Kuzitia Rangi Nyusi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuzitia Rangi Nyusi

Question

Ni ipi hukumu ya kuzitia rangi nyusi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba zake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Makusudio ya ibara ya (kuzitia rangi nyusi) ni kuziweka rangi ncha mbili za nyusi, ambapo mtazamaji hudhani kuwa nyusi ni nyembamba na nyepesi; kwa sababu ncha mbili za nyusi ya juu na ya chini zikawa hazionekani, na kwa kawaida rangi inayotumika inalingana na rangi yenyewe ya ngozi, na pengine kutiwa rangi juu ya nyusi zote kwa rangi ya ngozi, kisha zinachorwa kwa kalamu nyusi nyembamba na nyepesi; na pengine michoro hii inatumika kwa njia ya kupiga sindano (Chale) ambayo inajulikana sana kwa (tatoo); na pengine unatumika unga wa madawa na rangi za viwandani, na makusudio ya hayo yote ni kupata urembo tu.
Lakini kama rangi hii inatumika kwa kupiga sindano (Chale) basi ni haramu kabisa, na mwenye kufanya hivyo amelaaniwa, na ni mwenye kufanya dhambi kubwa. Na dalili ya hili ni kama ilivyopokelewa katika Vitabu Sahihi vya Sunna vya Bukhari na Muslim, kutoka katika Hadithi ya Ibn Umar, kuwa mtume S.A.W, anasema: “Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kuunga na mwenye kuungwa (nywele), na mwenye kupiga chale na mwenye kutaka kupigwa chale”. Na kitisho cha laana ni alama ya kuwa dhambi hiyo ni kubwa.
Na kama rangi hii inatumika kwa mada za mapambo kama vile rangi za viwandani, hakika mtazamo wa Fiqhi una tofauti kuhusu msingi wake, na kwa kufuata hukumu yake. Ni dhahiri kuwa msingi wa tofauti ni mambo mawili: Kwanza: je inakatazwa kufanywa; kwa kuwa ni sababu ya kuzichonga nyusi? hakika kuzitia rangi nyusi kwa kutumia mada za viwandani zinazojulikana, ambapo nywele za nyusi hazirejei katika hali yake ya kawaida bali huzidi kutokana na uwingi wa nywele, na kuimarisha mizizi yake, na hii hupelekea kuziondosha ziada, na hii ndiyo ni hali ya kuzichonga nyusi. Pili: Je kuzitia rangi nyusi ni miongoni mwa maana ya kuzichonga nyusi na sifa zake, kwa hiyo huchukua hukumu yake au la?
Kuhusu ya kwanza: iliyotahadharishwa na kuhofiwa, nayo ni ziada ya ukubwa wa nywele, na hilo si jambo la kawaida wala la kuainishwa, kwa kuwa kuitekeleza sababu hutegemea kuwa itapelekea lililokatazwa kwa yakini au kwa mara nyingi.
Kuhusu ya pili: Kauli ya kuwa kuzitia rangi nyusi ni aina ya kuzichonga nyusi, na hiyo inategemea kujua mambo haya mawili ni aina moja au la kwanza linalingana na la pili kwa njia ya Qiyasi. Linalokubaliwa na wanazuoni wa Madhehebu Nne kuwa kuzichonga nyusi kunaambatana na nyusi tu, mbali na mabaki ya uso, kisha walikubaliana, isipokuwa wafuasi wa madhehebu ya Hanbal, itekeleze kwa kunyonyoa au mfano wake miongoni mwa njia za kuziondosha, kinyume na wafuasi wa madhehebu ya Hanbal ambao wanaiainisha kuwa ni kunyonyoa, na siyo njia nyingine. [Rejea: Fat-h Al-Qadiir; 6/426, Ch. ya Dar Al-Fikr; Tuhfat Al-Muhtaj: 6/315, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy; Sharh Kifayat At-Talib Ar-Rabaniy; 8/83, Ch. ya Dar Al-Fikr; Sharh Muntaha Al-Iradaat; 1/53, Ch. ya A’alam Al-Kutub].
Kuna mtazamo wa kuelekea kuwa: Je makusudio ya hali ya kuziondosha yanaambatana na kuzifanya nyusi ziwe nyembembe, au ni hali ya kuziondosha tu bila ya kuwa nyembemba?
Wengi wa wanazuoni, isipokuwa wafuasi wa madhehebu ya Hanbal, walitaja kuwa ni kuziondosha pamoja na kuwa nyembamba, na Ibn Al-Humam katika kitabu cha [Fat-h Al-Qadiir] anasema: “Mwenye kuchonga nyusi ni yule anayenyonyoa nyusi kwa ajili ya kuwa nyembamba”. [6/426]; na katika kitabu cha: [Al-Mjmuu’ na An-Nawawiy: “mwenye kuchonga nyusi ni yule anayechukua sehemu ya nywele za nyusi na kuifanya nyembamba ili iwe nzuri’. [3/141]; na katika kitabu cha [Hashiyat Al-jamal]: “Mwanamke (Muhiddah) yaani yuko katika kipindi kinachofuata kifo cha mume, anakatazwa kunyonyoa nyusi, kwa sababu hii ndiyo ni kuzichonga nyusi”. [4/460]; na An-nafarawiy mfuasi wa madhehebu ya Malik katika kitabu cha [Al-Fawakih Ad-Dawaniy] anasema: “kuzichonga nyusi ni kuzinyonyoa nywele za nyusi ili ziwe nyembamba na nzuri”. [2/314].
Kuhusu kauli ya kuwa Qiyasi ya kuzitia rangi nyusi kwa kuzichonga nyusi ni sahihi, kauli hii inaundwa kwa kuelewa sababu ya kuharamisha kwa kuzichonga nyusi, ambayo ni tofauti. Na kurejea Vitabu vya Fiqhi vya Madhehebu Nne, tunaona kuwa wao walitofautiana katika kuainisha sababu; wanazuoni wa madhehebu ya Hanafi walitaja kuwa sababu ni kuonesha mapambo, na kwa mujibu wa hayo haiharimishwi ila katika hali ya mapambo; na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Shafiy na ya Hanbal walitaja kuwa sababu ni kughushi; na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy wanaona kuwa sababu ya kuharamisha ni kusababisha udhuru; na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Hanbal wanasema kuwa: Ni alama ya mafasiki; na baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa sababu ni kubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu, na dalili ya hayo ni muktadha wa Hadithi ya Ibn Masu’ud: “Mwenyezi Mungu amewalaani wenye kupiga chale, na wenye kupigwa chale, na wanaochonga nyusi, na wanaochonga meno, wakaacha mwanya kwa sababu ya uzuri, wanaobadilisha maumbile aliyoyaumba Mwenyezi Mungu…”. [Muttafaq].
Kwa kuchukuliwa kuwa sababu ya kukataza kuzichonga nyusi ni kudhuru mwili, hakika hayo hayadhihiriki katika hali ya kuzitia rangi nyusi, hasa katika hali ya maendeleo ya ufundi wa watu wanaoshughulika na kazi hii.
Na kuhusu maelezo ya baadhi ya wanazuoni kuwa kuzichonga nyusi ni alama ya mafasiki au inabadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu, hakika hii haisihi iwe maelezo, lakini ni miongoni mwa hekima zenye faida kwa kuelewa kusudio la kukataza, na siyo sababu ya lazima. Kwa hiyo kundi la wanazuoni waliyapinga maelezo kama haya, miongoni mwao ni Al-Qarafiy na Al-A’adawiy wafuasi wa madhehebu ya Malik; katika kitabu cha: [Adh-Dhakhirah] na Al-Qarafiy: “Ilivyotajwa katika Hadithi kuhusu kubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu, hakika sikuifahamu maana yake, kwa sababu mabadiliko kwa ajili ya uzuri hayakanushwi kisheria, kama vile: tohara, kukata kucha na nywele, kupaka Hina, kupaka nywele, na mengineyo”. [13/315; Ch. ya Dar Al-Gharb Al-Islamiy; Taz. Hashiyat Al-Adawiy Ala Al-Kifayah: 2/459]
Na At-Twahir Ibnn A’ashuur katika Tafsiri yake anasema: “Hayazingatiwi kuwa mabadiliko ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu, inavyofanywa katika uumbaji kwa idhini ya mwenyezi Mungu, na ilivyofanywa kwa ajili ya uzuri; hakika tohara ni kubadili uumbaji wa Mwenyezi Mungu lakini kwa faida ya kiafya, kuzinyoa nywele kwa ajili ya kuepusha madhara, kuzikata kucha kwa ajili ya kurahisisha kazi za mikono, kutoboa matundu ya masikio ya wanawake kwa ajili ya kuweka hirini na urembo. Na kuhusu ilivyopokelewa katika Sunna kuambatana na kulaani wanaounga nywele, wanaochonga nyusi, wanaochonga meno kwa uzuri, hakika hayo yote miongoni mwa masuala ya kutofautiana”. Kisha alihitimu kuwa kusudio la kukataza kuwa makatazo haya yalikuwa miongoni mwa alama za mafasiki wa zama hizo, au za washirikina. [5/205, Ch. ya Ad-Dar At-Tunusiyah Linnashr], na kwa mujibu wa hayo, ni dhahiri kuwa suala la kuzitia rangi nyusi halilingani na suala la kuzichonga nyusi hata kidogo kuhusu katazo.
Na kama baadhi ya wanazuoni walielekea kuwa kuzitia rangi nyusi kuna maana ya kuonesha mapambo na aina ya kughushi, na kwa hiyo kulingana na kuzichonga nyusi kwa uharamu, kutokana na kauli ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafi na ya Shafi, kwa kuangalia kuwa madhehebu hizi mbili ziliepusha uharamu wa kuzichonga nyusi hali ya kuwa kwa ajili ya mume, na mfano wake ni kuzitia rangi nyusi. Basi jibu ni: Inapinga Qiyasi hii maelezo ya wafuasi wa madhehebu ya Shafi kumkataza (mwanamke mwombolezaji), naye ni yuko katika kipindi kinachofuata kifo cha mumewe, kuzitia rangi nyusi, kutokana na ilivyotajwa katika kitabu cha: [Sharh Al-Manhaj] na Sheikh Zakariya Al-Answariy (kwa mabadiliko machache): “kuacha kutumia rangi zinazowekwa usoni, mikononi, miguuni, kama vile zafarani n.k… na hii inakusanya vidole, paji, nywele, na nyusi”. Katika kitabu cha Al-Bijirmiy (kwa mabadiliko machache): “Na kama mwanamke Muhiddah) amekatazwa kufanya hivyo, hakika ni kwa kuwa hayo ni mapambo na siyo haramu, na hii inamaanisha kuwa inajuzu kwa asiye (Mwombolezaji) kuifanya, kwa sababu ikiwa ni haramu kimsingi, basi hakuna haja ya kuitaja katika matini.
Kwa mujibu wa yaliyotangulia: tunaona kuwa rai yenye nguvu zaidi ni: Kujuzu kuzitia rangi nyusi, kwa kuangalia vigezo vilivyotajwa hapo juu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas