Hadithi ya Mwanamke Asiye Kuwepo Mu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hadithi ya Mwanamke Asiye Kuwepo Mumewe na Hukumu ya Mchanganyiko wa Wanaume na Wanawake.

Question

Ni ipi hukumu ya mchanganyiko wa wanaume na wanawake? Ni upi udhibiti wake? Hadithi inayosema: “Baada ya siku yangu hii hairuhusiwi kuingia kwa mke asiyekuwepo mumewe isipokuwa pamoja na mwanamume mmoja au wawili”, Je Hadithi hii inaonesha kwamba unaruhusiwa mchanganyiko huu? Je! Unaruhusiwa upweke wa mwanamke mmoja na zaidi ya mtu mmoja wasio maharimu? Au upweke wa mtu mmoja na zaidi ya mwanamke mmoja? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Al-Ikhtilaat (Mchanganyiko) ni kitenzi jina la kuchanganya, na kuchanganya kitu na kingine yaani kukusanya vitu hivi pamoja [Lisan Al-Arab kwa Ibn Mandhur, kidahizo cha (Kha la ta) 2/1229, Ch. Dar Al-Maarif] Al-Ikhtilaat maana yake ni kukusanya na mkutano na kuchanganyika kwa wanaume na wanawake wasio maharimu katika mahala pamoja.
Na inaruhusiwa mchanganyiko wa wanaume na wanawake kwa mujibu wa udhibiti maalumu, na ikiwa udhibiti huu haufuatwi basi mchanganyiko huu ni haramu, na udhibiti wa kwanza ni kutokuwepo kwa upweke wa mwanamume na mwanamke, na upweke haramu ni ule upweke wa mwanamume na mwanawake wasio maharimu katika mahali ambapo hawana wasiwasi kwamba watu hawatawaona, kama vile kuwepo katika nyumba iliyofungwa milango yake na madirisha yake, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Amer Ibn Rabia kutoka kwa Mtume, S.A.W. amesema: “Wakati mtu anapoachwa peke yake pamoja na mwanamke basi shetani ni wa tatu wao”. Na ilipokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka kwa Ibn Abbas, R.A. kutoka kwa Mtume, S.A.W. anasema: “Hairuhusiwi kwa mwanaume kuachwa peke yake na mwanamke ila kwa maharimu. Mtu mmoja alisimama na kusema: Ewe Mtume wa Allah, mke wangu ametoka kwenda kuhiji, na nimejiunga katika vita kadhaa. Mtume akamwambia: rudi ili ukahiji pamoja na mkeo”.
Al-Kasaaniy Al-Hanafiy amesema: “Kuhusu hukumu ya upweke kama vile kuwepo katika nyumba mwanamke asiye maharimu au miongoni mwa jamaa ambao ni maharimu basi mwanaume haruhusiwi kuachwa peke yake na mwanamke huyo kwa kuhofia fitina na kuangukia katika haramu. Vile vile imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W, anasema: Wakati mwanaume anapoachwa peke yake pamoja na mwanamke basi shetani ni wa tatu wao. {Bada'i Al-Sanai’ 5/125, Ch. Al-Maktabatul Elmiyah}
Ibn Qudaamah amesema: “Hairuhusiwi kwa mtu kuachwa peke yake na mwanamke; kwani ni haramu, naye inaogopwa katika hali hii ya upweke kufanya tendo la ndoa, Mtume, S.A.W. amesema: “Wakati mtu anapoachwa pekee yake pamoja na mwanamke basi shetani ni wa tatu wao”. {Al-Mughni kwa Ibn Qudaamah 7/96, Ch. Maktabatul Qahira}, Al-Bahwati amesema: “Ni haramu kabisa mtu kuachwa peke yake na mwanamke pasipo na maharimu yaani kwa matamanio na bila matamanio yoyote”. [Sharhu Muntaha Al-Iradat 3/7, Ch. Dar Al-Fikr].
Kuhusu upweke wa wanaume na mwanamke wasio maharimu, na upweke wa wanawake na mwanaume, hali hii haiitwi upweke, lakini kama watu hawa hawaaminiwi basi hairuhusiwi kuchanganyika nao na kinyume cha hali hii ni sahihi.
Na kuhusu Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Muslim kwamba: Abdullah Ibn 'Amr ibn Al-Aas amesema: “Kwamba baadhi ya watu wa Bani Hashim waliingia kwa Asmaa binti Umays Abu Bakr akaingia, ambapo ni mke wake wakati huo, akawaona, akachukia jambo hilo, akamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., akasema: sijaona chochote isipokuwa kheri tu, Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. anasema: “Mwenyezi Mungu amemsafisha na visingizio hivi” kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. akasimama juu ya mimbari, akisema: “Mtu asiingie baada ya siku ya leo, kwa mwanamke asiyekuwa na mumewe, ila pamoja na mtu mwingine au wawili”. Hadithi hii inaonesha kwamba inaruhusiwa upweke wa mwanawake na mwanaume zaidi ya mmoja akiwa na mtu mwingine kwani kunakosekana upweke haramu wakati huu, pia inaonesha kuwa imeruhusiwa mchanganyiko unaodhibitiwa kwa vidhibiti vya kisheria vifuatavyo.
Abu Abbas Al-Qurtubiy Al-Malikiy amesema: “Baadhi ya watu wa Bani Hashim waliingia kwa Asmaa binti Umays” katika wakati huo Abu Bakr R.A. alikuwa hayupo, lakini hakuwa safarani na alikuwa akifahamika ni mwema na mwenye kheri, ambapo walikuwa kabla ya Uislamu watu wema pia, lakini Abu Bakr R.A. alikana hivyo kutokana na wivu wake wa kimaumbile na wa kidini, wakati Mtume S.A.W. alipoambiwa kuhusu watu hawa walioingia kwa Asmaa, Abu Bakr R.A. akasema: sijaona chochote isipokuwa kheri tu, yaani kwa pande mbili (watu wa bani Hashim na Asmaa) kwani anawajua wote, kwa sababu walikuwa miongoni mwa waislamu wa Bani Hashim, kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alimhusisha Asmaa akisema: “Mwenyezi Mungu amemsafisha na masingizio haya”, yaani visingizio ambavyo Abu Bakr R.A. alivifikiria, hali hii ilikuwa fadhila kubwa miongoni mwa fadhila zake Asmaa R.A. Ingawa hivyo, Mtume S.A.W. akakusanya watu na kusimama juu ya mimbari, akiwakataza hivyo na akiwafunza yaliyoruhusiwa akisema: “Mtu asiingie kwa mwanamke asiye kuwa na mumewe, ila pamoja na mtu mmoja mwingine au wawili”. kwa kuzuia kisingizio cha upweke, na kuzuia yanayopelekea tuhuma”. [Al-Mufhim lima Ushkil min Talkhiis Muslim 5/503, Ch. Dar Ibn Katheer, na CD. Dar Al-Kalim Al-Twayyib]
Al-Nawawiy amesema katika Sharhi Sahihi Muslim: “Basi dhahiri ya Hadithi hiyo ni ruhusa ya upweke wa wanaume wawili au watatu na mwanamke asiye maharimu. Na rai ambayo ni maarufu zaidi kwa wenzetu ni kuharimisha upweke huu, basi Hadithi hii inagusia watu wasiofanya tendo la ndoa, na Al-Qadhi aliashiria tafsiri hii”. [Sharh Sahihi Muslim kwa Al-Nawawi 14/155, Ch. Al-Martbaha Al-Misriya huko Al-Azhar]
Al-Adawiy amesema katika maelezo yake juu ya maneno ya Abu Al-Hasan katika kitabu cha: [Sharhu Ar-Risalah]: “Abu Al-Hasan amesema: (Hairuhusiwi kwa mtu kuachwa peke yake na mwanamke), anakusudia mwanamwari ambaye (si maharimu kwake) kwani Mtume S.A.W. alikataza hivyo akasema: (wa tatu wao ni shetani), kisha Al-Adawiy amesema: (kusema: Hairuhusiwi kwa mwanaume kuachwa peke yake na mwanamke) Al-Tataiy amesema: katazo hili kwa ajili ya kuiharimisha hali hii na mwanaume na mwanamke hawa wanastahiki adhabu, kisha akasema, mwanamume na mwanamke na hakusema wanawake wawili, kwani inaruhusiwa upweke wa wanawake wawili na mwanamume mmoja, na vile vile upweke wa wanaume wawili na mwanamke mmoja, ila akiwepo kijana pamoja naye anazuiliwa kwa sababu pamoja nao mashetani wawili, na pamoja na mwanamke shetani mmoja, lakini tumeainisha tukisema: (mtu) kwa kusema kijana, kwani inaruhusiwa upweke wa mzee na mwanamwari au na kizee. Na tumeainisha tukisema: (mwanamke) kwa kusema mwanamwari kwani inaruhusiwa upweke wa mtu hata akiwa kijana, pamoja na kizee.” (Hashiatul Al-Adawi Ala Sharhu Ar-Risalah 2/458, Ch. Dar Al-Fikr)
Sababu ya kuruhusiwa kwa mchanganyiko katika hali hii ni kwamba uharibifu uko mbali zaidi kwa wanaume wawili, kwani mara nyingi mmoja wao anastahi mwingine, na Ibn Rushd Al-Malikiy anasisitiza maana hii, Al-Adawiy amesema katika Hashiya yake Ala Sharhu Ar-Risalah kwa Abi Al-Hasan: “(Kauli yake: shetani ni wa tatu wao) Ibn Rushd amesema, maana ya kuwa ni wa tatu wao: Anajizungumza kuhusu mwanamke yule na matamanio yake yanaimarishwa, lakini kama akiwa pamoja na mwingine alimtazama na kuogopa kumwona katika hali ya dhambi hii. (2/458)
Inayothibitisha maana hii ni Hadithi iliyopokelewa na Bukhari kutoka kwa Anas Ibn Malik, R.A. amesema: “Mwanamke alikuja kutoka kwa Ansar kwa Mtume, S.A.W. akaachwa naye”, upweke hapa una maana ya kuachwa kwa mtu binafsi na mwanamke mbele ya watu, ambapo hawafichiki wawili hao, lakini watu hawasikii maneno yao tu, mchanganyiko huu ni halali, na Al-Bukhariy aliweka kichwa kwa Hadithi hii, akisema: “Mlango wa yanayoruhusiwa kwa mtu anayeachwa na mwanamke mbele ya watu» [Sahih Muslim 7/37, Ch. At-Tabaah Al-Turkiyah], Ibn Hajar akasema: “Hairuhusiwi kwa mtu kuachwa na mwanamke ambapo hawafichiki kwa watu, lakini watu hawasikii maneno yao tu, kama kitu ambacho wanawake wanaona haya kukitaja miongoni mwa watu. [Fath Al-Bariy kwa Ibn Hajar 9/333, Dar Al-Maarifah]
Al-Nawawiy amesema: “Jambo ambalo ni maarufu ni kuruhusiwa kwa upweke wa mtu na wanawake wasio maharimu kwake, kwa ajili ya kuondoka uharibifu; kwani wanawake wanaona haya kila mmoja kutokana na mwingine kuhusu jambo hili” [Al-Majmuu Sharhul Muhadhab 7/86, Dar Al-Fikr.], Na katika Hashiyatul Jamal kwa Al-ejiili: “Inaruhusiwa kwa mtu kuachwa pamoja na wanawake wawili waheshimiwa na rai hii imechaguliwa” [Hashiyatul Jamal Ala Sharhul Manhaj 4/466, Dar Al-Fikr], na Ibn Abidin alitaja kuwa: “Upweke haramu pamoja na mwanamke asiye maharimu unaondolewa kwa kuwepo kwa mtu mwingine pamoja nao, au mwanamke mheshimiwa, na inaonekana kwangu kwamba maana ya mwanawake mheshimiwa ni kuwa kizee kwa amabaye mfano wake hafanyiwi tendo la ndoa” [Radul Muhtaar Ala Ad-Durrul Mukhtaar 5/236, Ch. Ihyaa Al-Turath]
Udhibiti wa pili ni: Kuvaa mwanawake vazi linalositiri mwili wake mzima na kuficha uchi wake, na uchi wake ni mwili mzima isipokuwa uso na viganja vya mikono, Mwenyezi Mungu anasema kuhusu wanawake: {Wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika. Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao} [AN NUUR: 31] na Mwenyezi Mungu amesema pia: {Nanyi mnapowauliza (wakeze) waulizeni nyuma ya pazia} [AL AHZAB: 53], na imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud kutoka kwa Aisha, R.A.: “Kwamba Asmaa binti Abi Bakar aliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. ambapo alivaa vazi linaloonesha rangi ya mwili Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. akageuka mbali naye na kumwambia: “Ewe Asmaa hakika mwanawake atakapofika baleghe haachi wazi sehemu yoyote ya mwili isipokuwa hivi tu, akiashiria uso wake na vijanga viwili vya mikono yake”.
Imam Ad-Dardeer amesema katika kitabu cha: [Ash-Sharhus Saghiir]: “Na uchi wa mwanamke pamoja na mwanaume asiye maharimu wake ni sehemu yote ya mwili isipokuwa uso na viganja viwili vya mikono, sehemu hizi si uchi lakini ni wajibu kuzisitiri kwa ajili ya kuogopa fitina”. [Ash-Sharhus Saghiir katika Hashiyatus Swawi 1/289, Ch. Dar Al-Maarifa) Al-Shirazi amesema katika kitabu cha [Al-Muhadhab]: Na uchi wake ni mwili mzima isipokuwa uso na viganja viwili vya mikono kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika. Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao} [AN NUUR: 31], na Ibn Abbas amesema: Uso wake na viganja viwili vya mikono yake. Na kwa sababu Mtume, S.A.W: alimkataza mwanamke aliyevaa ihramu (wakati wa kufanya ibada ya hija huko Makka) kuvaa soksi na nikabu”. Na kwa sababu kuna haja ya kuonesha uso kwa ajili ya kuuza na kununua na kuonesha viganja vya mikono kwa ajili ya kutoa na kupokea, kwa hivyo hakujaalia sehemu hizi kuwa ni uchi”. [Al-Muhadhab kwa Al-Shirazi pamoja na Al-Majmuu 3/167, I. Ch. Dar Al-Fikr]
Udhibiti wa tatu: Kutoruhusiwa mtu kumuangalia mwanamke kwa matamanio na mwanamke kumuangalia mwanaume kwa matamanio kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu amesema: {Waambie Waislamu wanaume wainamishe macho yao} [AN NUUR: 30], na Mwenyezi Mungu almesema vile vile: {Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao} [AN NUUR: 31]. As-Sarkhasi amesema katika kitabu cha Al-Mabsoot: “Inaruhusiwa kuangalia viungo vya mapambo vinavyodhihirika tu, siyo vilivyofichikana, kufuatana na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika.} [AN NUUR: 31]”. [Al-Mabsoot kwa As-Sarkhasiy 10/152, Ch. Dar Al-Maarifah], Ad-Dardeer katika kitabu cha: [Ash-Sharul Kabiir] amesema: “Na sehemu zisizo za uchi hairuhusiwi kuziangalia kwa ladha”. [Ash-Sharul Kabiir kwa Ad-Dardeer pamoja na Hashiyatu Dusuqi 1/214, I. Ch. Dar Al-Fikr]
Udhibiti wa nne: Kutokugusa mwili kama inavyotokea katika baadhi ya harusi na maonesho. Imepokelewa kutoka kwa At-Twabaraniy na Al-Baihaqiy kutoka kwa Maqil Ibn Yasaar amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. amesema: “Kupigwa mtu kati yenu kwa sindano ya chuma kichwani mwake ni kheri kwake kuliko kumgusa mwanamke asiyeruhusiwa kwake”.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, kama udhibiti ukizingatiwa kwa ajili ya mchanganyiko, basi mchanganyiko huo unaruhusiwa, vinginevyo ni haramu. Na Hadithi ya mke asiyekuwa na mume wake inaonesha kwamba inaruhusiwa mchanganyiko kwa masharti ya kisheria, na inaruhusiwa kwa wanaume waheshimiwa kuachwa pamoja na mwanamke na vile vile inaruhusiwa kwa mwanamume kuachwa pamoja na wanawake kwani hakuna uharibifu, kwa sharti la kusalimika na fitina.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas