Kuongeza Muda wa Kukodisha.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuongeza Muda wa Kukodisha.

Question

 Baba yangu ana nyumba ya kukodisha katika mji wa Nasr City tangu mwaka 1972, alifariki mwaka 1998 na ametuacha katika nyumba hii mimi, mke, dada mdogo, na dada mwingine aliyeolewa baada ya kifo chake baba kwa miezi 8 na akahamia nyumba ya mume wake, na ndugu zangu wengine, ni: kaka na dada wote wako katika ndoa na wametengana nasi kabla ya kifo cha baba yetu. Swali langu kuhusu nyumba hii: mwenye nyumba anataka kuibomoa na kuhamisha watu na kuwalipa fidia kwa jumla ya kiasi cha paundi za kimisri 500,000, nani ana haki ya pesa hizi? Na kama ikinunuliwa nyumba itakuwa ya nani? Na fahamu kwamba nitaoa baada ya miezi mitatu.

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Mkataba wa kukodisha una sheria zinazoupanga, na sheria hizi zikiwa ni pamoja na zile zinazohusiana na zile zinazoitwa “kuongeza muda wa kukodisha”, na dhana ya kuongeza hapa ni kwamba mkataba wa kukodisha hauishi kwa kufikia mwisho wa muda wake, lakini huongezwa moja kwa moja na kutokana na hukumu ya sheria kwa upendeleo fulani kama lilivyoainishwa katika Sheria.
Sheria ya Misri imelazimisha kuongeza muda wa mikataba kwa muda usioainishwa, na bila ya haja ya kukubaliana kwa uwezo wa mkandarasi juu ya hivyo, kutokana na matini zinazohusiana na mfumo wa umma.
Sheria imeainisha wanaopendelewa kwa kuongeza muda wa kukodisha katika idadi ndogo ya jamaa, na ilivyoelezwa katika Ibara ya 29 ya Sheria (49) ya 1977 kuhusu kukodisha nyumba ni kwamba: “Mkataba wa kukodisha nyumba hauishi kwa kifo cha mwenye kukodishwa au kuacha nyumba kama akikaa mke au watoto au yeyote kati ya wazazi wake, ambao walikuwa wakazi pamoja naye hadi kifo chake au uhamisho... katika hali hizi zote, lazima mwenye kukodisha akubali kuubadilisha mkataba wa kukodisha kwa wale ambao wana haki ya kuendelea kuchukua nyumba hiyo, na kwa njia ya mshikamano wakazi hao wanalazimishwa na masharti yote ya mkataba”.
Kutokana na ibara hii, inajulikana kwamba inawanufaisha kwa kuongeza muda wa kukodisha, wafuatao: wanandoa, watoto wa kiume na wa kike, na wazazi ambao walikuwa wanakaa pamoja na mwenye kukodishwa mpaka kufikia tarehe ya kifo au uhamisho.
Jamaa wote wanafaidika na kuongeza muda wa kukodisha wa kisheria, na haikutajwa katika maandiko ya sheria yanayosema kwamba wanapangiwa katika maisha yao, lakini sheria inathibitisha kuongeza muda wa kukodisha kwa pamoja, kama wao wote walivyokuwa wakinufaika na makazi kabla ya kifo au uhamisho, basi wao wote wanashirikiana pia baada ya kifo au uhamisho katika kufaidika na nyumba husika. Kama mmoja wao atakuwa ameihama nyumba hiyo, basi atakuwa amewaachia haki yake watu wengine.
Kinachokusudiwa katika makazi kwenye ibara iliyotangulia ni makazi ya jengo,la kawaida, la kuendelea mpaka kifo au uhamisho, ambapo nia ya mkazi ni kutoka na kurudi katika nyumba hii; wala hana nyumba nyingine isipokuwa nyumba hii tu, basi hali ya kukaa kwa wakati maalumu inafutwa, akiwa na nia yeyote na sababu yeyote.
Vile vile, sheria haikutia sharti kuhusu kukaa kwa wanandoa, watoto na wazazi kipindi fulani cha ukaaji makazi, bali inatosha kukaa tu mpaka wakati wa kifo au uhamisho.
Kutokana na hali hii pia inajulikana kwamba si muhimu kuwa mfadhiliwa ni mrithi, na pengine ana haki ya kuongeza muda wa kukodisha na ana haki ya kurithi, na pia si lazima kwamba kila mrithi ni mfadhiliwa, lakini inawezekana mrithi akawa hana haki ya kukaa katika nyumba hii kama hayumo kwenye masharti yanayotajwa katika ibara la «29”.
Sheria hii ni miongoni mwa masuala yanayofuata mtazamo wa mwenye madaraka kuhusu maslahi muhimu zaidi. Sheria hii inafuatana na maslahi ya umma, na maslahi hapa ni kuthibitisha kwamba nyumba hii ni ya kifamilia; ambapo mwenye kupangishwa anapanga ili akae ndani yake yeye na familia yake, na jamaa zake wanaweza kukaa pamoja naye, na jamaa zake hawa ni familia yake.
Iliamuliwa katika misingi ya sheria kwamba mwenye madaraka anatenda kwa mujibu wa maslahi ya umma, na kwamba mwenye madaraka ana mamlaka ya kuainisha yaliyoruhusiwa, yaani ana haki ya kuchagua moja kati ya mambo mawili: kufanya au kuacha jambo linaloruhusiwa, kisha kuwawajibisha watu kuchagua jambo hili kufuatana na mamlaka aliyopewa na Sheria.
Asili ya kauli hii ni aya ifuatayo: {Enyi mlio amini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi} [AN NISAA: 59]. Ibn Ashour anasema katika tafsiri yake: “Kama wenye madaraka ni miongoni mwa watu ambao wanategemewa kusimamia mambo ya watu, ... na hawa wenye madaraka ni kama vile: Makhalifa, Wasimamizi, viongozi wa majeshi, na wanavyuoni wa fiqhi na masahaba wenye jitihada na wananvyuoni wa zama hizi. Na hawa wenye madaraka wanaitwa ‘Ahlu lhalli wal Aqd’ [5/97, 98, Ad-Dar Al-Tunisiyah]
Imepokelewa kutoka kwa Masheikh wawili kutoka kwa Abdullah Ibn Omar R.A kwamba Mtume, S.A.W. amesema: "Ni wajibu kwa Muislamu kusikia na kutii kama hakuamrishwa kufanya dhambi, na anapoamrishwa kufanya dhambi, basi hakuna kusikia wala kutii".
Imepokelewa kutoka kwa At-Tirmidhiy -na asili yake katika Sahihi ya Imamu Muslim- kutoka kwa Wael Ibn Hajar, R.A. kwamba Mtume, S.A.W, aliulizwa na mtu, aliesema: "Je, kama tuko na wakuu wanaotunyima haki yetu na wanatuomba haki yao? Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W akasema: ni wajibu juu yenu kusikia na kutii, basi wao wana majukumu kwa mliyowabebesha, kama ambavyo nyinyi mna majukumu yenu kwa mliyoyabeba".
Imepokewa kutoka kwa Al-Hafiz katika Sunan yake na imepokewa kutoka kwa Ibn Abi Shaybah katika utunzi wake kwamba Hudhayfah Ibn Al-Yaman R.A, alimwoa mwanamke Myahudi, Omar akamwandikia kuwa amwache, aliandika: akamwandikia kwamba kama ni haramu kumwoa nitamwacha. akamwandikia kwamba: Mimi sikudai kuwa ni haramu, lakini ninachelea kwamba mnaowaoa ni makahaba miongoni mwao.
Huyo ni Omar R.A, amezuia kuwaoa wanawake wa Watu wa Kitabu katika zama zake, kwani alikuwa anachelea kwamba pengine watu hawajali kuchagua wanawake wenye Maadili mazuri kwa ajili ya kuwaoa, kisha jambo hilo si kuharamisha lililo halali, lakini ni kuweka mipaka kwa mambo yanayoruhusiwa kwa mujibu wa maslahi ya umma.
Na dalili ilioyo wazi zaidi ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Al-Azraqi katika habari za Makka kwamba wakati Msikiti Mtukufu ulipokuwa umebanwa kwa kuzungukwa na nyumba za watu, Omar ibn Khattab R.A alizielekea nyumba zilizouzunguka na akazinunua kutoka kwa wamiliki wake na akazibomoa kwa ajili ya upanuzi wa msikiti, na wakati baadhi yao walipokataa kuchukua fedha na kuziuza, fedha za nyumba hizo ziliwekwa katika hazina ya Kaaba mpaka wakaja wenyewe kuzichukua, Omar akawaambia kuwa: “Hakika nyinyi ndio mliojenga nyumba zenu kandoni mwa Kaaba, wala siyo Kaaba iliyojengwa kando kando ya nyumba zenu”. Matini hii ni dalili ya kuruhusiwa kwa kuingilia kati kwa mwenye madaraka katika umiliki binafsi, na bila shaka kumlazimisha mwenye kupangishwa kuongeza muda wa kupanga ni rahisi zaidi kuliko kumlazimisha kuuza.
Wanavyuoni wamesema maana hii, pia ilitajwa katika vitabu vya mabwana Maimamu wanaofuata madhehebu ya Shafi kwamba kama mwenye madaraka akiamrisha kufanya mambo yanayochukiza au yanayopendeza au yanayoruhusiwa ni wajibu kuyatenda. Imam Ibn Hajar Al-Haytamiy katika fatwa yake ya kifiqhi [1/278, Al-Maktaba Al-Islamiyah] anasema: “Kauli yao: ni wajibu kumtii mwenye madaraka wakati anapoamuru na anapokataza isipokuwa katika mambo yaliyo kinyume na hukumu ya Sheria. Inaonekana kuwa walichokikusudia kwa tamko la mambo yaliyo kinyume na hukumu ya Sheria: ni kuamrisha kufanya dhambi au kukataza wajibu, na hali hii ni pamoja na mambo yanayochukiza pia. Na kwa hivyo basi kama akiamuru ni wajibu kutekeleza aliyoayaamrisha, kwani hairuhusiwi kutomtii. Kisha maana ya maneno yao ni kwamba kutoa sadaka kuwa ni lazima kama ataamrisha itolewe, na hivyo ndivyo ilivyo, lakini uwajibu unapatikana kwa pesa chache sana zilizoweza na kuitwa sadaka, kama ilivyooneshwa”.
Kuhusu mpangaji kuchukua malipo kutoka kwa mwenye nyumba kwa ajili ya kuuvunja mkataba wa kupanga ulio sahihi, nayo ni malipo ambayo watu wanayaita siku hizi “Malipo mbadala kwa ajili ya kuiacha nyumba” au “kuhama” au “kuuza ufunguo”, na hakuna kizuio kwa mujibu wa Sheria kama watu wawili walikubaliana juu ya kiasi cha kulipwa, kwa sababu hali hii inafuata suala la mauzo ya faida, na ukweli wa kukodisha ni umiliki wa nyumba kwa faida maalumu, kama vile mwenye kupangisha anaacha haki yake ya kufaidika na pesa maalumu. Al-Quraafi anasema katika kitabu chake, Al-Furuuq kuhusu tofauti ya thelathini kati ya msingi wa umiliki wa kutumia na msingi wa umiliki wa manufaa [1/187, Alam Al Kutub]: “Kuhusu mmiliki wa manufaa, ni kama aliyepanga nyumba au aliyeikopa, anaweza kuipangisha kwa mwingine, au anaweza kukaa katika nyumba hiyo bila ya kulipa malipo yeyote, na anaweza kufanya kama anavyofanya mmiliki katika nyuma yake kwa mujibu wa utaratibu wao wenyewe. Hali hii ni umiliki usio na mipaka katika wakati maalumu kama ilivyotajwa katika mkataba wa kukodisha au kwa mujibu wa utaratibu wao, na kwa hivyo basi utaratibu huu umeshuhudia kwamba mtu fulani ana haki ya kukaa katika nyumba hii kwa muda maalumu, basi ana haki ya umiliki huu na anaruhusiwa kufanya anavyopenda katika nyumba hiyo na kwa muda huu, na umiliki wa manufaa haya ni kama umiliki wa shingo yake”.
Imamu wa wananvyuoni wa madhehebu ya Maliki katika wakati wake, Sheikh Mohammed Aleesh katika maelezo yake ya kitabu cha [Muhtasar Khalil 7/493, Darul fikr] anasema: “(Msingi): mmiliki wa manufaa ana haki ya kulipwa, na mmiliki wa kutumia manufaa hana haki ya kulipwa. Kama vile wanaokaa shuleni, msikitini au barabarani. Hakuna mtu mwenye haki ya kukodisha nafasi yake msikitini, shuleni, au barabarani, kwa sababu hakuwa na mamlaka ya manufaa yake yeye mwenyewe katika maeneo hayo.”
Wanasema hivyo baadhi ya wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Malik, baadhi yao walikuwa na ujumbe huu ambao unaosema: (Ripoti na Fatwa kadhaa kuhusu kuacha nyumba na kuacha haki kwa Watunisia), Mufti kutoka kwa wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Malik nchini Tunisia, Sheikh Ibrahim Ar-Riahi M. 1266 AH, Sheikh Mohammed Peram wa nne ambaye Mtunisia, Mufti wa wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Malik Sheikh Al-Shadhli ibn Saleh Bass, na Sheikh Mohammed Al-Sunusi Qadhi wa Tunisia, wote wameamua kwamba inaruhusiwa kuchukua pesa kwa kuacha nyumba, kwa mujibu wa mila na desturi zao, na kwa sababu mwenye kukodisha anamiliki manufaa (kama vile nyumba), na kwa hivyo basi anaweza kuyaacha manufaa yake hayo kwa mkabala wa malipo kama kukodisha nyumba, na pasipo na malipo kama kumpa mtu yeyote nyumba pasipo na malipo. Al-Banaani alitaja Fatwa ya watu wa Magharibi kuhusu kuruhusiwa kuchukua malipo mbadala kwa kuiacha nyumba. Sheikh Mohammed Peram anasema: “Hali ya kuacha nyumba inafanana na hali ya kuafikiana na mtu maalumu kulima ardhi, lakini hali ya kuacha nyumba haisababishi haki ya kumiliki shingo kwani yenyewe inashikilia manufaa”.
Na pia Sheikh Ahmed Al-Fayoumiy Al-Gharqawiy miongoni mwa wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Malik alitunga ujumbe mwingine, usemao: “Onyo kwa manufaa ya kuacha makazi katika utekelezaji wa suala la kuacha nyumba iliyokodishwa kwa ajili ya kukaa”, Sheikh Aleesh katika Fatwa yake aligusia suala hili: [Fatah Al-Ali Al-Malik Fi Alfatwa ala Madhhab Al-Imam Malik 2 / 250, Dar Al-Marifa] na ametaja maneno mengi kutokakatika ujumbe wa Al-Gharqawi uliotajwa hapo juu.
Kwa mujibu wa uamuzi wa Baraza la Kimataifa la Fiqhi ya Kiislamu la Jeddah Na. (6) kwa mwaka 1408 AH, sawa na mwaka 1988 kwamba: «Ikiwa mwenye nyumba atakubaliana na mpangaji wake wakati wa kukodishana, kwamba mmiliki huyo ampe kodi mpangaji kwa mkabala kuiacha haki yake ya kumiliki muda uliobakia ndani ya mkataba wao, kwa hivyo basi malipo mbadala ya kuiacha nyumba yanaruhusiwa kwa mujibu wa Sheria kwa sababu ni fidia ya kuacha mmiliki haki ya mwenye kupangishwa kwa kumuuzia mmiliki haki hii”.
Kwamba inapaswa kufahamu kwamba kiasi hiki kilichopokelewa kutoka kwa mmiliki hakigawanywi kati ya watumiaji kwa kuongeza mkataba wa kukodisha kama urithi; kwa sababu nyumba iliyokodishwa haiko katika urithi wa mpangaji aliekufa, na kwa kuwa pesa hizi hazikuwa katika urithi wake wakati wa kifo chake, kwa hivyo zitagawanywa kati yao kwa usawa, kwa sababu wote ni sawa kutokana na Sababu ya haki ya fedha hizo katika kuachia mkataba wa kupanga.
Hivyo, katika hali halisi ya swali hili: wenye kunufaika tangu kuongeza muda wa mkataba wa kukodisha ni: mke na dada watatu waliokuwa wakikaa katika nyumba hiyo iliyokodishwa wakati wa kifo cha baba yao kama walikaa katika nyumba hii kama tulivyoelezea hapo awali, hakuna ubaya kwao kupata malipo maalumu kutoka kwa mmiliki wa nyumba kama wakikubaliana kwa ajili ya kuuacha mkataba huo wa kukodisha na kuiacha nyumba, na kuwa malipo haya ni haki kamili kwao isipokuwa ndugu na dada yao waliooa na kuolewa na walioenda kukaa katika nyumba zao kabla ya kifo cha baba yako, mtagawana malipo hayo kwa usawa, na kama mkiafikiana kununua nyumba nyingine ya mtakayoimiliki, basi nyumba hiyo itaandikwa kwa majina yenu. Hizi ni haki, lakini kama mkitaka kutuliza ndugu zenu ambao ni kaka na dada waliotajwa hapo awali, kwa kuacha kila mmoja wenu sehemu yake; kwa ajili ya undugu wa kuzaziliwa pamoja na kuwaridhisha, ni jambo zuri na mnapata thawabu kwa kufanya hivyo. Mnafanya hivyo kwa ridha na usamehevu wenu, siyo kwa kulazimishwa na kutenzwa nguvu, kama ilivyoelezwa katika swali hili.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas