Kukaa Mwanamke Aliyetalikiwa katika...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kukaa Mwanamke Aliyetalikiwa katika Nyumba ya Mumewe

Question

Nimetaliki mke wangu talaka rejea, ninao watoto wadogo, na mke wangu niliyemtaliki anataka kwenda nyumbani kwa baba yake, ili kukaa eda yake, je, ni halali kwake kukaa katika nyumba nyingine isiyo nyumba ya ndoa? Kama hairuhusiwi, namna gani tukae pamoja katika nyumba moja -ambayo ni nyumba ya ndoa – ingawa nimemtaliki? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Talaka rejea au isiyo rejewa, na kila moja ina hukumu yake, miongoni mwa hukumu hizi ni eda, na miongoni mwa masuala ya eda ni mahali pa kukaa kwa mwanamke aliyetalikiwa. Ofisi ya kutoa Fatwa ya Misri imetoa Fatwa kadhaa kuhusu suala hili, ikiwa ni pamoja na Fatwa ya Sheikh / Ahmed Haridi iliyotolewa tarehe ya 15 mwezi wa Rabi’l Akher mwaka wa 1385 AH, sawa tarehe 12 mwezi wa Julai mwaka wa 1965, ambapo ilitajwa katika swali kuwa: mwanamume amemtaliki mkewe talaka isiyo rejewa baada ya kujaaliwa watoto watano wadogo, na yeye alikuwa akiishi pamoja naye wakati wa ndoa katika nyumba yake, baada ya talaka mke aliiacha nyumba hii na akakaa katika nyumba ya familia yake, kisha akarejea nyumbani kwake na kuomba kuishi pamoja naye kwa nia ya kutunza watoto wake tu. Mwanamume huyo akaomba kujua hukumu ya kisheria kuhusu suala hili, Je, inaruhusiwa kwa muulizaji aliyetajwa kuishi pamoja na mke wake wa zamani aliyetalikiwa katika nyumba moja kwa kisingizio cha kuwatunza watoto wao? Je! Kuna matini inaharamisha kuishi kwao katika nyumba moja? Sheikh akajibu kwamba: “Kinachotajwa kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu ni kwamba kama mwanamke ametalikiwa na mume wake talaka isiyo rejewa atakuwa kama mgeni kwake na haruhusiwi kwake kuchanganyika naye, lakini atakaa eda yake katika nyumba ya ndoa, na ni lazima kuwepo kizuizi kati yao kinachozuia kukutana kwao kama wanandoa na kinachozuia fitna, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jingine baada ya haya.} [AT TWALAAQ:1]
Vile vile Mwenyezi Mungu amesema: {Wawekeni humo humo mnamo kaa nyinyi kwa kadiri ya pato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwadhiki. Na wakiwa wanamimba, wagharamieni mpaka wajifungue. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwengine} [AT TWALAAQ: 6]. Allaah amewaagiza waume wasiache wake zao kutoka nyumbani mwao na kuwaagiza wake wenyewe wasiondoke. Suala hili linahusika mke aliyetalikiwa talaka rejea na isiyo rejewa, kama muda wa eda yake umekwisha, lazima aondoke katika nyumbani ya eda na kwenda nyumbani kwake au nyumba ya familia yake, kwa sababu sheria ya Kiislamu imeharamisha kuchanganyika na wanawake wasio maharimu. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasioneshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasioneshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafuwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo husu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.} [AN NUUR: 31]. Ilitajwa katika Sahih ya Muslim kuwa Mtume, S.A.W., alisema: "Jihadharini na kuingia wanawake", Mtu mmoja kutoka Al-Ansari akauliza ewe Mtume wa Allaah: Je, nikikaa pamoja na shemeji yangu au ndugu wa mume wangu? Mtume akasema: “Shemeji ni mauti”. Shemeji ni mmoja wa jamaa za mke au mume asiye miongoni mwa maharimu, ikiwa hali hii ni kwa mtu wa karibu asiye miongoni mwa maharimu, basi ni hali ile ile kuhusu mwanamume asiye karibu kama vile mume ambaye aliyemtaliki mke wake talaka isiyorejewa na akawa mgeni kwake, basi kwa muulizaji asikae pamoja na mke wake wa zamani aliyetalikiwa na hairuhusiwi kwake kukutana naye au kuishi pamoja naye katika nyumba moja baada ya kukaa eda yake hasa katika wakati huu ambapo ufisadi umeenea, kama mchunga anayechunga pembezoni mwa mpaka, huhofiwa kuingia ndani yake. Ama kuhusu kuwatunza watoto isiwe sababu ya kupelekea kufanya jambo hilo la aibu ambalo linakanushwa na sheria, na Mwenyaezi Mungu amehakikisha kutunzwa kwa watoto kupitia kumlazimisha mume atoe matumizi kwao, kuwalea na kuwaelimisha”.
Wanavyuoni wa madhehebu manne ya Kiislamu wameafikiana kuwa mwanamke aliyetalikiwa ni lazima kukaa eda yake katika nyumba ya ndoa ikiwa nyumba hii ni ya mume au ya mwingine, kama mke akitalikiwa alipokuwa mbali na mumewe ni lazima arudi kwake mara moja na asitoke isipokuwa kwa udhuru, na hekima ya kukaa mke eda yake katika nyumba ya ndoa ni kumhimiza kila mmoja wa wanandoa akumbuke baraka ya ndoa na asiisahau. Vile vile baadhi ya wanavyuoni wanasema kuwa hali ya kukaa kwa wanandoa katika nyumba moja wakati wa kukaa eda labda inamfanya mume kujutia kumtaliki mke wake, na pengine atamrejea tena, basi hali hiyo ni rahisi zaidi.
Ni wajibu kwa mke aliyetalikiwa talaka rejea kukaa katika nyumba ya ndoa, na dalili yake ni aya hii: {Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi amejidhulumu nafsi yake Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya} [AT TWALAQ: 1]
Vile vile iliyopokelewa kutoka kwa wenye Sunan kutoka kwa Zainab binti Kaab Ibn Ujrah na alikuwa mke wa Abu Sa'eed Al-Khudarey kwamba dada yake Al-Furaiah binti Malik alisema: mume wangu alitoka kwa ajili ya kuwasaka watumwa wake waliotoroka waliokimbia, alipowafikia wakamuua, nikapata habari ya kifo chake nilipokuwa katika nyumba ambayo ni mbali ya Al-Ansar ambayo ni nyumba ya familia yangu na ndugu yangu, mume yule aliyekufa hakuacha chochote wala hakuacha nyumba, kama unaona inafaa kuniruhusu niende nyumbani kwa familia yangu na ndugu yangu, basi hilo litakuwa jambo jema kwangu. Mtume S.A.W. akasema: "Fanya upendavyo", yule mke wa marehemu akasema: nikatoka kwa furaha kutokana na kauli ya Mtume S.A.W. Nilipokuwa msikitini au nilipokuwa katika nyumba moja, niliitwa na Mtume S.A.W. akaniambia “Umefanyaje?” Nikamwambia nilivyofanya, kisha akaniambia: "Kaa ndani ya nyumba yako, ambayo ulipata habari ya Msiba wa mumeo, mpaka eda yako imalizike", mke akasema: nilikaa katika nyumba ile miezi minne na siku kumi.
Vivyo hivyo, haruhusiwi mwanamke aliyetalikiwa talaka rejea kutoka nyumba ya ndoa isipokuwa kwa umuhimu unaoonekana. Wanavyuoni wa madhehebu manne ya Kiislamu wameafikiana hivyo.
Al-Marghinani anasema katika kitabu cha Al-Hidayah: "(Haruhusiwi kwa mwanamke aliyetalikiwa talaka rejea au isiyorejewa kutoka nje ya nyumba yake wakati wa usiku na wala wakati wa mchana), kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: {Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi.},” Al-Babrtiy anasema akieleza kuwa: “(Haruhusiwi kwa mwanamke aliyetalikiwa talaka rejea au isiyorejewa kutoka nje ya nyumba) ambayo alikuwa ndani yake wakati wa kutalikiwa kwake isipokuwa akilazimishwa, kama vile akiogopa kuanguka au akaogopa juu ya nafsi yake mwenyewe au fedha zake au kama akifukuzwa na watu wa nyumba hiyo kwa sababu anakaa katika nyumba ya kodi na yeye hawezi kulipa kodi ya nyumba hii” [4/343, Dar Al-Fikr].
Al-Kharashi anasema katika maelezo yake juu ya kitabu cha Mukhtasar Khalil: “Mwanamke aliyetalikiwa au aliyefiwa mumewe anakaa kama alivyokaa pamoja na mumewe, yaani: anakaa katika nyumba yake ya ndoa, na kama ikiwa atakaa katika nyumba nyingine kabla ya kutalikiwa au kabla ya kufiwa mumewe atarudiwa katika nyumba yake ya kwanza ili akae eda yake, na mumewe atatuhumiwa kuwa alitaka kuondoa haki ya mkewe katika kukaa eda yake katika nyumba ya ndoa, na eda ni haki ya Mwenyezi Mungu.” [4/156, Dar Al-Fikr]
Al-Nawawi anasema katika kitabu cha [Ar-Rawdhah]: “Mwanamke anayekaa eda yake na aliyestahili kukaa katika nyumba ya ndoa anakaa ndani ya nyumba ile ambapo alikaa wakati wa kutalikiwa isipokuwa kama kuna kikwazo, na hairuhusiwi kwa mume wala kwa familia zake kumfukuza kutoka katika nyumba ya ndoa, na hairuhusiwi kwa mke kutoka nje ya nyumba ile” [8/410, Al-Maktab Al-Islami].
Vile vile Al-Nawawiy anasema katika kitabu cha “Al-Manhaj”: “Mwanamke anayekaa eda yake kwa ajili ya kutalikiwa au kufiwa mumewe ni lazima kukaa katika nyumba ya ndoa aliyokaa wakati wa kutalikiwa isipokuwa mwanamke aliyeonesha uasi wake kwa mumewe, na hairuhusiwi kwa mume wala kwa familia zake kumfukuza kutoka katika nyumba ya ndoa, na hairuhusiwi kwa mke mwenyewe kutoka nje ya nyumba ile” [uk 256, Dar Al-Fikr].
Al-Bahwatiy Alisema katika kitabu cha: [Kashaful Qina], “Ni lazima mwanamke aliyefiwa mumewe akae eda katika nyumba ambayo eda imewajibika (ndani yake nayo ni) nyumba (ambayo mume wake alipokufa na mwanamke bado anaishi ndani yake) ... (kama akitaka) aliyetaliki (kumweka mwanamke humo katika nyumba yake) au nyumba nyingine, ambayo ni nzuri kwa ajili yake (ili kuhifadhi kitanda chake lazima mwanamke kumtii); kwa sababu haki ni yake mume na madhara ni juu yake pia, basi ilikuwa na uchaguzi wake kama haki nyingine (na kama si lazima juu ya mume matumizi ya mwanamke aliyemtaliki kwa sababu ya jambo la shaka au ndoa batili) ni lazima juu ya mwanamke kukaa humo (na kuhusu mwanamke aliyetalikiwa talaka rejea ni lazima kukaa eda yake katika nyumba ya ndoa kama anavyokaa mwanamke aliyefiwa mume wake) na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe} iwapo mume amempa ruhusa atoke au hakumpa; kwa sababu hali hi ni haki ya eda nayo ni haki ya Mwenyezi Mungu pekee yake, mume hawezi kuondoa haki moja miongoni mwa haki zake. [Kashaful Qina’ 5/431 na kurasa zijazo baada yake, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Ingawa wanavyuoni walikubaliana juu ya uwajibu wa kuishi mwanamke aliyetalikiwa talaka rejea katika nyumba ya ndoa, lakini walimruhusu kukaa eda yake nje ya nyumba ya ndoa katika baadhi ya hali, hali hizi ni pamoja na dharura au udhuru, baadhi ya wanavyuoni wameeleza udhuru huo ambapo wengine hawakuueleza.
Imam An-Nawawiy anasema: “Ni lazima juu ya mwanamke aliyetalikiwa talaka rejea kukaa eda yake katika nyumba ya ndoa na hatoki nje isipokuwa kwa dharura au udhuru, na kama akitoka basi ametenda dhambi, na juu ya mume wake kumzuia, na kama mume amekufa basi kwa warithi wake kumzuia mke kutoka nje ya nyumba ya ndoa, lakini anasamehewa katika baadhi ya hali:
Miongoni mwa hali hizi ni: Kama akiogopa juu ya nafsi yake mwenyewe au akiogopa juu ya mali zake kutokana na uharibifu au kuungua moto au kuzama basi anaweza kutoka nje ya nyumba ya ndoa, iwapo katika nyumba hii ni eda ya kufiwa mume au eda ya talaka, na pia ikiwa nyumba haikulindwa vizuri na akiogopa wezi, au akiishi kati ya watenda-maovu na anaogopa au anaudhiwa na majirani au jamaa za mumewe wasio miongoni mwa maharimu, au kama akiwatukana kwa maneno machafu, yanayo ruhusiwa kumtoa katika nyumba ile, kisha katika kitabu cha Al-Tahdhiib: kama akiwatukana jamaa za mumewe wasio miongoni mwa maharimu hana haki ya kukaa eda yake katika nyumba ya ndoa na juu yake kukaa eda nyumbani mwa familia yake. Kisha mahali pa kumhamisha kwa sababu ya uovu wake kama jamaa za mumewe wasio miongoni mwa maharimu wanaishi pamoja naye katika nyumba kubwa lakini kama wakiishi katika nyumba ndogo mume anaweza kuwahamisha jamaa zake na kuacha nyumba kwa mke, na kama jamaa za mume wanaishi katika nyumba nyingine hairuhusiwi kwa mume kumtoa mke katika nyumba ya ndoa kwa sababu ya uovu wake. Al-Mitwalliy ametaja kuwa inaruhusiwa mke kutolewa katika nyumba yake ya ndoa kama akiwaudhi majirani au jamaa za mume wasio miongoni mwa maharimu. Kwa hili kama akiwa katika nyumba ya jamaa za mumewe katika vijiji hatolewi katika nyumba yake ya ndoa kwa sababu ya uovu wake kama nyumba yao si karibu na nyumba yake. Lakini kama uovu unatokana na jamaa za mumewe wanatolewa katika nyumba yake ya ndoa. Kama mke anaishi katika nyumba ya wazazi wake; kwani mume alikuwa anaishi pamoja nao na mke akiwatukana kwa maneno machafu au wazazi wake wamemtukana hawatolewi katika nyumba yao, kwa sababu uovu hauendelei kati yao, na kama jamaa za mume wake wapo katika nyumba ya wazazi wake na amewatukana kwa maneno machafu wanatolewa katika nyumba hii kwa sababu mke ana haki katika nyumba hii ya wazazi wake.
Vile vile kama akihitaji kununua chakula au pamba au kuuza uzi n.k., kama mke huyo ametalikiwa talaka rejea basi yeye ni mke wake na ni lazima juu ya mume wake kukidhi haja zote za mkewe na hairuhusiwi kwa mke kutoka nje isipokuwa kwa idhini yake tu. Kuhusu mke aliyetalikiwa talaka isiyo rejewa kuna maoni mawili: hatoki nje, na maoni ya pili ni: anaruhusiwa kutoka nje kama aliyefiwa mumewe.
Miongoni mwao hali hizi pia ni: akihitaji kukaa eda yake ambapo yeye yupo katika nyumba ya vita, ni lazima kuhamia nyumba ya Uislamu. Al-Mitwalliy amesema: isipokuwa katika mahali ambapo haogopi, wala haogopi juu ya dini yake, basi hatoki nje mpaka kukaa eda yake.
Pia: Kama akitakiwa haki, basi akiweza kulipa haki hii kutoka nyumba yake kama vile deni au amana anaweza kuilipa, lakini kama akitakiwa kwenda kwa hakimu kwa ajili ya hukumu au kiapo kwa kutuhumiwa anaweza kutoka kama alizoea hivyo halafu atakaa eda yake, lakini kama hakuzoea kutokakwenda kwa hakimu anaweza kumtumia naibu au kumleta mwenyewe.
Vile vile kama nyumba ya ndoa ilikopwa au kukodishwa basi imerejeshwa na mwenye nyumba ameiomba ni lazima mke atoke nje.
Pia kama mke ni Bedui anaweza kutoka nje ya nyumba na kusafiri na watu kama wakisafiri.
Tawi: Hasamehewi katika kutoka nje kwa malengo yanayozingatiwa kuwa maongezeko yasiyo muhimu, kama vile kuwazuru watu, kuimarisha, uzalishaji mali kwa biashara, na kuharakisha kuhiji n.k. [Ar-Rawdhah: 8/415].
Imam An-Nawawiy amehisabu baadhi ya udhuru unaoruhusisha kukaa eda nje ya nyumba ya ndoa, udhuru huo ni kama mfano tu ili kujua kiasi cha udharura unaoruhusisha kukaa eda nje ya nyumba ya ndoa, na kama tukitazama kwa maoni ya Imam An-Nawawiy katika hali halisi ya kisasa, tutaona kuwa wanawake wengi waliotalikiwa hawawezi kabisa kukaa eda katika nyumba ya ndoa, na ukitazama udhuru wa kwanza katika maneno ya Imam An-Nawawiy utajua ukweli wa kile tunachosema.
Jibu hili linahusiana na sehemu ya kwanza ya swali la mwenye kuuliza, nalo linalohusu kukaa eda nje ya nyumba ya ndoa.
Kuhusu sehemu ya pili ya swali hili linalohusu kukaa pamoja na mke aliyetalikiwa, tunajibu kwamba mke aliyetalikiwa talaka rejea ni mke au ni kama mke sawa sawa kufuatana na makubaliano ya wanavyuoni, na jibu la swali hili linategemea tofauti katika talaka rejea, je aina ya talaka hii inaondolea mkataba wa ndoa au la, pia aina hii ya talaka inategemea namna gani kurejea, je, ni lazima talaka kutokea au ni lazima kuitamka?
Wanavyuoni wa umma wanaamini kuwa talaka ya rejea haiondoi mkataba wa ndoa na kutokana na hivyo haiharamishi ngono na mambo yaliyo chini yake. Pia Wanavyuoni wa umma wanaona kwamba kurejea hutokea kwa kutenda vitendo vya ndoa, na wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Abu Hanifa, Maliki, na Ahmad Ibn Hanbal wote wanaona hivyo isipokuwa kila madhehebu ina maelezo yake kuhusu suala hili, kwa hivyo talaka rejea haimzuii mume kukaa pamoja na mke wake aliyemtaliki, kama akifanya ngono na mkewe katika siku za eda akamrejea, Lakini wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Maalik walisema kuwa ni lazima mume kunuia kumrejea mkewe kwa ngono au kwa vitendo ambavyo ni chini yake.
Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Shafiy wamesema kuwa: mke aliyetalikiwa talaka rejea ni mgeni, na ni sharti kutamka neno linalomaanisha kuwa amemrejea, na hairuhusiwi kwa mume kukaa pamoja naye katika nyumba moja; kwa sababu mwanamke huyo akiwa kama mkewe lakini katika suala la kutoanza mkataba mpya, na si maana yake kuhalilisha yaliyoruhusiwa kwa wanandoa.
Ingawa waliyoyasema wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Abu Hanifah kuhusu kukaa kwa mume pamoja na mke aliyemtaliki, walisema pia suala hili linachukiza.
Ibn Abidin anasema: “(Talaka rejea haiharimisha kufanya ngono) kinyume na wanavyosemwa na wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Shafiy R.A. (kama Akifanya ngoni hana dhambi); kwa sababu ni ruhusa (lakini inachukiza kukaa pamoja pekee yao) (kama hanuii kumrejea au) haichukizwi. Imetajwa katika kitabu cha Al-Bahr kutoka kwa kitabu cha Al-Badaai’ kwamba: wanavyuoni walisema kuwa mume anaruhusiwa kumpiga mkewe kwa sababu ya kuacha kujipamba na hali ile ile kwa mke alitalikiwa talaka rejea” [3/409, Dar Al-Fikr].
Sheikh Al-Dardeer katika kitabu cha “Asharhul Saghiir” alisema: “(na) mke (aliyetalikiwa) talaka rejea ni (kama mke) kuhusu uwajibu wa matumizi yake, mavazi yake, kukaa kwake, na kumtaliki pia (isipokuwa katika kufanya ngono au kukaa pamoja naye peke yake) na (kula pamoja naye) pasipo na nia ya kumrejea basi hairuhusiwi” [2/614, Dar Al-Ma'arif]
An-Nawawiy amesema katika kitabu cha: [Ar-Rawdhah]: “Inaharimishwa kwa mume kukaa pamoja na mkewe aliyemtaliki katika siku za eda; kwani hali hii inapelekea kukaa pamoja naye pekee, na kukaa pamoja naye pekee ni kama kukaa pamoja na mwanamke mgeni, isipokuwa katika hali mbili tu: ya kwanza: kuwa katika nyumba pamoja nao mwanamume miongoni mwa maharimu wa mke, au mwanamke miongoni mwa maharimu wa mume, au katika maana ya maharimu, kama mke mwingine au kijakazi, na ni lazima kuwa maharimu na ambaye katika maana yake kupambanua, hairuhusiwi kuwa mwenye wazimu na mtoto asiyeweza kupambanua. Imam Shafiy R.A. aliweka sharti nalo ni kubaleghe. Al-Qadhi Abu At-Twayeb alisema: kwa sababu ambaye hakubaleghe hakukalifishwa kwa hivyo hawezi kukataa mambo maovu. Sheikh Abu Hamed alisema: kwangu inatosha kuhudhuria kijana tu, na wanawake ambao ni kama maharimu, na inatosha kuhudhuria mwanamke mmoja mwenye imani thabiti, na mwenye kitabu cha Al-Shamil aliafikiana na mtazamo huu pia. Na hadithi ya kundi la wanavyuoni (Al-Ashaab) ambao wamesema kuwa hairuhusiwi kwa wanamume wawili kukaa pamoja na mwanamke mmoja pekee yao, lakini inaruhusiwa kwa mwanamume mmoja kukaa pamoja na wanawake wawili wenye imani thabiti pekee yao; kwa sababu mwanawake anastahi mwanamke mweigine zaidi kuliko mwanamume anayestahi mwanamume mwingine. Vile vile inadhihirika kwamba kukaa kwa mume na maharimu na ambaye katika maana yake inadhaniwa kama nyumba ni kubwa, lakini kama nyumba siyo kubwa ni lazima kuachwa kwa mke anayekaa eda yake pekee yake. Na kama hali ya kukaa mume pamoja na mke aliyetalikiwa katika siku za eda inaruhusiwa kwa sababu ya kuwepo kwa maharimu basi kuchukizwa bado kwa sababu inadhaniwa mume anamtazama mke. Hali ya pili: Kama katika nyumba kuna chumba kimoja na mmoja wao alitaka kukaa katika chumba hicho na mwingine anataka pia, kama viambatisho vya nyumba ni jikoni, ukumbi, kisima, na ngazi mpaka paa katika nyumba ile ile hairuhusiwi isipokuwa tu kwa sharti ya kuwepo kwa maharimu, na kama viambatisho ndani ya chumba inaruhusiwa kama vyumba viwili na nyumba mbili ambazo ni karibu” [8/418].
Ni Wazi kutokana na mtazamo wa Imam Shafiy kwamba kutokaa kwa mume pamoja na mke aliyemtaliki talaka rejea kwa sababu ni kama mwanamke mgeni kwake. Na ufahamu kauli ya Al-Nawawi aliposema: “Na kama hali ya kukaa mume pamoja na mke aliyetalikiwa katika siku za eda inaruhusiwa kwa sababu ya kuwepo kwa maharimu basi kuchukizwa bado kwa sababu inadhaniwa mume anamtazama mke.”
Al-Mardaawiy alisema katika kitabu cha “Al-Inswaaf” wakati akizungumza juu ya talaka rejea: kauli yake: (na ni halali kwa mume wake kufanya ngono naye, kukaa pamoja naye pekee yao, kusafiri pamoja naye, na kwa mke kujipamba kwa mume) na madhehebu hii inakubaliwa na wengi wa wanavyuoni “Al-Ashaab” [9/153, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi].
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu: inaruhusiwa kwa mke aliyetalikiwa talaka rejea kukaa eda yake katika nyumba ya mumewe, na hairuhusiwi kwake kutoka nje isipokuwa katika hali maalumu -kama ilivyotajwa hapo juu- lakini kwa sababu kesi nyingi za talaka katika wakati wetu hazitokei kwa mujibu wa sheria, ambayo inahitaji kuwa kuachana kuwa kwa wema na pasipo na madhara yoyote, lakini hutokea katika hali ya migogoro na ugomvi watu kwa mazoea wanaona ubaya wa kukaa mke aliyetalikiwa katika nyumba ya mumewe hata ikiwa talaka rejea, na tunaona baada ya kuangalia kesi za talaka kwamba mke aliyetalikiwa talaka rejea ana haki ya kukaa eda yake nje ya nyumba ya ndoa, hasa kwamba mtazamo huu ni mtazamo wa madhehebu ya Imam Abu Hanifa ambayo tunafuata katika sheria ya familia. Na imetajwa katika marekebisho ya sheria ya familia nambari (100) ya mwaka 1985 kwamba hukumu za kisheria zinazohusu hali ya familia kama hazitolewi kwa maneno yake basi zinahukumiwa kwa mujibu wa mitazamo iliyosahihi zaidi kwa mujibu wa madhehebu ya Abu Hanifa, isipokuwa hukumu zile zilizosamehewa. Mtazamo wa Abu Hanifa umetangulizwa, na ni mtazamo uliochaguliwa vile vile.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas