Haki za Mke Aliyenyonyeshwa na Mama...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Mke Aliyenyonyeshwa na Mama Mkwe Wake.

Question

 Ni kipi kinachomtokea mke ambaye imethibitika kwamba yeye pamoja na mume wake walinyonyeshwa na mama mmoja zaidi ya mara kumi kwa ushahidi wa mama aliyewanyonyesha?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Unyonyeshaji katika lugha maana yake ni kunyonyesha kwa matiti na kuyanywa maziwa yake. [Tazama: Tahdhib Al Lughah 300/1, Ch. Dar Ihyaa At Turaath Al Arabiy, na At Taqiif ala Mohemaat At Taariif 178/1, Ch. Aalam Al Kutub].
Na maana ya unyonyeshaji katika Sharia ni jina la upatikanaji wa maziwa ya mwanamke au kinachopatikana kutokana na maziwa hayo ndani ya tumbo la mtoto au kichwa chake. [Tazama: Tuhfatu Al Muhtaaj 283/8, Ch. Al Maktabah At Tojariyah Al Kubra]
Na inashurutishwa katika unyonyeshaji kwamba uwe katika wakati wake wa kisheria, nao ni miaka miwili ya mfumo wa mwezi kuanzia tarehe ya kuzaliwa. Na unyonyeshaji wa kuharamisha ndoa ni wa kunyonya mara tano mbali mbali au zaidi ya mara tano, na kwa kunyonyesha awe mwanamke aliyenyonyesha mama kwa kunyonyesha kwa hao waliyonyonyeshwa. Na watoto wake wote watakuwa ndugu kwa wale aliowanyonyesha, na haiwi halali ndoa baina yao kama vile ndugu kwa nasaba.
Na Ushahidi wa mwanamke aliyenyonyesha peke yake ni moja kati ya njia za kuthibitisha unyonyeshaji kwa mujibu wa Jamhuri ya wanavyuoni wa Salafi (wema waliotangulia); kama vile Othman Bin Afaan, Ibn Abbas, Zuhariy, Hassan, Is-haq na Auzaaiy na wote ni wa madhehebu ya Hanbali. Mwanachuoni Mkubwa Al Bahutiy anasema katika kitabu chake: [Kashaafu Al Qinaa' 456/5, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]: "(Na ikiwa atatoa ushahidi wa kunyonya huko): yaani unyonyeshaji wa –kuharamisha - (mwanamke mmoja mwenye kuridhia kwa kitendo chake hicho cha unyonyeshaji), kwamba akatoa ushahidi kuwa yeye alimnyonyesha mara tano ndani ya kipindi cha miaka miwili ya kimwezi basi unyonyeshaji huo utakuwa umethibitika) kwa njia hiyo na hakuna kiapo chochote juu ya anayetoa ushahidi wala yule ambaye ushahidi umetolewa kwa ajili yake, kutokana na Hadithi aliyoipokea Auqbah Bin Al Haarith anasema: "Mama wa Yahya Binti Abu Ihaab aliolewa, basi mjakazi mweusi akaja kisha akasema: Mimi nilikunyonyesheni, na nilimwendea Mtume S.A.W. na nikamtajia jambo hilo, basi na yeye Mtume S.A.W. alisema: Iweje ayaseme hayo hayo? Basi Mtume S.A.W akamwamrisha amwache huru. Na katika Mapokezi mengine anasema; mwache huru! Imepokelewa na Al Bukhariy.
Na kadhalika kusadikika kwa mke na mume kwa mwanamke aliyewanyonyesha ni kukiri kuwa aliwanyonyesha, na kukiri kwake huko ni kuuthibitisha unyonyeshaji.
Na iwapo itathibitika kisheria kuwa walinyonya pamoja, basi lazima watenganishwe baina yao. Na mwanamke huyo ataharamishwa kwa mwanamume huyo uharamu wa milele, kwani yeye ni dada yake, na lazima watenganiswe baina yao. Kwani kinachoharamisha ndoa milele, ndicho kinachoharamisha kuanzisha uhusiano wa ndoa na kuendelea kwake.
Ama kuhusu haki anazowajibika mume kwa mwanamke katika hali hiyo ya kuvunjika kwa mkataba wa ndoa, basi mwanamke akiwa hajakutana kimwili na mume wake basi ana haki ya nusu ya mahari iliyoahidiwa kutolewa. Ama ikiwa mume alikutana naye kimwili, basi ana haki ya kuchukua mahari kamili, mahari inayotolewa papo hapo, akiwa na mahari inayoahidiwa papo hapo, na hana kitu chochote zaidi ya hicho. Na kukutana kimwili kulikotokea kunakuwa ni kukutana kimwili kimakosa kwa kufananisha, kwa kuwa wao hawakuwa wanayajua hayo kabla ya ndoa yao. Na mke analazimika kukaa Eda kutokana na kukutana kimwili kimakosa kama vile mwenye Eda iliyotokana na takaka, na kama ikitokea kuzaliwa watoto kutokana na ndoa hiyo basi watanasibishwa kwa nasaba ya baba yao kisharia, na gharama za mahitaji yao yote yatakuwa juu ya baba yao. Na ulezi wa watoto wachanga miongoni mwao utakuwa kwa mama yao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas