Je Rehani ni Mikataba ya Kujitolea ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je Rehani ni Mikataba ya Kujitolea au Ina Malipo?

Question

Je Rehani ni makubaliano ya kujitolea au kuna malipo? 

Answer

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa Njema za Mwenyezi Mungu, na Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake, na Masahaba wake, na waliomfuata. Na baada ya hayo:
Mwanadamu wakati mwingine ni huhitaji mkopo kwa ajili ya mahitaji yake pamoja na kumiliki baadhi ya mali ambayo hapendi kuiuza, basi hekima ya uhalali wa rehani au bondi ni pamoja na kurahisisha mtu kama huyu kupata mali ili kukidhi mahitaji yake, ambapo bondi au rehani wakati huo huo inapelekea hali ya utulivu kwa mwenye mali kwenye mali yake na hufanya haraka kumsaidia mtu pasi ya kuwa na wasi wasi wowote wa kupotea kwa mali yake, kwa sababu bondi ni makubaliano yenye kudhamini deni lake.
Kumekuwa na maelezo tofauti kuhusu maana ya neno bondi au rehani kwa wanachuoni wa fiqihi, kwa sababu ya tofauti zao katika hukumu ya bondi na wajibu wake pamoja na masharti yake na mengineyo.
Wafuasi wa Imamu Abu Hanifa wameilezea bondi kuwa ni: Kuzuia kitu kwa uhalali kidini kinachowezekana kutumika. Kitabu cha: [Al-Bahru Ar-Raiq Sherehe ya kitabu kanzu Al-Daqaiq kwa Ibn Najeem 6/62 Ch. Dar Al-Kitabu Al-Islaamiy]
Kwa upande wa Wafuasi wa Imamu Malik yeye ameelezea bondi kuwa ni: Kitu kinachoweza kutumiwa na mtu mwenye kukimiliki na anachoweza kukiuza au kukiwekea kiwango kinachoweza kuuzwa au kisicho na dhamana, ikiwa kutakuwa na sharti hilo kwenye makubaliano. [Kitabu cha: Taaju wal ikleel 6/538 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] Hii ni kutokana na kuruhusu kwao kitu kisichokuwa na dhamana katika uwekaji bondi.
Watu wa Imamuu Shafiy wanaona kuwa bondi ni: Kuifanya mali ikawa dhamana ya deni ikatumika mali hiyo wakati unapokuwapo ugumu wa kulipa. [Kitabu cha: Mughny Al-Muhtaaj 3/38 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Kwa watu wa Imamu Hambali wanaona kuwa bondi ni: Mali inayofanywa dhamana ya deni ili kulipa thamani ya deni ikiwa kutatokea uzito wa kulipwa kwake kwa yule mwenye kudaiwa. [Kitabu Al-mughny kwa Ibn Qudama 4/215 Ch. Dar Ihyaau At-Turaath Al-Arabiy].
Ni wazi katika maelezo haya kuwa bondi ni dhamana ya deni ili mwenye kuweka bondi mali yake aweze kulipa deni lake.
Mikataba au Makubaliano yanagawanyika sehemu tatu:
Makubaliano ya Kulipia: Nayo ni yale yanayokuwa kwa msingi wa kuanzisha haki na wajibu kati ya wenye kuingia makubaliano kama vile kuuza na kukodisha.
Makubaliano Kujitolea: Nayo ni makubaliano yanayosimama kwa msingi wa kuhurumiana kwa kupeana msaada toka kwa mmoja kwenda kwa mwengine, kama vile kutoa zawadi na kukodisha.
Makubaliano yenye maana ya kujitolea kwa hatua za mwanzo na kulipa kwa hatua ya mwisho: Kama vile mkopo na udhamini kwa amri ya mwenye kudai, na kutoa kwa sharti la mbadala, mwenye kukopesha huwa anajitolea kwa hatua ya kwanza kumsaidia mwenye kutaka mkopo, na mdhamini kwa amri ya mwenye kudai ni mwenye kujitolea kutekeleza udhamini wa deni kwa mdaiwa, na mwenye kutoa kwa sharti la malipo pia anajitolea kwa kile anachotoa, lakini pindi mkopaji anaporudisha kile alichokopa, na udhamini unaondoka kwa mdaiwa kwa kile kilicholipwa, na mwenye kutoa anachukua mbadala kwa aliyepewa sawa na kile alichopewa – hapo makubaliano yanakuwa yamekwisha kwa kufanyika malipo. [Kitabu al-qawaaid cha Ibn Rajab uk 74 chapa a Dar al-fikri. Na kitabu Fathul Qadeer kwa Ibn Al-Himamu 6/523 Ch. Dar Al-Fikr].
Inatofautiana hukumu ya makubaliano ya mbadala kwa maana ya malipo na yale makubaliano ya kujitolea kwa kila kinachopaswa kutekelezwa kwa wale wanaokubaliana katika makubaliano yenye malipo kama vile uuzaji ukodishaji na mafano wa hayo ambapo ni lazima, ikiwa yatakamilika kwa usahihi masharti yake, hilo ni kufanyia kazi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Timizeni ahadi} [AL MAIDAH: 01].
Kwa sababu kukosekana kutekelezwa ni kuna madhara kwa upande mmoja makubaliano, kwa kupoteza juhudi alizotoa mkabala na malipo, tofauti na makubaliano ya kujitolea, kama vile kutoa kitu bure kumiliki bila ya malipo mkopo usio na malipo usia na mfano wa hayo, si lazima kulipa kwa kile kilichofayika makubaliano kwa kujitolea bure, kwa sababu ni katika wema na kwa watu wema hawana sababu ya kulipwa, pamoja na upambanusi wa makubaliano mbalimbali. Pamoja na hayo wanachuoni wameeleza kuwa inapendeza kufanyika makubaliano ya kujitolea, kwa sababu yenyewe ni katika mambo mema, Sharia imehimiza kufanyiana wema katika maeneo mbalimbali. Mwenyezi Mungu Amesema: {Na saidianeni katika wema na uchamungu} [AL MAIDAH: 02], haya ni kwa upande wa jamhuri ya wanachuoni. Ama kwa upande wa Imamu maliki na wafuasi wake, wao wanaona ni lazima kufanyika makubaliano ya kijitolea, kwani kumiliki bila malipo kwa muda fulani kwao ni wajibu mpaka pale utakapo malizika muda. [Kitabu cha: Hashiyatu Dusouqiy kwenye Sherhu Al-Kabeer 3/439 – 442, Ch. Dar Al-Fikr], kama ilivyo ni lazima kwao kukubalika kilichotolewa bure, ikiwa atajizuia huyu mwenye kutoa bure kukabidhi alichokitoa basi atalazimishwa. Kitabu cha: [Jawahir Al-Ekleel Sherehe ya Mukhtasar Khaleel 2/212 Ch. Dar Al-Fikr].
Malipo kwenye makubaliano yenye malipo sharti zake ni kuwa malipo yenye kufahamika, kama vile thamani ya kitu, na malipo ya kukodi na mfano wa hayo, isipokuwa katika malipo ya urafiki na malipo ya kujivua, kwani kutokujua kwake hakubatilishi, kwa sababu yenyewe ni mrejesho wenye kufahamika, nao ni mfano wa mahari. Ama makubaliano ya kujitolea yenyewe hayana malipo, kwa sababu ni hakuna makubaliano na kidogo kutofahamika, kwa sababu makubaliano haya yanajengeka kwa wepesi na uwezo.
Wanachuoni wa Imamu Abu Hanifa, Shafiy na Hambali wanasema kuwa, makubaliano ya kuweka bondi ni makubaliano ya kujitolea, wala hawajatofautiana kati ya kuwa kwake ni sharti katika makubaliano mwanzoni au hapo baadaye baada ya kuthibitika haki. Zailaii katika wafuasi wa Imamu Abu Hanifa amesema katika [kitabu cha: Tabiyeen Al-Hakaaik 6/63 pamoja na kitabu cha Shalaby Ch. Dar Al-Kutubi Al-Islaamiy]: “Bondi hailazimiki kujibu na kukubali, kwa sababu yenyewe ni kujitolea kama vile kutoa kitu bure au sadaka”].
Na katika [kitabu cha Ahmad Shalaby katika kitabu cha: [Tabyeen Al-Hakaik]: “Nguzo ni kula kutikia tu, kwa sababu kujitolea kunakamilika kwa mwenye kujitolea kama vile kutoa kitu bure”. Na wakatoa sababu ya hilo kuwa bondi hailazimishi kitu chochote kwa kile kilichothibiti kwa muwekewa bondi].
Anasema Rafiy katika watu wa Imamu Shafiy katika [kitabu cha Fathu Al-Azeez Sherehe ya Al-Wajeez 10/58 Ch. Dar Al-Fikr]: “Ni sharti kwa wenye kukubaliana: kuingia gharama ni kama ilivyo katika mauziano, lakini bondi ni kujitolea, ikiwa itafanyika kwa watu waliojitolea basi inakuwa ni hivyo”].
Na anasema al-bahuuty mfuasi wa Imamu Hambali katika [Kitabu cha Kas-Shaaf Al-Qinaai 3/322 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Inafaa kuweka bondi kwa yule mwenye kufaa kuuza na kujitolea, kwa sababu kujitolea ni jambo si la lazima”. Na mwenye kufanya kisichokuwa lazima kufanywa kwake basi atakuwa amejitolea.
Ama kwa upande wa Maliki, ni wazi kupitia ibara zao kuwa ikiwa kimewekewa sharti katika makubaliano basi si cha kujitolea, ikiwa baada ya makubaliano na kuthibiti haki basi hiyo ni kujitolea au sehemu ya kujitolea. [Katika kitabu cha Dusuuqy kwenye Sherhul Kabeer 3/231, Ch. Dar Ihyaa At Turaath Al-Arabiy]: “Inafaa kwa mtu mwenye kujitambua mjinga na mtumwa, inafaa kwa kutumia msImamuizi wao, kwa maana ikiwa imewekwa sharti katika makubaliano ya kuuza au kukopa, kinyume na hivyo basi kujitolea kulikokuwa batili”.
Anasema Al-Adawy katika [kitabu chake juu ya Sharhe ya Kharshy 5/236, Ch. Dar Al Fikr]: “Inafaa kwa mtu mwenye akili ya kujitambua” kwa maana imekuwa ni sharti katika asili ya mkataba, kinyume na hivyo inakuwa ni batili kwa sababu inakuwa ni sehemu ya kujitolea”.
Haya yameelezewa na kadhi na kuzidisha maelezo ya sababu za watu wa Abu Hanifa ya kuwa bondi ni makubaliano ya hiyari, anasema katika [kitabu cha: Takmilatu Fathul Qadeer 10/136, Ch. Dar Al-Fikr]: “Hakika ya bondi hata kama haitolazimisha kuwa kitu kwa mwenye kuweka bondi, lakini inalazimisha kitu kwenye kubakia, nacho ni kitu kwa mwenye kuwekewa bondi kitakachodhamini deni lake wakati wa kupotea, kwani makubaliano ya kuweka bondi si makubaliano ya kujitolea kwa sura zake zote, bali kumekuwa na maana ya malipo kwa pande zake, ambapo amekuwa huyu mwenye kuwekewa bondi na dhamani ya deni lake wakati wa kupotea kwa bondi mikononi mwake”.
Anaongeza kwa kusema: “Inapaswa kutokamilika kwa kujibu mwenye kuweka bondi peke yake, bali ni lazima kuwe na kukubali mwenye kuwekewa bondi pia, mpaka ikamilike kumilikishwa yeye kama dhamana ya deni lake ni hukumu wakati wa kupotea kama ilivyo kwenye madhehebu yetu”.
Mtazamo huo unaoungwa mkono na kauli ya Al-kasany katika [kitabu cha: Badaai Swanaaii 6/135 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: “Ama kufikia umri wa utambuzi sio sharti, vilevile kuwa huru, hivyo inafaa kwa mtoto mdogo aliyepewa ruhusa au mtumwa aliyepewa ruhusa, kwa sababu katika hilo ni katika mwendelezo wa kufanya biashara, ana miliki hilo kwa mwenye haki ya kumiliki biashara, na kwa vile bondi na kuweka bondi ni katika utekelezaji wa deni na kudhamini, na wao wanamiliki hayo”.
Anaelezea Al-Kasaany kuwa katika bondi kuna maana ya malipo, anasema kwa kutenganisha kati ya bondi na kuuza: “Sura inayoonesha tofauti ni kuwa kuuza kuna malipo moja kwa moja…[tofauti na bondi kwa sababu yenyewe haina malipo moja kwa moja, pamoja na kuwa na maana ya malipo…”. [Kitabu Badaai Swanaai 6/154].
Hili ni lazima kwa madhehebu ya Abu Hanifa wenye kusema kuwa mwenye kuwekewa bondi kunamthibitikia kitu cha dhamana, ikiwa kitaharibika mikononi mwake inakuwa malipo yamefanyika. Na katika maelezo ya Raafiy yanayokubaliana na uwazi wa madhehebu ya Imamu Maliki, anasema katika [kitabu cha: Fathu Al-Azeez ya Sharhe fupi 10/41, Ch. Dar Al-Fikr]: “Hakika ya masharti kwenye uwekaji wa bondi upo wa aina mbili: ya kwanza ni katika kadhia ya bondi, haidhuru kuweka sharti si katika bondi ya kujitolea wala bondi yenye masharti katika makubaliano”.
Kutokana na hayo, kauli yenye nguvu ni kuwa bondi ikiwa imewekewa masharti kama ya makubaliano ya kuuza au kukopa basi hiyo inazingatiwa ni kujitolea kunakoendana na malipo, na ikiwa baada ya kuthibiti kwa haki hiyo inakuwa ni kujitolea moja kwa moja.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas