yaa) ambalo ni mama wa mlango, yaani neno kuu la kuanzia, na aliyetukuka mwenye utukufu yuko karibu na mja anayemwita, na kwa ajili hii, neno la kuitia likaondoshwa.
Na imethibitika kwamba Bilal R.A. alipoadhibiwa na makafiri alikuwa akisema: Mmoja Mmoja (Ahadun Ahad), na haikutajwa kutoka Mtume S.A.W., kwamba akampinga au akamkana kwa dhikiri hiyo. Imesimuliwa na Ibn Majah kutoka kwa Ibn Masuod R.A., Na Al-Busweriy akasema katika kitabu cha: [Al-Muswbah 23/1, Ch. Dar Al-Arabiya]; “Isnadi hiyo watu wake ni wenye kusadikika”
Na katika anayoanza nayo ni yale aliyoyataja Muhyi Ed-Diin Bin Al-Arabiy, alisema: niliingia kwa Sheikh wetu Abi Abbas Al-Ariiniy ambaye ni katika wanazuoni wakubwa huku akiwa na shauku kubwa ya kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu (Allah) bila ya kuzidisha chochote, nikamwambia: ewe bwana wetu, kwanini husemi laa ilaaha illa llahu? (hakuna Mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu)? Akaniambia: ewe mwanangu: pumzi ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wala haziko mikononi mwangu, na kwa hivyo ninachelea Mwenyezi Mungu Mtukufu asije akaichukua roho yangu wakati ninasema hakuna Mungu (laa ilaaha) nikawa nimetolewa roho katika hali mbaya kama hiyo ya kukanusha. Na nilimuuliza Sheikh mwingine kuhusu jambo hili akaniambia: jicho langu halijawahi kumwona wala sikio langu halijawahi kumsikia mtu anayesema: Mimi ni Mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, anasema: sikumkuta wa kumkanusha nikasema kama nilivyomsikia: (Allah, Allah). [Rejea: Risalat Al-Qaulu Al-Mua’tamad Fii Mashru’yat Az-zekr Bi Al-Esm Al-Mufrad kwa Ahmad Mustafa Al-Alawiy Uk. 63, Ch. Al-Mtwuba’h Al-Alawiyah].
Na asiyekubali kuwa kudhikiri kwa jina moja la Allah kunasihi anaweza kuleta pingamizi kama vile: kulitaja jina Moja la Mwenyezi Mungu Mtukufu (Allah) kwa kuweka kiwakilishi jina hakujapokekewa katika Sunna kutoka kwa Mtume S.A.W. na wema wote waliotangulia R.A. Na jibu ni: Kwamba wanazuoni wanakubaliana kuwa kuacha si njia ya kutoa dalili kwa peke yake, na kwa hivyo njia yao ikawa ni Matini au Ijmaa (Makubaliano ya wanazuoni) au Kiasi (Kipimo cha Kisheria) na wakatofautiana katika mapito mengine ili kuthibitisha hukumu ya Kisheria siyo miongoni mwao kuacha, na kuacha hakufai hukumu ya kisheria kwa peke yake na hili liko katika makubaliano ya waislamu. Na kuna vithibitisho vingi na Hadithi nyingi kwamba Maswahaba R.A. wote, hawakufahamu kuwa kuacha kwake Mtume S.A.W ni kwa ajili ya uharamu au kuchukiza kwake; na hivyo ndivyo walivyofahamu wanazuoni katika zama mbalimbali zilizopita.
Na Ibn Hazm amejibu juu ya hoja ya wanazuoni wa Kimaliki na wa Kihanafi juu ya ukaraha wa kuswali rakaa mbili kabla ya Swala ya Magharibi, kwa sababu kwamba Abu Bakar na Omar na Othman walikuwa hawakuiswali, ambapo alisema: “Na hili si chochote; kwanza kabisa ni kwa kuwa limekatika kwani Ibrahim hakumuwahi yeyote miongoni mwao tuliokwisha wataja, na hakuzaliwa isipokuwa baada ya mauaji ya Othman kwa miaka miwili, kisha kama hili lingekuwa sahihi basi pasingelikuwepo hoja yoyote ndani yake; kwani ndani yake hakuna katazo lolote la kwamba wao. R.A, walizikataza au kuonesha kuwa zinachukiza, na sisi hatuendi nao kinyume katika hali ya kwamba kuziacha swala zote za kujitolea (Za Sunna) kunakubalika. [Kitabu cha: Al-Mahaliy 22/2, Ch. Dar Al-Fikr] Ibn Hazim hakuzungumzia sana kuhusu kuiacha swala ya rakaa mbili, na akasema kwamba kuiacha kwao swala hiyo sio kitu chochote kwa kuwa wao hawajasema wazi wazi kuwa Swala hiyo inachukiza, na wala hawakunukuliwa kwa jambo hilo.
Na katika Hadithi ya Refaa Bin Rafe Az-Zarqiy alisema: “Siku moja tulikuwa tunaswali nyuma ya Mtume S.A.W na aliponyanyua kichwa chake kutoka katika rakaa alisema: Mwenyezi Mungu Mtukufu amemsikia anayemhimidi, mtu mmoja akasema nyuma yake: ewe Mola wetu hakika wewe unasifika kwa sifa njema nyingi na nzuri na zilizobarikiwa ndani yake, na alipomaliza swala akasema: ni nani aliyesema maneno yale? Yule mja akasema: ni mimi. Akasema Mtume S.A.W: nimewaona malaika thelathini na kitu wakiigombania kauli yako nani aliyeiandika mwanzo.” Imepokelewa na Ahmad Na Al-Bukhariy.
Ibn Hajar anasema baada ya utajo wake Hadithi hiyo: “Imetoa dalili juu ya kujuzu kuleta dhikiri katika Swala ambayo sio Sunna kama haipingani na ya Sunna.” [Fathu Al-Bariy 287/2, Ch. Dar Al-Maarifah]. Ametoa dalili kwayo juu ya kujuzu kuleta dhikiri katika swala ambayo sio Sunna kama haipingani na ya Sunna. Kama hali hii itakuwa katika kuanzisha utajo usio kuwa Sunna katika Swala, basi jambo hili nje ya Swala ni bora zaidi.
Kupinga kunaweza kuwa kwamba kulitaja jina la Allah peke yake hakuna maana ya utukuzo, na kwamba ni lazima kutimilizi sentensi inayoeleweka ikamilike mpaka ilete maana ya kutukuza. Na Jawabu: ni kwamba kulitaja jina "Allah" peke yake ndani yake kuna maana ya kutukuza na hivi ndivyo walivyojua wanachuoni, na hapa kuna huyu Imamu wa Maimamu Abu Hanifa R.A, anapitia uamuzi huu katika suala: je inakubalika katika kuanzia swala kwa kutaja tu jina moja la Mwenyezi Mungu Mtukufu (Allah)?
Basi mtunzi wa kitabu cha: [Al-Bada’e 131/1, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] akataja matini hii: “Na ama ikiwa mja atalitaja jina peke yake, akasema kwa mfano: Allah, kwa upande wa Muhammad mtu huyu haanzi katika Swala na Alhasan amepokea kutoka kwa Abi Hanifa kuwa mtu huyo atakuwa ameanza Swala, na vile vile Bishr amepokea kutoka kwa Abi Yusufu, kutoka kwa Abi Hanifa kwa Muhammad kwamba matini imepokelewa kwa jina na sifa na kwa hivyo haisihi kutosheka na jina peke tu, na kwa Abi Hanifa anaona kuwa matini inatumika kama sababu ya kutukuza, na hutokea kwa jina peke yake tukufu la Allah, na dalili ya kwamba mja anapolitumia jina hili huwa ameanza Swala kwa tamko lake: "Hakuna Mungu mwingine anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu" na kuingia katika Swala unatokea kwa kusema: Allah, na wala sio kwa kukanusha”.
Na kwa hivyo, Imamu Abu Hanifa anaona kuwa Jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu kama lilivyo (Allah) hutokeza kwalo utukuzo bila ya kutia sharti la kuwa kwake katika sentensi yenye maana. Kama ambavyo mtu anayelitaja jina hili pekee hazungumzi na kiumbe chochote kile na kwa hivyo haishurutishwi maneno anayoyasema kuwa lazima yawe na maana, kwani lengo lake ni kufanya ibada kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu ambalo ni "Allah" na wala lengo sio kumwambia mtu mwingine; kwani mtu huyu, yeye anamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye anaijua fika nafsi yake na anaangalia kilichomo ndani ya nafsi ya mja huyu.
Na wala hawazi kuwa kulikariri jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu Allah peke yake hakuna maana yoyote iliyopo ndani yake na wala hakufidishi maana yoyote inayoelekewa na nafsi kwa yule mwenye kujishughulisha na neno hili Tukufu kuliko yote Ulimwengu, na kwa hivyo katika jina hili kuna aina zote ya maana na ukamilifu na linanasibishwa jina hili na sifa za juu pamoja na kheri nyingi na baraka zake. Umbali ulioje wa kauli ya mwenye kudai kuwa kulikariri jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu "Allah" hakuleti maana yoyote, hakika mambo yalivyo kwa upande wa ukweli wake ni kiini hakihitajii kiarifu kiasili kulikamilisha ndani yake linajitosheleza vya kutosha na halihitaji kitu chochote na kwa ajili hii, jina hili lina siri nyingi na ajabu kubwa ambazo hazipatikani kwa lingine lolote. Na katika wema walikuepo wanaoanza njia yao ya uongofu kwa kukariri utajo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kulitamka neno "Allah" peke yake hadi nafsi isafike kwa kulitaja kwake neno hili na likapita katika moyo mapito ya damu katika mishipa, akawa mtu hatulizani wala hahisi utulivu isipokuwa kwa kuhisi kwake katika hali ya kuendelea kuwa yuko pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu na akauhisi uzuri na radhi zake Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Hoja ya Uislamu Abu Hamed Al-Ghazaliy akasema katika kitabu chake: [Ihyaa Uluum Ad-Diin 19/3, Ch. Dar Al-Maarifah]: “Kwa hiyo Mitume na Mawalii walifunukiwa na Jambo na Nuru ikatanda vifuani mwao, si kwa kujifunza na kusoma na kuandikia vitabu, bali kwa kuupa nyongo Ulimwengu, na kujiepusha na maambatano yake na kuusafisha moyo kutokana na vishughulishaji vya Ulimwengu na kuelekea katika kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani mtu anayekuwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu basi naye Mwenyezi Mungu Mtukufu huwa wake, na wakadai kuwa njia ya hili ni kwanza kabisa ni kwa kukata mahusiano na viambatano vyote vya dunia pamoja na kuvitoa moyoni na kwa kukata mawasiliano ya karibu na ndugu na jamaa, mali na watoto, nchi na elimu, madaraka na cheo, bali ni moyo ukawa katika hali ya kwamba uwepo kila kitu au kutokuwepo kwake kunalingana ndani yake. Kisha anaitenga nafsi yake katika kona pamoja na kujilazimishia Swala za Faradhi na Swala za Sunna na akaketi akiwa mtupu moyoni na mwenye mjumuiko wa majonzi wala hatofautishi mawazo yake kwa kusoma Qur’ani Tukufu wala kwa kuizingatia tafsiri yake wala kwa kusoma vitabu vya Hadithi au vinginevyo, bali anajitahidi kutofikiria moyoni mwake kitu chochote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, bado anaendelea baada ya kukaa kwake huko peke yake akimtaja Mola wake kwa ulimi wake akisema "Allah Allah" huku moyo wake ukiendelea kuwa hadhira mpaka atakapoimaliza hali hiyo akaacha kuutikisa ulimi wake na akawa anaona kama vile neno hilo linaendelea kutoka katika ulimi wake kisha akavumilia mpaka athari yake ikafutika katika ulimi wake ikakutana na moyo wake, na moyo ukaendelea kufanya hivyo. Kisha anaendeleza mpaka atakapofuta moyoni mwake picha ya tamko na herufi zake na umbile la neno na kubakia maana ya neno lenyewe moyoni mwake likiendelea kuwemo humo halitengani naye, naye ana hiari ya kufikia kikomo hicho, na kuchagua kudumu katika hali hii kwa msukumo wa ushawishi na wala hana hiari ya kuileta rehma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Bali kwa alichokifanya anakuwa ni mwenye kupingana na mazuri ya rehma za Mwenyezi Mungu Mtukufu hakibaki isipikuwa kungojea rehma atakazozifungua Mwenyezi Mungu Mtukufu kama alivyozifungua kwa Mitume na Mawalii wake kwa njia hii, na katika hali hiyo iwapo utashi wake utakuwa wa kweli, na ari yake ikawa safi na mwendelezo wake ukawa mzuri na matamanio yake yakawa hayakumvutia wala nafsi yake haikumshughulisha kwa kuyazungumza mambo ya dunia ukweli ukawa unang'aa ukiwa sehemu ya yanayong'aa moyoni mwake.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas