Kuambatanisha Deni na Thamani.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuambatanisha Deni na Thamani.

Question

Ikiwa mkopeshaji wa paundi za Kimisri ameweka sharti la kulipwa deni lake pamoja na kuchunga thamani ya pesa na nguvu yake ya kununulia ambapo inakadiriwa wakati wa kukopa kiwango cha dhahabu inayowezekana kununuliwa kwa pesa iliyokopeshwa, kisha mkopeshaji analazimisha wakati wa kulipwa pesa iwe sawa na bei ya kiwango kilekile cha dhahabu, na hilo ni badala ya kujitokeza baadhi ya pesa zengine kwa kuhofia kushuka nguvu yake ya kununua kufuatana na wakati, ni ipi hukumu ya sharia ya Kiislamu?  

Answer

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa Njema za Mwenyezi Mungu, na Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake, na Masahaba wake, na waliomfuata. Na baada ya hayo:
Ukweli wa deni kwa sura iliyotajwa kupitia swali unaonesha kuwa ni makubaliano mawili yaliyokuja katika muundo wa masharti mawili kwa sababu asili ya makubaliano: Ni mkopo sawa na fedha iliyokopwa lakini mkopo huo una masharti mawili:
Sharti la Kwanza: Kulazimisha mkopeshaji kulipwa deni kwa thamani ya dhahabu sawa na bei ya soko ya siku mkopo ilipotolewa.
Sharti la Pili: Kumlazimika mkopaji kuwa wakili wa mkopeshaji kulipa dhahabu inayohitajika – wakati wa kulipa deni – kisha katika kuiuza kwa bei ya soko siku ya kulipwa kwake kwa fedha sawa na mkopo huo: Kwa maana ya kutoangalia kufanana kwake katika kiwango chake cha idadi ikiwa ni chenye kuhesabika, au ujazo ikiwa ni wenye kupimika kwa, au uzito ukiwa ni wenye kupimika kwa uzito, na mara nyingi kunatokea ongezeko si la kisharia na kutouwiana na upande huu, na huonekana kwa baadhi ya watu kuwa ongezeko hilo ni sahihi hakuna dhuluma kwa mkopaji, lakini kilichopo ni kuondoa dhuluma kwa mkopeshaji kwa kufahamu kudondoka kwa nguvu ya ununuzi na sarafu, ambapo kiuchumi inafahamika kama tatizo la mfumuko wa bei ikiwa ni chenye kuwezekana kununulika kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita kwa mfano paundi mia ambapo kwa sasa haiwezekani kukinunua chini ya mia mbili, hii inaonesha kuwa kinyume chake pia ni sahihi, kwa sababu ikiwa itaongezeka thamani inakuwa kwa mkopaji analipa fedha ndogo zaidi ya ile aliyokopa kwa upande wa idadi au kipimo, wakati ambapo inakuwa ni sawa na mkopo kwa upande wa maana thamani na nguvu ya kununua, ambayo ni manufaa yanayokusudiwa katika asili ya kumiliki thamani na sarafu.
Lakini mwelekeo huu hata kama utaonesha ni wenye kukubalika kiakili na wenye kulenga kufikia usawa na mfanano kati ya deni na badala yake kadiri itakavyowezekana, isipokuwa wenyewe unagongana na kile kilichoelezewa na andiko la kisharia na misingi asili ya kifiqih, kwani makubaliano kwa sura yake ya kukutana kwa mkopo na kuuza kwa uwakala ni jambo la haramu kisharia, kwa katazo la Mtume S.A.W., kuuza na kukopesha na kuuza vitu viwili kwa uuzaji mmoja, kutoka kwa Abdillah Ibn Amru amesema: Amesema Mtume S.A.W.,: (Si halali kukopa na kuuza, wala masharti mawili katika uuzaji, wala faida isiyokusanya, wala kuuza kitu usichokuwa nacho).[Imesimuliwa na wenye Sunani nne].
Na mkopo unaingia kwa mauzaji kwa maana ya ujumla; kwa Kukopa mwanzo ni kuazima, kwa tamko lake mwishowe linafaa kuwa mbadala, yaani ni mbadala wa mkopo mfano wake au kadiri ya thamani yake, na hii ni kutokana na wanazuoni waliposema kwamba mapatano ya mkopo ni mbadala mali kwa mali kwa kuafikiana baina ya wawili na hii ni kutokana na maoni ya ya baadhi ya wafuasi wa Hanafiya, wakasema: "Na dhana hii inaambatana na mkopo pia" [Kitabu cha Al-Shalabi juu ya kuzibainisha hakika 4\2, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy].
Na akasema Ibn Aabideen katika kitabu chake cha: [Ad-durru Al Mukhtaar 5/161 Ch. Dar Al Kutub Al-Elmiyah]: “Kukopa mwanzo ni kuazima, kwa tamko lake mwishowe linafaa kuwa mbadala, na hili haiji kwa kitu kisichokuwa chenye mfano”, pindi mkopaji anaporejesha kile alichokopa, wakati huo makubaliano humalizikia kwenye mbadala wa deni mfano wake au thamani yake, kwa hili wamesema wanachuoni kuwa makubaliano ya deni mwanzo ni kujitolea mwisho ni mbadala, kwa hili lenyewe huingia katika maana jumla ya mauzo, kukutana kwake uwakala na uuzaji – hata kama utakuwa kinyume na sharia – kunapelekea kuingia kwenye makatazo ya kuuza vitu viwili kwa kimoja, hayo yamesemwa pia na baadhi ya watu wa Abu Hanifa katika maelezo juu ya uelewa uliotolewa na mtunzi wa kitabu cha Kanzu ad-dakaaik kuhusu uuzaji kuwa: Ni mabadilishano ya mali kwa mali kwa njia ya ridhaa, wakasema: “Uelewa huu unaelezea pia kuhusu mkopo” [Kitabu cha: HashiyatuS Alaa Tabyiin Al-Hakaaik 4/2 Ch. Dar Al-kutub Al-Islaamiyah].
Amesema Ibn Abideen katika kitabu chake cha: [Ad-Durru Al-Mukhtaar 5/161, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Mkopo mwanzo ni kuazima, mwisho imefaa kuita badala, kwa sababu haiwezekani kunufaika nalo isipokuwa ni kwa kutumia mkopo wenyewe, inalizimisha kupata mfano, na hili haliji katika kitu kisichokuwa na mfano” pindi mkopaji anapolipa mfano wa kile alichokopa, humalizikia wakati huo makubaliano kuwa mbadala. [Kitabu Al-Kawaaid kwa Ibn Rajab Uk: 74 Ch. Dar Al-Fikri, na Fathu Al-Qadeer kwa Ibn Al-Himaam 6/523 Ch. Dar Al-Fikr]
Vilevile ukopeshaji wenye kupelekea manufaa unaingia katika katazo, kwa sababu uwakala wenye masharti ya mkopo wenye manufaa ya ziada ya kile kilicho lazima kulipa, amesema haafidh Ibn Abdulbarr katika kitabu cha: [Al-Kaafiy Fii Fiqh Ahlu Al-Madinat 2/728, Ch. Maktabat Ar-Riyaadh Al-Haditha]: Wala haifai mtu kukopa kitu na kuzidishiwa kile alichokopa au kunufaika mkopeshaji kutokana na alichokopesha ima kiwe kidogo au kingi kwa namna moja au nyingine, na kila ongezeko katika mkopo au manufaa anayonufaika nayo mkopeshaji hiyo ni riba ni haramu ikiwa imekuwa ni sharti”.
Katika makubaliano haya pia kuna shaka ya ulaji riba kwa kuitaji uwakala katika uuzaji usiokuwa wa kisharia wa dhahabu iliyokadiriwa na mkopo, kwa sababu lau itakamilika uuzaji wa dhahabu kama ilivyowekwa sharti inakuwa ni uuzaji wa bidhaa mbili kwa moja au uuzaji na ukopeshaji, ikiwa hakuna dhahabu iliyouzwa utajo wake katika makubaliano unakuwa ni hila ya kula riba.
Kisha katika kukadiria deni kwa dhahabu au kitu chochote cha madini mengine ni uharibifu mwingine, nayo ni kuwa madini hivi sasa kama vile dhahabu na fedha yamekuwa sehemu ya bidhaa ya biashara ambayo bei yake hubadilika kwa kupanda na kushuka kila wakati kutokana na uwepo wa bidhaa na kuhitajika kwake kwenye masoko ya fedha ya kimataifa na yale ya ndani, kwani dhahabu na madini ya fedha hayana kipimo thabiti inawezekana kukirejea katika kupangilia thamani ya vitu, jambo lenye kumaanisha kuwa kuliunganisha deni na hivyo vipimo kunapelekea mkopeshaji na mtakaji mkopo kuingia kwenye hasara ya wazi isiyotarajiwa hasa ikiwa kiwango cha mkopo ni kikubwa, jambo linaloonesha kuwa mashirikiano haya yanakusanya udanganyifu na ujinga, na kupelekea ugonvi na mvutano, ambapo kwa ujumla wake kunapingana na makusudio matakatibu ya sharia katika kuleta uhuru wa mashirikiano na uwazi wa haki na wajibu, ikiwa kuepuka uharibifu mbaya na tofaotu pamoja na mivutano kati ya pande mbili, kwani kuondoa mivutano ni muhimu, ambapo ni mada ya uharibifu, kwa sababu hii imekuwa udanganyifu wa uhakika na ni lazima kwa Waislamu kwa lengo la kuufikia umuhimu huo. [Kitabu cha: Badaaii As-Swanaaii 5/143, 7/2 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya], anasema mwanachuoni Al-Kuraafy katika kitabu cha: [Al-Furuuk 3/290 Ch. Aalam Al-Kutub]: “Na hii hapa kanuni nayo ni kuwa kile kinachohitajika na sharia ni maslahi na kuondoa uharibifu na fitina mpaka lifikie hilo kwenye kauli ya Mtume S.A.W.: "Hamtoingia Peponi mpaka mpendane".
Wanachuoni wa Kiislamu wanagawa mali sehemu kuu mbili: Mali yenye mfano na mali ya thamani. Mali yenye mfano: Ni mali yenye mfano wake ndani ya soko pasi ya kuwepo tofauti iliyozoelekea, nayo katika hali ya kawaida: Ima (ya ujazo) kwa maana ya kukadiriwa kwa kipimo cha ujazo kama vile unga wa ngano, ngano mzima na mfano wake, au yenye kupimwa kwa uzito kama vile madini ya dhahabu fedha chuma na mfano wake, au mali ya (kipimo cha mita) kama vile aina za mavazi ambayo hayana tofauti kati yake, au mali ya kuhesabika kwa idadi kama vile fedha na vitu ambavyo hukadiriwa kwa idadi.
Na mali ya thamani: Nayo ni mali isiyokuwa na mfano sokoni, au ina mfano sokoni lakini pamoja na kuwepo tofauti iliyozoeleka kwenye thamani, na imeitwa aina hii ni katika mali yenye thamani ikinasibishwa na thamani ambayo hutofautiana kwa kila mtu na mwengine, na katika mfano wa mali ya thamani: Ni vitu vyote vyenye kubadilika kwa upande wa aina au thamani au vyote viwili kwa pamoja, kama vile wanyama wa aina moja waliotofautiana ikiwa ni katika aina ya farasi ngamia ng’ombe na mbuzi, na kama vile vitu vyenye kutengenezwa kwa mikono miongoni mwa mapambo vyombo na fanicha za ndani na mfano wake miongoni mwa vitu vyenye utofauti kwa kila mtu kwa vitu hivyo kwa kuwa na sifa isiyokuwepo kwa mwengine, mpaka kwake inakuwa na thamani maalum.
Mali ya mfano wakati mwengine hubadilika na kuwa mali ya thamani, kama vile ikiwa kwa watu ni mara chache kupatikana au kukosekana kabisa kwenye masoko, kama vile baadhi ya vilivyotengenezwa zamani na sarafu za kale kama mabaki ambazo hazitumiki na zina thamani ya kiistaarabu na kihistoria, mfano wa mazingatio kama haya huondoka mali kutoka mzunguko wa mali zenye mfano na kuwa kwenye mzunguko wa mali ya thamani, vilevile hubadilika mali ya mfano na kuwa mali ya thamani ikiwa sifa zitabadilika kama vile kuwa na kasoro au kwa upande wa matumizi na yasiyokuwa hayo, kwa mabadiliko haya huondoka sifa ya mfanano wake zile zilizopo sokoni kwa kupungua thamani yake, kama vile inavyofahamika hivi sasa kwa upande wa vyombo vifaa na magari baada ya kutumika.
Wanachuoni wa fiqih wamesema kuwa deni linalazimika kulipwa kwa mfano wake na kwa mali yenye mfano wake, na ulipaji wa thamani katika mali zinazo kadiriwa kwa thamani, kwa mujibu wa rai ya mwenye kusema inafaa kuikopesha.
Watu wa Abu Hanisa wametoa ufafanuzi wa mali kuwa: Ni makubaliano maalum yanayoelezea kutoa mali yenye mfano kwa mwengine ili kulipa mfano wake.
Akasema Al-haskafii katika kitabu cha: [Ad-Durru Al-Mukhtaar 5/161, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “(Inafaa) kukopesha (katika mali ya mfano) ni kila mali yenye sifa ya mfano wakati wa kutumika (na wala si katika isiyokuwa hiyo) katika mali za thamani, kama vile wanyama, kuni, nyumba na kila chenye tofauti, kutokana na ugumu wa kurudisha mfano wake”.
Anasema Al-Kasany katika kitabu cha: [Badaaii As-Swanaaii 7/395, Ch. Dar Al Kutub Al-Elmiyah]: “Miongoni mwake – kwa maana ya masharti ya kitu cha kukopa – kiwe miongoni mwa vile vyenye mfano kama vile vyenye kupimwa kwa ujazo, au kwa uzito na kwa idadi, wala haifai kukopa kitu kisicho na mfano wake kama vile vya kupimwa kwa mita, na kwa idadi inayokaribiana, kwa sababu hakuna njia ya kurudisha kitu wala kurudisha thamani, kwa sababu hutekelezwa kwa mvutano, kwa tofauti ya thamani kutokana na kutofautiana kutathmini kwa wana tathmini, na kuonekana kuwa wajibu ni kurudisha mfano, inahusisha kufaa kwake kwa ile mali yenye mfano”.
Wametaja kuwa kuweka sharti la kurudisha mali ya mfano sawa na mkabala wa thamani yake huzingatiwa ni mchezo haijazoeleka wala haiathiri kukubalika mkataba wa kukopa wala katika yanayowajibisha, amesema mwanachuoni As-Sarkhasiy katika kitabu cha: [Al-Mabsuutw 14/30, Ch. Dar Al-Maarifah]: “Ikwa atasema: Nikopeshe dirhamu kumi kwa dinar moja, akampa dirhamu kumi basi anadaiwa mfano wake, pasi ya kuangalia kupanda kwa dirhamu, au kushuka kwake, vilevile kila chenye kupimwa kwa ujazo au kwa uzito, ambapo kinakabidhiwa kwa njia ya mkopo ni kile kilicho na mfano, na kila chenye kuwa na mfano na kinafaa kutaka mkopo, na mkopo haufungamani na kufaa kwa masharti, kilicho haribika masharti hakibatilishi mkopo, lakini huondolewa sharti la kurejesha kitu kingine, na mkopaji anapaswa kulipa mfano wa kilicho kabidhiwa”.
Ufupi wa maelezo haya ni kuwa, ulazima katika mkopo wa vitu vyenye mifano ni kurudisha mfano wake, mwenye kutakiwa thamani hatoiangalia madamu tu mfano wake haujakatika, wala hatoangalia wakati wa kulipa mfano wake kupanda kwa bei wala kushuka kwake, ni lazima kulipa mfano wa idadi kwa mali ya kuhesabika kwa idadi, na kwa uzito wa ujazo kwa mali ya kupimwa kwa ujazo, na kwa uzito wa kilo kwa zenye kupimwa kwa kilo, na mfano wa hivyo pasi ya kuzingatia thamani, ama ikiwa mkopeshaji ameweka sharti kwa maana ya kuongeza zaidi ya hiko kilichokopwa hilo ni haramu kwa kauli za wanachuoni.
Amesema Haafidh Ibn Abdilbarr katika kitabu “at-tamhiid lima fil muwat-twa minal maany wal asaaneed” [4/68 Ch.Wizara ya Waqfu na Mmambo ya Kiislamu – Morocco]: “Waislamu wamekubaliana kwa kunukuu toka kwa Mtume wao S.A.W., – kuwa kuweka sharti la kuongeza kwenye mkopo ni riba hata kama kinacholipwa ni kingi au kidogo kama alivyosema Ibn Masuud”.
Na anasema Al-Kassaaniy katika kitabu cha: [Badaaii As-Swanaaii 7/395, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Ama yule anayarejea kwenye mkopo huo huo: basi huo mkopo wala usiwe na manufaa, ama ukiwa nayo basi haifai, mfano wa mtu amekopesha dirham nyingi kwa makubaliano ya kulipa malipo sahihi, au amekopesha na kuweka sharti kulipa pamoja na manufaa au faidi, kutokana na hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W., – kuwa amekataza mkopo wenye faida, kwa sababu faida iliyowekewa sharti kwenye mkopo ni riba, kwa sababu hiko kiwango ni ongezeko lisilolipwa kwa mbadala, na kujikinga na riba ya kweli na ile inayofanana na riba ni jambo la lazima. Hii ikiwa faida imekuwa ni sharti katika mkopo”, kwa maelezo haya haifai sharti la kuchunga thamani ya mkopo wa paundi wakati wa kulipa bali chenye kuchungwa ni idadi yake maadamu muamala haujakatika.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia, inaonesha wazi kuwa haifai kuweka sharti kwa mkopeshaji dhidi ya anayetaka mkopo, kuunganisha mkopo wa kitu chenye mfano kwa thamani au nguvu ya manunuzi kwa upande wa bidhaa nyengine au sarafu nyengine ambapo huangaliwa badala ya idadi kwa vitu vya kuhesabika kwa idadi au uzito wa kilo kwa vyenye kupimwa kwa uzito au kipimo cha ujazo kwa chenye kupimwa kwa ujazo, na hilo ni kutokana na kufungamana na kuingia kwenye katazo la kuuza na kukopesha na katazo la kuuza mara mbili katika uzo moja, vile vile yale yaliyokubalika na Waislamu juu ya uharamu wa kukopesha kitu na kupelekea faida kwa mkopeshaji.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas