Kutumia Njia za Kuzuia Mimba Bila ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutumia Njia za Kuzuia Mimba Bila ya Mume Kufahamu au Mume Kumpa Mkewe Bila ya Kujua.

Question

Ni ipi hukumu ya mke kutumia njia za kuzuia mimba bila mumewe kuruhusu au kufahamu? Na vile vile kumpa mke bila ya kufahamu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mmoja wa wanandoa anafanya kitendo cha kuzuia mimba yeye mwenyewe au upande mwingine kumpa bila ya yeye kufahamu, na misukumo inayopelekea hali hii ni tofauti, na watu wanajiuliza je kuna hukumu moja inayotekelezwa katika hali zote? Na ipi asili ya hilo? Na je kuna hali zilizo nje ya asili hii? na ni zipi?
Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameumba asili ya watu kupenda kizazi, Mola Amesema: {Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na watoto} [AAL IMRAAN, 14]. Na Akatupa habari kuwa miongoni mwa wateule wake wapo walioomba hilo, hivyo Ametuelezea kuhusu Nabii Zakaria A.S. kauli yake: {Na Zakariya alipomwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi} [AL ANBIYAA, 89]. Na kutuhadithia kuhusu Nabii Ibrahim A.S. kauli yake: {Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema} [SAFFAAT, 100]
Na kuhusu Bi. Asia naye ni katika wanawake waliokamilika kama ilivyokuja katika Hadithi, Mwenyezi Mungu Amesema: {Na mkewe Firauni alisema: atakuwa kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu}. [AL QASAS, 09]
Mwenyezi Mungu hakuacha njia ya kupata hicho kizazi kwa kupuuza, bali Amejenga uhusiano ambao unaweza kupatikana kizazi kupitia uhusiano huo, Amesema Mtukufu wa kusema: {Na ambao wanazilinda tupu zao * Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa * Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka} [AL MUUMINUN, 5 : 7]. Na Akasema: {Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya} [AL ISRAA, 32].
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amehalalisha ndoa na kuharamisha mambo machafu ikiwa lengo ni kulinda heshima na kizazi, vile vile imewekwa sharia ya kukaa mwanamke siku maalumu baada ya kuachika au kufiwa na mumewe, hekima ya hilo: Ni pamoja na kuokoa kizazi, na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amezuia nasaba isipokuwa kwa njia Aliyoiweka kwa waja wake, na siyo kwa njia ya uchafu kama vile kujipatia mtoto, na katika hili Mola Amesema: {Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayesema kweli, naye ndiye anayeongoa Njia}. [AL AHZAAB, 4: 5]
Kwa ufupi: Kutafuta kizazi ni jambo linalofaa na ni halali, wala haizingatiwi kuwa na pupa katika hilo ni jambo lenye kuchukiza; kwa kuwa wateule walifanya hilo.
Wanachuoni wamezungumzia suala la kuzuia mimba kwa njia za muda mfupi kwa wanandoa wawili au mmoja wao hasa katika kitabu cha ndoa.
Hukumu ya kisharia katika hilo ni kuwa haifai kutumia njia za kuzuia mimba pasi na ruhusa ya upande wa pili, kwani wanandoa wote wawili hawana haki ya kila mmoja peke yake kupangilia kizazi pasi na mashauriano.
Dalili ya hilo ni kuwa kutaka mtoto kunazingatiwa ni mahitaji ya kila mmoja, kama vile ni mahitaji ya wote kwenye ndoa, imepelekea baadhi ya waja wema waliotangulia kusema kuwa utasa ni kasoro inayorejea kwenye ndoa. Al-Hassan Al-Basriy amesema: “Ikiwa mmoja wa wanandoa wawili ni tasa basi mwenzake huhiyarishwa, Ahmad akasema: Huenda mke wake akawa anataka mtoto”. Rejea kitabu cha: [Al-Mughniy cha Ibn Qudama, 7/186, Ch. Maktabat Al-Kahira].
Imepokelewa kutoka kwa Umar Ibn Al-Khatwab amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu amekataza kinga za mimba bila ya ruhusa ya mke huru” imepokelewa na Ibn Maja ikiwa na ushahidi unaotokana na Ibn Umar na Ibn Abbas, nayo ni kauli ya Said Ibn Jubeir na Ikrima pamoja na Atwaa, kama katika kitabu cha: [Abdullrazziq] na kitabu cha: [Al-Sunan Al-Kubra cha Al-Baihaqiy].
Ibn Abdullbar alisema: “Imepokelewa katika mlango huu Hadithi Marfui ambayo mapokezi yake ni dhaifu, lakini wanachuoni wamekubaliana kuwa maana yake ni sahihi”. Kitabu cha: [Tamhid cha Ibn Abdullbarr, 3/150, chapa ya Wizara ya Waqfu na mambo ya Kiislamu – Morocco].
Mfano wa tuliyoyataja wamezungumzia wanachuoni wengi:
Ibn Qudama amesema: "Asitoe manii nje isipokuwa kwa ruhusa ya mke wake. Al-Qadhi amesema: Uwazi wa kauli ya Ahmad ni lazima kutaka ruhusa ya mke katika kutoa manii nje, na inachukuliwa kuwa ni jambo linalopendeza; kwa sababu haki yake ni katika kukutana kimaumbile na mume wake, siyo katika kushusha manii, kwa dalili kuwa mume anamwacha kwenye hali ya upweke na kutojamiiana, na watu wa Imam Shafi katika hilo kuna mitazamo miwili, mtazamo wa kwanza ni bora zaidi, kutokana na yaliyopokelewa kutoka kwa Umar R.A. amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu amekataza kinga za mimba bila ya ruhusa ya mke huru". imepokelewa na Imamu Ahmad katika kitabu chake cha Musnad na Ibn Maja, kwa sababu ana haki ya kuwa na mtoto, na kwamba kutoa manii nje kuna madhara basi wala haifai isipokuwa kwa ruhusa yake”. Kitabu cha: [Al-Mughniy, 7/298].
Al-Kharshiy Al-Malikiy amesema katika kitabu cha: [Sharh Al-Mukhtasar]: “Na mume wake anaweza kutoa manii nje ikiwa mke amempa ruhusa, na bwana wake ni kama mwanamke huru ikiwa atatoa ruhusa, kwa maana inafaa kwa mume kutoa manii nje, lakini akiwa ni mjakazi ni lazima apate ruhusa yake na ruhusa ya bwana wake kwa mumewe, ambapo mjakazi atakuwa ni mwenye majukumu hapo baada ya mtoto hivyo hawezi kuwa na utulivu bila ruhusa ya bwana, akiwa ni mwanamke huru inatosha ruhusa ya mwanamke tu”. Kitabu cha: [Sharh Al-Mukhtasar cha Khalil Al-Kharshy, 3/225, Ch. Dar Al-Fikr].
Al-Marudy amesema: "Kutoa nje manii kuna aina mbili: Utoaji wa manii nje, na kuwa mbali na kuingilia, aina zote hizo mbili ni halali kwa mjakazi na kwa mke, lakini inapaswa kuiridhisha nafsi ya mke kwa hilo, pamoja na kutopaswa kuiridhisha nafsi ya mjakazi, kwa sababu mke huru ana haki kwa mtoto kuliko mjakazi, ama kutoa manii nje ni kule kuingiza uume kwenye tupu ya mwanamke ikiwa atahisi kuwa manii yanashuka atatoa uume wake na kutolea manii nje, kutoa manii huku hakuzuii kupata mtoto". Kitabu cha: [Al-Hawiy Al-Kabir, 11/159, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya].
Maelezo haya yaliyopita yanafahamika kutofaa mume kutoa manii nje isipokuwa kwa ruhusa ya mkewe. Hii ni kutokana na haki yake ya kuwa na mtoto.
Lakini ikiwa kuna sababu za kisharia, basi inafaa upande mmoja kuwa peke yake, kama kusababisha madhara kwa mke kutokana na mimba alionao na mume kutokuwa makini na hilo au kutomjali, au mume akawa ni mtu fasiki na asiyejali na mke akawa yupo ndani ya kipindi cha kusubiri kuachana, naye mume vile vile ikiwa yupo katika mazingira anahofia kizazi chake kuharibika.
Ibn Abidiin amesema katika kitabu chake: "Kuwa si halali bila ya ruhusa ya mke, na wakasema ndani ya nyakati zetu: Ni inafaa kutokana na nyakati mbaya zilizopo". Na katika Fatawa amesema: Ikiwa atahofia ubaya na uovu kwa mwanawe basi anaweza kutoa manii nje bila ridhaa ya mke hii ni kutokana na ubaya wa nyakati, basi na azingatie mfano wa hali hiyo kuwa ni katika udhuru unao ondoa ruhusa yake.
Imefahamika kuwa maelezo yaliyonukuliwa kwenye madhehebu ni kuwa si halali, na maelezo haya ni kutoka kwa Masheikh wa madhehebu ili kubadilisha baadhi ya hukumu kutokana na mabadiliko ya nyakati, yamepitishwa haya kwenye kitabu cha: [Al-Fat-h] na pia kupitishwa na Al-Kahastany ambapo alisema: haya ikiwa hatahofia juu ya mwanawe uovu na ubaya wa nyakati tofauti, na kama atahofia hilo basi inafaa bila ya ruhusa yake. lakini kauli ya Al-Fat-h: "Basi na azingatie mfano wake .. n.k." Inachukuliwa kutakiwa mfano wa udhuru kama huo, kama vile kauli yao: mfano wako haufanyiwi ubahili. Kauli hii inachukuliwa kuwa anataka kuwa na udhuru kama huu kama vile kuwa kwenye safari ndefu, au kuwa kwenye nchi za vita akawa na hofu kwa mtoto wake, au mke akawa ni mwovu wa tabia na akataka mume kuachana naye lakini akahofia kushika mimba, vile vile ikapelekea uharibikaji wa mimba”. Kitabu cha: [Radd Al-Muhtar ala Dur Al-Mukhtar, 3/176].
Kutokana na maelezo yaliyotangulia: Ni wazi kuwa haifai kwa mwanamke kutumia njia za kuzuia mimba kwa muda bila ruhusa ya mumewe, kama vile haifai kwa mume kumpuuzia mke na kumfanya atumie njia za kuzuia mimba bila ya mke mwenyewe kufahamu wala kupata ruhusa yake, isipokuwa ikiwa ipo haja halali ya kisharia ya kufanya hivyo kama ilivyoelezewa hapo juu.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas