Kufuatilia kasoro za watu na makosa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufuatilia kasoro za watu na makosa yao

Question

Je, kufuatilia makosa na dhambi za watu na kutafuta kujua ni haramu? Je, unatubu vipi kutokana na hilo?

Answer

Hii inazingatiwa kufuatilia kasoro za watu, na hairuhusiwi kufuatilia kasoro za watu. Kwa sababu kufuata kasoro za watu wengine ni maadili mabaya na haramu mambo ambayo yanapandikiza chuki katika nafsi na kueneza ufisadi katika jamii.

Mwenye kufuatilia aibu za watu ni lazima atubie, na awaombe msamaha wale aliowadhulumu, bila ya kuwa hiyo itakuwa ni sababu ya kujifedhehesha, la sivyo, atubie yaliyo baina yake na baina ya Mola wake Mlezi, na awaombee msamaha kwao, na yale aliyoyafahamu kutoka kwao hayamfanyi awachukie watu au kuwashusha hadhi.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Mwenye kumsitiri Muislamu, basi Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya Qiyaamah.” Hadithi hii Imekubaliwa.

Ni bora kwake kujishughulisha na makosa yake na kutubia dhambi zake.

Share this:

Related Fatwas