Gharama za Kuwaozesha Watoto.
Question
Je, baba analazimika kumwozesha mwanawe kama akihitaji hivyo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Baadhi ya watoto wanahitaji kuozeshwa, baadhi ya nyakati watoto huwa wanahisi kuwa ni aibu kubwa kwao na wanahofia kuangukia katika uzinzi, na hakuna njia isipokuwa kuhifadhi nafsi zao kupitia ndoa, na wanawaomba wazazi wao wawasaidie katika jambo hili la ndoa.
Pengine mwenye jukumu la kisheria ana hali maalumu inayoifanya ndoa iwe ni wajibu kwake, hivyo wanavyuoni wamegawa ndoa katika hukumu tano za kukalifisha.
Al-Hafidh Ibn Hajar alisema: “Wanavyuoni wamegawa watu katika ndoa kwa sehemu maalumu: Mwenye kuitaka ndoa mwenye uwezo wa majukumu yake na anayeiogopea nafsi yake. Wanavyuoni wameafikiana kwamba ndoa inakokotezwa kwa mtu huyo, na Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Ahmad Ibn Hanbal wameongezea kwamba ndoa katika hali hiyo ni lazima, hivyo Abu Awana Al-Isfiriniy miongoni mwa wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Al-Shafiy alisema mtazamo ule ule katika Sahihi yake, na Al-Masisi pia amesema mtazamo ule ule katika kitabu cha: [Sharhu Mukhtasar Al-Juiniy], vile vile Dawudi na wafuasi wake wamesema mtazamo ule ule ... ambao wamesema kwamba ndoa katika hali ile ni wajibu kama kutaka hakukuondolewa kwa kumwoa kijakazi, basi kama hakukuondolewa, kuozesha ni lazima. Ibn Hazm alisema kauli hiyo hiyo akisema: Ndoa imefaridhishwa kwa kila mwenye uwezo wa kuoa akipata mwanamke huru au kijakazi analazimishwa kumwoa mmoja wao, lakini kama hakuweza kufanya hivyo, aongeze kufunga saumu, na kundi la Maulamaa waliotangulia wamesema mtazamo huo huo. Ibn Daqiiq Al-Id alisema: Baadhi ya wanavyuoni wameigawanya ndoa katika hukumu tano, na akaifanya ni wajibu kama ukiogopwa ugumu na akiwa na uwezo wa ndoa na hakuweza kumwoa kijakazi. Vile vile mtazamo huu umepokelewa kutoka kwa Al-Qurtobiy kutoka kwa baadhi ya wanavyuoni kama Al-Maziriy, akisema: uwajibu ni kwa asiyeweza kuacha uzinzi, isipokuwa kwa ndoa halali kama ilivyotangulia”, [Fathul -Bari 9/110, Ch. Dar Al-Marifa].
Na anayejiogopea kuzini kama hakuoa, hukumu yake ni aoe kama akiweza hivyo, lakini kama hakuweza na akiwa tajiri analazimika kusaidia anayehitaji kuozeshwa miongoni mwa jamaa zake katika hali hii.
Ushahidi wa hili ni kauli yake Mwenyezi Mungu kwa ujumla: {Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto} [AT-TAHRIIM: 6].
Inaweza kutoa dalili hii ambayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na waozeni wajane miongoni mwenu} [AN Nuur: 32], na hii ni amri ya kijumla, nayo ni ya kwanza ambayo inaelekezwa kwa wazazi kama wakiwa matajiri.
Kama kwamba lililotajwa katika matini hii ni wajibu ni kwa ajili ya kuashiria mambo yanayosababisha madhara kwa mtoto kwa kuyakosa, vile vile yasiyotajwa yanaingia kwa mujibu wa kipimo.
Katika baadhi ya wakati kutofanya tendo la ndoa kunasababisha magonjwa, na kwa hivyo, baadhi ya wanavyuoni wamesema kwamba inaruhusiwa kuvunja saumu yake na hata kuvunja saumu ya mwingine, Al-Bahwatiy alisema: “(Na mwenye hamu ya kufanya tendo la ndoa anayejiogopea) kutokana na madhara yoyote (anaweza kufanya tendo la ndoa pasipo na kutoa kafara) imepokelewa kutoka kwa Ismail Ibn Sayid Ash-Shalingiy, Ahmad akasema: Mtu yule anaweza kufanya tendo la ndoa pasipo na kutoa kafara lakini analazimika kufunga siku nyingine badala yake, kwani katika hali hii kama mtu hakufanya tendo la ndoa anaogopewa madhara. (Na kama matamanio yake yakiwa na nguvu kwa kingine) yaani kwa njia nyingine badala ya tendo la ndoa (kama vile kujitoa manii kwa mkono wake au kwa mkono wa mkewe au) kwa mkono wa (mjakazi wake n.k.) kama vile kuupenyeza uume wake kati ya mapaja ya mwanamke) (haruhusiwi) kufanya tendo la ndoa, ni kama vile mporaji anaeparamia kitu chepesi na wala haelekei kwenye kitu kingine. (vile vile kama akiweza kutoharibu saumu ya mke wake) au mjakazi wake (ambaye ni Muislamu aliyebaleghe kwa kufanya tendo la ndoa na mke wake au mjakazi wake miongoni mwa waliopewa kitabu) au kufanya tendo la ndoa na (mke wake au wajakazi wake wadogo) au ambao wenye wazimu (au) alikuwa na matamanio yenye nguvu ya kuingilia (isiyokuwa tupu ya mbele) haruhusiwi kwake kuharibu saumu yake kwani hakuna dharura, nikasema, pengine hali hii inapimiwa kama akiweza kufanya tendo la ndoa na aliyelazimika kufunga kama aliye twaharika katika wakati wa mchana; kwa sababu kufunga tu ni chini ya kufunga saumu ya kisheria, hasa kwa saumu yenye mgogoro katika uwajibu wake (lakini) kama hakuweza kutovunja saumu ya mke wake au mjakazi wake ambaye ni Muislamu na aliyebaleghe (anaruhusiwa) kuvunja saumu yake (kwa dharura) kama kula nyama ya mfu kwa anayelazimishwa (na pamoja na dharura ya kufanya tendo la ndoa na mwanamke mwenye hedhi na mwenye kufunga aliyebaleghe) kwamba hana wengine (basi kufanya tendo la ndoa na mwenye kufunga ni bora zaidi) kufanya tendo la ndoa na mwanamke mwenye hedhi, kwani kukufanya tendo la ndoa na mwenye hedhi kumeharimishwa kwa Qur`ani, (lakini kama) mke au mjakazi aliyefunga (ni mwenye kubaleghe ni lazima kuepuka mwenye hedhi) kwa ajili ya kutohitaji kwake bila kuzuia, anaweza kufanya tendo la ndoa na mwanamke mdogo na pia mwenye wazimu. (kama hawezi kulipa) yaani: mwenye hamu ya kufanya tendo la ndoa (kwa kuendelea hamu yake kama mzee ambaye hawezi kufunga kama ilivyotangulia) basi anaweza kumlisha masikini mmoja kwa kila siku na hana kulipa isipokuwa pamoja na udhuru wa kawaida kama vile ugonjwa au udhuru wa msafiri halishi wala halipi kama ilivyotangulia kwa mzee, na pengine hukumu ya mke wake au mjakazi wake ambaye hana mwingine isipokuwa yeye tu ni hukumu ile ile. (na hukumu ya mgonjwa ambaye ananufaika na kufanya tendo la ndoa) katika ugonjwa wake (ni sawa na anayejiogopea kutokana na madhara ya kufanya tendo la ndoa) kuhusu kuruhusiwa kwa kufanya kufanya tendo la ndoa pamoja na kafara na kuvunja saumu ya mke wake na mjakazi wake. "[Kashaf Al-Qinaa ‘An Matn Al-Iqnaa 2/311, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Pia mtazamo huu unatiwa nguvu na iliyopokelewa kutoka kwa tendo la Omar Ibn Abdul Aziz, ambaye ni mmoja wa makhalifa kwamba alikuwa akitoa anayehitaji kufunga ndoa kutoka katika nyumba ya fedha, ilipokelewa kutoka kwa Asim Ibn Abi Habib alisema, Omar Ibn Abdul Aziz, alikuwa na mpigaji wito anayeita kila siku: Wenye kuoa wako wapi? Wenye madeni wako wapi? Masikini wako wapi? Mayatima wako wapi? [Rejea: Tarikh Dimeshq kwa Ibn Assaker 45/194, Ch. Dar Al-Fikr].
Kundi la wanavyuoni walisema kama tulivyotaja:
Al-Bahoutiy alisema: (na) pia ni lazima (kwa mtu ambaye analazimishwa kulipa matumizi kwa mmoja wa jamaa yake anapaswa kulipa matumizi yake yote kutoka kwa baba na babu), vile vile kutoka kwa mtoto na mjukuu na wengine kama ndugu na baba mdogo (na kama akihitaji kuoa mke huru au wa kisiri ili amwepushe na haramu au mwenye kulipa anamlipia) matumizi yasiyoozesha mke huru au yasiyonunulia mjakazi, kwani mambo haya yanahitajika na kama hayakuwepo yanasababisha madhara, kwa hivyo, anayelazimishwa kulipa anapaswa kulipia hayo. Wala hayafananishwa na halua, kwani hakuna madhara kama akiipoteza. (Na kuchagua) kuhusu yaliyotajwa (kwa aliyelazimishwa hivyo). [Kashaf Al-Qinaa 5/486].
Ibn Qudaamah alisema: “Wenzetu walisema:. Juu ya baba kumwozesha mwanawe kama akilazimishwa matumizi yake, na akiwa na haja ya kuoa, nayo ni maoni ya baadhi ya wenzake Al-Shafi. Na baadhi yao walisema kuwa si lazima kwake hivyo, na maoni yetu ni kwamba mtoto huyo anatokana na nasaba yake, na ni wajibu juu yake kumlipia matumizi yake, vile vile ni lazima kumwozesha akihitaji hivyo. Al-Qadhi alisema: Na pia ni sawa na huyo watu wote wanaopaswa kuwalipia matumizi, kutoka kwa ndugu au mjomba au wengine, kwa sababu Ahmed amesema kuhusu mtumwa: Ni wajibu juu ya bwana wake kumwozesha akihitaji hivyo” [Al-Mughniy 8/217, Ch. Maktabat Al-Qahirah].
Wanavyuoni wengi wamesema kinyume cha tuliyoyataja, walisema, si lazima juu ya baba kumwozesha mwanawe, lakini ni wajibu juu ya mtoto kumwozesha baba yake.
Sheikh Zakaria Al-Ansaryi alisema: "(Upande wa tatu ni wajibu juu ya mtoto kumwozesha baba hata akiwa kafiri) kwa sababu jambo hili ni miongoni mwa mahitaji yake ya kimsingi, basi ni wajibu juu ya mtoto ambaye ana uwezo (kama wa kugharamia matumizi yake) ili asielekee katika njia ya uzinzi, hivyo haifai kwa heshima ya uzazi na huku sio kuwa pamoja naye kwa wema kunakoamrishwa, kama alivyoamirisha Mwenyezi Mungu”. [Asna Al-Matwalib 3/189, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy]
Katika kitabu cha: [Ar-Rawdha kwa An-Nawawiy]: “Imamu ametaja sababu za kutolazimisha kumlipia matumizi kwa mke wa mtoto kwani halazimishwi kumwozesha mwanawe.” [9/86, Ch. Al-Maktab Al-Islami]
Na yaliyotajwa kutoka sababu zisizo na nguvu, na baadhi ya dalili zao kuhusu uwajibu wa kumwozesha baba ni dalili pia inayohusiana na uwajibu wa kumwozesha mtoto, kama kauli yao: “Kwa sababu jambo hili linahitajika sana… ili asielekee njia ya uzinzi” Ndivyo ilivyo kwa mtoto, bali inahitajika zaidi kwake; kwa sababu ya nguvu wa matamanio kwa mtoto mara nyingi zaidi kuliko kwa baba.
Na kwamba uharibifu unaotokana na kutofanya tendo la ndoa ni zaidi kuliko uharibifu unaotokana na kulipa matumizi katika baadhi ya wakati, baadhi ya wanavyuoni walisema hivyo katika suala la kukosekana kwa Mheshimiwa kwa mama wa mtoto wake na madhara yake.
Al-Mardaawi alisema: “Faida: kama Mheshimiwa alipoteza mama wa mtoto wake, naye alihitajika matumizi: Akaozeshwa kufuatana na madhehebu sahihi, alisema katika kitabu cha: [Al-Furuu]: Akaozeshwa kufuatana na mtazamo sahihi zaidi, na ilisemekana: Haozeshwi. Hata kama akihitaji kufanya tendo la ndoa: Haozeshwi. Alitaja hivyo katika kitabu cha: [Al-Furuu]. Na alisema: Wanavyuoni waliosema kuwa ni sawa na kulipa matumizi walisema inaruhusiwa tu. Nikasema: hili suala ni sahihi, na uharibifu unaotokana na hivyo ni mkubwa kuliko uharibifu kutokana na kulipa matumizi. Ibn Rajab alichagua rai hii na aliitaja katika kitabu chake kinachoitwa: [Al-Qawul Al-Swawab fii Tazwiij Umahat Awlad Al-Ghiyab], na alitaja katika kitabu hicho hukumu za ndoa yake, ndoa ya wajakazi, mwanamke aliyepotezwa, na akaongeza katika suala hili vizuri, na akatoa dalili zinazoonesha usahihi wa ndoa yake kufuatana na na maneno ya marafiki na matini za Imam Ahmad, Mwenyezi Mungu amrehemu. [Al-Enswaaf 9/410, Ch. Dar Ihyaa AT-Turath Al-Arabiy]
Rai ambayo ni sahihi zaidi ni uwajibu wa kulipa matumizi kwa mtoto ili kumwozesha kama akihitaji hivyo na aliiogopea nafsi yake kuelekea njia ya uzinzi, hali hii kama akiwa baba yake au babu yake au anayelazimishwa kumlipia matumizi ni Tajiri.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.