Anayoweza Kuyaangalia Mchumba wa K...

Egypt's Dar Al-Ifta

Anayoweza Kuyaangalia Mchumba wa Kiume kwa Mmchumba Wake wa Kike

Question

 Ni yapi yaliyo halali kuaangalia mchumba wa kiume kwa yule anayetaka kumwoa? Je, ni sharti kuangalia uzuri wake ambao unapelekea kuolewa kwa kujiiba bila mwenyewe kujua wala kuhisi? Au inafaa kuangalia baada ya kuomba na kuruhusiwa ili kuangalia yaliyo halali kisharia katika uzuri wake?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Uchumba: Kusudio lake ni ombi la kuoa. Na uchumba: Kwa maana ya haja, kisha ukahusishwa na ndoa, kwa sababu baadhi ya haja husemwa: ujumbe wako ni nini? Kwa maana ya haja yako ni nini? Katika mpasuko wake kuna aina mbili: Aina ya kwanza ina maana ya jambo na kitu, husemwa: Ujumbe wako ni nini? Kwa maana ya jambo lako ni lipi? Kusema kwao: Fulani amechumbia fulani, ina maana: Amemtaka jambo na kitu kwenye nafsi yake. Aina ya pili: Asili ya uchumba ni maneno. Na huwa inasemwa: Fulani amemchumbia mwanamke, kwa maana: Amemwambia jambo la ndoa. Uchumba: Ni jambo kubwa, kwa sababu linahitaji maelezo mengi. [Kitabu cha Al-Misbah Al-Muneer cha Al-Fayoumi, mada: Uchumba, chapa ya Al-Maktaba Al-Elmiya, na kitabu cha Alubab fi ulum Al-Kitab cha Siraj Al-Deen Al-Hambaly, 4/198, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya].
Ukubwa wa jambo la ndoa na utakatifu wa mfungamano wake ambao unawakutanisha mume na mke na kujenga familia zao, uhusiano wa nasaba na ukwe, kuna madhara makubwa uhusiano huu mtakatifu kuuharibu kwa vitendo vya udanganyifu na ulaghai, na kuficha yale yanayowezekana hapo baadaye kuleta mvutano kati ya pande mbili, kutokana na haya kumekuwa na haja kubwa ya uhalali wa uchumba na kuupa mtazamo kati ya mchumba wa kiume na wa kike ili kuhakikisha kuwepo hali inayoendana na kukubaliana kikamilifu kati ya wawili kabla ya kuingia katika makubaliano ya ndoa na yatakayofuata miongoni mwa ubadilishanaji wa majukumu haki na wajibu kati ya pande mbili. Sharia ya Kiislamu imekuja ikiwa ni yenye kukidhi haja zote hizi kwa ukamilifu, ikaruhusu kwa mwanamume aliyekuwa tayari kuoa kumwangalia mwanamke ili kuthibitisha kuendana sawa na yeye pasi na kutaka ruhusa kwake wala kwa wasimamizi wake kwa sharti la uhalali wa kuangaliwa na mchumba, inafaa kwake kumwangalia hata kama mwanamke hajui kama walivyosema wanachuoni [Sharh An-Nawawy kwa Muslim, 9/210, chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby], bali wamesema baadhi ya wanachuoni kama vile Al-Adhra’ii katika wafuasi wa Imam Shafi na wengineo kuwa lililo bora kwa mchumba wa kiume ni kumwangalia mchumba wake bila mwanamke kujua wala kumtaka ruhusa, ili kuepuka kutojua kasoro ya wazi iliyopo au kuonekana kwenye pambo zuri la kutengeneza kisha akapoteza lengo la kutaka kumwangalia, vile vile kuepukana na kero ikiwa atamtaka ruhusa ya kumwangalia kisha akapuuza. Wafuasi wa Imamu Hambal hawapo mbali na suala la mchumba kumwangalia mwanamke bila ya ruhusa yake, na wanaona kuwa kufanya hivyo ni bora [Kitabu cha Tuhfat Al-Muhtaj, 7/191, chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby. Kitabu Matalib Auli Anuha fi Sharh Ghayat Al-Muntaha, 5/12, chapa ya Al-Maktab Al-Islamy]
Asili ya mlango huu ni Hadithi ya Abi Huraira R.A. katika Hadithi iliyopokelewa na Imamu Muslim katika kitabu chake kutoka kwa Abi Huraira amesema: “Nilikuwa kwa Mtume S.A.W akaja mtu mmoja na kumwambia Mtume kuwa yeye ameoa mwanamke wa kiansar, basi Mtume S.A.W akamuuliza je ulimwangalia? Akasema: hapana, akasema Mtume S.A.W. mwangalie, kwa sababu katika macho ya watu wa Ansar kuna kitu".
Hadithi hii Takatifu inaonesha kuwa kilichohalalishwa kuangalia mchumba na yule mwenye nia na dhamira ya kuoa, na ni kuhakikisha mwanamke ameepukana na kasoro za wazi au sifa zisizohitajika, au kuhakikisha kuwa mchumba wa kiume anamkubali mwanamke huyo vile alivyo mwanamke, na hilo ni kuepusha kutokea ugomvi na mpasuko wa uhusiano kati yao pale itakapogundulika sifa hiyo au kasoro hiyo baada ya ndoa. Hadithi hii pia inaonesha kwa ufahamu wake kuwa kuangalia huku ni haki pia kwa mwanamke, kwa sababu ya kushirikiana wote wawili katika haki kuepusha ugomvi kwenye maisha ya ndoa, na kwa kushirikiana pia katika madhara ya kupatikana mtengano, bali madhara kwa mwanamke na ndugu zake mara nyingi yanakuwa ndio makubwa zaidi.
Na Hadhithi ya Al-Mughira Ibn Shu’ba R.A katika Hadithi iliyopokelewa na Tirmidhiy, An-Nisai na Ibn Maja kutoka kwa Al-Mughira Ibn Shu’ba amesema: “Kuna mwanamke alichumbiwa zama za Mtume S.A.W. basi Mtume akauliza je umemwangalia? Nikasema: hapana, Mtume akasema: Mwangalie, kwa sababu kunapelekea kudumu zaidi mapenzi kati yenu”.
Maana ya kauli ya Mtume S.A.W. (Kudumu kwa mapenzi kati yenu) maana yake ni: Njia iliyo bora ya kudumisha mapenzi kati yenu kama alivyosema Imamu Al-Tirmidhiy katika kitabu cha [Sunan Al-Tirmidhiy, 3/389, chapa ya Mustafa Al-Halaby].
Hadithi pia inaonesha kuwa kumwangalia mchumba ni jambo halali kwa lengo la kuangalia namna ya kuendana pia kuangalia uwezekano wa kuungana na kuwa mume na mke, na kuiandaa nafsi ya kila mmoja kuwa pamoja na mwenzake ndani ya familia moja na maisha yaliyo bora, hivyo kumwangalia mchumba ni jambo linalopendekezwa, kwa sababu linapelekea maandalizi ya hayo na kusaidia kuyafikia.
Hadithi ya Jabir Ibn Abdillah R.A. katika yale yaliyopokelewa na Abu Daud katika kitabu chake na Imamu Ahmad katika upokezi wake kutoka kwa Jabir Ibn Abdillah, amesema: amesema Mtume S.A.W. “Pindi mmoja wenu anapochumbia mwanamke, ikiwa ataweza kumwangalia yale yanayopelekea kumwoa, basi na afanye hivyo}, akasema Jabir nilichumbia msichana wa kazi nikawa ninajificha kwake mpaka nikaona yale yanayonisukumia uchumba na nikamwoa.
Katika mapokezi mengine kwa Ahmad: “Ikiwa mmoja wenu atachumbia mwanamke na akaweza kumwangalia sehemu ya yale yanayomsukumia kuendea ndoa basi na afanye”.
Na Hadithi ya Muhammad Ibn Muslima R.A katika Hadithi iliyopokelewa na Ibn Maja na Ahmad, kutoka kwa Muhammad Ibn Muslima, amesema: Nilichumbia mwanamke nikawa ninajificha na kumwangalia kwa kumchunguza, akaulizwa: unayafanya haya hali ya kuwa wewe ni Sahaba wa Mtume S.A.W? Nimemsikia Mtume S.A.W. anasema: “Mwenyezi Mungu Anapokutanisha ndani ya moyo wa mtu upendo wa kuchumbia mwanamke, basi hakuna ubaya kumwangalia”.
Uwazi wa Hadithi mbili unaonesha uhalali wa mchumba wa kiume kumwangalia mchumba wake wa kike katika yale ya kawaida kuangaliwa kwa wema na dhamira ya kuoa, ni sawa sawa kumwangalia huku ni kwa ruhusa ya mwanamke kufahamu kwake au kutofahamu au kinyume na ruhusa yake, Hadithi imeacha wazi katika hili, dalili yake imesisitiza moja kwa moja kitendo cha Masahaba wawili Jabir Ibn Abdillah na Muhammad Ibn Muslima baada ya kusikia kwao na kuangalia kwao bila ya kuomba ruhusa, kama inavyosisitiza Hadithi iliyopokelewa na Ahmad na Tabraniy katika kitabu cha Al-Ausat, kutoka kwa Abi Humaid R.A amesema: “Mmoja wenu akichumbia mwanamke, basi hakuna ubaya kwake kumwangalia ikiwa atamwangalia kwa lengo la uchumba hata kama mwanamke hajui”.
Kutokana na kauli yake Mtume S.A.W. “Hakuna ubaya kwake kuangalia yale yanayopelekea kumwoa” na kutoainisha ni nini ya kuangaliwa, basi kuna jitihada nyingi za wanachuoni pamoja na rai zao katika yale yaliyo halali kwa mchumba wa kiume kuangalia kwa mchumba wake wa kike, wanachuoni wamekubaliana ni yale maeneo yasiyokuwa tupu kwenye Swala, wakasema inafaa kuangalia sura na viganja viwili vya mikono na siyo maeneo mengine, kwa sababu maeneo haya yanazingatiwa siyo tupu kwa mwanamke, pia uso ni alama ya kujua uzuri wa mwanamke na kinyume chake, na viganja viwili hutumika kufahamu afya ya mwili au kinyume chake, kama alivyosema Imamu An-Nawawy katika kusherehesha kwake kitabu cha [sahihi Muslim 9/210], lakini pia ni maeneo yanayotumika kuonesha pambo lililoashiriwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu (wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika){AN NUUR: 31} wanachuoni miongoni mwa Masahaba na waliofuata baada yao wamefasiri neno pambo ni sehemu inayoonekana usoni na kwenye viganya, haya yamenukuliwa kutoka kwa Ibn Abbas, Anas na Aisha R.A., anasema Imamu At-Twabariy ambaye ni katika wanachuoni wakubwa wa tafsiri na ni mmoja wa Maimamu wakubwa wa jitihada baada ya kunukuliwa tafasiri mbalimbali toka kwa Masahaba na waliofuata baada yao neno pambo la wazi lililoelezewa kwenye Aya [Tafsiri ya Al-Twabariy Jamii Al-Bayan, 19/158 – 159 chapa ya Muasasat Al-Risala], “Na kauli iliyo bora kwenye usahihi: Ni kauli ya mwenye kusema – inamaanisha – sura na viganja viwili”.
Kwa kiwango hiki inapatikana haja ya mchumba na kumalizika ruhusa yake ya kumwangalia maeneo yanayopelekea msukumo wa kuoa mwanamke, asili ni kutofaa kumwangalia mwanamke, si halali isipokuwa kwa haja na kwa kiwango chake [Kitabu Tuhfat Al-Muhtaj, 7/191, chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby] na yaliyokubaliwa na wanachuoni ndio kauli yenye nguvu katika masuala.
Wafuasi wa Imamu Hambal wana kauli yenye kukubalika kwao katika mapokezi matatu kutoka kwa Imamu Ahmad ya kufaa kuangalia uso na viganya viwili na vile vinavyoonekana kwa kawaida kwa mchumba wa kike, kwa maana akiwa nyumbani kwake kama vile nywele za kichwa, magoti, dhira, nyayo na ugoko [Kitabu cha Matwalib Aulu Anuha cha Rahaibaniy, 5/12, chapa ya Al-Maktab Al-Islamy], na madhehebu yao yameelekeza kuwa Mtume S.A.W. pindi alipotoa ruhusa ya kumwangalia mchumba wa kike bila kufahamu kwake, imefahamika kuwa ameruhusiwa kuangalia maeneo yote yanayooneka kwa kawaida ambapo haiwezekani kuhusisha kuangalia uso tu peke yake pamoja na uwepo wa maeneo mengine yanayoshiriki kuonekana, na kwa vile mara nyingi huonekana, basi ikahalalishwa kuangalia kama vile uso, na kwa vile ni mwanamke imehalalishwa kumwangalia kwa amri ya Sharia, ikahalalishwa kuangaliwa sehemu hizo, kama vile ilivyohalalishwa kwa watu walio haramu kumwoa [Kitabu cha Al-Mughniy cha Ibn Qudama, 7/74 chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby]. Huenda ikapingwa sababu hii ya uhalali wa mchumba kumwangalia mchumba wake wa kike panapokuwa na haja, basi hukadiriwa kwa kiwango chake, na kunapatikana kuangalia huko ni kwenye uso na viganja, zisizokuwa sehemu hizo si halali kuangalia, na kipimo cha watu walio haramu kumwoa ni pamoja na tofauti ya kudumu kwa uhusianao na kuepukana na hali ya matamanio na fitina ni tofauti na anayetaka kumwoa na kutimiza hilo, ruhusa ya kumwangalia mchumba wa kike kwa upande wa madhehebu ya Imamu Hambal si ruhusa ya moja kwa moja isipokuwa ina sharti, kwani si ruhusa kuangalia maeneo yote ya mwili wake na kama sio hivyo basi ingekuwa ni ruhusa kuangalia maeneo ya kuoga na yale yanayoonekana kwa kawaida wakati wa kuoga, na wala siyo ruhusa katika hali zote kinyume na hivyo ingesemwa inafaa kumwangalia akiwa hana nguo, hakuna tamko la kisharia linaoonesha sharti ya maeneo ambayo mara nyingi yanaonekana akiwa nyumbani, wakati ambapo sharti la kuangalia uso na viganja ni sharti limeelezewa na Sharia kwa vile ni maeneo ya pambo lake huwa yanaonekana, na pia maeneo hayo hayazingatiwi kuwa ni tupu akiwa kwenye ibada ya Swala au ibada ya Hija, na kufaa kumwangalia katika mashirikiano ya kawaida ni pale panapokuwa na haja, kusimama kwenye mpaka huu na kuuwekea sharti ni kusimama kwenye tamko la kisharia na sharti za kisharia, wala hakupewi nguvu kupingana kwake na sharti za Imamu Hambal kuwa ni maeneo yale kawaida huwa ni yenye kuonekana, kwa sababu ni sharti za mtazamo na rai mkabala na sharti za kisharia na tarataibu zilizozoeleka.
Imamu Al-Auzai amesema inafaa kumwangalia sehemu za nyama za mwili wake. Na akaelezea Ibn Aqil mapokezi ya madhehebu ya Imamu Hambal kuwa mchumba wa kiume anaweza kumwangalia mchumba wa kike sehemu zote za mwili isipokuwa sehemu nzito za uchi, nazo zi tupu mbili [Kitabu cha Al-Inswaf cha Mardawiy, 8/18, chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby]. Baadhi ya wafuasi wa dhehebu la Dhahiriya na dhehebu la Imamu Ahmad katika yale yaliyopokelewa toka dhehebu la Hambal wanasema inafaa kumwangalia mwili wake wote, maeneo yanayoonekana na yale yasioonekana, yakiwa ni tupu au siyo tupu, na amesema Ibn Al-Qayyim kuwa Imamu Ahmad katika mapokezi amesema inafaa kumwangalia mchumba wa kike akiwa uchi kabisa [Kitabu cha Al-Mahali cha Ibn Hazm, 9/161, chapa ya Dar Al-Fikr, kitabu cha Ibn Qayyim kupitia kitabu cha Sunan Abi Daud 6/68 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]. Wanachuoni wengi wamepinga mitazamo kama hii na kuona kuwa ni makosa ya wazi kabisa yanayopingana na misingi ya Sunna na kauli za wanachuoni kama anavyosema Imamu An-Nawawy [Kwenye sherehe ya Sahih Muslim, 9/210].
Na akasema Imamu Ahmad katika mapokezi yake ya tatu – nayo ni katika maneno ya Imamu Hambal – kuwa inafaa kumwangalia usoni tu, kwa mujibu wa moja ya kauli mbili za madhehebu kuwa mkono ni sehemu ya tupu kwa mwanamke {Kitabu cha Al-Inswaaf cha Mardawy 8/17 – 18}.
Na wakaelezea baadhi yao kuwa haifai kumwangalia sehemu yoyote ile, wakasema “Halifai hilo kwa yule anayetaka kuoa mwanamke, wala si kwa yule asiyetaka kumwoa isipokuwa kwa aliye mume wake au yule aliye haramu kumwoa” [Kitabu cha sherehe ya Maani Al-Athar cha Imamu At-Tahawiy, 3/14, chapa ya Dar Al-Maarifa], amesema Imamu An-Nawawy katika sherehe ya Sahih Muslim {9/210}. “Ameelezea Kadhi kwa watu kuchukiza kwake – kwa maana ya kumwangalia usoni kwa mwenye kutaka kumwoa – hili ni kosa la wazi linalopingana na Hadithi hii – kwa maana ya Hadithi ya Abi Huraira – ina kauli yenye kupingana na makubaliano ya wanachuoni wa Umma ya kufaa kumwangalia pale panapokuwa na haja ya hilo”.
Rai na mitazamo ni mingi miongoni mwa mitazamo hiyo ipo iliyo kinyume na misingi pamoja na kauli za wanachuoni na miongoini mwake ipo iliyo karibu, na ukati na kati, na makubaliano ya wanachuoni ya sharti la kuangalia ni uso na viganya vya mikono.
Kuhusu sharti la mchumba wa kike kufaa kumwangalia mchumba wa kiume, au kutokuwepo sharti kiasi ambacho ni sawa na kufanya hivyo au kuacha, au sharti la kutotaka ruhusa ambapo inafaa kumwangalia hali ya kuwa mwenyewe hafahamu, wala haifai katika hali ya kufahamu kwake, kwa mujibu wa mitazamo na rai zilizotangulia kutajwa wanachuoni wamesema inafaa kuangalia uso na viganja tu ni sawa sawa kwa kutaka ruhusa yake au bila ruhusa, na akasema Imamu Hambal kuwa kuangalia maeneo yaliyo wazi mara zote kama vile nywele, magoti nyayo na sehemu za ugoko bila kujua wala ruhusa yake hilo huenda likawa ndio bora zaidi, inafaa kwa madhehebu yao kutaka ruhusa ya kuangalia maeneo hayo, japokuwa kinyume na hivyo ni bora zaidi, wakaweka masharti kama vile wanachuoni wengine ya kumwangalia bila kuwa peke yao, na wakasema: Ikiwa kutakuwa na uzito kwa mwanaume kumwangalia au akachukia hilo mchumba wa kike basi anaweza kutumwa mwanamke anayeaminika kumwangalia kisha kumwelezea wasifu wake mchumba wa kiume ili awe na ufahamu kwa mchumba wake wa kike {Kitabu Matalib Aulu Anuha katika sherehe ya kitabu cha Ghayat Al-Muntaha, 5/12}, madhehebu ya Imamu Malik yanasema inachukiza kwa mchumba wa kiume kutomjulisha na kumwangalia bila ruhusa yake hali ya kuwa hafahamu, ili jicho lake lisidondokee maeneo yasiyofaa kwake mwanaume kuyaangalia kama vile tupu {Kitabu Adhakhera cha Qurafiy, 4/191, chapa ya Dar Al-Gharb Al-Islamiy – Beirut}, ili isitumike nafasi hiyo kwa watu waharibifu kuangalia wanawake na kuleta hoja kuwa: Sisi ni wachumba. Na sehemu ya kuchukiza kutojua ni ule uwezekano wa kukataa na kutojibiwa ikiwa atamwomba au kuombwa msimamizi wake kumwangalia kwa ajili ya uchumba, ama ikiwa anajua hilo basi ni haramu kumwangalia na kumjulisha ikiwa atahofia fitina. [Kitabu Hashiyat As-Sawiy sherehe ya As-Saghir, 2/340, chapa ya Dar Al-Maarif], ambalo hatufikirii lingine ni kuwa mitazamo ambayo imehalalisha kwa mchumba wa kiume kuangalia maeneo yote ya mwili wa mwanamke ni sawa sawa maeneo hayo ni uchi au si uchi ni kuwa sharti la kufaa kuangalia tupu ni kutojua na wala si kutaka ruhusa, kwa sababu mwanafiqhi kusema kuwa Sharia inahalalisha kwa mchumba kumuangalia mwanamke akiwa hana vazi au mwanamke kumwangalia mwanaume katika hali hiyo, hili linapingana kwa ujumla wake na Sharia ya mbinguni uelewa wa kijamii na maadili mema.
Maelezo yaliyotangulia yanabainisha kuwa, inapendeza kwa mchumba wa kiume kumwangalia mwanamke ambaye anataka kumchumbia na kumwoa ili awe na ufahamu wa jambo lake, na ni halali kumwangalia usoni na viganya viwili kwa ruhusa yake na bila ruhusa yake kwa kauli yenye nguvu na kupitishwa na jopo la watu wa elimu pamoja na kulitolea fatwa.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas