Kubadilisha Jjinsia kwa Ajili ya K...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kubadilisha Jjinsia kwa Ajili ya Kutibu Tatizo la Utambulisho wa Kijinsia.

Question

 Yamejitokeza Majadiliano mengi ya hivi karibuni katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu ugonjwa uitwao (tatizo la utambulisho wa kijinsia) na watu wengi wakadai kwamba hakika wao wapo katika mateso na kwenye maisha ya tabu kwa sababu ya tatizo hili, na kwamba ufumbuzi wa kimsingi wa tatizo lao ni kufanyiwa upasuaji na kubadilishwa kuwa na jinsia tofauti, kwa madai kuwa mawazo yao na nafsi zao ni za jinsia nyingine, lakini zimo katika miili isiyo sahihi, na wanaelezea upasuaji kama marekebisho ya jinsia na si mabadiliko ya jinsia ili kuepuka tuhuma ya kuchezea na kubadilisha viumbe wa Mwenyezi Mungu, na wanathibitisha kauli yao kwa kauli ya baadhi ya madaktari kuthibitisha kuwa tatizo hili halina ufumbuzi wa matibabu ya homoni au matibabu ya kisaikolojia, bali halina tiba yoyote hadi sasa isipokuwa tu kubadilisha jinsia. Je, tatizo hili ni udhuru wa kisheria unaoruhusu mchakato wa kubadilisha jinsia?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Tatizo la utambulisho wa kijinsia au kile kinachoitwa kwa Kiingereza: (Gender identity disorder) linajulikana kwa ufupisho wa jina la (GID) nayo ni utambuzi wa tatizo uliotolewa na madaktari na wanasaikolojia juu ya watu ambao wanateseka kutokana na hali ya usumbufu au wasiwasi kuhusu jinsia waliozaliwa nayo, ambayo ni aina ya kisaikolojia, inayoelezea matatizo yanayohusiana na mabadiliko ya jinsia na utambulisho wa mabadiliko ya jinsia na kuiga jinsia tofauti, shida hii ya kisaikolojia kwa ufupi inamaanisha kwamba mgonjwa anajikuta akiwa na hisia isiyokusudiwa kuwa ni ya jinsia tofauti, ingawa kuna ukamilifu wa kuumbwa kwa mwili na uzima wa viungo vyake vya uzazi.
Jinsia (Gender): Ni neno la Kiingereza lenye asili ya Kilatini, ambalo linamaanisha kilugha: jinsia. Kwa suala la uume na uke, na hutumiwa kuainisha nomino, viwakilishi na vivumishi.
Shirika la Afya Duniani linajulisha istilahi hii kuwa ni: tabia ambazo ni za wanaume na wanawake kama tabia za kijamii zinazopangwa na zisizo na uhusiano na tofauti ya viungo, na Encyclopedia ya Britannica inajulisha istilahi hii pia kuwa ni: hisia za binadamu mwenyewe akiwa ni mwanamume au mwanamke, na wakati huo huo akiwa kama mwanamume akifanya kazi za kike, au mwanamke akifanya kazi ya kiume, basi hatakuwa mwanamume au mwanamke, lakini itakuwepo «aina» yaani «Jinsia». Hii ina maana kwamba tofauti ya kibayolojia kati ya wanaume na wanawake haina uhusiano wa kuchagua shughuli za kijinsia zinazofanywa na kila mmoja wao. Na huu ni utambulisho wa wazi wa upungufu wa kijinsia, pia ina maana ya kuwa mwanamume anafanya kazi ya kike, na mwanamke anafanya kazi ya kiume; kwani kazi hizi zilizoainishwa kwa kila mmoja wao ziliainishwa na jamii yenyewe wala hazikuainishwa na tabia ya kiume na kike kama wanavyodai, hii pia ina maana kwamba hali hii ni uharibifu wa familia, ambayo ni kiini cha jamii zote na pasipo na familia jamii huharibika.
ukweli wa binadamu kuwa yeye ni kiumbe maskini na dhaifu, huhitaji mara kwa mara kupata uwepo wake na mambo ya maisha yake kutoka kwa Muumba wake, ambaye Amemuumba katika ulimwengu huu, na Mwenyezi Mungu alimwamuru Mtume wake Mtakatifu S.A.W. kuonesha ukweli wa binadamu na ukweli wa kile anachomiliki kwa kusema: {na mwanaadamu ameumbwa dhaifu} [AN NISAA: 28], {Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu.} [YUNUS: 49] na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa. Akitaka atakuondoeni na alete viumbe vipya. Na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu} [FATWER: 15 - 17], na labda mwanadamu anadhani kuwa yeye mwenyewe ana umiliki wa halisi ambao mjinga anaudai kinyume na hali halisi kama Mwenyezi alivyosema: {Na dhara inapo mgusa mtu hutuomba. Kisha tunapo mpa neema zitokazo kwetu, husema: Nimepewa haya kwa sababu ya ilimu yangu. Sio! Huo ni mtihani! Lakini wengi wao hawajui!} [AZ ZUMAR: 49], na imepokelewa kutoka kwa At-Tirmidhi katika Sunan yake kutoka kwa Abu Barza Aslami R.A alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema: “Nyayo za mja hazitaondoka Siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe juu ya umri wake alivyoumaliza, elimu yake alivyoifanyia, mali yake ameichuma kutoka wapi na ameitumia kwa mambo gani, na mwili wake aliutumia kwa kazi gani”. Vile vile imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhariy na Muslim kutoka kwa Abdullah Ibn Umar, R.A kuwa Mtume wa Allah S.A.W. akamwambia: “Hakika mwili wako una haki, na macho yako vilevile yana haki, na mgeni wako vilevile ana haki, na mkeo vilevile ana haki”.
Matini hizi za kisharia zinathibitisha kwamba mtu hamiliki mwili wake umiliki halisi; kwa sababu yeye atahojiwa kwa ayatendayo mbele ya Mwenyezi Mungu, na atalipwa kwa ayatendayo na udhalimu wake dhidi nafsi yake mwenyewe na mwili wake, wakati ambapo mmiliki wa haki hahojiwi wala halipwi kwa ayatendayo katika miliki yake, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Sema: Ewe Mwenyezi Mungu uliye miliki ufalme wote! Wewe humpa ufalme umtakaye, na humwondolea ufalme umtakaye, na humtukuza umtakaye, na humuangusha umtakaye. Kheri yote iko mikononi mwako} [AAL IMRAAN: 26], na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema pia: {Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanao hojiwa kwa wayatendayo} [AL-ANBIYAA: 23], na kama inaonesha kuhesabiwa binadamu kuhusu mali yake - ameichuma kutoka wapi na ameitumia kwa mambo gani - kwamba yeye haimiliki umiliki halisi ambao unamruhusishia uhuru kamili wa kutenda, na vile vile kuhesabiwa kwake kuhusu mwili wake aliutumia kwa kazi gani.
Ibn Al-Hajj Al-Malikiy katika kitabu cha: [Al-Madkhal 1/132, Ch. Dar At-Turath.]: “Kama mwanadamu akiwa na haki ya kutenda kwa mali yake lakini kitendo chake si kamili bali amezuiliwa kutumia mali yake; kwa sababu hana umiliki kamili kwake; kwani inaruhusiwa kwake kuitumia katika sehemu maalumu na amezuiliwa kwake kuitumia katika sehemu maalumu. Mali, kwa kweli si mali yake lakini ni ipo katika mkono wake kama ni mkopo ili aitumie katika jambo kadhaa na asiitumie katika jambo kadhaa, na hali hii iliainishwa katika Qur'ani na Hadithi pia”.
Kwa msingi huu mwanadamu hana haki ya kuvitumia viungo vya mwili wake isipokuwa kwa kiasi inayooneshwa na sharia ya Kiislamu, kupitia matini maalumu au matini ya kijumla, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa? (116) Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi Tukufu} [AL-MU'MINUUN 115.116], Mwanadamu hakuumbwa bure na hataachwa bure bila ya utaratibu na makatazo na kuhesabiwa, basi ni mja aliyepewa jukumu katika maisha ya dunia kwa kazi maalumi kazi ambayo ataifanya na atalipwa au kuadhibiwa kulingana na alivyofanya, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda} [AT-TAWBAH: 105].
Kwa upande wa kuingilia kwa upasuaji katika viungo vya uzazi vya binadamu, hukumu yake ni kuzuia isipokuwa kwa dharura tu au kwa haja ambayo ni sawa na dharura; kwa sababu sharia ya Kiislamu imeharamisha kuhasiwa na mambo ambayo yapo katika maana yake kwa sababu ni mabadiliko ya viumbe wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mtukufu amesema: {Wao hawawaombi badala yake Yeye ila wanawake, wala hawamuombi ila Shet'ani aliye asi, Mwenyezi Mungu amemlaani. Naye Shet'ani alisema: Kwa yakini nitawachukua sehemu maalumu katika waja wako. Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shet'ani kuwa ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahiri} [AN NISAA: 117-119], Qur'ani Tukufu inaweka wazi kwamba mabadiliko ya viumbe wa Mwenyezi Mungu ni haramu, kwani ni kufuata amri ya shetani na upendo kwake badala ya Mwenyezi Mungu na hasara ya dhahiri. Kuhasiwa na hivyo ni kubadilisha kwa viumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni kinyume na umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu na suala hili ni haramu, ilipokelewa katika tafsiri kutoka kwa Ibn Abbas na Anas Ibn Malik, R.A., na pia kutoka kwa masahaba wengine, kwamba makusudi ya kubadilisha viumbe wa Mwenyezi Mungu iliyopo katika aya: ni kuhasiwa. [Rejea: Tafsiri ya Imam Al-Tabari, Jamiil Bayan 9 / 215-216, Ch. Muasastu Resalah.], Lakini kama kuna kukata kwa viungo vya mwili katika upasuaji kwa ajili ya kuendelea uhai au kwa ajili ya manufaa ya viungo vingine, basi msingi ni kwamba hali ya dharura inaruhu kinachoharamishwa, na kwamba kama madhara yakipingwa yanazingatiwa yale ambayo ni makubwa zaidi kwa kuyafanya yale ambayo ni mepesi zaidi. [Rejea: Al-Ashbaah walnadhair kwa Al-Suyuti, uk. 84, 87, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Shida ya utambulisho wa kijinsia kwa baadhi ya watu ni tatizo linalojulikana tangu wakati wa zamani uliotangulia wakati wa Uislamu, lakini maana yake ni kukutana katika mtu mmoja ishara na viashiria vya kubadilika kwa maumbile na tabia ya kiume na ya kike pamoja na tofauti katika uwiano kati ya mgonjwa na mwingine, lakini tatizo hili lina hali mbili: inawezekana kuwa tatizo la kweli na hakuna uwezo kwa mtu katika tatizo hili, na inawezekana kuwa tatizo hili si kweli kwa uwezo wa mtu mwenyewe, na kila hali ina hukumu na matibabu yake. Ambaye ametahiniwa kwa tatizo hili anaitwa (hanithi) kama tatizo hili lilikuwa la kimwili na ana kiungo cha uzazi wa kiume na kike, kama kukiwa na utata wa kuchanganyika kuhusu suala hili wakati ambapo hakijulikani kiungo kipi ni cha asili na kipi ni cha ziada huitwa: (hanithi mchanganyo), vile vile kama akiwa hana kiungo cha uzazi kabisa.
Wanavyuoni walisema kuwa hanithi mchanganyo hazingatiwi kwa mielekeo yake isipokuwa katika hali mbili tu, ya kwanza: Wakati wa kutoweza kutambua alama zinazoonekana, na ya pili: Kama hakuwa na kiungo cha uzazi wa kiume wala wa kike, na isipokuwa hali hizi mbili hanithi haruhusiwi kuwa pamoja na jinsia yoyote kulingana na mielekeo yake au kulingana na hisia yake ya ndani [Rejea: Rawdhatul Talibiin 1/79, Ch. Al-Maktab Al-Islamiy].
Kwa mujibu wa kitabu cha: [Al-Ashbaah wa An Nadhair kwa Al-Suyutiy, Uk. 241- 242]: “Al-Nawawi amesema: Hanithi aina mbili: ya kwanza ana kiungo cha uzazi wa kike, na wa kiume pia. Ya pili ambaye hana kiungo cha uzazi wa kike, wala wa kiume. Lakini ana tundu ambalo vinatokea vitu, tundu hili halifanani na kiungo cha uzazi wa kiume wala wa kike, basi aina ya kwanza inajitokeza hali yake kupitia mambo maalumu: jambo la kwanza ni mkojo, akikojoa kwa kiungo cha uzazi wa kiume peke: basi ni mwanamume, au akikojoa kwa kiungo cha uzazi wa kike: basi ni mwanamke, au kwa kiungo cha uzazi wa kiume na wa kike pia: basi huzingatiwa kwa kiungo kinachotangulia. Na jambo la pili na la tatu ni kutoka kwa manii na hedhi. Kama manii yakitoka kutoka kwa kiungo cha uzazi wa kiume, basi ni mwanamume, au kwa kiungo cha uzazi wa kike, basi ni mwanamke. Kwa sharti la kutoka manii na hedhi zaidi ya mara moja kwa ajili ya kuthibitisha dhana hii. Vile vile Masheikh wawili walisema hivyo. Al-Isnawiy alisema kuwa: kutotaja kwa mkojo kunamaanisha kuwa hauhitajiki. Al-Isnawi alisema kuwa: idadi ya marudio ni kama ilivyosemwa kuhusu mbwa wa uwindaji: kwamba inakuwa ni ada yake. Jambo la nne ni: Uzazi. Nao unathibitisha uke wake tu, na hutangulia ishara zote zinazopingana. Al-Isnawi alisema katika kitabu cha “Al-Muhadhab”: hata kama akitoa kipande cha nyama na Wanavyuoni waliotangulia walisema: ni mwanzo wa uumbaji wa mwanadamu: inahukumiwa kwa hali hii. Na kama kuna shaka tatizo liliendelea. Akasema: kama tumbo lake likijaa, na alama ya ujauzito ilionekana: haikuhukumiwi kuwa ni mwanamke, mpaka ujauzito unathibitishwa. Al-Isnawiy alisema: Ni sahihi kutosheka kwa alama inayoibuka. Ar-Rafiy alisisitiza hivyo mwishoni mwa maneno yake kuhusu hanithi. Na Wanavyuoni walimfuata katika Rawdhatul Talibiin. Vile vile katika Sharhul Muhadhab katika nafasi nyingine na mtazamo huu ndio unaoafikiana na misingi inayotajwa katika majibu kwa kasoro, na kuharimishwa kwa talaka, mke aliyetalikiwa na anastahiki matumizi, na kadhalika. Jambo la tano ni: hali ya kukosa hedhi katika muda wake ni alama ya kiume, inayothibitishwa kwake wakati wa usawa katika kukojoa, mtazamo huu ulipokelewa kutoka kwa Al-Isnawi kutoka kwa Al-Mawardiy, akisema: hili ni suala nzuri wachache wanaolizungumzia. Jambo la sita ni: kusababisha ujauzito kwa mwingine, mtazamo huu umepokelewa kutoka kwa Al-Isnawi katika suala la eda, kwa Abu Abdullah At-Twabariy, Ibn Abi Al-Fotouh, Ibn Al-Muslim. Alisema: kama akiwa na ujauzito hali hii inatangulizwa, hata kama mahanithi mchanganyo wakiingiliana, akawa mmoja wao ni mjamzito, inahukumiwa kwa wao wawili ni wakike. Jambo la saba ni: mwelekeo unaothibitishwa kwake wakati wa kukosa kwa alama zilizotajwa hapo juu, alama hii inatangulizwa pia, kama hanithi akipenda wanamume basi yeye ni mwanamke, na akipenda wanawake basi yeye ni mwanamume, na kama akisema, napenda wote yaani wanaume na wanawake kwa uwiano sawa, na sipendi jinsia moja, basi hanithi huyu ni mchanganyo. Jambo la nane ni: kujitokeza kwa ujasiri, kupanda farasi, na kustahimili adha zote za adui, kama ilivyoelezwa na Al-Isnawi kulingana na mtazamo wa Ibn Al-Muslim. Jambo la tisa ni: kuota ndevu, kutoka matiti, kutoa maziwa, na tofauti ya mbavu. Na rai ambayo ni sahihi zaidi ni kwamba alama hizi hazithibitishi chochote. Kuhusu aina ya pili -yaani hanithi ambaye hana kiungo cha uzazi wa kiume wala wa kike- Katika kitabu cha Sharhul Muhadhab kutoka kwa Al-Baghawi: hanithi hadhihiriki ukweli wake isipokuwa kupitia mwelekeo wake. Al-Isnawi alisema: Ukweli wa hanithi unadhihirika pia kwa kutoka manii. Alisema: Kuhusu kupata hedhi huzingatiwa pia, na inawezekana kinyume na mtazamo huu pia. Kwa sababu damu si lazima kuwa hedhi ingawa ina sifa ya hedhi, kwani inawezekana kuwa damu mbaya kinyume na hali ya manii.
Lakini kama tatizo hili la uhanithi lisilokusudiwa si la kawaida katika tabia, kuzungumza na mwenendo wa mtu huyu anaitwa hanithi kama akiwa mwanaume, na anafanana na wanaume kama akiwa ni mwanamke, na haadhibiwi wala halaumiwi isipokuwa akiweza kushinikiza tatizo hili lakini ikawa hakufanya hivyo.
Lakini yule aliyezua uwongo katika tatizo hili la uhanithi kwa kuiga jinsia tofauti, kama akiwa mwanamume anaitwa hanithi, kama akiwa mwanamke basi anajifananisha na wanaume, na katika Hadithi ya Mtume iliyopokelewa kutoka kwa Al-Bukhari katika Sahihi yake kutoka kwa Ibn Abbas, alisema: Mtume S.A.W. amewalaani wanaume wanaojifananisha kike, na wanawake wanaojifananisha kiume. Na akasema: “Wafukuzeni (mahanithi) kutoka kwenye nyumba zenu.” Akasema: Mtume S.A.W. akamfukuza mtu fulani, vile vile Omar R.A. akamfukuza mtu mwingine. [imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhariy], na katika mapokezi mengine ya Hadithi hii ambayo yanaonesha iliyokusudiwa kwa wanaume wanaojifananisha kike, na wanawake wanaojifananisha kiume kwa kuzua uwongo na kwa uchaguzi, ambapo alisema: “Mtume S.A.W. amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha wanaume”.
Al-Hafidh Ibn Hajar anasema katika kitabu cha: [Fathul Bari 10/332, Ch. Dar Al Maarifah): “At-Twabariy alisema: maana ya hivyo ni kwamba hairuhusiwi wanaume kujifananisha na wanawake katika kujipamba na mavazi yanayohusiana na wanawake na siyo kinyume chake. Nikasema, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na mwendo ama kuhusu mavazi hutofautiana kulingana na ada za kila nchi, pengine kuna watu ambao mavazi ya wanaume wao hayatofautiana na mavazi ya wanawake wao, lakini wanawake hao wanajitambulisha kwa hijabu, na kulaani kwa kufananisha katika kuzungumza na kutembea huhusiana na mwenye kufanya hivyo kwa makusudi. Lakini aliyeumbwa kwa tabia hii ya uhanithi anaamrishwa kujitahidi kuacha tabia yake pole pole, na kama hakuiacha tabia yake hii huwa analaumiwa hasa kama akionesha ridhaa yake kwa tabia hii. Maana hii inafahamika kutokana na neno la “wanaojifananisha” katika Hadithi iliyopita. Lakini kuhusu mtazamo uliotajwa na An-Nawawi kwamba hanithi aliyeumbwa kwa tabia yake hii halaumiwi kwani hawezi kuacha tabia yake katika kuzungumza na kutembea baada ya kupata matibabu, na kama akiweza kuiacha tabia hii ya uhanithi hata pole pole na hakuiacha pasipo na udhuru, basi analaumiwa.
Tatizo la uhanithi lililokusudiwa ni upotovu wa tabia unaohitaji kuadhibiwa, kama tatizo hili likizidi mpaka kufikia upasuaji ili kujifananisha kwa jinsia nyingine, hatua hii ni uhalifu na hairuhusiwi pia inastahili adhabu; kwa sababu ni kubadilisha kwa viumbe wa Mwenyezi Mungu na kufuru kwa neema zake, vile vile ni kujidhuru na hali hii hairuhusiwi kisharia, na inasemekana katika hali hii ilivyosemwa na Wanavyuoni kuhusu upasuaji kwa ajili ya kuhasiwa, na kadhalika.
Al-Hafidh Ibn Hajar anasema katika kitabu cha: [Fathil Bari 9/119): “Kauli yake: (tulikatazwa kuhusu suala hilo) – yaani kuhusu kuhasiwa – suala hili ni haramu kwa wanaadamu kulingana na makubaliano ya Wanavyuoni kwa sababu zilizotajwa hapo juu, na pia kuna mateso na ukeketaji na kuwepo kwa madhara yanayoweza kusababisha kifo, na katika hali hii tunaondoa maana ya uume na tunabadilisha viumbe wa Mwenyezi Mungu na kukufuru kwa neema; kwa sababu kuumbwa mtu ni miongoni mwa neema kubwa, kama hanithi akiondoa tabia yake ya kiume basi akajifananisha na wanawake na amechagua uhaba juu ya ukamilifu”.
Imam Al-Qurtwubiy anasema katika tafsiri yake [Al-Jamii Liahkam Al-Qur'an 5/391, Ch. Dar Ash-Shaab]: Kuhusu suala la kuhasiwa kwa mwanadamu ni tatizo kubwa, kwani mwanadamu akihasiwa moyo wake na nguvu zake zitakuwa dhaifu kinyume na wanyama na kuua vizazi wake ambapo ameamirishwa kuwalinda kwa mujibu wa kauli yake Mtume S.A.W: “Oaneni, mfanye muwe wengi kwani mimi nitajisifu kwa ajili yenu mbele ya umma nyingine siku ya kiyama”, Kisha kuna maumivu makubwa katika kuhasiwa yanayoweza kusababisha kifo kwa mwenye kuhasiwa, hivyo itakuwa kupoteza fedha na kuua na mambo yote haya ni haramu, halafu hali hii ni upotoshaji wa viungo vya mwili na Mtume, S.A.W. alikataza hali hii, vile vile kundi la wanavyuoni wa Al-Hijaz na Al-Kofa wamechukiza kununua mwenye kuhasiwa na walisema kuwa: kama hamkununua mwenye kuhasiwa watu hawatahasi wanadamu, na watakubaliana kwamba hali ya kuhasiwa haina kutatua wala hairuhusiwi kwa sababu hiyo upotoshaji wa viuongo vya mwili na kubadilisha kwa viumbe wa Mwenyezi Mungu pia ni kukata kwa viungo vya mwili pasipo na kuwepo kwa adhabu, mtazamo huu ulitajwa na Abu Omar”.
Kuhusu tatizo la uhanithi lisilokusudiwa, ni mtihani wa ugonjwa na ni lazima kutibiwa na kuzingatiwa alama za kiume na kike kwa ajili ya kuainisha utambulisho wa mgonjwa ipasavyo, na inaruhusiwa kufanya upasuaji na matibabu yanayohitajika baada ya kuainisha utambulisho wa kijinsia kuonesha utambulisho wa kweli, na kuondolewa kwa mambo ya kikaboni na madhara ya kisaikolojia yanayosababisha tatizo la utambulisho wa kijinsia wa mgonjwa, kwa sababu msingi wa kisharia ni (madhara yanaondolewa), na hakuna shaka kuwa kufanana na kuchanganyika ni madhara, na kuondolewa kwake ni lazima kadiri iwezekanavyo, kwani kuacha hali hii pamoja na uwezekano wa kuzuia ni dhambi ya kujifananisha jinsia nyingine hali inayostahiki kulaaniwa.
Kwa mujibu wa yaliyotangulia hapo juu, hairuhusiwi kufanya upasuaji uitwao: kubadilisha jinsia au kusahihishwa tu isipokuwa katika hali ya hanithi ambaye ana viungo vya kiume na kike (kama viungo vya uzazi, kwa mfano), pia ni wazi kwamba hairuhusiwi kisheria katika kuainisha utambulisho wa (hanithi mchanganyo) wa kijinsia kutegemea tabia yake na mwelekeo wake isipokuwa katika hali mbili tu: ya kwanza: wakati wa kutoweza kuainisha alama za kimwili zilizotajwa hapo juu, na ya pili: kama akiwa hana kiungo cha uzazi wa kiume wala wa kike, na isipokuwa hali hizi mbili hairuhusiwi kuwa anafuata jinsia yoyote kulingana na mwelekeo wake au anayoweza kuelezea kwa hisia yake ya ndani kwamba nafsi yake ni ya jinsia tofauti. Hivyo, kama madaktari wa nchi za Magharibi na Mashariki wakishindwa kuwatibu wale wanaoitwa wagonjwa wa (tatizo la utambulisho wa kijinsia) kisaikolojia hali hii hailazimishi kusema kwamba hakuna matibabu kwao isipokuwa kwa upasuaji na kugeuza ubinadamu wao, ni nini kama kuelewa Uislamu na kufuata sharia yake na adabu zake ambazo ni msingi asili katika kuwatibu wagonjwa ambao wanataka matibabu ya kweli, sio wanaotaka kufuata matamanio yao ya kishetani yasiyo ya kawaida, na wanataka kutambua uhalali wa uhalifu wao katika haki ya nafsi zao na haki ya ubinadamu wao na katika haki ya Muumbaji S.W, na pasuaji zote alizofanya hanithi kwa ajili ya kumgeuza kuwa jinsia tofauti bado hajageuzwa kidini, na haikutolewa kwake haki za kimwili na haki za kimaadili isipokuwa haki zinazofaa kwa ukweli wake kabla ya kugeuzwa na kubadilishwa kwake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas