Mahali pa Kukaa Eda kwa Aliyefiwa n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mahali pa Kukaa Eda kwa Aliyefiwa na Mumewe na Hana Nyumba.

Question

Mke aliyefiwa na mumewe na hana nyumba ya ndoa atakaa eda yake wapi? Kama vile kukaa katika hoteli au baada ya kumalizika muda wa kukodisha nyumba, kwa mfano. Je mke anaruhusiwa kuuza nyumba ya ndoa kabla ya kumalizika muda wa kukaa eda yake? Na katika hali hii atakaa eda yake wapi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu. Sifa zote njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya utangulizi huo:
Eda katika sharia ni kipindi maalumu anachokaa mwanamke kwa ajili ya kujua uwezekano wa kuachwa na mimba, hali hiyo inatokea kwa kuzaa, idadi ya twahara na miezi. Neno la eda linatokana na idadi, na limekuwa ni sharia kwa ajili ya kuhifadhi nasaba na kumhifadhi mwanamke mwenyewe kutokana na kuchanganyika na kwa ajili ya kulinda haki ya wanandoa na mtoto, na asili yake imechukuliwa kutoka katika Aya za Qur'ani, Hadithi za Mtume na makubaliano ya wanavyuoni. Kama ilivyokuja katika kitabu cha: [An-Najm Al-Wahaj 8/123, Dar Al-Minhaj].
Kwa mwanamke ambaye amefiwa na mumewe hukaa katika nyumba ya ndoa kwa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi mine na siku kumi} [AL BAQARAH 234], kwa kufiwa mume lazima mke kuomboleza, kwa maana hukaa katika nyumba ya ndoa hadi mwisho wa eda yake, lakini kuna hali ambazo hakuna nyumba ya ndoa, kama aliyeishi katika nyumba ya kukodi na kodi yake ikaisha, au kubomoa nyumba, au alikuwa anaishi katika hoteli, katika hali hizi swali linaulizwa: inapaswa kwa mke kuomboleza au la?
Wanavyuoni wa zamani wamezungumza juu ya suala hili kwenye nyanja zote za maisha, na walikubaliana kuwa ni muhimu kwa mke aliyefiwa na mumewe kukaa katika nyumba kwa jumla, lakini walitofauti katika baadhi ya maelezo ya jambo hilo, je, itachukuliwa gharama za makazi kutoka katika mirathi au ni lazima mke kulipa kutoka katika fedha zake, au hukumu hii inaondolewa kwani sababu yake imeondolewa?
Dalili ya hivyo kutoka katika Qur'ani ni: {Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi mine na siku kumi. Na wanapo timiza eda yao basi hapana ubaya kwao kwa wanao jifanyia kwa mujibu wa ada. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda.} [AL BAQARAH 234].
At-Twabariy alisema: “Na kauli yake:{wangoje peke yao}, ina maana: wanakaa pekee yao wakiomboleza mbali na waume na mapambo na kuondoka kutoka makazi ambayo walikuwa wanakaa katika maisha ya waume zao miezi minne na siku kumi, isipokuwa wao wakiwa ni wajawazito watakuwa juu yao kukaa nyumbani mpaka kujifungua, na wakijifungua, basi eda zao zitakuwa zimetimia.” [Jamii Al-Bayaan 5/79, Muasastur Risalah].
Al-Qurtwubi alisema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “{wangoje} maana ya kuongojea ni: kuwa na utulivu, subira katika ndoa, na kutotoka nje ya nyumba ya ndoa, na hasa katika usiku.” [Al-Jamii LiAhkaam Al-Quran 3/176, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Dalili kutoka katika Hadithi za Mtume S.A.W. ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Zainab binti Kaab Ibn Ugrah, kwamba Furai’ah binti Malik Ibn Sinan, naye ni dada ya Abu Sa'id Al-Khudary, "Nilimwambia kuwa amekuja Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., akimwuliza kuhusu kurudi kwa familia yake katika Bani Khadrah, na kwamba mumewe alikwenda kuomba watumwa waliokimbia, akauwawa nao, alisema: Nilimwuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., kuhusu kurudi katika familia yangu, kwani mume wangu hakuniachia nyumba wala pesa, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., alisema: Ndiyo, alisema Basi, nikaenda, hata nilipokuwa katika chumba, au katika msikiti, Mtume wa Allah S.A.W., aliniita, nikamjia akasema: Je, umesemaje? Nilisema: nilimsimulia hadithi niliyoitaja kuhusu mume wangu, alisema: kaa katika nyumba yako mpaka eda ifike mwisho wake", mke akasema: nilikaa katika nyumba ile miezi minne na siku kumi, mke alisema, wakati wa ukhalifa wa Othman alinitumia, akiniuliza kuhusu jambo hilo, nikamwambia, akafuata hivyo na akahukumu hivyo." Imepokelewa kutoka kwa wenye Sunan, Al-Tirmidhiy akasema: Hadithi hii ni hasana na sahihi, na wameifanyia kazi Hadithi hii wengi wa wanavyuoni miongoni mwa masahaba wa Mtume, S.A.W., na wengine, hawakupokea kwa mwenye eda kuondoka katika nyumba ya mumewe mpaka amalize eda yae, wote hawa wanaona kwamba mke anayekaa eda yake haruhusiwi kutoka nyumbani mwa mumewe mpaka kutimiza eda yake. Vile vile mtazamo huu ni wa Sufian Al-Thauri, Ahmad, Ishaq, na baadhi ya wanavyuoni wa maswahaba wa Mtume, S.A.W. na wengine: kwa mwanamke kukaa eda yake popote anapotaka, hata asipokaa eda yake katika nyumba ya mumewe, mtazamo wa kwanza ni sahihi zaidi”.
Abu Omar Ibn Abdul-Barr alisema: “Hadithi hii ni maarufu na inajulikana kwa wanavyuoni wa A-Hijaz na wa Iraq kwamba mke aliyefiwa mumewe ni lazima kukaa eda yake katika nyumba yake na hatoki nje, na mtazamo huu ni wa wanavyuoni wa Fiqhi katika Al-Hijaz, Sham, Iraq na Misri, miongoni mwao Imam Malik, Shafiy, Abu Hanifa na wafuasi wao na Al-Thauri Al-Awzai na Al-Laith Ibn Saad, vile vile ni kauli ya Omar, Othman, Ibn Umar, Ibn Masoud na wengineo.” [Al-Tamhiid 21/31, Wizarat Umum Al-Awqaf wal-Shuun Al-Islamiyah - Morocco]
Kama ikithibitika hivyo, ni lazima kukaa eda katika nyumba hiyo ya ndoa, ni sawa ikiwa inamilikiwa na mumewe au ya kukodi au imeazimwa, kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W aliposema kwa mke: "kaa katika nyumba yako", na hakuwa katika nyumba inayomilikiwa na mumewe. Kama ikionekana haja ya kumhamisha mke kutoka katika nyumba ambayo ni lazima kukaa eda yake ndani yake, anaweza kuhamia nyumba nyingine, kama mwanamke huyo anajihofia uharibifu au adui, au alijitokeza mwenye nyumba akamfukuza, kama nyumba iliazimwa au kukodishwa na muda wa kukodisha umemalizika, au akizuiliwa kukaa katika nyumba yake, au alitakiwa kulipa pesa zaidi.
Au kama hana kodi ya nyumba, au hana kodi isipokuwa kutoka fedha zake tu, inaruhusiwa kwake kuhamia nyumba nyingine, kwa sababu ana udhuru, na halazimishwi kulipa kodi ya nyumba, lakini analazimishwa kukaa nyumbani, sio kupata nyumba, na kama akiwa na udhuru, wajibu umeondoka, na anaweza kukaa popote anapotaka, kwa sababu wajibu umeondolewa kwa udhuru, na Sharia haikutaja badala yake, basi haipaswi, kama Hija ikiondolewa kwa sababu ya kutokuwa na uwezo na pia kutohakikisha masharti yake, vile vile anayejitenga msikitini kwa ibada kama hana uwezo wa kukaa msikitini. Mtazamo huu ni wa wafuasi wa madhehebu ya Imama Ahmad Ibn Hanbal.
Ibn Qudaamah alisema: “Mke aliyefiwa mumewe, analazimiswha kukaa eda yake katika nyumba yake aliyo kaa wakati mume wake alipokufa, kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Rurai’a binti Malik Ibn Sinan, dada yake Abu Said: "Amekujia Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., akimwuliza kuhusu kurudi kwa familia yake katika Bani Khadrah, na kwamba mumewe alikwenda kuomba watumwa waliokimbia, akauwawa nao, alisema: Niliuliza kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., kurudi katika familia yangu, kwani mume wangu hakuniachia nyumba wala pesa, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., alisema: Ndiyo, alisema Basi, nikaenda, hata nilipokuwa katika chumba, au katika msikiti, Mtume wa Allah S.A.W., aliniita, nikamjia alisema: Je, umesemaje? nilisema: nilimsimulia hadithi niliyomtajia kuhusu mume wangu, alisema: kaa katika nyumba yako mpaka eda ifike mwisho wake", mke akasema: nilikaa katika nyumba ile miezi minne na siku kumi, mke alisema, wakati wa ukhalifa wa Othman alinitumia, akiniuliza kuhusu jambo hilo, nikamwambia, akafuata hivyo na akahukumu hivyo)).” Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud, At-Tirmidhiy akasema:. Hadithi hii ni hasani na sahihi. Kama mke akijihofia uharibifu au kuzama au adui, au amefukuzwa na mwenye nyumba, au hakuweza kuishi katika nyumba isipokuwa kwa kulipa kodi tu, basi anaweza kuhamia popote anapotaka, kwa sababu wajibu umeondolewa kwa udhuru, na Sharia haikutaja badala yake, basi si vibaya, na hana badala ya kodi, hata kama akiweza kuilipa; kwa sababu analazimishwa kukaa nyumbani tu, sio kupata nyumba ya kukaa”. [Al-Kafi 3/207, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Kutolazimishwa makazi kwa mali ya urithi - kama alivyotajwa katika madhehebu ya Imam Shaafi- kwa sababu zilizotajwa hapo juu, na kwani Aya iliyotajwa ilitaja eda tu na haikutaja makazi, na kama ingelikuwa ni wajibu yangetajwa, kama ilivyoelezwa katika talaka kwa kusema: {Msiwatoe katika nyumba zao}.
Kwani kama tukiwajibisha makazi kwa mali ya mirathi kama hakuna nyumba, hali hii itapunguza sehemu ya warithi, ambayo wakati mwingi inafuata sharia maalumu, na kwa hivyo, suala hili ni lazima kufuata sharia ya mirathi, ili pasiwe na upinzani baina yao.
Kama tukikubaliana kwa mtazamo wa madhehebu ya Hanbali na rai iliyochaguliwa kutoka madhehebu ya Imam Al-Shafi na warithi wamefanya bidii kwa ajili ya kumpatia mke nyumba kwa ajili ya kutunza nasaba analazimishwa kukubali.
Al-Omrani alisema: “Kama tukisema kwamba: mke haipaswi kuwa na makazi, kama warithi wakichangia kumpatia nyumba kwa ajili ya kutunza nasaba, analazimika kukaa katika nyumba waliyompatia kama inafaa kwa ajili ya kukaa, lakini kama hawakuchangia na mtawala akaona kuwa maslahi yake ni kumlipia kodi ya nyumba kutoka hazina ya Waislamu, kwa ajili ya kutunza nasaba, anaweza kufanya hivyo, kwani maslahi ni hayo, na kama akifanya hayo, mke analazimika kukaa ndani ya nyumba hii, kwa sababu jambo hili linahusiana na kutunza nasaba. Na kama warithi hawakuchangia wala mtawala hakumlipia, basi mke anaweza kuishi popote anapotaka” [Al-Bayaan 11/61]
Wanavyuoni wa madhehebu ya Abu Hanifa wamegeuza suala hili wakisema kuwa ni lazima kumpatia mke kodi ya nyumba kutoka katika mirathi ya mume aliyefiwa akiwa hana nyumba, mtazamo huu pia ni wa madhehebu ya Imam Maliki.
Hili suala jibu lake limetanguliwa hapo juu, inaweza pia kusemwa kwamba nyumba ni sababu ya uwajibu, naye mke hatakiwi kujipatia nyumba.
Al-Sarkhasiy alisema: “Katika eda ya kifo kulipa kodi ya nyumba ni jukumu la mke kwa sababu halazimishi mumewe kumpatia makazi hali hiyo hiyo kwa matumizi, kama akiwezeshwa kukaa nyumbani kwa kulipa kodi anayoweza kuilipa, basi ni wajibu juu yake kukaa, na kama hana uwezo wa kuilipa anaweza kuhamia nyumba nyingine, kwa sababu kukaa kwake katika nyumba hii ni haki ya Sharia, kama akiweza kuilipa kodi yake basi hana budi kukaa, hali hiyo hiyo kama msafiri akipata maji kwa bei yake, kama akiwa na uwezo wa kulipa basi hana haja ya kutayamamu, na kama hana uwezo wa kulipa bei ya maji anaweza kutayamamu… Na kama mke yuko katika nyumba ya mumewe, na mumewe alifariki kama sehemu yake ya mirathi inamtosha basi ni wajibu juu yake kukaa kutoka katika mirathi yake wakati wa eda, na hairuhusiwa kwake kukaa pamoja na asiye maharimu kwake miongoni mwa warithi wa mumewe. Na kama mirathi yake haimtoshi basi kama warithi wa mumewe wakiridhika kukaa katika nyumba atakaa lakini kama wakikataa atakuwa na uwezo wa kuhamia nyumba nyingine kwa mujibu wa udhuru wake. Na kama akiwepo katika nyumba ya kutisha juu ya nafsi yake au pesa zake na hana mwanamume alikuwa na uwezo wa safari, kwani hali ya kutisha haiwezekani, na kuna madhara kwa nafsi yake na pesa zake na hali hii ina udhuru unaoondoa haki ya Sharia, kama akiwa kati yake na maradhi ya macho au adui, na kama hofu inaweza kubadilika kwa kuhamia nyumba nyingine anaweza kuhamia.” [Al-Mabsuut 6/33, 34, Ch. Dar Al-Maarifa]
Sheikh Ileesh alisema: “(kwa) mke (aliyefiwa na mumewe) aliyekuwa ameshaolewa naye ana (makazi) wakati wa kukaa eda yake (kama) mume (akijamiiana naye) kama akikaa pamoja naye au la (na) hali ni kwamba (nyumba ni wajibu kwa mke) ikiwa ikimilikiwa na mume (au) ni ya kukodishwa au kwa (fedha) yaani mume akalipa kodi yake kabla kifo chake, na kama mume akilipa baadhi ya kodi yake anaweza kukaa kwa muda aliolipia, na kama muda umemalizika kabla ya kumalizika kwa eda yake basi warithi hawana haja ya kulipa kodi inayobaki na mke anaweza kuilipa kutoka kwa pesa zake yeye”. [Manh Al-Jaliil 4/330, Dar Al-Fikr].
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu inadhihirika kwamba, mke aliyefiwa na mumewe anakaa eda yake katika nyumba ya ndoa, ikiwa hakuna nyumba warithi au mtawala anawajibika kumpatia nyumba - inayofaa kwa mfano wake - ili akae eda ndani yake, na kama hakuna nyumba, anaweza kukaa eda mahala popote anapotaka.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi


 

Share this:

Related Fatwas