Suala la Mwizi Mwenye Busara katika...

Egypt's Dar Al-Ifta

Suala la Mwizi Mwenye Busara katika Vitabu vya Fiqhi.

Question

Mmoja wa wanafunzi aliniulizia katika hali ya changamoto kuhusu “Mwizi mwenye busara” na akaniahidi kunipa pesa iwapo nitamjua! Nikawaambia: Mwizi huyo ni "Arsène Lupin", akacheka kwa kejele, akasema: Nakuuliza katika Fiqhi. Nikasema: Kuna Uhusiano gani kati ya mwizi mwenye busara na Fiqhi? Lakini alikataa kunipa alichoniahidi, na kushikamana na madai yake, je! Katika Fiqhi kuna istilahi hii? Ina maana gani? Na kwa nini Mwizi huyu aliitwa kwa jina hilo? Natumai kujua na shukrani nyingi kwenu. 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni zake Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Arsène Lupin ni mhusika wa kubuni aliyeundwa na mwandishi wa Ufaransa, Maurice Leblanc na kumfanya kuwa nguli wa hadithi kadhaa za upelelezi. Hadithi hizi zimepokelewa vyema na wasomaji, haswa wale wanaopenda kusoma uhalifu, kuchambua nia yake na kufichua wahusika mbalimbali ili kuwafikisha katika haki.
Sababu ya kumwelezea “Arsène Lupin” kama “mwizi mwenye busara” ilikuwa kwamba hadithi ya kwanza ilikuwa na kichwa cha “Arsène Lupin mwizi mwenye busara”, kisha zikatoka riwaya nyingine kadhaa zilizo na vichwa tofauti, ikiwa ni pamoja na: “Pembe tatu ya dhahabu” na “Kisiwa chenye makaburi thelathini” na “Kanisa Jekundu”. Riwaya hizi zimetafsiriwa kwa lugha kadhaa, ikiwamo ya Kiarabu.
Kuhusu istilahi ya: “Mwizi mwenye busara” inayopatikana katika vitabu vya Fiqhi inajumuisha maneno matatu, "mwizi", na “mwenye busara”, Abul Makarem Al-Mtarizi alisema: busara iliyomo akilini na imepokelewa kutoka kwa Ibn A-Aarabi: busara iko ulimini (maneno) Na Hadithi ya Umar (R.A.) alisema: “Ikiwa mwizi ni mtu mwenye busara, haadhibiwi.” Yaani akiwa mwenye busara katika maneno yake anaondoshewa adhabu kwa sababu ya hoja yake. [Moroko: Kidahizo cha Dh R F, uk. 298, Ch. Dar Al-Kitab Al-Arabi].
Kwa hivyo, mwenye busara hakuwa mwongo, kwa sababu angeweza kwa ulimi wake kufikia kile alichotaka bila ya kusema uwongo. Maelezo haya ya “mwizi mwenye busara”, ambayo yalitumiwa na zaidi ya wanavyuoni mmoja, yanaitwa mwizi ambaye ana akili na taarifa nzuri na pia ana uelewa na dhamana ili aweze kuyatumia haya yote kwa ajili ya kuondoa adhabu akiwa amekamatwa kwa kuchochea tuhuma kadhaa ambazo zinaweza kupelekea akaondoshewa adhabu ya wizi.
Hii inachukuliwa kutoka katika msingi ambao ni maarufu katika Fiqhi kuwa adhabu zinaondolewa katika mambo yenye shaka, matini nyingi zimetajwa kuhusu jambo hilo, zimejumuishwa kwa muhtasari wa Imamu katika kitabu chake cha Misingi ya Fiqhi ya Imamu Shafi, As-Suyuti alisema: Msingi wa sita, Adhabu: zinaondolewa kwa mamabo yenye shaka kama alivyosema Mtume S.A.W.: “Ondosheni adhabu katika mambo yenye shaka”. Imepokelewa kutoka kwa Ibn Adiy katika sehemu ya Hadithi ya Ibn Abbas, na Ibnwa Majah kutoka Hadithi ya Abu Hurayrah: “Ondosheni adhabu kadiri mnavyoweza”. Na imepokelewa kutoka kwa Imamu Tirmidhi, Hakim na Al-Baihaqiy na wengine kutoka katika Hadithi ya Bi. Aisha R.A.: "Waondosheni adhabu Waislamu kadiri mnavyoweza, kama mkipata njia kwa ajili ya muislamu, basi mwachieni huru. Imam akikosea msamaha ni bora zaidi kuliko kukosea adhabu". Imepokelewa kutoka kwa Al-Baihaqiy kutoka kwa Umar na Uqbah Ibn Amir, na Mu'ath Ibn Jabal. Na imepokelewa kutoka katika Hadithi ya Ali, akisema, “Ziondosheni adhabu.” tu. Musaddad alisema katika Musnad yake: Tumeambiwa kutoka kwa Yahya Al-Qatwan kutoka kwa Shu’bah kutoka kwa Asim kutoka kwa Abu Wael kutoka kwa Ibn Masuod amesema: "Ziondosheni adhabu katika mambo yenye shaka.". Vile vile imepokelewa kutoka kwa At-Twabaraniy kuwa amesema: “Ziondosheni adhabu na kuua kwa Waja wa Mwenyezi Mungu kadiri mnavyoweza.” Yaani mambo yenye shaka yanaondoa adhabu. [Al-Ashbah wan Nadhair: Uk. 123,122, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Sababu ya kuondoshwa kwa adhabu na mwizi huyu kuwa wanavyuoni wameujua wizi na kuweka masharti ambayo lazima yakamilishwe ili kumuadhibu mhalifu, wakati sharti moja lilipopotezwa au lilikuwepo kwa jambo lenye shaka inaondolewa adhabu.
Al-Khatwib As-Sherbiniy amesema katika kitabu chake [Sharhul Minhaaj]: “(Vivyo hivyo) hairuhusiwi kutekeleza adhabu ya kukataa kwa mwizi (akidai kuwa ni zake) yani pesa zilizoibiwa au akidai (nusu yake) na hakuna yeyote aliezidai pesa hizo baada ya wizi nao umethibitishwa kwa ushahidi; inawezekana mtu yule akawa anasema kweli kwa hivyo lilikwepo kwa shaka liliosababisha kuondolewa kwa adhabu ya kukata. Imepokelewa kutoka kwa Imam As-Shafiy – R.A. - kuwa alimwita mwizi yule ni mwenye busara: yaani mwenye ujuzi wa fiqhi, na kuna mtazamo mwengine unasema: inaruhusiwa kutekeleza kwa adhabu ili watu wasichukue jambo hili ni kama kisingizio cha kuondoa kwa adhabu, na kuchukua matini juu ya kama akitoa ushahidi wa kile alichodai. [Mughni Al-Muhtaaj: 5/470, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Ibn Qudaamah anasema: "Imepokelewa kutoka kwa baadhi ya masahaba wa Mtume waliotangulia kuwa walisema: Hairuhusiwi kutekeleza adhabu kwa mwizi mwenye busara. Yaani kama kuna ushahidi na akidai jambo lenye shaka linaloondoa adhabu ya kukataa, basi hairuhusiwi kutekeleza kwa adhabu. [Al-Mughni: 9/81, Ch. Maktabat Al-Qahirah]
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia hapo juu: istilahi ya “Mwizi mwenye busara” imetajwa katika vitabu vya Fiqhi, naye ni mwizi mwenye busara ambaye anaweza kujiepusha na adhabu ya wizi kwa akili na utambuzi wake, bila ya kusema uwongo, na hii ni kwa kupitia kuchochea tuhuma, ambazo zinaondoa adhabu; Kwa hivyo, ameitwa kwa jina hilo, na hakuna uhusiano wowote kati ya mtu yule na istilahi iliyotajwa katika baadhi ya Hadithi na fasihi za Ulaya.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas