Kuvaa Kitambaa cha Kuziba Pua kwa ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuvaa Kitambaa cha Kuziba Pua kwa Mwenye Kuhirimia Hija

Question

 Je, ni ipi hukumu ya kuvaa kitambaa cha kuziba pua kwa mwenye kuhirimia Hija kwa ajili ya kujikinga na maradhi?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Mwenye kuhirimia ni yule aliyejiandaa kuitekeleza ibada ya Hija au Umra; na mwenye kuhirimia analazimika kuangalia makatazo ambayo ni lazima ayatekeleze, na miongoni mwake ni kuhusu mavazi: haijuzu kwa mwanamume kufunika mwili wake au baadhi yake au kiungo chake kwa mavazi yanayoshonwa wala yanayofunika mwili wote, na anafunika mwili wake kwa sehemu mbili: sehemu inayofunika nusu ya juu ya mwili, na nyingine inayofunika nusu ya chini ya mwili. Na mavazi yanayoshonwa ni yale yaliyopimwa kadiri ya mwili, kama vile; kanzu, suruali, na joho. [Taz.: Kashful Qinaa’: 2/407, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Dalili ya hayo, imepokelewa na Maimamu Bukhari na Muslim, kutoka kwa Adullahi Ibn umar R.A., kuwa: “Mtu alimuuliza Mtume S.A.W.: Ni mavazi gani anayoyavaa mwenye kuhirimia? Na Mtume S.A.W., akajibu: Msivae kanzu wala suruali wala kofia wala joho, na kama mtu asipokuwa na viatu basi achukue Khofu (viatu vya ngozi tu) na avikate chini ya vifundo, na msivae kitu chochote chenye manukato”.
Kuhusu kufunika uso inaharamshwa kwa rai ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafi na Malik, na atakayekiuka katazo hili atalazimika kutoa fidia. Sheikh Ad Dardiir anasema: “Inaharamishwa kwa mwanamume afunike uso wote au baadhi yake, na kichwa chake vile vile, kwa kitambaa chochote kama vile leso n.k., maana uso na kichwa ni kinyume na mwili, kwa hiyo inaharamishwa kufunikwa kwa kitambaa chochote kiwacho”. [Ash-Sharh Al-Kabiir Ala mukhtasar Khalil: 155, cH. ya Dar Al-Fikr]
Imamu Al-Mirghinaniy mfuasi wa madhehebu ya Hanafiy anasema: “Na hafuniki uso wake wala kichwa chake; kwa kauli yake Mtume SAW,: “Msifunike uso wake wala kichwa chake, kwa sababu atafufuliwa Siku ya Kiyama akitamka Labbaika”, akisema hivyo iwapo mwenye kuhirimia atakufa; na kwa sababu mwanamke hafuniki uso wake hali ya kuhirimia, basi kwa mwanamume analazimika hivyo kwa uwazi zaidi”. [Al-Hidayah: 2/142, Ch. ya Al-Amiriyah]
Kwa rai ya wafuasi wa madhehebu ya Shafi na Hanbali, inajuzu kufunika uso, na halazimiki mwenyekufanya hivyo kulipa fidia. Ash-Shiraziy katika Al-Muhadhab anasema: “haiharamishwi kwa mwenye kuhirimia kufunika uso, kwa kauli yake Mtume S.A.W., kwa aliyeanguka na ngamia: “Msifumnike kichwa chake”, hapa alikiainisha kichwa kwa katazo”. [Al-Muhadhab; 7/269, Ch. ya Dar Al-Fikr]
Imamu An-Nawawiy anasema: “Madhehebu yetu kuwa; inajuzu kwa mwanamume kufunika uso wake na halazimiki kutoa fidia, na hii ni rai ya wengi wa wanazuoni. Na Abu Hanifa na Malik wanasema: haijuzu mfano wa kichwa chake, dalili yao ni kauli yake Mtume S.A.W, kutoka kwa Ibn Abbas kuwa “Mtume S.A.W, alisema kwa aliyeanguka na ngamia wake: msimfunike uso wake wala kichwa chake”. [Ameipokea Muslim], na kutoka kwa Ibn Umar akisema; “inavyokuwa juu ya ndevu na kichwani, mwenye kuhirimia hafuniki”. [wameipokea Malik na Al-Baihaqiy], na hii ni sahihi kutoka kwake. Na wanazuoni wenzetu walitoa hoja ya mapokezi kutoka kwa Shafiy, kutoka kwa Sufiyan Ibn U’yainah, kutoka kwa Abdur-Rahman Ibn Al-Qasim, kutoka kwa baba yake kuwa: Uthman Ibn A’ffaan, Zaid Ibn Thabit, Marwan Ibn Al-Hakam, walikuwa wakifunika nyuso zao hali ya kuhirimia, na hii ni Isnadi Sahihi, na Al-Baihaqiy alipokea hiyo hiyo; lakini Al-qasim hakukutana na Uthman, na akakutana na Marwan, na walihitilafiana kuhusu uwezekano wa kukutana na zaid; na Malik na Al-Baihaqiy walipokea kwa Isnadi Sahihi, kutoka kwa Abdullahi Ibn Abi Bakr, kutoka kwa Abdullahi Ibn A’amir Ibn Rabia’ah akisema: Nilimwona Uthman mahali pa Al-A’arj, hali ya kuhirimia katika siku za kiangazi, akifunika uso wake kwa kitambaa laini chenye rangi ya zambarau.
Jibu kwa Hadithi ya Ibn Abbas kuwa: Hakika amekataza kufunika uso wake kwa ajili ya kujikinga kichwa chake, na si kwa ajili ya kufunua uso wake, kwa sababu wakifunika uso wake, huenda hawakuweza kufunika kichwa chake; hapa inapasa kuielewa zaidi: kwa sababu Malik na Abu Hanifa wanasema kuwa: uso wa maiti unaambatana na kichwa chake utakapofunikwa, na shafiy na waliomfuata wanasema: inajuzu kufunika uso bila ya kufunika kichwa, kwa hiyo inapasa kueleweka Hadithi zaidi, na kuhusu kauli ya Ibn Umar ndiyo inapingana na kitendo cha Uthman, Na mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa yote”. [Al-Majmuu’: 7/269, Ch. ya dar Al-Fikr].
Ar-Ruhaibaniy mfuasi wa madhehebu ya Hanbali anasema: “Mwenye kuhirimia mwanamume akifunika uso wake kwa kitu kisichoshonwa basi hana dhambi wala hatoi fidia kwake, kwa sababu hakuambatana na kasoro ya Sunna, ambapo uso ni kinyume na mwili kuhusu kufunika; au aliweka mkono wake juu ua kichwa; au kupaka uso kwa asali na sandarusi, n.k., kwa kujikinga na mavumbi na uchafu, basi hakuna kitu kwake, kwa Hadithi ya Ibn Umar: “Nilimwona Mtume S.A.W, akipaka uso hali ya kuhirimia”. [Matalib Ulin Nuhaa Fi Sharh Ghayt Al-Muntahaa: 2/327, Ch. ya Beirut]
Kwa hiyo haja ya wenye kuhirimia kwa vitambaa vya kuziba pua, vinavyowakinga na maradhi ya kuambukiza kwa njia ya pumzi na hewa ni dharura ya kiafya, na wengine hawawezi kuviacha, hivyo wanaweza kuifuata kauli inayojuzisha; kwa mtazamo wa haja ya matibabu, na kwa sababu kujikinga nafsi ni miongoni mwa makusudio ya Sharia.
Na kwa Mujibu wa hayo: inajuzu kwa mwenye kuhirimia kuvaa kitambaa cha kuziba pua cha matibabu, na halazimiki kutoa fidia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas