Kuharibu Taasisi za Umma na Uchoche...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuharibu Taasisi za Umma na Uchochezi wa Kufanya Hivyo.

Question

 Ni ipi Rai ya kisheria kwa mchochezi na mharibifu wa Tasisi za Umma hata kama ni kwa kusema neno dogo na mfano wa hayo, na anayeridhika kufanya hivyo na hakukana?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni zake Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wafuasi wake, na baada ya Utangulizi huo:
Mali ni nguzo muhimu katika maisha, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha tuihifadhi, na asili ya hayo kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msiwape wasio na akili mali zenu ambazo Mwenyezi Mungu amezijaalia ni tegemeo kwenu.} [AN NISAA 5] Na katika Aya hiyo kuna katazo kwa walezi kuwapa pesa wale wasio na uelewa, wakaja kuzipoteza, kwani sababu ya kutowapa hapo ni kuzipoteza.
Na kuhifadhi mali ni makusudio muhimu kabisa ya Sheria ya Kiislamu, bali hata katika sheria zote nyingine. Imamu Abu Haamed Al Ghazali amesema katika kitabu cha: [Al Mustaswfa, Uk. 173, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]; "Na makusudio ya kisheria yatokayo kwa Mwenyezi Mungu ni kuyalinda Mambo matano: Dini, Nafsi, Akili, Kizazi na Heshima yake na Mali. Kwa hivyo kila kinachohusika na kuvilinda vitu hivi vitano vya Kimsingi kinazingatiwa kuwa ni masilahi, na kila kinachoyapita mambo haya kinazingatiwa kuwa ni uharibifu, na kuuondoa uharibifu huo ni masilahi".
Na Umiliki wa Mali ni wa binafsi na wa Umma; na Umiliki binafsi unafungamana na mtu mmoja mmoja, wakati ambapo Umiliki wa Umma unafungamana na watu wote. Kwa namna ambayo inawanufaisha wote bila ya kumtenga mtu yeyote maalumu; kama vile Barabara, Madaraja, Taasisi za Umma, na kila kilichomo katika aina hizi mbili kinatakiwa kuheshimiwa na kutunzwa.
Na Imamu Muslim amepokea katika Kitabu chake: [Sahihul Muslim] kutoka kwa Abu Huraira R.A. amesema: kwamba Mtume S.A.W., anasema: "Na kila Muislamu kwa Muislamu mwenzake analindwa Maisha yake, Mali yake na Heshima yake."
As Swana'aniy anasema katika kitabu cha: [Subel As Salaam 671/2, Ch. Dar Al Maarifah]: "Na katika kauli yake: Na kila Muislamu kwa Muislamu mwenzake analindwa Maisha yake ni kutuelezea uharamu wa Damu yake, Mali yake na Heshima yake, na hili linajulikana kisheria bila ubishi wowote.
Kwa hiyo kushambulia Mali ya Umma ni kitendo kiovu zaidi kuliko kushambulia Mali ya mtu binafsi; kwani kushambulia huko kunakotokea katika Mali ya Umma na ni kuushambulia mjumuiko wa watu, na athari yake hasi haiishii kwake yeye binafsi bali inarejea kwa watu wote.
Kwa hiyo, Mtu anayeharibu Taasisi za Umma ni mhalifu mwenye dhambi aliye adui mkubwa, na ni lazima aadhibiwe kwa adhabu anayoistahiki na yenye kumkanya yeye na wanaofanana naye ambao wanafanya kila wawezavyo kufanya ufisadi katika dunia na wala sio kuijenga na kuiimarisha. Na mwenzake katika madhambi na mshirika katika Uhalifu na Ufisadi: ni yule anaemchochea afanye hivyo, na pia anayemsukuma hata kama ni kwa kiasi cha kusema maneno tu. Na kila anaemtetea au kumtafutia udhuru; kwani kila mmoja wao anazingatiwa kushirikiana naye kwa kumuunga mkono katika ufisadi wake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na saidianeni katika wema na uchamungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Munguni ni Mkali wa kuadhibu}. [AL MAIDAH 2]
Ikiwa mwenyekutoa habari za kheri ni kama mfanyaji wa kheri hiyo, vile vile mtoaji wa habari za shari ni kama mfanyaji wa shari hiyo.
Na atakaeweza kukanusha jambo hili na hakulifanya, bali aliliridhia na akalinyamazia basi yeye ni mwenye kufanya maasi na anapata dhambi; kwani hii ni aina ya msukumo wa kulikubali kosa hilo. Na Imamu Muslim amepokea katika Kitabu chake: [Sahihu Muslim] kutoka kwa Abu Saiid Al Khudriy R.A. kwamba Mtume S.A.W. anasema: "Atakaeona jambo ovu katika nyinyi basi alizuie kwa mkono wake, na kama hakuweza basi kwa ulimi wake, na kama hakuweza basi kwa moyo wake, na kwa moyo wake ni udhaifu wa imani".
Imamu An Nawawiy anasema katika sharhu yake kwa Muslim [25/2, Ch. Dar Ihiyaa At Turath Al Arabiy]; "Kauli ya Mtume S.A.W, Basi kwa moyo wake; maana yake: alichukie kwa moyo wake, na hivyo sio kwa kuliondosha au kulizuia yeye mwenyewe, lakini hivyo ndivyo awezavyo".
Na Abu Dawud amepokea kutoka kwa Al Urs Bin Umairah Al Kanadiy R.A. kwamba Mtume S.A.W, anasema: "Pindi linapofanyika kosa ardhini, aliyelishuhudia na akalichukia na akasema mara moja: nimelichukia – atakuwa kama mtu ambaye hakuwepo wakati linatokea, na asiyekuwapo na akaliridhia atakuwa kama mtu aliyelishuhudia".
Al Haafedh Ibn Rajab Al Hanbaliy anasema katika kitabu cha: [Jame' Al Uluum na Al Hekam 245/2, Ch. Musasat Ar Risala: Kuyaridhia makosa ni katika mambo mabaya mno yaliyoharamishwa, na hupelekea kutokanusha ovu kwa moyo wake, na ambapo jambo hili ni faradhi kwa kila muislamu, na kwa hali yoyote faradhi hii haindoki kwa mtu yeyote.
Na Ibn Mas'uod alimsikia mtu mmoja anasema: "Ameangamia yule ambaye hakuamrisha Mema na hakukataza Mabaya". Na Ibn Mas'uod akasema: "Ameangamia yule ambaye Moyo wake haujui Mema na Maovu. Anaashiria kuwa kuyajua Mema na Maovu kwa moyo ni jambo la lazima kwa kila mtu na haliachiki, na asiyejua hivyo ameangamia".
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia unadhihirika wazi uharamu wa kuharibu Taasisi za Umma, na Uchochezi wa kufanyika kwa jambo hilo, na kuridhika nalo, au kulipinga kwa mwenye kuweza kulizuia na akawa hakufanya hivyo, na kwamba dhambi inayotokana na jambo hilo ni kubwa mno kuliko dhambi inayoambatana na ubadhirifu wa Mali ya Mtu binafsi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas