Kumzuia Mke wa Kitabu (Myahudi au ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumzuia Mke wa Kitabu (Myahudi au Mkristo) Kunywa Vilevi.

Question

 Je, ni haki mume Muislamu kumzuia mke wake anayetokana na watu wa Kitabu kunywa kilevi?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Katika Sharia za ndoa ndani ya Uislamu ni kupata usalama, starehe na utulivu kwa mume na mke kupitia uhusiano wa kina unaounganisha kati ya mwanamume na mwanamke, Sharia inalinda na kuainisha yale yanayotokana na ndoa miongoni mwa haki na wajibu, na kulinda kwa nguvu kubwa kutotokea tofauti na mvutano na kupatikana ugumu wa usuluhishi na kuridhiana kwa wema – ambao ndio msingi – katika ufumbuzi wa matatizo ya ndoa. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake} [AN NISAA: 19].
Na Akasema tena Mola: {Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao} [AL BAQARAH: 228].
Na yale yanayofungamana na kifungo cha ndoa miongoni mwa haki ni kuwa mume Muislamu – vyovyote atakavyosimamia wajibu wake kwa mkewe – ni haki kwa mke kumtii katika kila jambo lisilokuwa maasi katika Dini ya Kiislamu na Dini ya mke akiwa ni katika watu wa kitabu, ambapo hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumwasi Muumba, vile vile kwa upande wa mume ana haki ya kutii katika yale hayatakuwa na ubaya dhidi ya haki ya mwanamke, kama vile kumtaka mke kuuza kitu anachomiliki au alichopewa kama zawadi, au kuachana na Dini au haki yake kwenye Dini, hakuna utiifu kwa mume katika dhuluma na uovu juu ya haki ya mke. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa ni kipawa. Lakini wakikutunukieni kitu katika mahari, kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke kwa raha} [AN NISAA: 4] anasema Sheikh Al-Maraghiy katika kufasiri Aya hii Tukufu [Tafsiri ya Al-Maraghiy, 4/184, chapa ya Mustafa Al-Halaby] “Kwa maana ikiwa nafsi zao hao wanawake zimeridhia kukupeni kitu chochote katika mahari pasina madhara yoyote wala udanganyifu, basi kuleni kiwashuke kwa utulivu, hakuna ubaya kwenu wala dhambi kuchukua, kisha haifai kwa mwanamume kula kitu katika mali ya mke wake, isipokuwa pale atakapojua mume kuwa nafsi ya mke wake imeridhia hilo, ikiwa mume atahitaji kitu kwa mkewe, lakini mke akawa na wasiwasi au woga wa kumpa hiko kitu alichoombwa na mumewe, basi mume hana uhalali wa kuchukua”.
Miongoni mwa haki za mke akiwa ni katika watu wa kitabu (Myahudi au Mkristo) ni kuwa na uhuru wake kamili katika kutekeleza mambo yake ya kidini na bila kulazimishwa kufanya lililo haramu kwenye Dini yake, wala haifai kumzuia kutekeleza kile anachoamini kuwa ni wajibu kwake katika Dini. Mola Amesema: {Hapana kulazimisha katika Dini} [AL BAQARAH: 256]. Mwenyezi Mungu Amehalalisha kwa Waislamu kuoa wanawake wa watu wa kitabu (Wayahudi na Wakristo) pasina kuwalazimisha au kuwashurutisha kuingia kwenye Uislamu, kama walivyosema jopo la Masahaba na watu wa elimu. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu wa Kusema: {Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba} [AL MAIDAH: 5]. Abdillah Ibn Omar R.A. wote wawili alikuwa haoni sababu ya kuoa mwanamke wa Kinasara (Mkristo) na alikuwa anasema: “Sifahamu shirki iliyo kubwa zaidi ya kusema: Hakika mungu wake ni Isa, lakini Masahaba wengi walioa wanawake wa kinasara, na wala hawakuona ubaya katika hilo, wakiyafanyia kazi maandiko ya Aya hii Tukufu [Angalia tafsiri ya Ibn Kathir, 3/42 chapa ya Dar Tiba cha uchapishaji na usambazaji], na imekuja pia katika kitabu cha: [Mawahib Al-Jalil, 2/454 chapa ya Dar Al-Fikr] “Amesema Asbagh: Nimemsikia Ibn Al-Qasim akiulizwa kuhusu mwanamke wa kinasara aliyeolewa na Muislamu je atafungua kwenye funga anayofunga pamoja na watu wa Dini yake? akasema: Sioni sababu ya kumlazimisha kwa yale yaliyopo kwa watu wa Dini yake na mila zake – kwa maana ya sharia zake – wala ulazima wa kula kile wanachojitenga nacho katika funga yao, au wanachojitenga na kukila hilo halipo kwenye hukumu, amesema Asbagh: Wala mwanamume Muislamu kumzuia na hicho anachokula kwa kumlazimisha. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema {Hapana kulazimisha katika Dini} na akasoma {Sema: Enyi makafiri! * Siabudu mnacho kiabudu} mpaka alipofikia {Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu}. Amesema Ibn Rushd: haya kama alivyosema, ni katika yale yasiyokuwa na tofauti ndani yake kuwa mume hana sababu ya kumzuia katika yale yaliyokuwa sharia kwenye Dini yake…..na akasema katika kitabu cha Ibn Al-Muwaz: ….. Ana haki ya kumzuia kwenda Kanisani isipokuwa katika mambo ya lazima”.
Ama yasiyokuwa ya lazima na yale yaliyo haramu na mambo halali yanayopendeza na yale yanayochukiza, mume ana haki ya kumruhusu au kutomruhusu lakini katika mipaka ya wema pasi na ubaya wa wazi katika kuitumia haki hii, mume ana mamlaka ya usimamizi kwa mke na kiongozi kwa mke madamu tu bado yupo kwenye mamlaka yake, hili halina maana kuwa mume ana haki ya kumlazimisha na kumtawala pasi na kuwepo masilahi au kuondoa uharibifu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amemfanya mwanamume kuwa ndiye msimamizi kwa mwanamke kwa kuamrisha kuelekeza na kusimamia kama wanavyosimamia wenye madaraka kwa wananchi, katika yale Aliyohusisha Mwenyezi Mungu kwa mwanamume katika mambo ya kimwili na kinafsi, na kwa yale Aliyoyalazimisha kwake katika wajibu wa mali. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayoyatoa} {AN NISAA: 34}. Anasema Imam Al-Baydhawiy katika kufasiri Aya hii Tukufu: [Tafsiri Anwar At-Tanzil wa Asrar At-Taawil, 2/72, chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby] “Wanaume ni wasimamizi wa wanawake” wanawasimamia kama usimamizi wa viongozi kwa wananchi, akatoa sababu mbili za hilo: Sababu ya kupewa na sababu ya kupata, akasema: “kwa kufadhilishwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi” kwa sababu ya ufadhilishaji wa Mwenyezi Mungu kwa wanaume juu ya wanawake ni kutokana na ukamilifu wa akili na upangiliaji nzuri na nguvu zaidi katika matendo mema na utiifu, kutokana na hilo Mola Akahusisha Utume uimamu uongozi usimamizi wa mambo ya Dini, ushahidi katika kadhia mbalimbali, ulazima wa jihadi, Swala ya Ijumaa na mfano wa hayo kwa wanaume”.
Kutokana na maelezo yaliyopita mume ana haki ya kumzuia mke wake akiwa mtu wa kitabu kutumia vinywaji vya kulevya, hata kama ataamini mwanamke kuwa vinywaji hivi ni halali katika Dini yake, hata kama Sultani wa watu wa dhima (watu wasiokuwa Waislamu wanaishi kwa makubaliano ndani ya jamii ya Kiislamu) akapitisha amri ya kunywa pombe kwa kuruhusu moja kwa moja, kwa sababu pombe pamoja na vilevi vingine vina athari na madhara si kwa mnywaji tu isipokuwa yanavuka mpaka kwa yule anayeishi naye pamoja na kumletea kero na maudhi, wala sio ruhusa ya moja kwa moja ya Sultan kuwa ni msukumo wa kumpinga mume, ambapo mume ana mamlaka yake kamili kwa mke wake na wala siye Sultan, kwani Sultan hana haki ya kuvutana na mume katika mamlaka haya yanayo muhusu mume, amri ya Sultan haipewi nguvu ya kupinga zuio maalumu la mume, kama vile Sultan ikiwa atahalalisha kula kitunguu saumu na kitunguu maji mume akazuia ili kuepusha harufu mbaya, lakini pakitokea mvutano basi amri ya kadhi ndiyo itakayo tatua masuala haya.
Wanachuoni wametofautiana katika masuala haya kundi la madhehebu ya Imamu Shafi linasema mume anaweza kumzuia mke wake katika watu wa kitabu kunywa pombe au ulevi kwa kiasi ambacho ikiwa atakunywa kitamlewesha, lakini kiasi cha chini ya kulewa pia mume ana haki ya kumzuia kwa upande mwingine si kumzuia moja kwa moja, isipokuwa ikiwa kunywa huko kutaleta kero kwa mume kumchafua na nafsi yake kuchukia.
Amesema Al-Khatwib As-Sharbeniy katika kitabu cha: [Mughniy Al-Muhtaj, 4/313, chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy], na angalia kitabu cha: [Nihayat Al-Muhtaj, 6/292 – 293, chapa ya Dar Al-Fikr] “Atalazimishwa mke asiye na hisia akiwa Muislamu au mwanamke wa kitabu na vile vile kijakazi (kuoga hedhi na nifasi) kwa maana ya uhalali wa kumlazimisha kufanya hivyo pindi anapokuwa tahara kuleta uhalali wa mume kuingilia….na kulazimishwa kuacha kula nyama ya nguruwe na mfano wake katika yale yanayosimamisha ukamilifu wa starehe kwa kuondoka kwake, kama vile anavyolazimishwa kuondoa najisi. Jambo la pili: Hakuna kulazimisha, kwa sababu haizuii kustarehe, sehemu yenye tofauti katika kumlazimisha mwanamke wa kitabu ni kumzuia kula nyama ya nguruwe ikiwa mwanamke anaamini ni halali kama ilivyo kwenye Unasara, ikiwa anaamini ni haramu kama ilivyo kwenye Uyahudi anazuia tu moja kwa moja… mume atamzuia kula kile chenye kuchukiza harufu yake, kama vile kitunguu maji na kitunguu saumu, na kula kile ambacho anahofia kusababisha ugonjwa, mume pia anaweza kumzuia mkewe mtu wa kitabu kunywa chenye kulevya na vingineyo pamoja na kuuza kumzuia kwenda Kanisani kama vile anavyoweza kumzuia mke wake Muislamu kunywa mvinyo ikiwa mwanamke anaamini ni halali kwa kiasi ambacho hakileweshi, pamoja mengine kama kwenda msikitini na Swala za jamaa”.
Amesema Al-Umraniy katika kitabu cha: [{Al-Bayan nayo ni sharhu ya kitab Al-Muhadhab cha Abi Is-Haq As-Shairaziy, 9/498, 499 chapa ya Dar Al-Minhaj] “Ikiwa mwanamke ni dhimmiya na akataka kunywa pombe….mume ana haki ya kumzuia na kulewa, kwa sababu huko kutamzuia na kustarehe naye. Lakini je ana haki ya kumzuia kunywa kiasi ambacho hakileweshi? Ameelezea Sheikh Abu Is-haqa kuwa kuna mitazamo miwili, wengine wameelezea kuwepo kauli mbili: ya kwanza: Hapaswi kumzuia nacho, kwa sababu haitomzuia kustarehe naye. Kauli ya pili: Ana haki ya kumzuia nacho, kwa sababu haipambanui kiasi cha kulewesha na kile kisicholewesha hivyo atamzuia kwa hali zote, na kwa vile harufu yake inaleta kero na maudhi na kumzuia kukamilisha kustarehe naye…. Je, mume ana haki ya kumzuia mwanamke dhimmiya kula nyama ya nguruwe? Amesema Sheikh Abu Hamid kuwa kuna kauli mbili, kama vile kunywa kiwango kidogo cha pombe. Na kuelezea Sheikh Abu Is-haqa kuna mitazamo miwili, na kuitolea sababu zilizopita. Amesema Ibn Asabagh: Uwazi wa maneno ya Imamu Shafiy R.A. ikiwa itamtia kichefuchefu katika nafsi yake na kuchukizwa basi ana haki ya kumzuia nayo, ikiwa nafsi yake haichukizwi…. hapaswi kumzuia kuila nyama hiyo”.
Na mfano wa madhehebu ya Imamu Shafi amesema pia Imamu Hambal, isipokuwa wao hawaruhusu kwa mume kumzuia mkewe kiasi ambacho hakipelekei kulewa kama ilivyoelezewa na Imamu Ahmad nayo kauli sahihi katika madhehebu yake, amesema pia Al-Bahutiy katika kitabu cha: [Kashaf Al-Qanaa, 2/190 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] “Ana haki ya kumzuia kutumia vilivyo haramu ikiwa ni pamoja na kunywa kiasi chenye kulewesha kwa sababu ni haramu, lakini hazuiliwi ikiwa chini ya kiasi chenye kulewesha, kwa maana kiwango cha chini ya kile kinacholewesha kwa imani kuwa ni halali kwenye Dini yake”. kwa upande wa Imamu Hambal kuna mtazamo mwingine kuwa mume ana haki ya kumzuia pia kwa kiasi kisicholewesha, katika kitabu cha: [Al-Mughniy cha Ibn Qudama Al-Hambaliy, 7/224 chapa ya Dar Ihayaa At-Turath Al-Arabiy] “Mume ana haki ya kumzuia mkewe na kilevi hata kama mke atakuwa ni katika dhimmiya, kwa sababu kutamzuia na kustarehe na mke wake, lakini pia kunaondoa akili na kumfanya kama vile mfuko wa ngozi uliojazwa hewa. Ikiwa mwanamke atataka kunywa kiasi kisicholewesha, pia mume ana haki ya kumzuia mwanamke Muislamu, kwa sababu wote wawili mume na mke wanaamini uharamu wake, ikiwa mwanamke ni dhimmiya hawezi kumzuia kwa kiwango hicho kisicholewesha, ameleezea hayo pia Imamu Ahmad, kwa sababu mwanamke anaamini uhalali wake katika Dini yake. Mume ana haki ya kumlazimisha kuosha mdomo wake kutokana na kinywaji hicho pamoja na najisi zengine ili aweze kustarehe naye kwa midomo yake. na inazingatiwa mume ana mamlaka ya kumzuia nacho kila chenye harufu yenye kuchukiza kama vile kitunguu saumu”. Katika kitabu cha: [Al-Inswaf cha Mardawiy Al-Hambaliy, 352: 353 chapa ya Ihyaa At-Turath Al-Arabiy] “Huzuiliwa mwanamke dhimmiya kunywa kilevi mpaka kikamlewesha. Lakini mume hana haki ya kumzuia kunywa kiasi kisicholewesha kwa kauli sahihi ya madhehebu, kinyume na kiwango hiko huzuliwa moja kwa moja”.
Wafuasi wa Imamu Abu Hanifa pia wametofautiana katika suala la kumzuia mwanamke wa kitabu kunywa pombe lakini ametofautiana mwanachuoni Ibn Najm kauli ya mwenye kusema: “Mume hana sababu ya kumzuia mke kunywa pombe”, na akasema kuwa kumzuia ni haki, amesema katika kitabu cha [Al-Bahr Al-Raiq sherehe ya Kanz Ad-Daqaiq, 3/111 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy]: Katika kitabu cha: [Al-Khaniya]: Muislamu mwenye mke dhimmiya hana haki ya kumzuia kunywa pombe, kwa sababu kunywa pombe ni halali kwake, lakini ana haki ya kumzuia kuchukuwa pombe na kuileta nyumbani, kwani hata kama ni halali kwa mwanamke lakini harufu yake ina madhara na kero kwa mwanamume basi anapaswa kumzuia kama vile kumzuia mwanamke wa Kiislamu kula vitunguu saumu na vitunguu maji, hivyo amesema Al-Karkiy katika kitabu cha Al-Faidh mlango wa kutayammam: Hakika Muislamu ana haki ya kumzuia mke wake dhimmiya kunywa pombe kama vile Muislamu au kula vitunguu saumu na vitunguu maji na mume wake akawa ni mwenye kuchukia hilo, basi ana haki ya kumzuia, na hii ni haki isiyojificha. Imamu Abu Hanifa anatofautisha kati ya pombe na kilevi kwani si kila kilevi kwao ni pombe tofauti na kauli ya jopo la wanachuoni, isipokuwa wao kama wengine wanakubali kuwa kunywa chenye kulevya ni haramu katika Sharia zote za mbinguni, amesema Ibn A’abideen katika kitabu chake cha: [Minhat Al-Khaliq ala Al-Bahr Al-Raiq, 5/28 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy]: "Katika fatwa za Qarii Al-Hidaya amejibu pale alipoulizwa kuhusu mwanamke dhimmiya ikiwa amelewa je ana haki ya kuadhibiwa, akasema: Ikiwa amekunywa pombe na kulewa madhehebu yake yanasema ni kuto adhibiwa, na akatoa fatwa Al-Hassan kuwa ana haki ya kuadhibiwa na kupitishwa fatwa hiyo na baadhi ya Masheikh, kwa sababu ulevi katika Dini zote ni haramu”. Akasema hoja ya Uislamu Abu Hamid Al-Ghazaliy katika kitabu cha: [Al-Mustasfiy uk. 174 chapa ya Al-Kutub Al-Elmiya]: “Sharia hazijatofautiana katika kuharamisha ukafiri, mauaji, uzinifu, wizi na kunywa kilevi”. Pombe katika madhehebu ya Abu Hanifa ni kimiminika chenye kulevya kitengenezwacho na zabibu maalumu na ni haramu uwingi wake na uchache wake, ama kimiminika cheye kulevya kisichotengenezwa na dhabibu basi katika uharamu wa kunywa kwake au uhalali wake kuna maelezo na masharti kwa Imamu Abu Hanifa na watu wake kama Abu Yussuf tofauti na Imamu Muhammad, amesema Al-Kasaniy katika kitabu cha: {Badaaii Aswanaai 6/2943 chapa ya Al-A’asima]: "Ama mwenye kuacha kilevi basi ni halali kwake kunywa kwa ajili ya matibabu kupendezesha chakula na kumpa nguvu katika utiifu haya ni kwa Abu Hanifa na Abu Yousuf R.A amepokea Muhammad R.A. kuwa si halali, nayo ni kauli ya Imamu Shafiy R.A. na kukubaliana kuwa si halali kunywa kwa ajili ya matamanio na kupendezesha nafsi", vile vile amepokea Abu Yousuf R.A. ndani ya kitabu cha Al-Amaliy, na amesema “Ikiwa atataka kunywa kilevi basi kiwe kichache au kingi ni haramu, na kukaa kwa ajili ya kusubiri kilevi pamoja na kukiendea pia ni haramu”. Kwa maelezo hayo ni halali kwa mwanamke wa kitabu kwa madhehebu ya Imam Abi Hanifa na Abu Yusuf kunywa pombe au kilevi kwa kiasi kisicholewesha ikiwa lengo la kunywa huko ni kwa matibabu, au kumpa nguvu, au kuongeza joto la mwili kwenye nchi zenye baridi, lakini pamoja na hayo ikiwa mume anaona kero kwa hilo basi ana haki ya kumzuia kunywa mke wake kama alivyosema mwanachoni Ibn Najm kwenye maelezo yaliyotangulia.
Ama kwa upande wa Imamu Malik mtazamo wenye nguvu kwao ni kuwa mume Muislamu hana haki ya kumzuia mke wake ambaye ni mtu wa kitabu kunywa pombe, au kula nyama ya nguruwe, kutokana na hili kuoa mwanamke wa kitabu ni jambo lenye kuchukiza kwao, amesema Ad-Dusuqiy katika {Kitabu chake cha sharhu Al-kabir, 2/268, chapa ya Dar Ihyaa Al-kitab Al-Arabiya} na angalia [Kitabu cha Asawiy katika sherehe ya kitabu cha Asagir 2/420 chapa ya Dar Al-Maarif] “Kwa hakika amelichukiza hilo Imamu Malik katika nchi ya Kiislamu, kwa sababu mke anakunywa pombe na kula nguruwe na kumlishia mtoto wake, lakini mume ikiwa anamkubali mkewe na kulala naye, basi hana sababu ya kumzuia, hata kama atadhurika kwa harufu yake, wala kumzuia kwenda Kanisani”. Katika mapokezi ya Imamu Malik kwa Ibn Al-Muwaz: Mume ana haki ya kumzuia kula nguruwe na kunywa pombe, kwa sababu hayo si katika mambo ya Dini yake na ana haki pia ya kumzuia kwenda Kanisani isipokuwa katika mambo ya lazima. [Kitabu Mawahib Al-Jalil, 2/454], na [Kitabu Al-Bayan wa At-Tahsil cha Abu Al-Waleed Ibn Rushd 2/349 chapa ya Dar Al-Gharb Al-Islamiy- Beirut].
Yaliyo karibu kwenye masuala haya ni jambo hili kuchukuliwa kwa njia ya wema na maridhiano ambapo asili ya uhusiano wa mume na mke lazima uwe kwenye msingi wa maelewano maridhiano na kuvumiliana, kinyume na hivyo mambo yenye tofauti yanaweza kuwa na mitazamo mingi ya kifiqhi na kihukumu sawa na vile aonavyo kadhi katika kutoa hukumu yenye nguvu na uzito kulingana na viwango vya masilahi na uharibifu na yale yanayokubaliana na makusudio ya Sharia ijapokuwa lenye kupewa nguvu na uzito zaidi ni mume kuwa na haki ya kuzuia, kwani huenda kunywa pombe hata kama ni kidogo kukapelekea uharibifu ni lazima mume amzuie, kama vile kuhofia watoto kuiga mwenendo wa mama yao na kuwazoesha kuona na kuangalia kilevi kununua na kunywa, ikiwa kuzuia huko kutapelekea madhara kwa mke kama kutumia kwake ni kwa ajili ya matibabu au kuleta nguvu mwilini na yanayofanana na hayo katika makusudio halali, hali ya mume akiwa ni mwenye kufahamu hilo kabla ya ndoa kisha akaridhia. Amesema Imamu Abu Is-haqa Asheraziy katika cha: [At-Tanbih uk. 169 chapa ya Aalam Al-Kutub] “Ni lazima kila mmoja kati ya wanandoa kuishi na mwenzake kwa wema na kufanya juhudi kwa yale yaliyo lazima kwake pasi na kuonesha kuchukizwa”.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia: yanabainika wazi kuwa ni halali kwa Muislamu aliyeoa mwanamke wa kitabu kumzuia kunywa kilevi kwa kiwango kinachofikia kwenye kulewa kama walivyokubaliana hayo jopo la wanachuoni wa madhehebu manne, ama kumzuia kunywa kiwango kisicholewesha haya ndiyo masuala yenye tofauti inapendeza ufumbuzi wa hayo kuhifadhi uhusiano wa ndoa pasina madhara wala ubishi kwa pande za mume na mke, na kuchunga hilo hali ya kila upande, pasina kueneza hukumu katika hali zote lengo ni kuchunga maisha mema ya ndoa kuridhiana na kufanyiana wema kati ya mume na mke.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas